William Malecela: ''Jonas Savimbi was a hero''

Pole sana William,
Mara nyingine tunasahau kuwa unapomnyoshea mwenzako kidole, vitatu vinakurudia wewe!
Ni kweli inategemeana na msimamo wako na huyo unayemwongelea! Savimbi ni mfano mzuri kwako!
Ila kwa wengine Savimbi aliongoza vita iliyoua watu wengi ili yeye apate madaraka!
Hata akina Mao na Castro wameongoza kiimla bila kujali haki za wananchi wenzao, hata sasa.
Kwangu sio mfano wa kuigwa bora ungesema Mandela.
 
i.d.i.o.t always will be :bange:

Comrades dont just get irked up for nothing! certain words means different things to different people, e.g: shimama in Japanese means Girrafe; so for WJSM he could take it for a corruption of the swahili word SIMAMA meaning "stop!"; so instead of getting yourselves worked up; simply ask WJSM what does he understand of the word HERO!!
 
Kimbunga,

..Savimbi na Unita walikuwa wanafuata Ujamaa lakini ule wa Kichina.

..Augustino Neto na MPLA walikuwa wanafuata Ukomunisti na USSR.

..halafu kulikuwa na FNLA ambao walikuwa wanasaidiwa na Mobutu hawa sina kumbukumbu walikuwa wanafuata mrengo gani lakini inawezekana walikuwa wameegemea nchi za magharibi.

..kuna kipindi Tanzania ilikuwa inamsaidia Savimbi kwasababu ya mahusiano yetu na Wachina.

..SAVIMBI aliharibu kila kitu pale alipoamua kushirikiana na MAKABURU wa Afrika Kusini.

..alipochukua uamuzi huo tu, basi nchi zote za Kiafrika zilizokuwa zinam-support zikamtupa mkono.

..kubwa zaidi ni kwamba uhusiano wa Savimbi na makaburu ulikuwa kikwazo cha harakati za uhuru wa maeneo mengine kama Namibia,Zimbabwe,na Afrika Kusini.

..wananchi wa Angola wameumia sana kutokana na mis-calculations alizofanya Savimbi ambazo zilisababisha Angola kuwa uwanja wa mapambano ya "vita baridi" kati ya nchi za magharibi na zile za mashariki.

NB:

..msimamo wa serikali ya Tanzania ni kwamba Jonas Savimbi alikuwa gaidi.

Mkuu JokaKuu hii analysis yako ni nzuri na ya kweli.

Msimamo wa Tanzania pia ulikuwa wa kisiasa zaidi hasa hivyo ambavyo serikali ya makaburu ilipoingia na kuwasaidia akina Savimbi. Pia kumbuka Malawi hata Kenya walikuwa na uhusiano wa kibiashara na Makaburu.
 
Last edited by a moderator:
..kuna kipindi Tanzania ilikuwa inamsaidia Savimbi kwasababu ya mahusiano yetu na Wachina.

..SAVIMBI aliharibu kila kitu pale alipoamua kushirikiana na MAKABURU wa Afrika Kusini.
Uko sawa Mkuu, hii ilikuwa ni baada ya 1966 wakati Savimbi aliporudi kutoka China na kukataa ofa ya kujiunga na MPLA na kuamua kuingia msituni pamoja na kundi la UNITA. Tanzania na Zambia walisaidia kumuingizia vifaa vya kivita toka China. Nakumbuka kipindi hicho tulimuona Savimbi kama mpiganaji wa ukweli lakini hali ilikuja kubadilika pale alipoamua kushirikiana na makaburu pamoja na CIA.
 
- Mimi sina nguo na wewe umekuja kujivua, sasa wenye akili wafanye nini mkuu? ha1 ha! ha!

ok sasa napumzika kidogo! ha! ha! ha!

William!

Mkuu nanona ha! ha! ha! ha! ni nyingi sana, na huko EALA ungeenda na mziki huu au ungekuwa tofauti?
 
-

- Uzuri ni kwamba maneno yangu ya bluu yanajisema wazi kwamba nimeongelea
UKOMBOZI as a common factor between Mbowe na Savimbi, FULL STOP! ha! ha! ha!

