William Malecela - Mbunge Mtarajiwa Afrika Mashariki

Status
Not open for further replies.
Nahiyo CCM ndio hatuitaki hata kuisikia mwaga damu ya CCM weka ya CDM otherwise kula itakuwa kwako na kura CDM
0004.JPG
 
- Katiba pia inaruhusu kupiga kura ambayo ndio njia pekee kwa mwananchi kumchagua ya nani anafaa na nani hafai!, kuliko kulalamika.

William.

Msipende kujificha kwenye katiba ilihali mnajua inamapungufu, na ndio maana tuko hapa kuhakiki ki nguvu ya Umma zaidi
 
You might be right lakini kumbuka sio kila anayetakiwa kutoa mawazo ni lazima awe na skills za kufanya hiyo presentation, kama kwako ni kazi sisi wengine ni jamvi tu la kutolea mawazo yetu. Uandishi na Udereva hauhitaji kuupatia ajira maana kila mtu anaweza akiamua

Dah! Umeongea point mkuu, ukosawa kabisaaa, badala kujadili hoja ilyopo mezani wanaanza kujadili uandishi! Bora ulivyo wakomesha.
 
Tulijua tu wengi watajificha chini ya kivuli cha hii katiba yenye mapungufu ambayo kila kukicha inatuletea viongozi wabovu lakini chujio lake lipo. ilihali umekuja mwenyewe embu jitetee tangu umetua bongo kipi umekifanyia taifa lako mpaka ukavutika kuchukua form ili ukimalizie ukiwa na mamlaka ya Umma
 
wewe Willy kaka yangu huwezi kutuambia unagombea post kubwa na muhimu kama hiyo alafu ukaamua kutuandikia historia yako kama muuza karanga anatafuta karanga yaani umeona sisi wana JF tunaakili za kupokeavitu kimzahamzaha tukaviacha hiyo CV kama umeamua kutupa highlights zake angalau weka miaka basi, acha kutuimbisha ngonjera ambazo wengine tulishaga sahau tuko fani nyingine bana.
 
- Ahsante sana mkuu, FACTS ni nimekulia Tanzania, nimezaliwa Tukuyu, shule ya msingi nimesoma Jamhuri Mnazi Mmoja, Sekondari nimesoma Kwiro, Mahenge /morogoro, Chuo nimesoma Kidatu, na DMTU DSM, JKT nimeenda Oljoro, nikashiriki kufufua kiwanda cha Kagera Sugar baadaya kubomolewa na Idd Amin, nimefanya field kwenye meli za MV. Bukoba, Mwanza na MV, Liemba na Mwongozo, Kigoma. Nikaenda kusoma Belgium, nikafanya kazi huko, baadaye nikarudi Tanzania na kufanya kazi Shirika la Tanzania na China Sinotaship, baadaye nikaenda US nikasoma na kufanya kazi huko, mpaka niliporudi nyumbani na sasa ninagombea ubunge.

- Ninaamini kwamba mwananchi yoyote mwenye akili timamu akisoma maelezo yangu ataamua kuhusu ukweli na uongo wa hoja zako, ingawa siamini kwamba umezitoa kwa nia mbaya sometimes ni misguidance na misinformation tu uwe na siku njema sana!

William.

Nakufurahia kwa unavyojitahidi kutupenda na kutuona ni kati ya jamii yako ndo maana unajibu hoja. Ila kaka yangu kumbuka JF sio kids-blog bana ukiamua kuwaona watu ni level yako na wanaweza kufanya kitu kwa ajili yako wape vyote basi mbona CV kama verse ya Juma Nature. Think Big
 
Mkuu!!
Nimeipenda sana hii, ilikuwa wapi hapo??
Na wewe sijui unaishi dunia gani!!??....hivi huoni kama hiyo ni picha ya jana tu kwenye mkutano wa kuwashukuru wana Arumeru kwa kumchaguwa Joshua Nassari? hapo aliyekaa chini kulia ni Kamanda Lema.
 
- Ahsante sana mkuu, FACTS ni nimekulia Tanzania, nimezaliwa Tukuyu, shule ya msingi nimesoma Jamhuri Mnazi Mmoja, Sekondari nimesoma Kwiro, Mahenge /morogoro, Chuo nimesoma Kidatu, na DMTU DSM, JKT nimeenda Oljoro, nikashiriki kufufua kiwanda cha Kagera Sugar baadaya kubomolewa na Idd Amin, nimefanya field kwenye meli za MV. Bukoba, Mwanza na MV, Liemba na Mwongozo, Kigoma. Nikaenda kusoma Belgium, nikafanya kazi huko, baadaye nikarudi Tanzania na kufanya kazi Shirika la Tanzania na China Sinotaship, baadaye nikaenda US nikasoma na kufanya kazi huko, mpaka niliporudi nyumbani na sasa ninagombea ubunge.

