Wimbi la Vibaka Jijini Arusha

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Kuna kundi la vibaka takriban 20 limezuka Arusha lenye mapanga, marungu na nondo kinapita katika Jiji la Arusha.
Jana alfajiri lilivamia nyumba moja Kwa Mrombo na kuwapora wapangaji vitu mbalimbali kama simu, fedha, laptop, redio, masanduku na wengine kujeruhiwa.

Wakazi wa Arusha chukueni tahadhari hasa kwa kutumia ulinzi shirikishi ili kukabiliana na jingi hili la kitaifa la vijana wasio na kazi.

Aidha kuepuka kununua vitu ambavyo vinadhaniwa kuwa ni vya uwizi.
 
Wanatokea lemara mkuu tumeshapeleka majina yao kwa polisi na tuko tayari kutoa ushahidi ila ndio hivyo tena kimyaaa
 
Hata Kituo cha Sombetini wana habari ila nchi wanajali kampeni za kisiasa kuliko usalama wa raia.
 
Wanatokea lemara mkuu na taarifa tumeishapeleka polisi ila hakuna kilichoendelea

Inawezekana wanatoka Lemara kwa maana huwa wanapitia Sokon One wakati wanaporudi kutoka kwenye ubaradhuli wao
lakini Polisi wamekaa kimya kana kwamba wana ubia hapo.
 
Hao ni machalii wa CDM. Ni staili yao ya kusherehekea ushindi wa Arumeru.
Mwulizeni Mhe G Lema atakuwa anawafahamu vizuri.
 
Back
Top Bottom