With Zero investment, Rites gains TZS.177bn 'profits'

RITES hata wanasiasa wa upinzani wanaogopa kuinadi majukwaani sababu ina mkono wa mkubwa. Si ajabu kusikia waziri wa fedha anaibuka na kusema lazima RITES walipwe kwa gharama yoyote! I love Tanzania nchi ya aman (wajinga).
 
I support your statement 100%
Kweli kabisa huyu Werema ni wakili mkuu wa ccm sidhani kama anajua anachofanya!!!!anaenda kwenye nec kumtetea jk ,Tundu lisu amempa ukweli wake kuwa amekuwa mwanasiasa badala kuwa mtendaji na pia mvivu wa kusoma!!anajibu kwa jazba bila research
 
RITES hata wanasiasa wa upinzani wanaogopa kuinadi majukwaani sababu ina mkono wa mkubwa. Si ajabu kusikia waziri wa fedha anaibuka na kusema lazima RITES walipwe kwa gharama yoyote! I love Tanzania nchi ya aman (wajinga).

WACHA UONGO KIJANA AU NDIO UGENI WA JUKWAA MUWE MNASOMA BASI NA RECORD ZA NYUMA!
HII ILISHASEMWA SANA HUMU NA WATU WAMESEMA MUDA BADO TUSUBIRI SIKU YA SIKU WATU WATAJIVUA GAMBA MARA YA PILI.


Dk. Slaa apasua kombora la TRL

Na Mwandishi wetu

Asema Wahindi wa RITES ni geresha, wamiliki ni wazawa


Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema anafahamu kuwa wanaomiliki Kampuni ya Reli (TRL) ni watu waliokaribu na watawala na kwamba atawafichua.


Dk. Slaa alisema uswahiba uliopo kati ya wamiliki hao na viongozi wa ngazi ya juu serikalini, ni miongoni mwa sababu za kushindwa kuchukuliwa hatua, licha ya kampuni kusababisha hasara kwa taifa.


Alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu katika mji mdogo wa Sirari mkoani Mara.


Dk. Slaa alisema TRL haiwezi kuleta ufanisi kwa vile inaendeshwa na marafiki wa viongozi serikalini.


"Kuna siku tutaifumua TRL kwa kuwataja wamiliki wake kwa majina, kwa sababu tunawajua, sio Wahindi ni maswahiba wa JK ndio maana wanashindwa kuwachukulia hatua," alidai.


Kwa upande mwingine, polisi kanda maalum ya Tarime/Rorya iliweka nguvu kubwa ya ulinzi katika mikutano ya Dk. Slaa wilayani Tarime jana.


Wilaya hiyo ni miongoni mwa maeneo yanayotawaliwa na mapigano ya mara kwa mara, lakini ikiwa ni miongoni mwa ngome za Chadema.


Askari polisi waliovaa mavazi yenye mabomu ya machozi huku wakiwa na silaha za moto na vifaa maalum vya kujikinga dhidi ya mashambulizi, walifurika katika mikutano ya Dk. Slaa.


Hata hivyo, Dk Slaa hakufurahishwa na hali hiyo aliyoielezea kwamba, inafaa kutokea zaidi katika maeneo yenye vurugu na vita.


Askari hao zaidi ya 20 wakiwa katika mavazi na kubeba silaha hizo, walishiriki mikutano ya kampeni za Dk. Slaa iliyofanyika Nyamongo, Sirari na Tarime mjini.


Pia kulikuwa na gari linalomwaga maji ya kuwasha wakati wa kudhibiti vurugu.


Dk. Slaa alisema ingawa kazi ya polisi ni kulinda raia, lakini muonekano wao ulilenga kuwatisha wapiga kura.


"Hizi ni kampeni tu mnajikinga utadhani mko vitani, hivi hata Kikwete akija huwa mnavaa hivi, kwa mavazi haya inaonekana polisi ndio chanzo cha vurugu hapa Tarime," alisema Dk. Slaa.


Alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Nyamongo, karibu na mgodi wa dhahabu wa North Mara.


Dk. Slaa alisema hapakuwa na sababu za polisi kuvaa mavazi yenye kuwatisha wananchi waliokuwa wanashiriki kampeni zinazoendeshwa kwa amani.


Katika mkutano wa Sirari, idadi ya polisi iliongezeka, akiwemo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Sebastian Massawe.


Massawe alifika kwenye uwanja huo saa 6 mchana kwa gari lenye namba PT 2057 na kuonekana akitoa maelekezo ya mara kwa mara kwa askari walio chini yake.


Dk. Slaa alisema Chadema ikishinda katika Uchaguzi Mkuu, itauza ndege ya Rais ili kununua helkopa inayofika maeneo mengi ikiwemo vijijini.


"Tukiingia Ikulu, ndege ya Rais tunaiuza na kununua helikopta, kwa sababu helikopta inatua kila kijiji," alisema.


Mgombea ubunge wa Tarime kupitia Chadema, Mwita Mwikabe, alisema akipata ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo, atashughulikia kero zinazosababishwa na mgodi wa North Mara.


Alisema miongoni mwa kazi atakayoifanya dhidi ya kero hizo kuwa ni kumfungulia kesi mwekezaji wa mgodi huo katika mahakama ya kimataifa, kwa kushindwa kudhibiti maji yenye sumu.


Tendwa akemea siasa chafu


Mkoani Mbeya, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, amebeza kampeni chafu zinazohusisha mambo binafsi katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.


Miongoni mwa mambo hayo ni tuhuma dhidi ya Dk. Slaa, kumtambulisha mchumba anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya, Tendwa alisema suala la mchumba wa Dk. Slaa kudaiwa kuwa ni mke wa mtu, halina msingi wowote kisiasa.


"Ni suala lenye mguso wa aibu kuwekeana mambo yenu ya ndani hadharani, kwangu kisheria halipo, uhuru wa kuoa upo kwa kila mtu na ni sawa, lakini pia kuna uhuru wa kuheshimiana ambao ni wa kikatiba," alisema.


Kauli hiyo ya Tendwa imekuja muda ambao tayari Dk. Slaa amefunguliwa kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania na kudaiwa fidia ya Sh bilioni moja.


Alisema hakuna sheria inayomruhusu kuingilia kati suala hilo, hivyo anachosubiri ni kesi hiyo kumalizwa na mahakama kama ilivyofunguliwa na mlalamikaji.


"Tungoje wamalizane wenyewe huko mahakamani, mimi wala Nec (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) hatuna sheria juu ya suala hilo," alisema.


Kuhusu wagombea wanaokabiliwa na kesi mahakamani, Tendwa alisema ni jukumu lao kupima jinsi ‘walivyochafuka' na kuona kama wanafaa kuomba uongozi kwa jamii.


Miongoni mwa wagombea ubunge wenye kesi mahakamani ni pamoja na Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), Basil Mramba (Rombo) wote kupitia CCM na George Mtasha (Lupa) wa Chadema.


Chenge anakabiliwa na kesi ya kuendesha gari kwa uzembe na kugonga bajaj na kusababisha vifo vya wanawake wawili.


Mramba anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 11 na Mtesha anahusishwa na kesi ya kukutwa mguu wa binadamu nyumbani kwake.


Tendwa alisema kesi hizo haziihusu ofisi yake wala Nec, hali ambayo haiwezi kuwaondolea wahusika sifa za kugombea.


Hata hivyo, alisema ulikuwa wajibu wa vyama vya siasa kuwaangalia wagombea hao kama wana sifa za kimaadili, kabla ya kuwasimamisha kugombea.


Alisema wagombea wenye kesi pia walipaswa kujipima kama wamechafuka machoni mwa jamii, kabla ya kuchukua uamuzi wa kusimama jukwaani kuomba kura.


"Ikiwa vyama vyao vinawaona hawana matatizo ya kimaadili, hilo sisi halituhusu, lakini hata mgombea mwenyewe anaweza kujipima kama hajachafuka, maana udhaifu huo unaweza kutumiwa na wapinzani wake kummaliza," alisema.


CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom