Wimbi la wafanyabiashara ya vileo Z’bar kumwagiwa tindikali halivumiliki- Haki iko wapi?

Relief

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
254
47
KUNA kitu kinatokea Zanzibar ambacho kisipotafutiwa dawa kinaweza kuleta sura mbaya katika jamii ya Tanzania na ya kimataifa.

Pamoja na kuonekana kwamba Zanzibar kuna utulivu, kumekuwa kukizuka matukio ya kutisha yanayoashiria kutokuvumiliana katika nchi ambayo haina dini ila watu wake wana dini.

Matukio tunayoyazungumzia hapa ni ya kuvurugwa kwa biashara mbalimbali zinazohusu ama vileo au kumilikiwa na watu kutoka Bara ambapo ama wahusika huchomewa moto au kumwagiwa tindikali hata kufanyiwa madhila mengine yanayotangulizwa na onyo ‘usipoacha kitu hiki tutakuua'.

Tunafikiri kuwa intelijensia ya Polisi na vyombo vingine vya usalama inatosha kubaini watu wanaotishia na hata kutenda matendo maovu kwa binadamu mwingine kwa sababu tu anauza kileo au anatoka Bara.

Tumelazimika kusema hayo kutokana na taarifa tuliyoiandika katika gazeti hili, kuhusu Mtanzania mmoja na mkewe kuvamiwa, kumwagiwa tindikali na kupigwa risasi kwa kuwa wanauza pombe mjini Zanzibar.

Katika tukio hilo la kusikitisha mke wa Mtanzania huyo Bimal Alvind (36) alinusurika kupoteza ujauzito wake wa miezi minne baada ya kupigwa risasi tumboni.

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Mtanzania huyu ambaye anajipatia riziki yake kwa kufanya biashara halali iliyohalalishwa na Serikali kwa sasa hawezi kuifanya kwani yupo hospitali yeye na mkewe.

Huku mke akiwa amejeruhiwa mwilini kuanzia usoni kifuani kwenye matiti, mikono yote miwili na tumboni, mumewe Alvind Asawla (42) japo ametoka nje ya hospitali kwa sasa amepooza upande mmoja wa sura yake baada ya kupigwa risasi katikati ya macho na kutokea nyuma chini ya shingo.

Hili ni tukio la kwanza kubwa na baya kwa maisha ya binadamu lakini mwaka jana kulikuwa na matukio mengi ya kutishiwa vifo, kuchomewa vibanda vya biashara kwa sababu ambazo kuzieleza hapa ni kukosa mwelekeo unaolaani matukio kama hayo.

Pamoja na kulaani tukio hilo na matukio mengine yaliyowahi kutokea kitu ambacho kinatushangaza ni kuonekana kwamba kuna ukimya juu ya ufuatiliaji wa matukio hayo na hakuna aliyeshikwa hata kwa kusingiziwa kuhusika na matukio hayo.

Pamoja na kuonekana kwa macho, lakini taarifa za waathirika za kupewa onyo kabla ya kufanyiwa zinaonesha kwamba kuna kitu kinakosekana miongoni mwa idara ya intelijensia kuhusu makundi yanayoamua kuendesha Serikali zao na kuungwa mkono huenda hata na hao waliopo serikalini.

Si wakati wa kutajana, lakini wafanyabiashara wengi wa pombe Zanzibar wamekuwa wakilalamikia kufanyiwa vitendo vya kumwagiwa tindikali, kupigwa risasi na hata kuchomwa moto na hakuna kitu cha msingi kinachoonekana kufanywa na idara zinazohusika na usalama wa raia na mali zao.

Kama inaonekana Zanzibar si nchi ya vileo na ina taratibu zake inafaa kabisa kutangazwa hivyo na leseni zake zisitolewe, lakini kama leseni zinaendelea kutolewa vitendo hivi vya kunyimana riziki na kuharibiana afya havina budi kukomeshwa kwani kwa kisiwa kidogo kama Unguja haiwezekani kamwe isijulikane nani amefanya hivi.

Kama visiwa vya Zanzibar vinategemea utalii kwa kipato chake na kwa kuwa Zanzibar ni mji wa kitalii na wanakuja watu wa aina mbalimbali, inatakiwa kuwekwa wazi kama biashara hiyo ya kileo haitakiwi au wakorofi hao wadhibitiwe.

Kwa watu wenye akili na busara, matukio hayo yanaonekana kuwa salamu ambazo taasisi husika na usalama imeamua kuacha ama kwa manufaa yao au makundi fulani.

Kama Mtanzania huyu bado anakumbuka tukio la baba yake kumwagiwa tindikali wakati wa Jumatatu ya Pasaka ya mwaka 2007 na kufa baadaye na kutotiwa mbaroni mpaka leo kwa watu waliofanya kitendo hicho, ipo sababu ya kuwa na shaka na utendaji na watendaji wa idara zinazohusika katika ulinzi na usalama na tafsiri yake katika siku za usoni inaweza kuwa mbaya.

Tunaomba wahusika waeleze wananchi, hali halisi ya Zanzibar ili kila mmoja ajue anafanya nini kuhusu ukweli huo badala ya watu kuwekeza kama msaada katika sekta ya utalii na kuishia kumwagiwa tindikali.


SOURCE: HABARI LEO


Je, hii ndio Tanzania tunayoitaka?
Bado najiuliza, Is Tanzania a Secular State or Religious State?
Viongozi mpo wapi mbona matukio haya yanazidi na hatuwasikii mkisema chochote kwani Muungano mmeususia?
 
Kuna kitu nyuma ya pazia.........hii yaweza kuwa sawa na Zenophobia iliyowahi kutokea SA, wanaingia Zbar na kuhodhi biashara za wazawa..............tena kwa kuja na cheap labour, inatakiwa wasme mazingira na kutaufa ubia na wazanzibar halafu maduka yao yawe na wazenji hutaona hali hii tena.....................kusema ni maduka ya vileo ni funika kombe tu lakini ukweli hata ya vinyago..hapo ndio ujiulize ................unahitaji kufanya upembuzi yakinifu katika hili......................hali hii ni sinonymous na mgeni njoo mwenyeji afe njaa...kitu ambacho hakiwezi kukubalika 9machoni mwao).................na wameamua kuifanya kwenye mob justice.........


Katika MISINGI NA kanuni za Haki za Binadamu (na Watu)............Haki yako inaishia pale pua ya mwenzio inapoanzia...TAFAKARI SANA!!!!!
 
wanzibar hawawapendi watu wa bara,hata na wageni wengine,ila huku bara wanaajiriwa kabisa,huu ni ujinga,kama wao wanataka wawe na utaratibu wao kwenye kijisiwa chao,then huku tunawakumbatia,sisi ndo twenye matatizo ya kiakili,inatakiwa wakiharibu mali za watu wa bara,na sisi tunawajibu kwa kuharibu biashara za wenzao wanaofanya huku,ili kama wao wameaanza,sisi na tuwasaidie ku-escalate hilo swala then tuje tuone ni nani atakuja ku-loose mwisho wa siku
washachoma baa,huko tumbatu hawataki hata watalii,wanadai wanadai wanaharibu utamaduni wao,na viongozi wao na wetu wanasupport
 
Back
Top Bottom