Wito: Gomeni kwenda kuangalia mechi ya Brazil na Taifa Stars!

Watz ni mapunda wana-ask for more MIZIGO..Gembe relax and chill dude, mabadiliko kwa kizazi hiki cha punda haiwezekaniki.

Kwenye red: 'Herds of sheep instead of humans' somebody said in these forums!

I cant agree the more! It's quite nauseating!
 
Watanzania wenzangu,

Siku zote nimekuwa nikiwahurumia sana kwa ajili ya matatizo yanayowakabili,ila hili la ujio wa timu ya Brazil nimelifurahia sababu ni moja ya michezo ambayo mnaipenda

Kwa kuwa tumesikia na kuona na nimeukuu hapa chini basi nawasihi sana mgome kwenda kuwatazama Brazil na njia sahihi ni kutazamana kupitia TV zenu huku mkiburudika na ulanzi au coca cola

Sababu za kugomea mechi hizo ni hizi hapa


2.Hii wizara imekaa na kuamua kutoa Dola billioni sita,Hii pesa imetoka kwenye bajeti ipi?

3.Gharama hizi ni za juu sana na tunaomba kupatiwa mchakato mzima wa jinsi ya makubaliano yalivyofanyika


4.Sulivan Summit ilifanyika hapa ,Wor;d Economic Forum pia.Je ni faida gani tumepata kutokana na Mikutano hiyo?Je na huu utalipatia faida taifa kiasi gani?au ni kutafuta Sifa tu zisizo na tija?

.

Baba hebu tujuze ni wapi hizi habari ziliko (serikali ilikuwa na budget ya $6m?)

Hii ni kuwakashifu wafanyakazi wote wa Tanzania walioambiwa kuwa serikali haina pesa za kuwalipa. Hii ni kashifa na kuwatukana mama na dada zetu wanaolala watano kwenye hospitali zetu wakiwa wametoka kujifungua, haya ni matusi ya nguoni.

Tusiishie kugomea mchezo tu bali tusiwachague ifikapo tarehe 31 Oct 2010 kwa kututukania wazazi na ndugu zetu, au haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania??
 
Every country got bunch of black sheep, Tanzania are blessed with flock and flocks of black sheep.......!
 
tusilalamike sana jamani bora hzo fedha zimetumika na tuione brazil hapo uwanjani maana hata wasingelipwa unafikiri hzo ela zingetumia kwa manufaa ya taifa? zingepgwa tu kama zileee za kipindi kileeeee cha kina waleeee!!! kwa hyo mimi naona bomba kabisa hata kama hawaitangazi nchi!! wacha wakale huko brazil waruke ruke huko ground na kichwa cha wendawazimu
 
Sina uhakika sana ni kwa kiasi gani watanzania watakubaliana na wito huu wa kugoma kwenda kutazama mechi katika hatua hii.

Kwa upande mwingine, labda wachezaji wa timu yetu ya taifa watapata fursa ya kujinoa na kujiuza katika ngazi za kimataifa.
 
Kwa ufahamisho tu Manji wa Yanga amejitolea kuwalipia kila mwanachama wake akayehudhuria mkutano ulioititishwa tiketi za Tshs 30,000/- kuingilia na usafiri, je mpo ? Sasa hapa mswahili gani aliyezoea vya bwerere atagoma ? Wanachosahau ni kuwa hizo hela zimetokana na kodi zao zinazoliwa na hawa maharamia. Lazima tukubali kuwa wajinga ndio waliwao na watanzania hapa tumetia fora - hebi tazama huyu moja wao !!

Sina uhakika sana ni kwa kiasi gani watanzania watakubaliana na wito huu wa kugoma kwenda kutazama mechi katika hatua hii. Kwa upande mwingine, labda wachezaji wa timu yetu ya taifa watapata fursa ya kujinoa na kujiuza katika ngazi za kimataifa.

Yaani mtu unaweza kulia kwani huyu Kakuye eti ndio hao tunawaomba kugoma - watu wananenepa kwa makombo wanayotupiwa wakiwa chini ya meza huku the Manjis wako meza kuu, inasikitisha.
 
Mkuu Gembe you truly have a patriotic agenda lakini tatizo ni kubwa kuliko hata hili suala la appearance fee ya Brazil, Ni kubwa kuliko uwezo wa kufikiri wa watanzania wengi wakiwemo hata viongozi. Nchi yetu inaendeshwa na mfumo wa kifisadi, mfumo ambao Hospitali Mwananyamala hakuna vitanda, dawa wala enough qualified staff lakini just some 2.5km away gavana wa benki wa hako kanchi masikini kabisa anakaa kwenye nyumba tunayoambiwa ni $1.2 mn.

Mfumo ambao afisa wa serikali anatumia gari ya Tshs 150 million ofisini kwake hakuna computer. Mfumo ambao wizi ni sehemu ya maisha just like that old joke "Did u know that all the people in the world are thieves and liars and those who are not are fools" Mfumo ambao wala rushwa, wezi, wauza madawa ndiyo role models kwenye jamii. Mfumo ambao..........just pathetic. The list goes on and on and on!!!!!!!!!!!!