- Ninaamini kwamba mwananchi yoyote mwenye akili timamu akisoma maelezo yangu ataamua kuhusu ukweli na uongo wa hoja zako, ingawa siamini kwamba umezitoa kwa nia mbaya sometimes ni misguidance na misinformation tu uwe na siku njema sana!

William.

A very impressive CV and a good template too....next time na mimi ntatumia hii template kuombea kazi......who needs dates and places in a CV?
 
- SAwa sawa mkuu tupo pamoja, ingawa sifai kulinganisha na Kiongozi gani anayefaa? Otherwise tupo wote hapa na FB sijawahi kuwakimbia wananchi ninaotaka kuwaongoza na sijawahi kuogopa kusema wazi hapa kwamba mimi ukinikata mwili wangu umejaa damu ya CCM, UBARIKIWE MKUU!

William.

Navutiwa na wewe hasa unavyo go down when you realize kama kuna point. Nikiendelea kusoma comments zako naweza nyanyua simu yangu na kuwapigia wapiga kura wako hapa ili tubembeleze ulajji nahisi unaweza tufaa vijana. Anyway tusubiri tuone maana hata Nape alianza hivihivi
 
Hisia za watanzania wengi akiwepo mimi tunamini tunatawaliwa kisultan kind of: why kids of the top past and current leaders: Hili limewangusha kule Arumeru, tunajua ni haki yao ya kikatiba, kikatiba hata kupelekwa kusoma nje ya nchi???? wakrudi watutawale sisi tunasoma shule za Kata? Ni kwali atafanyia nini taifa akipewa chance hiyo ni muhimu kuliko lingine but is he going to be elected kwa uwezo wake ama cause his dad alikua waziri mkuu, Mashaka yetu ni ile kawaida yetu ya kuhoji wabunge wanaosema ndio waseme ndiooooooo na wale wasemao sio waseme siooooo mwisho wa siku tunapata mbunge wa afrika mashariki:
 
CV yake ni kwamba alikuwa baharia ameishi nje ya nchi kwa miaka kama 30 hivi na amerudi nchini rasmi kama mwezi mmoja uliopita.

Bado hajitoshelezi ulitakiwa useme :CV yake ni kwamba alikuwa baharia ameishi nje ya nchi kwa miaka kama 30 hivi na amerudi nchini rasmi kama mwezi mmoja uliopita baada ya baba yake kushindwa kwenye chaguzi zilizopita na hela za ufisadi kuanza kupigiwa kelele kwahiyo akashindwa kumtumia hela za matumizi huko ughaibuni maisha yaka mshinda akaamua kurudi ili asije akafia huko kwa shida ili aje kutumia jina la baba yake kujinufaisha kisiasa au kurithi kama walivyo masultani wa oman
 
Kuwapenda ccm
yakupasa uwe usha
kufa ukafufuka
baada ya kufufuka
ukawa taahira.
 
Leo wana jf wamenifurahisha mno.....
kitu kimoja ni kwamba enzi za watu kuogopa viongozi au majina ya viongozi zimekufa kabisa
watu wanamshambulia William bila kujali yeye ni nani hapa jf wala nchini...saafi saana..

nikija kwenye mada Wiliam ana kitu kimoja ambacho nafikiri
kwa wana jf ni muhimu....yuko engaging....yupo reachable...na haogopi kukosolewa..

anaweza kuwa hafai lakini angalau kwa kutumia JF na FACEBOOK unaweza kumfata na kuwakilisha mawazo yako

hii kitu ni muhimu mno kwa sasa kiongozi awe accessible na watu.....

katika wagombea woote wa ubunge wa Afrika Mashariki....ni William peke yake tuna 'uhuru wa kuongea nae na kumshambulia' tunavyotaka.......hii inaweza hata yeye kumsaidia 'kuwa kiongozi bora' akitaka...

hao wengine hatuwazungumzi kwa sababu hatuwajui kabisa....wanaweza kuwa ni wabovu kuliko William

lakini hatuna namna ya kuwajadli...........


Umeanza vizuri unakuja kumalizia na fb, hivi wewe unayetumia mtandao kwasasa ndio unataka ukawakilishwe au yule mtu ambaye bado anatumia jembe la mkono na kutembea umbali mrefu na kukosa maji kama tulivyoona Arumeru mashariki. Ni bora kuwa not reachable kwa wananchi alafu ukaonekanna unachokifanya kuliko kila kukicha unapost watu wafanye nini wakati unaowapostia na wao wako kwenye key board wakisubiri lunch time na muda wa kulala wazime na kutimua then who will work with those idears kwenye keyboard na ukumbuke maaidea kibao humu hayana business plan wala strategic plan and analysis zake na mifano utasikia US, UK mkikosea sana China. ndo walewale hamna mpya
 
Mbwembwe zako tu kwani nimesema kawa mbunge? Si nimeweka dash kumaanisha topic ni W. J. Malechela na subject ni Mbunge EA

Kumbe William Malechela ni Topic na Mbunge Afrika mashariki ni Subject......Aiseeeee!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom