Wilson Mukama: Public and Private Profile

Japo nafahamu ya kuwa bado haijatolewa rasmi na CCM kwamba huyu ndugu Mukama amejitwalia ukatibu mkuu wa CCM, nimeona niwape reflection ya nchi yetu na jinsi tulivyo na muelekeo mbaya. KWa mujibu wa taarifa za kuaminika (Ref. Mwananchi la Leo), huyu ndugu Mukama alihusika moja kwa moja na kufanya tathmini juu ya wizi wa kura wa CCM uliowapa ushindi kiduchu mwaka jana na inasemekana kamati yake ndio iliyotoa recommendations za umuhimu wa CCM "kujivua gamba". Na hili ndilo linalonifanya niongelee muelekeo wa nchi yetu Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Mkama ambaye mpaka leo hii ni mfanyakazi wa serikali na kwa maana hiyo analipwa mshahara kwa kutumia kodi za watanzania wote bila kujali itikadi yao ya kisiasa. Sasa najiuliza, anawezaje baada ya hapo kufanya kazi ambayo kimsingi inakusudiwa kukipa chama kimoja ushindi dhidi ya kingine? Katika hili sisemi kwamba hana right ya kuwa mwana CCM, la hasha. Lakini ethics za kikazi zinamruhusu vipi kuwa mfanyakazi wa serikali na hapo hapo wa CCM?

Ikumbukwe pia kuwa Mkurugenzi anekaimu wa Daily New anyeye pia akiwa mfanyakazi wa CCM aliwahi kuandika editorial wakati wa uchaguzi mwaka jana akisema wazi na namnukuu, "Slaa asahau kwamba anaweza kuuchukua uraisi" kwa maana kuwa alikuwa akiipigia campaign CCM. Ni lipi sasa linalofanya magazeti ya TSN (Daily News na Habari leo) yatambulike kama ya serikali na ya-exist kwa kodi ya watanzania wapatao milioni 43 wakati yanafanyakazi za CCM yenye wanachama wasiozidi milioni 5 kwa mijimu ya takwimu zao wenyewe ambazo naamini zimechakachuliwa?

Niseme wazi kuwa simjui huyu ndugu Mukama lakini ile tu kwamba alikuwa akifanya kazi bega kwa bega na CCM wakati anaishi kwa kodi ya walalahoi ambao wengine si CCM inamfanya nayeye kuwa fisadi kama mafisadi wengine. Vinginevyo, Hawa Ghasia atueleze alitumia vigezo vipi kusitisha mkataba wa Prof. Baregu kwasababu tu ya kugombea uongozi CHADEMA. Au ni vigezo vipi vilitumika kumkatisha kazi Prof. Safari kazi yake pale katika chuo cha diplomasia kurasini?

Na ni kipi kinachofanya kuwa hadi leo baada ya miaka zaidi ya 10 ya kutofanya kazi UDSM, kwanini bado Prof. Lipumba anatambulika kama mkufunzi alie likizo ya kikazi ilhali amekuwa mwenyekiti wa CUF katika miaka yote hii? Wasiwasi wangu ni kwamba sheria tofauti zinatumiwa kushughulikiwa masuala yaliyo sawa. Nini mwisho wa yote haya?

Ama kweli katiba mpya inahitajika Tanzania.
Mkuu hii habari ni nzito lakini tunaweza kuipuuza tu! Kama ya lipumba nae ni kweli nipo hoi kabisaaa!
 
hapo ndipo utakapo wapenda great thinkers, mtu mmoja ka google article moja, then anakuja na private na public profile ya Mukama..big up jf

Mkuu kweli inabidi hawa ma-great thinkers wachunguzwe, mtu anaokota viji-information ndo anatuambia profile :bored:!!
 
mabadiliko haya tusubiri tuone kama yatasaidia maana sio kubadilisha tu watu but utendaji kazi
 
Back
Top Bottom