Hivyo basi mimi hii ishu ya Brazili is just another evidence in the statistics that our govt and its officials are out of touch!
 
..Kuna taarifa kuwa asilimia kubwa ya Ticket zimekwisha nunuliwa na makampuni ya SBL na Vodacom! Hapa TFF wamewashika watanzania pabaya, lazima watu wataenda tu. Ni life time opportunity!! No way, anayetaka kugoma agome!! By the way, nafasi katika uwanja ule zipo 60,000 tu. Hata wangeweka elfu moja moja, wengine wasingeona!!
 
Nimeuliza mahali humu humu jamvini. Kwanini ilikuwa kimya kimya hadi majuzi tu ndipo watu wajue ujio wa Brazil? Kama si dili nini? Kuna tafauti gani na ununuzi wa rada on commission basis!!!
 
Every country got bunch of black sheep, Tanzania are blessed with flock and flocks of black sheep.......!

masa, watanzania ni kama wale wanyama nyumbu wanaomigrate kwa maelfu, wakati wa kuvuka mto wanaona mamba anawachukuwa, pamoja na wingi wao na silaha za asili pembe, badala ya kupambana na mamba wao wanavuka wanajiona wajanja wakifanikiwa kuvuka mto. Wakati nyumbu wengine wengi wanakuwa wamekufa in the process na wangetafakari na kushauriana ni nyumbu wachache sana wangekufa.

Kondoo ni mtiifu na ana akili lakini kuuwawa ni nadra, nyumbu ni wengi kuliko predetors wao, wana nguvu na silaha ila hawana akili na wanauwawa sana. Na watanzania ni vivi hivi.
 
Gembe ni kweli kabisa hakuna sababu ya watu kwenda mpirani kwani kuna shida ngapi ambazo serikali inadai haiwezi kuzitatua kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha na shida hizo zipo miaka nenda rudi,sasa huu ujio wa Brazil billioni 3 zimepatikana ndani ya wiki moja! Kwa kugomea mechi hii sisi wananchi tutaonyesha kupinga serekali kwa matumizi yasiyo ya lazima yanayo maliza pesa ambazo zingeelekezwa kwenye sehemu muhimu.

Wazazi wanalala chini hakuna vitanda,wanafunzi wetu wanakaa chini hamna madawati, wanafuzi wa vyuo vikuu wanaburuzana na bodi ya mikopo kwa madai kuwa pesa hamana sasa hii fahari ya kuagiza Brazil tunapata wapi nguvu ya kufanya hivyo? Hizo billioni 3 zingenunua vitanda vingapi au madawati managapi kwa faida ya watu wetu?

Kwa nini kulikuwa na usiri wa hali ya juu kiasi hiki kulikuwa na nini nyuma ya huo usiri jamani, unajua kwenye exitement na ubishi kama sasa people never reason. Tuulize pia na gharama halisi za kuileta timu hapa Tanzania.
 
Watanzania wenzangu,

Siku zote nimekuwa nikiwahurumia sana kwa ajili ya matatizo yanayowakabili,ila hili la ujio wa timu ya Brazil nimelifurahia sababu ni moja ya michezo ambayo mnaipenda

Kwa kuwa tumesikia na kuona na nimeukuu hapa chini basi nawasihi sana mgome kwenda kuwatazama Brazil na njia sahihi ni kutazamana kupitia TV zenu huku mkiburudika na ulanzi au coca cola

Sababu za kugomea mechi hizo ni hizi hapa

1.Mpira wa miguu haujawahi kuwa anasa kiasi cha watu kulipa dola 25.(TSH 30,000)kuangalia mechi moja katika nchi iliyo na huduma mbovu za kijamii,maisha duni kwa kila mtannzania.

2.Hii wizara imekaa na kuamua kutoa Dola milioni sita,Hii pesa imetoka kwenye bajeti ipi?

3.Gharama hizi ni za juu sana na tunaomba kupatiwa mchakato mzima wa jinsi ya makubaliano yalivyofanyika

4.Sulivan Summit ilifanyika hapa ,Wor;d Economic Forum pia.Je ni faida gani tumepata kutokana na Mikutano hiyo?Je na huu utalipatia faida taifa kiasi gani?au ni kutafuta Sifa tu zisizo na tija?

Baada ya kutoa sababu hizo hapo juu naomba kuwauliza serikali.

1.Kama kuwaongezea walimu pesa kunahitajika pesa nyingi,kwanini wizara isikae na kutafuta pesa kwa ajili ya kuwaongezea mishahara?imeonekana wanaweza kukaa na kupata pesa.Ndiyo tupo tayari kukchangia hata kwa kwenda kuwaona Simba na Yanga ili mradi pesa iende kwenye Maendeleo

2.Nchi ambayo haina walimuwa kutosha,madawati ya kutosha na upungufu wa maji kwanini pesa kama hizi hata kama ni za kukopa zisielekezwe huko.

3.Hizo pesa mmezitoa kwenye Bajeti gani?nataka kupata jibu haraka iwezekanavyo ili nishauri nini cha kufanya.Haiwezekani pesa inachukuliwa chukuliwa ovyo ovyo kwa maamuzi ya wachache bila bunge kuidhinisha?

I don't buy this idea at all unless otherwise.Ila siwalazimishi kugoma kama Mnataka endeleeni tu kuunga mkono na mtakuwa mkifanya hivyo kuongeza kiwango ya umasikini mlionao..

hivi tenga kabla ya TFF alikuwa anafanya kazi wapi?i need to know sababu naona akili yake inakwenda tenge.

Nipo na wachungaji tunawaombea .


Asante sana kwa maneno yako mazuri sana ambayo nayaunga mkono kabisa. Mimi nadhani hela hii imetolewa na Serikali TFF haina uwezo wa kulipa hela hii, lakini kwa uamuzi wa kuilipa pesa hii nyingi unawatokea puani itabaki kuwa siri ni nani aliyeidhinisha malipo ya pesa hii nyingi na imetoka katika fungu lipi. Kwa kumbuka miaka ile ya nyuma ambapo mkuu wa nchi alitaka kuialika timu moja maarufu duniani na kuwalipa mapesa chungu nzima na pia kugharamia usafiri wao wa kuja na kurudi, basi naamini pesa hii mkuu wa nchi anahusika kwa karibu sana kutoa idhini ili ilipwe, lakini hila kamwe halitasemwa hadharani daima.
 
Ninachokielewa ni kuwa uwanja utajaa,mgomo ni batili kwa sababu wanaolipa hawalazimishwi.Wewe kama hutaki kaa nyumbani usiangalie hata kwenye tv.Huwezi kuwazuia watu wasiende kwenye mchezo wanaoupenda sana kama hela wanayo.
 
Mungu ni mkubwa!nilikuwa na hasira sana juu ya hii mechi ila naelekea kufarijika baada ya kupata hili wazo la kugoma na nimelipokea hata wengine wakienda ila mm nafsi yangu itaridhika,wajumbe naomba twende mbele zaidi ni kwanini tusiandaee maandamano ndani ya masaa 48?

Hapa la kutusaidia wale wote wenye uzoefu wa kuomba vibali vya maandamano watusaidie hatua za kupata kibali,haiwezekani hawa jamaa wakawa wanafanya mambo wanavyotaka na ss tunanyamaza kisa ooh tumaisha chelewa ,hata kama ila lazima wajue kuwa hii nchi si wajinga kama wanavyo fikiria.
 
Hayo mambo ya milioni sita dola,tartibu wakuu ccj wasije sikia.....Teh teh teh...!
 
Nitanunua popcorn za sh. 1000/= na juice ya 2000/=. Nadhani vinatosha kwa dakika 90 za mchezo wakati nikiangalia kupitia TV. Halafu ukiwa unaangalia kupitia TV unafaidi replay, wakati ukiwa uwanjani tukio likipita refarii hataweza kuamuru lirudiwe watu waburudike!
 
Hapa sasa naona tunavuka mpaka. Hii ni STAREHE kama zilivyo starehe zingine na ni Biashara. TFF wanawaleta Brazil, lakini ni lazima wabuni mbinu ya kupata fedha hizo kutoka kwa watazamaji wa mpira. Ni sawa na kuwaleta wanamuziki wenye majina makubwa. Wanaoingia mle hulipa fortune. Kwa hili niko na TFF 100%. Wanaoingia walipe gharama za kuwaleta na tax payer hatakuwa na mzigo wowote. Hizo gharama za kuwaleta inatakiwa zirudi through gate collections.

Jamani Tanzania imebadirika sana na wenye uwezo wapo!! Sasa kama wenye uwezo wapo, kwa nini biashara isifanyike? Tuwe progressive siyo cynical kila wakati na kwa kila kitu. Kuja kwa Brazil ni good news kwa wapenzi halisi wa SOKA hapa bongo hata hiyo laki mbili si issue. Ni wakati pekee wa kuona kitu halisi LIVE si live za kwenye TV.

Hongera TFF. Wale wasio na 30,000.00 poleni, lakini starehe si haki ya kila mtu. Starehe ni haki ya kila mwenye uwezo wa kuilipia!!
 
Nitanunua popcorn za sh. 1000/= na juice ya 2000/=. Nadhani vinatosha kwa dakika 90 za mchezo wakati nikiangalia kupitia TV. Halafu ukiwa unaangalia kupitia TV unafaidi replay, wakati ukiwa uwanjani tukio likipita refarii hataweza kuamuru lirudiwe watu waburudike!

Mi hata kwenye tv sitazami
 
Back
Top Bottom