Windows 8 ipo jikoni, je utaijaribu?

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Kwa siku kadhaa, nimetembelea kwenye blogu, tovuti na forums mbalimbaliza IT, majadiliano makubwa huko ni kuhusu ujio wa Windows mpya, kila mmoja akiongea kwa maono yake na wengine wakicharuana kama ilivyo ada ili hari mambo yanaenda na wataalam wanapata kitu cha kuwekea maoni.
Mara ya mwisho Microsoft kutoa mtambo endeshi mpya(Operating System) ilikuwa ni Januari 2009, mtambo ambao ulipata mapokezi makubwa toka kwa watumiaji wa kompyuta duniani kote, kitu kilichowafanya kufanikiwa kuuza nakala zaidi ya milioni tatu.
win8-main.jpg


Windows 8 ndio hiyo imepiga hodi, na Microsoft tayari wameshaiweka hewani kwa ajili ya majaribio. Kipya zaidi ni kuwa Microsoft safari hii ametambua mchango wa wataalamu nje ya kampuni yao hivyo kutaka kuwashirikisha zaidi. Zaidi zaidi ni kitendo cha Microsoft kuwapa nafasi madeveloper kushiriki kikamilifu kutengeneza applications zitakzotumika kwenye Windows 8, yaani ndani ya Windows 8 mambo yatakuwa kama vile Apple.

Je baada ya kusikia hayo umevutiwa na unataka kuijaribu Windows 8? Windows 8 kwa sasa inapatikana kwa majaribio, nenda kwenye ukurasa wa kudownload wa microsoft na ujipatie nakala yako.

Sasa nina swali dogo, je utaijaribu Windows 8?

Chanzo: Ughaibuni.com
 
Back
Top Bottom