William Malecela: Dissaster waiting to happen

Nafikiri watu wengi pamoja na hata mleta mada wamechanganya mambo. Sidhani kama suala hasa hapa ni Jumuiya ya Afrika Mashariki. Suala hapa ni kama kweli tunapekeka watu makini kutuwakilisha huko. Inawezekana aliyosema William ni ya kweli kabisa lakini mbona wanasiasa wetu wakati wa kampeni huwa wanafanya hivyo hivyo kwa kutuondhoreshea list ya matatizo yetu na jinsi watakavyoyatafutia ufumbuzi lakini wakishachangualiwa hawafanya chochote?

Wakati babake alivyopigwa chini na Lusinde watu hapa walishangilia weee, kumbe Lusinde mwenyewe mliokuwa mnamshangilia ndiye huyo. Leo mnapewa maneno matamu na William tayari kwishaney. Ukitaka kuwapiga bao Watanzania ongea tuu kile wanachotaka kusikia. Hata kama ukiwa kichaa watakuchagua tuu uwawakilishe. Muone hata Lusinde kadhibitisha yeye ni kichaa wa kuzaliwa lakini still walimchagua kuwa mbunge wao.

Hatuna tabia ya kwenda deep na ku-examine hawa watu kama kweli wana credentials zinazotakiwa kutuwakilisha hasa kwenye ngazi za kimataifa where the national interests are at stake. Kwa kweli inabidi ifike mahali tujiulize: Are we picking the right people to represent and defend our interests in the East African Community na kwingine kote duniani? Je, process nzima inayotumika kuwapata hawa wawakilishi ni fair na open kwa watu wote? Au watu wanapitishwa kwa kujuana tuu? Imefika wakati tuache kudanganywa na maneno ya watu wanaodai kuwa wanataka kutuwakilisha wakati wanataka tuu uongozi kwa faida zao binafsi.

Kama kweli kuna mtu aliyesikiliza interview ya William kuanzia mwanzo mpaka mwisho na ku-conclude kwamba anafaa kabisa kutuwakilisha EAC then we have got a long way to go. Seriously, utakuwa huna tofauti na yeye kusema kuwa tuna gap ya miaka 250 kufikia demokrasia ya Marekani. Kama ndivyo unavyotaka then muunge mkono lakini usilalamike kuhusu demokrasia mbaya Tanzania kwa muda wa miaka 250 kama bado utakuwa hai.
Mkuu EMT uko right kabisa kamanda.wanajamvi karibuni kwenye ulimwengu wa siasa.siasa ni mchezo wo kuigiza,period.viongozi wetu wengi wanakimbilia kuingia kwenye siasa kwaajili ya kujiongezea kipato na kuweza kujinufaisha wao na familia zao basi.siasa kwa viongozi wengi ni ajira kama ajira nyingine.kwamba imekuwa ni njia ya kutokea kimaisha.kwahiyo utakuta viongozi wengi walioongoza kwa miaka nenda rudi hawajaweza kutekeleza ahadi ambazo walitoa kwa wananchi ili wachaguliwe.kwahiyo inapofika wakati wa uchaguzi mwingine wanakosa cha kuongea manake ahadi zao zote walizowahi kuzitoa hawatekelezi.kwahiyo inabidi waendelee kudanganya wananchi.wenyewe wanajua kwamba wanadanyanya na wanaodanganywa pia wanafahamu wanadanganywa ila mwisho wa siku wanawapa tu kura.wananchi wanaelewa kabisa wanadanganywa mpaka sasa wamezoa na kuipenda hali hiyo.atleast nadhani inawapa walau matumaini japokuwa ni hewa.sasa wakuu tutakuwa tunajidanganya tu na kuumia vichwa kama tunataka kila kiongozi awe na credentials ambazo tunazitaka.cha muhimu atleast tujitahidi kwa kila njia,iwe ni maandamano,iwe ni kuongea sana ili Mungu atusaidie tupate Raisi smarthawa viongozi wachinichini hakuna hata mmoja anafikiria wananchi wake zaidi ya kupigania kujiendeleza yeye mwenyewe na kupata umaarufu.tukiwa na Raisi smart basi hakuna kiongozi wa chini ambaye atazuia nchi kuendelea.Ndo maana wakuu kwa mtu anayefahamu umuhimu wa jambo hili pia atafahamu kwamba suala la mchanganuo wa katiba ndio starting point ya kuelekea kwenye ukombozi wetu.kwamba ni lazima tuwe watu wakutaka kujua sababu kwenye kila step serekali inayofikia kwenye hili zoezi la katiba.tusiwe wepesi wa kujudge wengine wanapotoa points zao pasipo kujaribu kutadhmini mawazo yao.mfano ni kama mzee mtei alivyokuwa opposed kwa kuongea ukweli.kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anafahamu fika kuwa alichoongea mzee mtei ni common sense na kwamba mzee mtei ni mzee ambaye hatujawahi kumsikia akiropoka ovyo kama wazee wengine wengi,hivyo ni mtu ambaye mpaka kufikia hatua ya kutoa comments kama hizi tayari ameona mbali.tusipende ushabiki wa kijinga.tusiongelee hii issue kishabiki kama tunavyoshabikia simba na yanga.tuweke masuala ya vyama pembeni na tupambanue haya mambo kwa kisomi zaidi na kiutaifa zaidi.kwasababu yanafaida kwa sisi wote na vizazi vyetu vitakavyofuatia.mbarikiwe!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Lakini huyu ndugu ameishi sana marekani. Mambo ya ea anayafahamu vya kutosha? Huyu bwana kasema yeye by profession ni politician, then ni mhandisi. Halafu katuambia kuhusu 'GDNP per capiter'. Sijui kama alishasawazisha hayo. Hizi nafasi nadhani zingewafaa zaidi kina Bashe na wengine ambao siku zote tunapigana vikumbo humu nchini. Sasa kwa cigwi jr isingekuwa kwa nafasi na jina la baba yake angetoka all the way from ny kuja kugombea ubunge ea? Sidhani. Na ccm ingekuwa na akili ingemuweka benchi kwanza ea kisha ikampa kazi za chama at least kwa miaka miwili hivi. Asiporudi marekani ndio wajue kweli kijana ana nia
 
