Wito: Gomeni kwenda kuangalia mechi ya Brazil na Taifa Stars!

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, alafu Anakuja mtu kama Shukuru Kawambwa anasema ujio wa timu hiyo ni historia kwa Tanzania na "faraja" kwa mashabiki wa soka nchini.

Faraja gani kwa watanzania kama siyo kuwatusi watanzania..Yaani ni kuwapoza na matatizo yenu..

On top of that:Hawana pesa ya kuzunguka mikoani kuhakiki wanachama wa CCJ..
 
Kwa wale wanaoafiki Brazil kuja hapa bongo - ni kwamba wanafikiria ki-starehe zaidi : kufikiria kwa kutumia m*t*k*

Kwa wale wasioafiki Brazil kuja hapa bongo - ni kwamba wanafikiria mi-mantiki: kufikiaria kutumia ubongo

Na wakati wote starehe uwa ina-out-rule mantiki in Tanzania!

Ukiachana na wanasiasa, watanzania wengine wooote watakaudhuria mechi hii (Jumatatu usiku - of all the days in a week) ni wale sehemu ya asilimia 70 amabayo hata JK mwenyewe anadirki kusema ni fuata upepo!
 
Hapa sasa naona tunavuka mpaka. Hii ni STAREHE kama zilivyo starehe zingine na ni Biashara. TFF wanawaleta Brazil, lakini ni lazima wabuni mbinu ya kupata fedha hizo kutoka kwa watazamaji wa mpira.

Kipima Pembe uliyapima vizuri maneno yako?tatizo si kufanya biashara,tatizo lipo kutumia pesa za Serikali na za watanzania ote kufanya biashara?.Wanaowaleta wanamziki wanatumia pesa zao kufanya hivyo na hili mie sina ubaya wowote.

Hongera TFF. Wale wasio na 30,000.00 poleni, lakini starehe si haki ya kila mtu. Starehe ni haki ya kila mwenye uwezo wa kuilipia!!
Endelea Kuwapongeza tu..si wanawaletea Brazil ili mfarijike!

BTW the line:Do you know how much Zimbabwe wamelipa?
 
Mkuu Gembe sidhani kama unawafahamu vizuri hawa watu wanaoitwa waTanzania. Wao na tendo kugoma hawapaswi kuwekwa katika sentensi moja. WaTanzania ni sikio la kufa

Mgomo utakuja tu by default..........Kutokana na hali ngumu mifukoni,Usitegemee uwanja kujaa kwa kiingilio cha Tshs 30,000/-(kwa walala hoi),.......let's wait and see..................Hivi kuna TV Station itaonesha game hii??????????
 
Kwa wale wanaoafiki Brazil kuja hapa bongo - ni kwamba wanafikiria ki-starehe zaidi : kufikiria kwa kutumia m*t*k*

Kwa wale wasioafiki Brazil kuja hapa bongo - ni kwamba wanafikiria mi-mantiki: kufikiaria kutumia ubongo

Na wakati wote starehe uwa ina-out-rule mantiki in Tanzania!

Ukiachana na wanasiasa, watanzania wengine wooote watakaudhuria mechi hii (Jumatatu usiku - of all the days in a week) ni wale sehemu ya asilimia 70 amabayo hata JK mwenyewe anadirki kusema ni fuata upepo!

Ona zimbabwe wametumia kiasi gani

The Zimbabwe Football Association (Zifa) chief executive officer Henrieeta Rushwaya said it will cost a modest US$ 10 to watch the high profile international friendly match on Wednesday. However the VIP seats will cost US$ 40 and US$60.

The Zimbabwe National Soccer Supporters Association president Eddie Nyatanga confirmed they had a tough time convincing both Zifa and the Zimbabwe Tourism Authourity that the match should have a lower gate charge.

The Ministry of Tourism and Hospitality said the government was hoping to recoup some of the money they spent in bringing Brazil and were expecting a full house in the 60 000 seater National Sports Stadium. It is believed it will cost Zimbabwe US$ 1,8 million to bring the Brazil team.The government will foot 45 percent of the expenses while Zimplats, NetOne and CBZ Bank will pay part of the bill.

FACTS:

1.Zim Govt will pay only 45% of $1.8m

2.VIP will cost $60 dollar compare to $170 in Tanzania

3.Normal will be $10 and here it will be $25.

