Wimbo Wa Taifa La Zanzibar Kupigwa Baraza La Wawakilishi

Yale mauaji ya 64 ndio yalioleta Jamhuri
mauaji yapo TARIME na yale ya maalbino huko Tananyika.

Tunajua mbaya wetu ni nani anaeutufarakanisha na kutugombanisha. lakini naamini tukipata uhuru wetu yote yatabaki story
 
Wimbo huo utaimbwa hapo nje ya jengo la kusanyiko la genge pekee . Wimbo hauwezi kuvuka mipaka . Mkuu wa Mkoa ambaye ni Rais huko hawezi kuibiwa wimbo huo .Hata Passport ambacho kitu muhimu , pesa na jeshi .Kweli mko gizani nyie . Poleni sana . Endeleeni kuimba .

Nitawaona kama Nchi mkianza na pesa yenu, Passport yenu, Jeshi la polisi lenu, Amiri Jeshi mkuu wenu , nk
Duh! hapa umeamua kuwa-provoke wazenj why?..Zanzibar ni nchi iliyoungana na nchi inayoitwa Tanganyika kwa mambo maalum ikiwemo uliyoyataja kwa faida ya nchi hizi mbili .. ..
 
Kuwa na wimbo hakumaanishi kwamba mnakua taifa, hata shuleni tulikua tuna wimbo wa shule lakini umuhimu wa nyimbo zile ulikua unaishia palepale shuleni, hata tulipokua tukienda Umiseta tukua hatuwezi kuimba wimbo wa shule yetu.

Wimbo huu wa Zanziba ni kichekesho tu na ni sawa tu na wimbo wa shule maana hauwezi kuvuka mipaka ya Zanzibar. Kama kweli una maana wautumie wanapokwenda nje ya nchi ili tujue kua una maana, Otherwise ni sawa na wimbo wa shule tu...tena shule ya chekechea.

Acheni kushangilia wimbo wa chekechea

Wimbo wa Taifa unanguvu sana katika progress ya Freedom. Ukiangalia US history, utagundua kwamba vitu vidogo vidogo tu vilisababisha Freedom. Pamoja na kupigwa mabomu na Waingereza Scott Francis Key, alipoona bendera ya USA bado inapepea akaanza kuimba wimbo wa Star Spangled Banner; ambao baadaye ulikuwa USA National Anthem. Nikiangalia history zilizopita, na vitu ambavyo ZNZ wanapogress ktk Freedom; kuna dalili za ZNZ ikapata Freedom ya nchi kamili ktk muda si mrefu.
 
Zanzibar wana wimbo wa Taifa wa chekechea kAMA MNAVYOSEMA. Kwani jee Tanganyika wanao wao? Tatizo lenu nyinyi- Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnaifanya kama Tanganyika. Poleni sana. Busara ni kwa Wadanganyika kutafuta wimbo wa kwenu japo wa chekechea. Wenzenu wako hatua mbili mbele . Hamuoni nyinyi?
 
RE MUUNGANO BANDIA USIOKUA NA KICHWA WALA MIGUU.
Na mimi hapa nitawaeleza ukweli ndugu zangu Watanganyika hili zogo la Muungano linatusaidia nini sisi watu wa Tanganyika , hakuna isipokua record mbaya za zanzibar zinatuharibia jina la Tanzania nzima kwa vurugu za siasa za CCM na CUF zisizokisha , kwani bora Zanzibar wawe kivyao na sisi kivyetu , si tutakua majirani kama ilivyo Kenya , Rwanda au Burndi kuna uabaya gani.
Ukweli ni kuwa hakuna muungano kwani hakuna record yoyote kuwa Baraza la Wawakilishi lilikaa na kupitisha uamuzi wa kuwa muungano huu ndio ukweli na ndio ukakuta mpaka leo hii serikali inaficha mkataba wa Muungano kwani ki ukweli haupo ni muungano Bandia ambao haupo kisheria .
Na wazanzibari hata hao waliodanganywa kuwa watapewa vyeo ili kuwe na Muungano hawo wanamapinduzi wa Zanzibar hawautaki tena muungano.
Utaona 1984 Zanzibar imeunda Baraza lake la Wawakilishi,
Imetoa Bendera ya Rais
Bendera ya nchi
Wimbo wa Taifa
Zanzibar National ID card
Na sasa Wazanzibari wanataka uanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki
Pia wanataka mambo mengi yanayoitwa ya Muungano yatolewe wazanzibari wote wa CCM na CUF wako msimamo mmoja kwa hili.
Wazanzibari tayari wanaandaa sera ya mafuta . sera ya mambo ya nje na pia nasikia kuna mazungumzo ya Zanzibar kuwa na jeshi lake la Polisi ambalo halihusiani na la Tanzania, sera yake ya fedha kuwa na Benki kuu yake yote haya tayari nasikia yako kwenye mazungumzo baina ya CCM na CUF Zanzibar.
Haya ndio mambo yaliomfanya Njelu Kasaka na Malecela wajaribu kuirudisha serikali ya Tanganyika kwa kukuchoka na adha hizi na majigambo ya Wazanzibari inabidi Watanzania wa upande wa bara tujiulize tunanufaika nini kwenye muungano huu ?
Jee una umuhimu wa kuendelea au kugawana mbao kila mtu kivyake vyake ?
Tunawaona Wazanzibari wanavyonufaika na uchumi wa bara jee sisi tunapata nini
 
Msitoane macho......someni katiba....

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar
, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge: Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar
katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
 
Wimbo huo utaimbwa hapo nje ya jengo la kusanyiko la genge pekee . Wimbo hauwezi kuvuka mipaka . Mkuu wa Mkoa ambaye ni Rais huko hawezi kuibiwa wimbo huo .Hata Passport ambacho kitu muhimu , pesa na jeshi .Kweli mko gizani nyie . Poleni sana . Endeleeni kuimba .

Nitawaona kama Nchi mkianza na pesa yenu, Passport yenu, Jeshi la polisi lenu, Amiri Jeshi mkuu wenu , nk

yasungura aliyezikosa zabibu hayo ,jungu ndio linachemka hilo
 
I have a dream. A dream that one day the Tanzania union will be broken. That Tanganyika will come again and that Zanzibar will be fully autonomous. I have a dream. That a discussion will be conducted and then a new Union will be made, which will be transparent to both sides and will be formed on acceptance by both parties. That someone from Karagwe will be proud to be associated with Zanzibera and Someone from Chakechake will feel he belongs to Rombo. I have a dream. Then Tanzania will be able to convince other African states to form proper African Union. I have a dream.
 
si ndoto tena...sasa kweli.
Msitoane macho......someni katiba....

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge: Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
Ww bado unaishi karne ya 20, hii katiba ya TANU ya 1977,Zanzibar hatuitumii hata kumuapisha mjumbe wa nyumba kumi, ww baki nayo...sisi wenzako Mungu ametubarikia....sote tunashangiria....
Siwezi kuonea wivu watu walioamua kujifurahisha kwa kuimba nyimbo, Waache waimbe kama inawapa raha.
Mnaulizwa huo wenu nyinyi watanganyika upo wapi?
 
Back
Top Bottom