Wilson Mukama awa katibu Mkuu mpya CCM na CC Mpya

Wakuu nitawaletea kila kinachoendelea Dodoma, nipo live hapa...

Sasa kinachoendelea ni nyimbo za kushangilia, muda si mrefu mambo yatawekwa wazi.
 
Naam sasa hii naikubali kabisa. Mchanganyiko kati ya vijana na wazee na wapya na wazamani kidogo. Kilichobaki kwetu CCM kushirikiana na Rais wetu, katika haya:

1. Tuwe wazi katika majadiliano ya marekebisho ya Katiba bila jaziba wala vizuizi kwa wananchi na tuwe na hoja.

2. Tukae mbali kabisa wote wenye tuhuma za ufisadi na tusifanye kosa kuanza kufikiria Rais wa ajaye ambaye ana tuhuma yeyote ya ufisadi hiyo itakuwa ni kujimaliza kabisa! Na wale wanaothibitika wafikishwe mahakamani moja kwa moja bila kujali walikuwa ni akina nani wako CCM, CHADEMA, CUF n.k

3. Swala la Dowans tuachane nalo kabisa kwa kutolipa hata senti

4. Rais pitia safu ya watendaji wakuu Wizarani, Idarani, Tasisi za umma na ikibidi kama itakavyofaa fanya mabadiliko itakavyostahili kwa kuweka watu wanaokubalika, watu wanaojituma, watu wasio na tuhuma za ubadhilifu watu wasiotishwa na phobia au ushabiki wa udini bali wanaojali zaidi uzalendo wa nchi yetu.

5. Hatuna haja ya kukimbizana na kuzuia maandamano wala speech za watu majukwaani (tunawapa umaarufu wa bure) wacha waseme na sisi tuingie katika kuboresha maisha na tutasema majukwaani pia.

Tuangalie nje ya 'box'; wako wana CCM wenye sifa nzuri kibao huko mikoani. Tusingángánie majina ya watu yanayofahamika katika Chama. Aidha hilo ni sehemu ya mambo yayowakera wengine na kufikiri kuwa Chama kina wenyewe fulani wachache.

Kila la kheri, nimeanza kupangusa vumbi ya kadi yangu na kuchapa mzigo wa kuongeza uzalishaji nchini kwetu.

MTOTO WA NYOKA NI NYOKA

MKAMBA NDOGO KAWEKWA PALe NA LOWASSA NA RA

HUSITEGEMEE CHOCHOTE TOKEA KWA HUYU MWIZI MDOGO
 
Kweli ccm imepania,hzo figure hapo si mchezo eg mwigulu,very young and ambitious,an ex ilboru and pro-migomo udsm,a.k.a chief,jaman upin9ani utakosa agenda.be aware.
 
mwigulu mchemba, headboy ilboru sekondari. Mbunge tabora. Worked at bot. The rest his close buddies will provide. But all iborians mid 1990's remember him....at last! True colours. Colours true
hapa wamepata

i hope albedo atakuja kutupa more insight
 
Eti wenyewe wanasema Chama Kinajivua Gamba ha ha haaaa

Yaani licha ya madhambi yote ambayo CCM imeyafanya kuna watu bado wana matumaini na hawa jamaa? Nashindwa kabisa kuelewa!

Haya mamtu ya CCM ili somo liwaingie, yanatakiwa kuwekwa benchi kwa muda wa kutosha. Ni hapo tu ndipo yatakapojifunza.

Lakini hii ya kuyapigia makofi yafanyapo mabadiliko ya viini macho wala haitasaidia kitu. Tayari yashasoma yanadili na mijitu gani na yenyewe yalivyo majanja tayari yashajua namna namna ya kulicheza gemu. Yakiharibu kidogo tu yatakuja na vimisamiati vingine....safari ijayo huenda yakaja na "kujimenya".

Siasa za bongo bana.
 
Hapo muelekeo ni kupunguza hoja ya udini,kama kuna watu walokuwa wanaipenda chadema kwa mtizamo wa ukristo kama ilivyoenezwa na c2m,hao nao watarudishwa c2m,bado kazi ndo inaanza..
 
Tusingeweza kuelekea uchaguzi 2015 tukiwa na wazee kama mzee Makamba... Ni lazima tubadilike
 
Jamani tuwe objective kidogo, hapa CCM wamepiga bao kiaina. Kumweka Nape na January kwenye Sekretarieti (sp) wamepata hazina ya vijana wa kidotcom ambayo ni upgrade mara 50 ya iliyopita. Kama Nape na January wakiamua kufanya kazi kwa mapenzi ya nchi, na January akawaweka pembeni hao kina RA & EL, itasaidia sana.

Tuwape pongezi vijana wenzetu wanapopata nafasi, then uko mbele tutawajudge namna watakavyoact.

Hongera sana January na Nape.

Inaonekana na Mwigulu Mchemba, naye ni kijana mwenzetu. Hongera Mwigulu na wewe, tunawatakia mafanikio mema.

Msimamo mnaotakiwa kusimamia ni very simple, Maslahi ya walalahoi yawe mbele siku zote na mafisadi wapingwe hata kama waliwasaidia uko nyuma kipesa.

Mbona unashindwa kukumbuka nadharia rahisi kabisa ya madaraka na ubinadamu? Kumbuka CCM sasa hivi ni mwendo wa MJANJA KUWAHI NA KUPATA (kula).. AMINI AMINI NAKWAMBIA WANACHOSEMA WENYE UFAHAM HUMU JF KUWA KWA HATUA ILIPOFIKIA CCM HAIOKOLEKI,MAANA YAKE NI KUWA MLE NDANI KUNA MAKUNDI,ILI MAMBO YANYOOKE WALAU UWA-PLEASE KILA KUNDI KWA KUTEUWA MTU WAO..OTHERWISE NI MATAMKO NA KUSIRIBIANA..WAPO WATAKAOONA KUMTEUA JANUARY NI DHIHAKA..NK...Pia hii dhana ya kuteua vijana kama vijana na kigezo kuwa vijana...si sawa..LABDA WAZEE WENYE MAWAZO YA VIJANA..NA MWISHO KINACHOIUA CCM NI MAGAMBA ( UFISADI),,,NA TAMKO LA KUVUA MAGAMBA HALIWEZEKANIKI KUTEKELEZWA..KWANI MISINGI YA SASA YA UHAI WA CCM NI MAGAMBA HAYOHAYO..
Period
 
Yaani licha ya madhambi yote ambayo CCM imeyafanya kuna watu bado wana matumaini na hawa jamaa? Nashindwa kabisa kuelewa!

Haya mamtu ya CCM ili somo liwaingie, yanatakiwa kuwekwa benchi kwa muda wa kutosha. Ni hapo tu ndipo yatakapojifunza.

Lakini hii ya kuyapigia makofi yafanyapo mabadiliko ya viini macho wala haitasaidia kitu. Tayari yashasoma yanadili na mijitu gani na yenyewe yalivyo majanja tayari yashajua namna namna ya kulicheza gemu. Yakiharibu kidogo tu yatakuja na vimisamiati vingine....safari ijayo huenda yakaja na "kujimenya".

Siasa za bongo bana.

Teh teh teh
 
Back
Top Bottom