nakutajia viongoz tuliowatoa nje na wanafanza madudu WAZIRI NUNDU,NYALANDU, Nimekutajia wawili tu kwanza je wana jipya gan hawa!na wewe unayeshikilia hoja ya MTEI jaribu kupunguza udin hata kama unao weka moyoni,na watanzania mnatakiwa muwe mnapenda kuambiwa ukweli hata kama unachukiza
 
316444_2385989848381_1209820481_32959751_2885080_n.jpg

Ukiangalia sura yake tu utaona kila kitu. chain shingoni kidani kikubwa ambacho ni kodi za watanzania alizochota babake. Na pia hii Bold head shows ubongo umetikisika kidogo.
 
Ukiangalia sura yake tu utaona kila kitu. chain shingoni kidani kikubwa ambacho ni kodi za watanzania alizochota babake. Na pia hii Bold head shows ubongo umetikisika kidogo.

Uchaguzi umekwenda je kwa bwana mdogo? Atatuwakilisha au anasubiri kufungua ZEUTAMU?
 
316444_2385989848381_1209820481_32959751_2885080_n.jpg

Nimesikiliza interview yake aliyoifanya ambayo imepostiwa michuzi blog. Inaonekana huyu yuko out of touch na maendeleo ya dunia

Hoja zake kubwa ni hizi:

1. Anasema hakuna haraka ya kujiunga na Federation kwa sababu wananchi hawajaelemishwa...ni kweli kabisa lakini amesahau kuwa hili suala halikuanza kuangalia leo wala jana na si kazi ya nchi zingine kuwapa wa Tanzania elimy juu ya hii federation.

2. Amesema kuwa Tanzania itapata matatizo ya uchumi kama Greece ambayo imepata matatizo ya uchumi kwa sababu imeingia kwenye Euro. Lakini ukweli ni kuwa si kweli matatizo ya Greece ya uchumi ya Greece hayakutokana na kujiunga na Euro bali matatizo ya Greece yametokana na Greece (serikali) kutokuwa makini kwenye spending yao,cheap lending and failure to implement financial reforms ambayo essentially iliacha Greece kuwa badly exposed wakati global economic downturn ilipostruck. Hii haiuhusiani na Greece kujiunga na EU .