Bado tu unataka tulipe zaidi..Hell No..ila kwa kuwa ni starhe na mnataka kufarijika zaidi ..Go On..wakati mwingine kuna haja ya kukataa

Source:RadioVop Zimbabwe: Zimbabwe latest news | Zimbabwe news | Zimbabwe situation | Zimbabwe online | Zimbabwe daily news | Your gateway to Zimbabwe news - Zimbabwe-Brazil Match One Of The Cheapest

Ni wivu tu unawasumbua kwa sababu tu upo USA, SA, UK nk karatasi zimebana huwezi rudi mnaleta za kuleta. Ile ni starehe kama starehe nyingine anae weza ataenda asieweza alipe Tsh 300 aone kwenye TV na nyie roho ya korosho mtakufa na vijiba vyenu vya roho.

Unataka kumuona Fabiano, Kaka nk kwa dola 3? wapi! UK premier lg mnalipa btw 20-80 pounds kuangalia Wigan tu itakuwa samba?

Mbona Miss Tanzania kiingilio 200,000 hamsemi na ipo miaka nenda miaka rudi, mnakosa ya kujadili sasa, wenzenu Kenya wanapiga kelele Tz inawapiga bao kwenye kutangaza nchi nyie mnaponda.
 
Jamani Tanzania ni shamba la bibi, yeyote akija anaruhusiwa kuvuna maboga!
 
Ni wivu tu unawasumbua kwa sababu tu upo USA, SA, UK nk karatasi zimebana huwezi rudi mnaleta za kuleta. Ile ni starehe kama starehe nyingine anae weza ataenda asieweza alipe Tsh 300 aone kwenye TV na nyie roho ya korosho mtakufa na vijiba vyenu vya roho.

Unataka kumuona Fabiano, Kaka nk kwa dola 3? wapi! UK premier lg mnalipa btw 20-80 pounds kuangalia Wigan tu itakuwa samba?

Mbona Miss Tanzania kiingilio 200,000 hamsemi na ipo miaka nenda miaka rudi, mnakosa ya kujadili sasa, wenzenu Kenya wanapiga kelele Tz inawapiga bao kwenye kutangaza nchi nyie mnaponda.

FACT:

1.Uchumi wa Uingereza ni tofauti na khali ya uchumi wa nchi yetu.

2.Serikali huwa haitoi pesa kwa ajili ya watu kwenda kuangalia mpira

3.Kuwa marekani hakuhusiani na hoja niliyoiweka hapa.Acha kuleta Viroja

4.Miss Tanzania ,serikali haichangii pia na wanaolipa hizo si watanzania wote,sababu ya kuwaleta leta Brazil kama alivyosema Kawamba ni kuwafariji.sasa mtafarijiwa kwa kulipia kiasia kikubwa hivyo?yaani ndiyo yale yale aliyoyasema baba wa taifa..Mtu anakushauri jambo la kipumbavu

Wachungaji bado tunaendelea kukemea kwa nguvu.Siku nyingi sijachangia hapa ila leo nimeamushwa na mpwa wangu akitaka nimtumie pesa ya kiingilio.
 
Mungu ni mkubwa!nilikuwa na hasira sana juu ya hii mechi ila naelekea kufarijika baada ya kupata hili wazo la kugoma na nimelipokea hata wengine wakienda ila mm nafsi yangu itaridhika,wajumbe naomba twende mbele zaidi ni kwanini tusiandaee maandamano ndani ya masaa 48? hapa la kutusaidia wale wote wenye uzoefu wa kuomba vibali vya maandamano watusaidie hatua za kupata kibali,haiwezekani hawa jamaa wakawa wanafanya mambo wanavyotaka na ss tunanyamaza kisa ooh tumaisha chelewa ,hata kama ila lazima wajue kuwa hii nchi si wajinga kama wanavyo fikiria.

Down with brazil. down with the Sponsors of the brazilian national team huu ni wizi wa hali ya juu, Nike wanalipa mahela kibao kwa mwaka, Volkwagen nao walipa mahela kibao etc kwa nini watukamue sie maskini na vihela mbuzi vyetu?
 