William!

William, Kwa kutumia hiyo "common factor" uliyotupa tunaweza kuwa sahihi tukisema Hitler alikuwa mkombozi? And if you dont mind unaweza kutuambia kama kuna tofauti kati ya ukombozi na tyranny?
 
Uko sawa Mkuu, hii ilikuwa ni baada ya 1966 wakati Savimbi aliporudi kutoka China na kukataa ofa ya kujiunga na MPLA na kuamua kuingia msituni pamoja na kundi la UNITA. Tanzania na Zambia walisaidia kumuingizia vifaa vya kivita toka China. Nakumbuka kipindi hicho tulimuona Savimbi kama mpiganaji wa ukweli lakini hali ilikuja kubadilika pale alipoamua kushirikiana na makaburu pamoja na CIA.

Askari Kanzu,

..asante kwa mchango wako. nakubaliana na wewe 100%. labda niongeze yafuatayo.

..kitendo cha SAVIMBI kushirikiana na MAKABURU kilikuwa ni utovu usiovumilika ktk harakati za ukombozi wa kusini mwa afrika. maazimio kadhaa ya OAU yalimtambua Savimbi kama gaidi.

..mimi nadhani Savimbi aliyataka madaraka kwa namna yoyote ile na hilo ndilo lilikuwa tatizo lake kubwa.

..baadaye akageuka kuwa kikwazo ktk juhudi za kuleta amani Angola na eneo zima la Afrika Kusini na Kati.

..jinsi muda ulivyokwenda Savimbi akawa hahitajiki tena, nchi zilezile zilizokuwa zimkimfadhili zikamuingiza ktk mtego na Savimbi "Jogoo mweusi" akauawa kinyama.

..sasa hivi Angola inasonga mbele na inaanza kujitambulisha kama taifa lenye nguvu za kijeshi na kiuchumi barani Afrika. Kikwazo kikubwa kwa Angola hivi sasa ni rushwa.

..sijui kama mmejiuliza kama Angola wangekuwa na amani tangu wamepata uhuru wangekuwa wapi leo hii?

..Savimbi alitumia rasilimali za Angola kama almasi,dhahabu,na mbao, kupigana vita. Angetumia rasilimali hizo kuboresha maisha ya wananchi aliodai anawatetea wananchi hao wangekuwa mbali sana leo hii.
 
Dah...sasa kwa nini Le Kutuz usigombee ubunge dodoma mjini uwe kama mayor De Belasio wa NYC?
 
William ameshasoma sheria na haki za kiongozi wa upinzani?

Binafsi nimeshindwa kuelewa kwa nini ameona SAVIMBI yuko level moja na Castro au Mao? Huyu mtoto ana elimu gani?

Wakati Cuba walishawahi kupeleka jeshi nchini Angola kuwasaidia MPLA kuwapiga waasi wa UNITA iliyokuwa chini ya Savimbi
Leo bichwa mavi linakuja linatuambia Savimbi alikuwa mkombozi.
 
Wakati Cuba walishawahi kupeleka jeshi nchini Angola kuwasaidia MPLA kuwapiga waasi wa UNITA iliyokuwa chini ya Savimbi
Leo bichwa mavi linakuja linatuambia Savimbi alikuwa mkombozi.

- Ok wewe una tatizo lingine against me hili sio, by the way ni wapi niliposema Savimbi Was a Hero? Maneno yako mekundu yanaonyesha uwezo wako wa kufikiri unaponzia na kuishia so unafikiri maneno kama haya ndio yatakupa Dual Citizenship? ha! ha1 ha!

Le Mutuz
 
Dah...sasa kwa nini Le Kutuz usigombee ubunge dodoma mjini uwe kama mayor De Belasio wa NYC?

- Sasa nipo busy sana na biashara mkuu next week mimi na mbia mwenzangu tunafungua ICD kule Mbagala, that is a big project inahitaji kutulia kwanza hayo mengine tutayaona mwakani.

Le Mutuz
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom