Wireless Router inaweza kuchangiwa?

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,781
2,301
Ndugu wana JF kama ninatumia wireless rooter kwa mtandao X ninaweza kuhama nayo mtandao Y? Na kanuni hiyo inapply kwa decoder? Natumai wataalam mtanijuza kwenye ICT nipo ovyo ovyo
 
Last edited:
Ndugu wana JF kama ninatumia wireless rooter kwa mtandao X ninaweza kuhama nayo mtandao Y? Na kanuni hiyo inapply kwa decoder? Natumai wataalam mtanijuza kwenye ICT nipo ovyo ovyo

Tunaongelea decoder au wireless router?! Upande wangu naona swali lako kama limevurugika hivi, naomba ulinakshi kama waweza ili liweze kujibika kirahisi. Shukrani.
 
unatumia wireless router kwa mtandao x,unaweza kuhama nayo mtandao y? hapa lugha umetuchanganya itabidi ufafanue
 
Provider wangu voda( huu ni mfano) wakati wananiwekea mtandao walinipa na wireless rooter for free, sasa nafikiria kuhamia tigo, je itafanya kazi?
The same supplier pia walinipa na decoder kwa ajili ya TV channels, ninataka kuhama nayo kwenye labda DSTV (mf pia). Je inawezekana?
 
kuna wireless zingine huwa locked to a certain provider kwa hiyo itabidi uchunguze,yangu is locked and hence if i change providers itabidi nitafute router ingine
 
kuna wireless zingine huwa locked to a certain provider kwa hiyo itabidi uchunguze,yangu is locked and hence if i change providers itabidi nitafute router ingine
Na hiyo decoder mkuu au na yenyewe ni kihama ndio mwisho? Ninachunguza nini kwenye rooter?
 
Router haiko locked unaweza kutumia kokote.

Decoder ziko made specifically kwa ajili ya kampuni fulani, haita fanya kazi na kampuni yoyote nyingine.
 
Router haiko locked unaweza kutumia kokote.

Decoder ziko made specifically kwa ajili ya kampuni fulani, haita fanya kazi na kampuni yoyote nyingine.
mimi nina BT VOYAGER 210 adsl wireless router locked to british telecommunications
 
mimi nina BT VOYAGER 210 adsl wireless router locked to british telecommunications
Nadhani kama una Adsl Wireless Router inaweza ikawa locked ile Modem ya Adsl ndo inakuwa locked, kama una stand alone Wireless Router sidhani kama inaweza kuwa locked.

Mwanzisha mada tupe Model namba tujue kinachoendelea.
 
Ongeleeni na modem nayo vipi inaweza kutumika popote?
 
Ongeleeni na modem nayo vipi inaweza kutumika popote?

Modem

  1. Inabidi iwe the right technology, i.e Modem ya CDMA haitafanya kazi kamwe kwenye network ya Hspda etc.Hakuna njia ya kubadilisha technolojia ya modem.
  2. Inabidi iwe unlocked, kama modem iko locked kwa provider mmoja haita fanya kazi kwa provider mwengine. Mara nyingi locked modem inaweza kuwa unlocked by wataalamu.
 
Router haiwezi kuwa locked na unaweza kuhamanayo kutoka provider mmoja kwenda mwingine. Kitu cha kufainya inabidi uireset then unaweka configaration za provider mwingine.
 
Ikiwa free to any network....utaweza ila kama locked...balaa unalo hilo
 
Nadhani kama una Adsl Wireless Router inaweza ikawa locked ile Modem ya Adsl ndo inakuwa locked, kama una stand alone Wireless Router sidhani kama inaweza kuwa locked.

Mwanzisha mada tupe Model namba tujue kinachoendelea.
Na hii technilojia ya wireless na router kwa Tanzania ipo accessible. Maana najua zinatumika cable hapa nilipo. Je kuna njia nyingine ambayo Tz inatumika majumbani????
 
Na hii technilojia ya wireless na router kwa Tanzania ipo accessible. Maana najua zinatumika cable hapa nilipo. Je kuna njia nyingine ambayo Tz inatumika majumbani????

Inategemea hiyo router inapokea cable ya aina gani I guess, na service provider wako wa bongo anakupa vipi mtandao.

Kama utataka kutumia Voda/Zain/Zantel/Tigo etc router nadhani ni useless au sijui utaichomeka vipi.

Kama utatumia hawa Raha au SimbaNet basi inawezekana router hiyo ikatumika (maybe) hasa kama inaweza kupokea Ethernet cable za kawaida kama source ya internet.

Kwa kifupi kila kitu kinategemea.
 
Back
Top Bottom