Wimbo wa Ney wa Mitego wapigwa 'ban'

Matukio Jamii

Member
Sep 9, 2015
12
8
Baraza la Sanaa nchini(BASATA) limeufungia wimbo wa Ney wa mitego unaoitwa 'shika adabu yako' kutokana na matumizi ya lugha chafu ndani ya wimbo huo. Akiongea leo na kituo maarufu cha redio, katibu mkuu mtendaji wa baraza hilo amesema ni wimbo ambao haufai na anashindwa kumpima Ney ana akili za namna gani.

"Kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”

Wimbo huo mpya kutoka kwa Ney wa Mitego ulisika Live kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL.

Katika wimbo huo uitwao 'Shika Adabu Yako', Ney amewaumbua kwa kuwataja majina wasanii na watu maarufu nchini akianika ubovu wa matendo yao na kuwataka wabadilike.

Pia katika wimbo amewaimba baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) kwa kuwaita ni msumeno usiokata na kazi yao ni kufungia nyimbo ilhali hawajui shida wanayopata na kama wangekuwa watoto angewachumia fimbo.

Pia hakumuacha nyuma Magufuli na serikali yake kwa kusema amezoea wasanii ndio watu wanapenda umaarufu lakini safari hii ligi ya umaarufu ipo kwenye serikali kwa kila kiongozi kuwa na mwandishi kisha kushindana magazetini.


===== Mashairi =====

Bongo Movie imekufa wamebaki kuuza sura
Wote wanataka kuimba ka Shilole na Snura
Ray Kigosi kawa mkongo hadi leo anaishi kwao
Hela za kuuza movie zote ananunua mkorogo
Kama ni umri umeshaenda, au bado anajiona dogo?

Kama ni vumbi litaruka na mikia watafyata
Hizi taarifa zangu na ziwafikie BASATA
Nyie ni kuku au bata? Msumeno usiokata
Kazi kufungia nyimbo, mnajua shida tunazopata?
Hamjui wajibu wenu, mngekuwa watoto nshawachapa

Na wasanii wadananda, ila Shetta kazidi
Huyo ndo baba Qaila (okay!)
Gari kapewa na Chief Kiumbe utasikia, “my new ride!”

Huyu jamaa anajiita Dimpoz, Poz kwa Poz
Wanae wanalalamika hawamjui shemeji
Kitaani kuna tetesi mwana hapigi mechi
Mara oh jogoo hawiki, huwa haonyeshi shemeji

DJ Choka daily bata, hivi hauna familia?
Nasikia hata nyumbani huna godoro la kulalia

Wema Sepetu una mimba kweli, au ndo kiki za msimu?
Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu
Na siku hazigandi tayari ushakuwa bibi
Na unakoelekea utatafuta kiki hadi kwa Fid
View attachment 322888
Baraza la Sanaa Tanzania halina masikhara, wimbo wa Shika Adamu Yako wa Ney wa Mitego umepigwa marufuku kama baraza hilo lilivyofanya kwa wimbo wa Viva Roma Viva wa msanii Roma Mkatoliki.
===============

PRESS RELEASE


BASATA YAUPIGA MARUFUKU WIMBO WA SHIKA ADABU YAKO WA MSANII NAY WA MITEGO

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Sambamba na kuufungia wimbo huo, BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yoyote na tabia ya kuutangaza wimbo au kuusemea katika vyombo vya habari vinginevyo hatua kali zaidi na za kisheria zitachukuliwa.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 4 (1) (j) cha sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepwa mamlaka ya kuratibu na kufuatilia mienendo ya mtu yeyote anayehusika na kazi za Sanaa na kuhakikisha linalinda maadili ya kitaifa miongoni mwa Wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya Sanaa.

Aidha, kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa Baraza nguvu ya kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha kufanya majukumu yake kwa faida na ustawi wataifa.

Baraza la Sanaa la Taifa limekuwa likipokea simu za maswali na malalamiko kadhaa kutoka kwa waandishi wa habari na wadau wa Sanaa ambao kwa njia moja ama nyingine wameguswa na kuchukizwa na kazi hiyo ambayo si tu inadhalilisha tasnia ya Sanaa bali inawafanya watu makini kuanza kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya Sanaa kwa ujumla.

BASATA mara kadhaa limekuwa likikemea na kuchukua hatua kadhaa dhidi ya tabia hii chafu ambayo ilianza kujitokeza kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa 2015. Kukemea huku ni kwa msingi mmoja kwamba asili ya tasnia hii ya Sanaa ni kuelimisha jamii, kukosoa pale kunapokuwa na tatizo, kuburudisha na kujenga jamii yenye staha, umoja wa kitaifa, mshikamano na amani.