3. Amesema kuwa watanzania wengi walipo nje (diaspora) ni wepesi kukosoa serikali na utawala nyumbani kwa sababu ni CHADEMA...sijui kazitoa wapi hizi data lakini naaamini kuwa William amekuwa too simplistic na accusations zake. In short anataka kuwafanya waTanzania wajinga kiasi cha kuwa no one can think critically and independently na hatuna option zaidi ya CHADEMA.

4. William anasema kuwa angefurahi sana kama National Service ikarudishwa ili kurejesha uzaelndo kwa vijana lakini ukweli kasahau:

a) Kwa nini iliondolewa in the first place

b) Uzalendo hauwezi kupatikana kwa kulazimishana

c) Atapata wapi budget ya kuirudisha hiyo National service

d) Uzalendo haupatikani kama serikali haitazami wananchi wake

5. William amesema kuwa anaunga mkono kila kitu ambacho serikali ya sasa inakifanya. Hii inatisha sana kwa mwana JF na mtu aliyesoma na kuishi nje ya nchi. Inamaana William ana unga mkono mpaka mabaya ambayo serikali imeyafanya. This is dangerous thinking, hata huyo Nyerere hakuunga mkono kila kitu ambacho serikali ilikuwa inafanya iweje huyu amekuja na kutoa endorsement ya 100% bila ya kuwa critical kwenye mabaya, akiingia inamaana William atakuwa na rubbestamp kila kitu huko serikalini? Is this the hope we can believe in? kweli?

6. Amesema kuwa Tanzania middle class wamekuwa wengi....well ukweli ni kuwa tanzania ina population ya almost 44 million na the so called middle class ni less than 8% sasa na ni wale wale ambao ni watoto wa kishua na extension zao. Namshauri williama atoke aende rufiji, Mkuranga Kisarawe na tendahimba kama atakuta middle class hata mmoja.

7. Anasema kuwa watu walipo nje wasikae nje na kulalamika. ukweli ni kuwa the entire system imekamwata na wale wale. Na nathubutu kumwambia atuletee list ya wana diaspora waliorudi na wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko kama alivyofanya kagame wa Rwanda's government ambaye serikali yake ilikuwa aggresive kwenye ku recruit highly educated members of the Diaspora....na waliporudi wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko na yanaoneka. Sasa william nitajie idara hata moja iliyopewa watu waliokuwa Diaspora na ambayo imepewa nafasi ya kufanya mabadiliko?

Je william anajua:

a) It takes 4months to register a business in Tanzania na it costs about 800 usd? wakati Rwanda it only takes 15 minutes and costs nothing!

b) Je anajua kuwa 70% ya Watanzania ni under 30 ambao wako detached na political elites ambao wako out of touch na maendeleo

c) Je William anajua kuwa hao vijana ambao wamezaliwa early 1990's ambao amewapatronise kwenye interview ndio hao hao leo wanapiga kura?

d) Je william anajua kuwa BRELA walinunua software ya bilioni 2 ambaoilitakiwa ifanye kufanya biashara Tanzania iwe ni rahisi lakini mpaka leo ile kitu imefeli, pesa zimetumika na so far imefanyiwa sabotage ili watu waendelea kula rushwa pale BRELA...cha ajabu waziri Nyalandu analijua hili, Waziri Mary Nagu analijua hili and no one cares.


8. William anasema kuwa viongozi wafungue FACEBOOK pages lakini haoni kama hiyo ni ndoto ya alinacha kwani commander in chief ofisi yake (Ikulu) haina website sasa why should someone like Mary Nagu au Nchimbi have a facebook page?


9. William anasema kuwa achievements zake kubwa ilikuwa ni kuandaa sherehe ya kumpokea Asha Migiro alipoteuliwa kuwa Dpeuty SG wa Ban Ki Moon, mimi binafsi sioni kama hiyo ni issue na sioni kama ni achievement ya maana.


10 Anasema kuwa alikuwa instrumental kuanzisha jumuiya ya Watanzania New York na kwa hili nampa pongezi.


In short sijapenda generalisations zake na kwa inter interview ya 1 hour nilitegemea kupata mawazo yaliyobobea na mapya toka kwa mwana JF na mwana diaspora ambaye anaenda kutuwasilisha.


William kama mawazo yako ni hayo then I give up!
Ni wa kupuuzwa tu huyo kiumbe.
 
Back
Top Bottom