Ni wivu tu unawasumbua kwa sababu tu upo USA, SA, UK nk karatasi zimebana huwezi rudi mnaleta za kuleta. Ile ni starehe kama starehe nyingine anae weza ataenda asieweza alipe Tsh 300 aone kwenye TV na nyie roho ya korosho mtakufa na vijiba vyenu vya roho.

Unataka kumuona Fabiano, Kaka nk kwa dola 3? wapi! UK premier lg mnalipa btw 20-80 pounds kuangalia Wigan tu itakuwa samba?

Mbona Miss Tanzania kiingilio 200,000 hamsemi na ipo miaka nenda miaka rudi, mnakosa ya kujadili sasa, wenzenu Kenya wanapiga kelele Tz inawapiga bao kwenye kutangaza nchi nyie mnaponda.

Hii imetulia
 
Tulieni muangalie mechi, Mimi kinachonisikitisha zaidi ni kwamba hawa wanaopiga kelele sana ndo watakua mstari wa mbele kwenye milango ya kuingilia. Hilo ndo sikitiko langu kuu
 
Ona zimbabwe wametumia kiasi gani

FACTS:

1.Zim Govt will pay only 45% of $1.8m

2.VIP will cost $60 dollar compare to $170 in Tanzania

3.Normal will be $10 and here it will be $25.

Bado tu unataka tulipe zaidi..Hell No..ila kwa kuwa ni starhe na mnataka kufarijika zaidi ..Go On..wakati mwingine kuna haja ya kukataa

Source:RadioVop Zimbabwe: Zimbabwe latest news | Zimbabwe news | Zimbabwe situation | Zimbabwe online | Zimbabwe daily news | Your gateway to Zimbabwe news - Zimbabwe-Brazil Match One Of The Cheapest

Gembe tusisahau kuwa hii 2010, mwaka wa uchaguzi. Baada ya kupata fundisho la EPA ni dhahiri kuwa mwaka huu kila senti itatafutiwa stakabadhi ya jinsi ilivyotumika. Bado siamini kuwa $6m zitatumika solely for the match btn Brazil na sisi. Hapa ni lazima kuwe na win-win situation btn watafuta hela za uchaguzi na Brasil.

Ningekuwa Brasil ningekataa kabisa kucheza bongo kwani kashfa ijayo haitaiacha Brasil ikiwa safi kwenye hili. Hivi viingilio ni geresha tu. Itahitaji mashabiki 80,000 watakaolipa wastani wa $75 ili ku-break even, sasa bado cha juu. Je watanzania wana hizo hela?.
 
Ni wivu tu unawasumbua kwa sababu tu upo USA, SA, UK nk karatasi zimebana huwezi rudi mnaleta za kuleta. Ile ni starehe kama starehe nyingine anae weza ataenda asieweza alipe Tsh 300 aone kwenye TV na nyie roho ya korosho mtakufa na vijiba vyenu vya roho.

Unataka kumuona Fabiano, Kaka nk kwa dola 3? wapi! UK premier lg mnalipa btw 20-80 pounds kuangalia Wigan tu itakuwa samba?

Mbona Miss Tanzania kiingilio 200,000 hamsemi na ipo miaka nenda miaka rudi, mnakosa ya kujadili sasa, wenzenu Kenya wanapiga kelele Tz inawapiga bao kwenye kutangaza nchi nyie mnaponda.

Hapana..............Acha mipasho babu.............hakuna cha wivu wala nini......

-Kuna tofauti kubwa sana kati ya Miss Tanzania na Foot ball babu..........Binafsi sipendi mambo ya Miss Tanzania and the likes....Mpira wa miguu ni burudani kubwa kwa asilimia kubwa ya watanzania(katu usilinganishe na mambo ya mamiss)....Miss Tanzania ina walengwa wake(wachache)

-Cha kuangalia hapa ni kipato cha mtanzania wa kawaida(mlala hoi),pia unapaswa kuangalia kipato cha mtu aliye Uingereza(ambaye unadai analipa kati ya Paundi 20-80 kuangalia mechi ya Wigan).....Hapa tunaangalia Pato la Mtanzania ambaye analipwa let say Tshs. 70,000/- ama 105,000/- kwa mwezi anaenda kulipa Tshs 30,000/- kuwaangalia hao akina Fabiano,Kaka na wengine.........na huyu mtu ana familia yake inamtegemea...........Sijui itakuwaje tu................

-Sidhani kama ni sahihi kuitangaza nchi kwa kuwakamua wananchi.............Fikiria hao Brazil wameletwa kwa fedha za Watanzania,still watanzania wanakamuliwa mbaya............Si haki hata kidogo

-Mbona akina Eto'o,Song,Makoun,Kameni,Drogba,Kalou na wengine wanapokuja tunawaangalia kwa Tshs 5000/-(Na wote hawa wanacheza WC kama ilivo kwa hao akina Kaka,Fabiano,Robinho na wengine?).............Mi sioni tofauti ya Eto'o na Maicon ama Lucio(wote wapo Inter),nawaona sawa tu japo wanatoka nchi tofauti

Swali hapa ni je?,pesa ya kuwaleta Brazil imetolewa na nani?...ni TFF,Serikali ama wadhamini(SBL)?............Kama ni serikali kwa nini kiingilio kiwe kikubwa hivi???????

Huu ni Wizi...................Wizi Mtupu
 
Pamoja na haya yote mnayoyazungumza ni kwamba tu hadi kufikia jana tiketi za Shilingi laki mbili (200,000Tshs) zilikua zimeshakwisha... na hivyo kufanya kiasi cha shilingi milioni 140 kupatikana.

Habari ndo hiyo... kumbe watu wana hela mjini hapa?
 
Tanzania coup brings Brazil to Dar

It is the "once in a life-time" event for most Africans, so goes the most popular slogan of the moment.
You will follow the World Cup on television but only a tiny few will be able to say they saw Kaka, Drogba, Messi, Et'oo or Rooney perform from an almost touching distance.

The World Cup right on African soil; too good to miss out. You don't go to South Africa and you surely will not get a hundred percent of the real thing.

Not the Tanzanians, though. Next Monday, Kaka, Robinho, Maicon, Dani Alves, Gilberto Silva, Louis Fabiano and co, believe it or not, will be playing in Dar es Salaam against the likes of Mrisho Ngassa and Musa "Mgosi" Hassan of the Taifa Stars.

World Cup fever

If Tanzanians cannot go to the World Cup in South Africa, they have decided to bring the World Cup fever itself from South Africa to "Bongo" [musical youth name for Tanzania].

What happened, how did they pull off such a coup?

"In a record two weeks of talks with Brazil it is now a hundred percent confirmed that we play them on June 7, 6pm at the National Stadium, Dar es Salaam," said Tanzania Football Federation chairman, Leodegar Tenga, attending the Cecafa Kagame Cup championship in Kigali.

"It is a football treat to every fan in East Africa and we are telling them now; it's a happening of a life time, catch the plane, the bus or the boat and be there on Monday.

"We did not do it just for ourselves [the Tanzanian], we want all our neighbours to come and witness this."

Tenga is the President of the Council of East and Central African Football Associations (Cecafa) who just concluded a highly successful Kagame Cup Club Championship in Kigali.

He talked about how many African countries had dreamt of having World Cup teams to train on their soil before going to South Africa and how Tanzania had done well by recently hosting Cote d'Ivoire [on their way to the African Cup of Nations earlier in ten year] and clinching the spectacular deal with Brazil.

When TFF got the ball rolling the scoring shot was delivered not by themselves.

"We talked to our President [Jakaya Kikwete] and it's him, really, who made it all happen.

"He was enthusiastic right from the word go and got every needed state machinery moving to make this match.

"This is not just about a football match. TFF would not have the logistical capacity for a highly elaborate security operation to ensure the Brazilians safety, for example."

The Brazilians were being paid, according to Tenga, "a figure which, unfortunately, you will have to excuse me, I will not disclose," but sources said it was several million dollars.

Triple the ticket price
How could the TFF afford that? The best gate at Dar's National Stadium is normally $1 million (Sh78 million). Will they have to double or triple the ticket price to bridge the deficit.

"Absolutely not. We have to be practical; consider what our soccer loving people can afford.

Daily Nation

Monday

May 31, 2010

This is what Kenyan media, daily nation reported today about the international friendly Match.
Kutoka kwenye hilo gazeti:
>Hili linaonekana ni jambo kubwa sana kwa majirani zetu, na wanashangaa imewezekanaje.
> Tenga amesema kiingilio kitakuwa cha kawaida ili watanzania wapenda soka waweze kumudu!!
 
Pamoja na haya yote mnayoyazungumza ni kwamba tu hadi kufikia jana tiketi za Shilingi laki mbili (200,000Tshs) zilikua zimeshakwisha... na hivyo kufanya kiasi cha shilingi milioni 140 kupatikana.

Habari ndo hiyo... kumbe watu wana hela mjini hapa?
Amani..........Binafsi sishangai hizo tiketi kuisha.........Hizo ni tiketi chache sana,ni tiketzi za viti 748 tu(za V.I.P).........Uwanja unabeba karibu watu 60,000.........Usishangae ukiona mechi ikiangaliwa na watu 20,000 tu...........

DONDOO ZA MAPATO STARS V BRAZIL

VIP A kwa Sh 200,000: Viti 748 zitapatikana Sh 149, 600,000 VIP B Sh 150,000: Viti 2,260 zitavunwa Sh 339,000,000 VIP C Sh 100,000: viti 2,404 , zitahifadhiwa Sh 240, 400,000.

Rangi ya Chungwa mkabala na VIP Sh 80,000: viti 6, 460 Sh 516, 800,000, Rangi ya chungwa nyuma ya magoli Sh 50,000 viti 7, 300 zitapatikana Sh 365, 000,000.

Rangi ya Bluu 30,000: viti 18, 364 zitapatikana Sh 550, 920, 000. Kijani Sh 30,000: viti 19,590 zitapatikana Sh 587,700,000.
 
Kiingilio cha chini Stars Vs Brazil sh 30,000/=

NI historia katika soka la Tanzania, ambapo mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars na Brazil utakaofanyika Juni 7 mwaka huu utaingiza kiasi cha Sh 2,749, 420,000.

Hatua hiyo inatokana na viingilio vilivyotangazwa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambapo kiingilio cha juu ni Sh 200,000 na cha chini ni Sh 30,000 katika mchezo uliopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa kawaida michezo mingi inayofanyika kwenye uwanja huo, kiingilio cha juu huwa ni Sh 50,000 wakati kile cha chini huwa ni Sh 3,000 ama Sh 5,000, lakini kulingana na maelezo ya Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, ni kuwa gharama za kuileta nchini Brazil ni kubwa, hali inayofanya viingilio pia viwe vikubwa.

Hata hivyo, Mwakalebela akitangaza viingilio hivyo jana, hakusema gharama hizo ni kiasi gani zaidi ya kusisitiza wamefanya hivyo kutokana na gharama za kuileta nchini Brazil, jambo ambalo sasa litawafanya wananchi wa kawaida maarufu kama wenye uchungu na mpira kujikamua zaidi mifuko yao, vinginevyo wakae nyumbani kwenye televisheni waungalie kwani utaoneshwa, ama watengane na Sh 30,000.

Mwakalebela alisema Jukwaa la Viti Maalum A (VIP A) ni Sh 200,000, VIP B ni Sh 150,000, VIP C Sh 100,000.

Jukwaa la Rangi ya Chungwa Mkabala na VIP ni Sh 80,000 na Jukwaa la Rangi ya Chungwa nyuma ya magoli ni shilingi 50,000 na Jukwaa la Rangi ya Bluu Mzunguko pamoja na Jukwaa la Rangi ya kijani sehemu hizo zote itakuwa Sh 30,000.

Kutokana na hali hiyo kulingana na takwimu za uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 walioketi zilizotolewa mwaka 2007 na aliyekuwa Mkurugenzi wa Michezo, Henry Ramadhan, siku chache kabla ya mchezo wa Taifa Stars na Msumbiji, kwa kiingilio hicho cha Sh 200,000 kwa jukwaa kuu A (VIP), ambalo lina viti 748, zitapatikana Sh149, 600,000.

Jukwaa B kiingilio cha Sh 150, 000 na kuna viti 2,260 zitapatikana Sh 339,000,000, huku Jukwaa Kuu C kwa kiingilio cha Sh100,000 na kuna viti 2,404 zitahifadhiwa Sh 240, 400,000.

Jukwaa la rangi ya chungwa linaloangalia jukwaa kuu kwa kiingilio cha Sh 80,000 na kuna viti 6, 460, kiasi cha Sh 516, 800,000 kitapatikana, huku majukwaa ya nyuma ya magoli, ambapo kiingilio ni Sh 50,000 na kuna viti 7, 300 zitapatikana Sh 365, 000,000.

Jukwaa la bluu mzunguko lenye viti 18, 364 kiingilio cha Sh 30,000 zitapatikana Sh 550, 920, 000, wakati jukwaa G ambalo lina viti 19,590 linalojulikana pia kama jukwaa la kijani, ambalo ndilo Watanzania walio wengi hujihifadhi hapo kwa kiingilio hicho cha Sh 30,000 basi zitavunwa Sh 587,700,000.

Kutokana na hali hiyo kama zitauzwa tiketi zote hizo kiasi cha 2, 749, 420, 000 kitapatikana, ambapo kihesabu ni sawa na kusema Sh bilioni tatu.

Lakini kwa vile watakuwepo watu wachache watakaoingia bure kutokana na sababu mbalimbali, inawezekana labda kukawa na upungufu wa Sh milioni 200, lakini bado kiasi kitakachosalia ni kikubwa kwa maana itakuwa Sh bilioni 2.5.

Rekodi ya juu ya mapato yanayotokana na viingilio iliwekwa Septemba mwaka 2007 kwenye uwanja huo huo, wakati wa mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kati ya timu ya Taifa 'Taifa Stars' na Msumbiji, ambapo kiasi cha Sh 605,020,000 kilipatikana kati ya Sh 644,530,000 zilizotarajiwa kupatikana.

Kulikuwa na upungufu wa Sh 39,510,000 uliotokana na viti 1,612 ambavyo tiketi zake zilidaiwa hazikuuzwa. Kiingilio kilikuwa Sh 50,000, Sh 40,000, Sh 30,000 Sh 20,000, Sh 10,000 na Sh 3,000.

Mwandishi Wetu anaripoti kuwa, baadhi ya mashabiki wa soka wamelalamikia viingilio hivyo na kusema ni vya juu zaidi na havilingani na maisha ya Watanzania wa kawaida.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya mashabiki hao walidai kuwa walitarajia viingilio vingepanda kwa kima cha chini ambacho mara nyingi huwa kati ya Sh 3,000 na Sh 5,000 kingekuwa Sh 10,000 ama Sh 12,000, lakini kiingilio cha Sh 30,000 ni kuwaumiza Watanzania wa kawaida.

"Hapana hii ni kutaka tusiende kuona mechi, sawa tutaangalia kwenye televisheni," alisema Sadiki Shaaban aliyejitambulisha ni mfanyabiashara ndogo.

Kauli kama hizo pia zilizungumzwa kwa nyakati tofauti na mashabiki Mussa Juma, Idd Nassor na John Emmanuel waliosema TFF inapaswa kuangalia upya viingilio hivyo na kwamba vimewekwa kwa tamaa.

Wakati huo huo, mashabiki wa soka Tanzania hawatamuona kiungo nyota wa Brazil anayechezea Real Madrid, Ricardo Kaka akicheza kwenye mechi dhidi ya Taifa Stars kutokana na kuumia.

Taarifa zilizopatikana jana kwenye mtandao zilieleza kuwa Kaka hatacheza pia mechi kati ya Brazil na Zimbabwe itakayofanyika katikati ya wiki hii, ingawa haikufafanua ameumia nini.

Kutokana na kuumia huko, Kaka alishindwa kufanya mazoezi ya mwisho mwa wiki, huku ikielezwa atalazimika kupumzika kwa muda, ingawa anaweza kuwemo kwenye kikosi kitakachokuja nchini.

DONDOO ZA MAPATO STARS V BRAZIL

VIP A kwa Sh 200,000: Viti 748 zitapatikana Sh 149, 600,000 VIP B Sh 150,000: Viti 2,260 zitavunwa Sh 339,000,000 VIP C Sh 100,000: viti 2,404 , zitahifadhiwa Sh 240, 400,000.

Rangi ya Chungwa mkabala na VIP Sh 80,000: viti 6, 460 Sh 516, 800,000, Rangi ya chungwa nyuma ya magoli Sh 50,000 viti 7, 300 zitapatikana Sh 365, 000,000.

Rangi ya Bluu 30,000: viti 18, 364 zitapatikana Sh 550, 920, 000. Kijani Sh 30,000: viti 19,590 zitapatikana Sh 587,700,000.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
Back
Top Bottom