Ni wazi wasanii wengi wanafanya kazi zao vizuri, kwa kubuni kazi zenye ubora, zenye kujenga jamii na zaidi zinazoburudisha rika zote kiasi cha kuzifanya zililetee heshima taifa. Kati ya hawa wengi, kuna wachache ambao wanaipaka matope tasnia ya Sanaa na kwa kiasi kikubwa wanaonesha wazi kutokuwa na nia njema.

Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia hawa ‘wasanii’ wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya Sanaa na wasanii genge la wahuni, wasio na staha, wa kudharaulika na waliojipanga kuibomoa jamii na kuharibu amani na utulivu uliopo nchini.

BASATA linapenda kueleza yafuatayo:

1. Vyombo vya habari viwe vya kwanza kuchuja maudhui ya kazi yoyote ya Sanaa kabla ya kuingia kwenye mtego wa kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii kupitia kucheza kazi chafu za Sanaa. BASATA lilishaziandikia radio zote kuzishauri kuwa na kamati za maudhui ya kazi za Sanaa lakini inashangaza baadhi ya vyombo vya habari vinakuwa vya kwanza kushabikia nyimbo hizo chafu na kuwapa muda mrefu wa mahojiano wasanii hao na baadaye kurudi BASATA kuhoji uhalali wa nyimbo husika. Hii si sawa hata kidogo.

2. Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imejipanga kuwajengea mazingira bora ya utendaji Wasanii wote nchini kupitia kuboresha miundombinu ya Sera, Sheria na Kanuni. Hata hivyo, uwepo wa Wasanii kama hawa unafanya jamii kuhoji hadhi ya wasanii, nafasi yao katika jamii na kwa maana hiyo kukatisha tamaa juhudi za kuipa msukumo sekta hii maana wadau wakuu ambao ni wasanii wanaanza kuoneasha kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii.

3. BASATA linawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za Sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao watazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowatukana na kuwadhalilisha, Waelewe kwamba Sanaa si uwanja wa kutusi na kudhalilisha watu hata kidogo. Ikitokea wale wanaotukanwa na kudhalilishwa kughafilika Sanaa itakuwa uwanja wa vita. Hili halikubaliki.

4. Tunafahamu kuna wasanii wamekuwa wakifanya hivyo makusudi kutafuta ‘umaarufu uchwara’ ambao wanadhani utakuja kutokana na kuzungumziwa sana. Tunapenda kusema wazi kwamba umaarufu hauji kwa upuuzi wa namna hiyo unakuja kwa msanii mwenyewe kujiheshimu, kujituma, kubuni kazi bora na zenye kulifahamu vema soko la ndani na la kimataifa.

SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI


Godfrey L. Mngereza

KATIBU MTENDAJI, BASATA
 
Siku izi mambo ni rahisi. nashangaa !!!hivi zile exile za zama zile ziliishia wapi
 
[QUOT E="UncleBen, post: 15294398, member: 255818"]Tuwekee basi hapa wengine hatujauskia[/QUOTE]
Sijui jinsi kuapload hapa mkuu...but ukicheki Utube utaupata mkuu
 
Ndo kazi BASATA wanayojua. kufungia tu.. Tatizo la taasisi za kitanzania ni kujali mambo madogo ya kipumbavu na kuacha kushughulikia issue nzito zenye maslahi kitaifa. Tuna safari ndefu bado
Wasanii wanapigana vijembe sasa BASATA wameona cha ajabu nini hapo? Lugha mbaya kusema demu ana tako balaa! Wana issue muhimu kufuatilia wanafumbia macho kazi yao kufungia nyimbo, hawajui wameenda na beat ya NEY 'kazi yao kufungia nyimbo' wakati ni wazi jamaa hakuwa na nia ya kutoa hii nyimbo ila walivyoanza ku mind waliopigwa madongo ndio kautoa.
 
Hata wafungie, haisaidii. Sisi wa uswahilini tushaupakua tangu jana, tunaupiga magetoni, na tunausikiliza kwenye masaloon. Na wenye magari weshaupakua sana tu. So watulie 'makavu' ya Ney yawaingie vizuriii.

Eti Ray Kigosi bado anaishi kwao, hela yote ananunulia mkorogo! hahahahaa
 
Back
Top Bottom