Wimbo huu unavuma sasa..................

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Nimekuwa nikisikiliza nyimbo mbalimbali za hapa nchini lakini kuna huu unanivutia zaidi!
Naaam unanivutia maana kila uchwao una kibwagizo kipya, wimbo huu sio kama BG za mchina ni zile origino. wanapenda kuuimba sana wabunge na zidi mawaziri wetu hughani kwa hisia na mashairi yenye kuleta hamasa. Naam wimbo mtamu ka nini.
Hebu nasi tuongeze mashairi yetu kwenye hiki kibwagizo!

Naanza
Mgao huu wa umeme utatufikisha wapi!
Tangu nizaliwe sikuwahi kuuona umeme,
Niliusikia tu huko mjini kuna umeme
Unazalishwa kwa maji hata sikuelewa nini maana ya umeme

Kuja mjini nikajua umeme,
Lakini umeme huu ni wa mgawo
Nilizoea mgawo wa unga wa yanga
na sasa hata mgao wa umeme

Nyimbo zingine ziliimbwa
Zikachuja zoote
Tulipoanza bongo fleva
Ikazaliwa richmond
bahati mbaya rich ikafa

Naskia alimrithi dowa wa nzi
huyu kataka tumlipe
wakubwa wamekaa nao hawasemi
Kiranja naye ananung'unika kwa nini walipwe
aseme tu kuwa hatulipi yaishe,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Mhhh..huo nao kweli ni wimbo..nachelea kusema kuwa unaweza usichuje...ukaimbwa daima, labda kama kutakuwa na UMMA wenye kuweza kutaka na kutenda ili wimbo uchuje...
 
Back
Top Bottom