Wingu laigubika Ripoti ya Ngwilizi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
HABARI

makinda.png


Spika wa Bunge, Anne Makinda



Posted Monday, October 29 2012 at 21:37

IN SUMMARY

"Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo katika vyombo vya habari ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 31 (1) (g) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura 296," alisema Ndugai katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni.



Waandishi Wetu, Dodoma
WAKATI Bunge likianza mkutano wake wa Tisa leo, zipo taarifa Ripoti ya Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa haitasomwa na kisha kujadiliwa.

Badala yake, kwa mujibu wa watoa habari wetu, Kamati ya Uongozi, iliyokutana jana iliamua kwamba litatolewa tamko kuhusu ripoti ya kamati hiyo, hivyo haitasomwa wala kujadiliwa kama ambavyo wabunge wamekuwa wakitaka.

Kwa maana hiyo Spika wa Bunge, Anne Makinda huenda akatumia kanuni nyingine kutoa tamko kuhusu uchunguzi huo, hali ambayo haitatoa fursa kwa wabunge kuijadili kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakishinikiza.

Miongoni mwa kanuni ambazo Spika anaweza kuzitumia ni pamoja na ile ya 33 (2) ambayo inasema: "Wakati wa kikao, Spika anaweza kutoa taarifa nyinginezo kadri atakavyoona inafaa."

Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel jana alikataa kuzungumzia suala hilo akiahidi kulitoa ufafanuzi leo... "Ratiba ya shughuli za Bunge bado iko kwenye ngazi ya Kamati ya Uongozi. Sasa pengine tusubiri kesho (leo) ikiwa tayari kila kitu kitakuwa wazi, hakuna haja ya kuwa na haraka."

Jana, Kamati ya Uongozi wa Bunge ilikutana mjini Dodoma kujadili mambo mbalimbali na habari zinasema kwamba suala la Ripoti hiyo ya Ngwilizi, pia lilijadiliwa.
Agosti 2 mwaka huu, Spika Makinda aliunda kamati hiyo ndogo kuchunguza tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya wabunge ambao walidaiwa kwamba walihongwa ili kuikwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kuundwa kwa kamati hiyo, kulitanguliwa na tukio la kuvunjwa kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Julai 28, mwaka huu pia kutokana na tuhuma hizohizo.
Tayari kumekuwa na taarifa kwamba ripoti hiyo imevuja na maudhui yake kuchapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari, hali ambayo ilisababisha Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuonya kwamba waliohusika na kuvuja huko huenda wakajikuta matatani kwani ni kosa la kisheria.

"Kitendo cha kuchambua na kuchapisha maudhui ya taarifa hiyo katika vyombo vya habari ni kinyume cha sheria na kinaingilia uhuru, haki na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 31 (1) (g) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura 296," alisema Ndugai katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni.

Mmoja wa wabunge ndani ya kamati iliyochunguza suala hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa), ndiye anayedaiwa kwamba aliivujisha ripoti hiyo ya uchunguzi kwa makusudi, lengo likiwa ni kumshinikiza Spika Makinda aitoe hadharani ili kuwasafisha watuhumiwa.

Mbunge huyo alifanya hivyo kwa msukumo wa baadhi ya wabunge waliotuhumiwa kujihusisha na rushwa, pamoja na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kabla ya kuvunjwa.

Kadhalika, Ndugai katika mkutano wake na vyombo vya habari alisema suala la ripoti hiyo kusomwa bungeni au vinginevyo linategemea uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge.

Ndugai alisema baada ya kamati kuwasilisha ripoti kwa Spika, Kamati ya Uongozi ya Bunge itakaa kujadili na kama itaona kuna umuhimu wa kuingizwa katika ratiba ya vikao vya Bunge ijadiliwe.

Alisema Vifungu 114 (17) na 119 (1) hadi (6) vya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007 kwa pamoja vinampa madaraka Spika kuhusu utaratibu wa kufuata katika uwasilishaji wa taarifa bungeni.

Kamati hiyo iliyoundwa na Spika ilikuwa chini ya Ngwilizi ambaye ni Mbunge wa Mlalo, ina wajumbe; Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki), Goesbert Blandes (Karagwe) na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Omary Juma. Kamati hiyo ilimaliza kazi yake na kuiwasilisha kwa spika tangu Septemba 20 mwaka huu.

Kamati za vyama

Kamati za vyama bungeni zinatarajiwa kufanya vikao vyake leo asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja alisema

Kamati nyingine za Bunge hazijakutana kutokana na wabunge wengi kuwa safarini kwenda mjini Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge.

"Kwa taarifa tulizopokea sasa ni kwamba kamati zimeshindwa kukutana kutokana na wabunge wengi kuwa njiani kuja mjini hapa, hivyo kwa vyovyote kesho (leo) Bunge litakuwa ni fupi ili wabunge wapate nafasi ya kuandaa utaratibu mzima wa ratiba za vikao," alisema Minja.

Alisema leo mara baada ya kuanza kwa kikao hicho, Bunge litatoa nafasi ya maswali na majibu ambayo Serikali itayajibu kabla ya kuahirishwa.

Mara baada ya kuahirishwa saa nne asubuhi, kamati za vyama zitakutana kupitia mambo mbalimbali kabla ya kuingizwa kwenye kamati mbalimbali za bunge.

Moja ya mambo yanayotarajiwa kutawala katika kamati za vyama ni pamoja na wabunge wa CCM kujiweka sawa kwa ajili ya kusaidia kupitishwa kwa ripoti ya Kamati ya Ngwilizi.

Kingine kitakachojadiliwa katika Mkutano huu wa Bunge ni muswada binafsi kuhusu fao la kujitoa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tayari Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika wamewasilisha miswada yao kwa Katibu wa Bunge, Tomas Kashillilah.









 
Tatizo ni kuwapa mafisadi jukumu la kuwachunguza mafisadi,wapi na wapi?Tume pesa watu wamelipwa na walijuwa habari ikiwa leaked basi haitasomwa,yote usanii tu kwasababu pengine ripoti yenyewe ni ya kisanii.Bongo bana!
 
wabunge wako njiani? wabunge si walikua wanajua bunge linaanza leo sasa kwanini hawakusafiri siku mbili au zaidi kabla...yaani shuhuli za bunge zisimame kwa sababu wabunge wamechelewa kufika....
 
Hatuna muda mchafu wa kujadili mambo ya kipuuzi, wangetaka hata kuchapisha ripoti nzima tena kwenye gazeti la Uwazi na Ijumaa mi sioni shida, shida yangu na hamu yangu ni kuona fao la kujitoa linajadiliwa na linapewa ufumbuzi kabla hamjatoa ma..lio yenu bungeni
 
Fao la kujitoa limenifanya nipunguwe uzito nahisi hata akili yangu imesinyaa wakifanya tofauti na matalajio ya wengi lazima pachimbike
 
Back
Top Bottom