William J. Malecela kugombea ubunge wa EAC

- Na by the way vipi umeshapita ofisi za bongo ukaona Wa-Kenya walivyojaaa? Je unaamini na kule Kenya tukienda tutakuta Wabongo wamejaa kwenye maofisi yao?

Respect!

FMES!

Mtizamo wangu si vizuri mtu kuwa na aliases (sio IDs) kibao.......

Hilo la Wakenya ni zaidi ya uwezo wetu....hata humu ndani TZ tu makabila yanazidiana....nenda Tunduma ukute Wachagga ni wangapi TRA....ni lazima tukubali jamii kwa jamii huzidiana maarifa....Nakuombe jaribu kwenda Moshi kutafuta shamba
 
Sasa huyu Bashe atakuwa anawakilisha Tanzania au Somalia ?.

..Hussein Bashe naye nasikia anataka kwenda kwenye bunge la EAC!!

..wa-Tanzania tunatakiwa kupeleka "the cream of the cream" ktk bunge la EAC.

..kuna mambo mazito yanajadiliwa na kuamuliwa huko na ni vizuri tukapeleka wasomi, tena wale makini kwelikweli.
 
- Safari kuhusu IDs kama unazijua ina maana wewe ni Admin, then si ni rahisi sana kwako kuzizuia kuliko kuja kulia hapa kwenye public?

- Suala la Ajira zetu na wakenya ni letu kwa sababu wamekuja kwa mkataba wa EAC na it has nothing na kuzidiana kwa jamii au makabila, Japan ilikuwa inaiuzia USa magari lakini inakataa kununua ya USA, mpaka Clinton alipowalazimisha kununua kwa nguvu au atavunja mkataba, siku hiz Wajapan wananunua magari ya US wanayapeleka re-circle ndio maana ya mikataba ya Uchumi na biashara na Ajira, sio Wakenya wanakuja kwetu kuchukua ajira sisi hatuwezi huo sio mkataba mwema kwa Taifa!

- Ndio maana tunahitaji Wabunge imara huko EAC.

FMES!
 
Heshima FMES,

Mkuu ulikuwa wapi siku nyingi sijasikia nondo zako za uhakika.Back to topic ni kweli suala la EAC linatakiwa kutazamwa kwa umakini mkubwa sana kuanzia uwakilishi namuundo wake.Mkataba wa EAC itifaki zote zinazojadiliwa na zilizopitishwa hazifahamiki kwa wananchi wengi actually sehemu kubwa ya mikataba inafahamika kwa viongozi na wananchi wachache sana.

Ukiangalia EU baadhi ya mikataba haioperate kwa baadhi ya nchi mfano UK bado wanatumia sarafu yao ingawa ni mwananchama kamili wa EU.Kwa mfano huo Tanzania inaweza pia kujiondoa katika kipengele cha ajira,ardhi,usalama,fedha na nk.Hili litawezekana kama tutakuwa na wawakilishi imara na makini katika kutetea na kujenga hoja.

- Safari kuhusu IDs kama unazijua ina maana wewe ni Admin, then si ni rahisi sana kwako kuzizuia kuliko kuja kulia hapa kwenye public?

- Suala la Ajira zetu na wakenya ni letu kwa sababu wamekuja kwa mkataba wa EAC na it has nothing na kuzidiana kwa jamii au makabila, Japan ilikuwa inaiuzia USa magari lakini inakataa kununua ya USA, mpaka Clinton alipowalazimisha kununua kwa nguvu au atavunja mkataba, siku hiz Wajapan wananunua magari ya US wanayapeleka re-circle ndio maana ya mikataba ya Uchumi na biashara na Ajira, sio Wakenya wanakuja kwetu kuchukua ajira sisi hatuwezi huo sio mkataba mwema kwa Taifa!

- Ndio maana tunahitaji Wabunge imara huko EAC.

FMES!
 
- Ngongo nipo sana mkuu na heshima yako sana, ukweli ni kwamba Wananchi wengi hawajui hata kama kuna bunge la EAC, wacha hoja na ishus zenye utata huko, sasa swali linakuwa huko EAC tumekwua tukiwakilishwa na nani toka mwaka 1999 EAC ilipoanzishwa Rasmi na nchi tatu na 20007 baadaye zilipojiunga nchi zingine mbili?

- Sasa ukisoma hoja nyingi humu za kupinga Mkulu William kugombea kama akiamua kugombea, ni kumlinganisha na Mbunge gani wa huko EAC aliyewahi ku-raise any of these ishus za Ajira, Uchumi, na Forodha pamoja Siasa? Wananchi wa Tanzania wanahitaji kujua kila ishu ya huko EAC na interest yake wka Taifa lao, so ni lazima iwe moja ya mujibu wa Wabunge wetu tunaowapeleka huko, wapite wka wananchi na kuwaelimisha kuhusu EAC na pia hata kutafuta maoni ya wananchi kabla ya kuingia mikataba ya iana yoyote na members wengine wa EAC, ni more common sense kuliko matusi na kejeli ambazo hazina tija wka Taifa na wananchi, kwani wakati tunachafuana wenzetu wanapaiga plan za namna ya kufaidika na kuchafuana kwetu!

- Ningefurahi sana kusikia kuna member wa JF anayetaka kugombea nafasi ya uongozi wa Taifa maana yake ni moja tu kwamba JF ni strong instituion inayoweza kutoa Viongozi wa Taifa, lakini kukaa kuchafuana hapa tena kwa members wenyewe kwa wenyewe tunakuwa kama siasa za makundi zinazoikwamisha taifa letu, I mean JF anaposimama kutafuta uongozi tunatakiwa kumpa support kwa sababu kuingia kwake ni kuingia kwetu wote hapa, sometimes tujifunze kuangalia big picture people badala ya Short terms interests!

MUCH RESPECT!

FMes!
 
Mkuu wangu shukran sana lakini mimi hapa ni mmoja kati ya watu wanaopinga Umoja huu wa EAC kwa hatua ambazo tayari tumezifikia ilihali Tanzania haikujiandaa kwa lolote ktk ndoa hii. Kama ulivyosema kuhusu Kuvunjika kwa Jumuiya hiyo sisi tuliumia sana na sababu kubwa ni kwamba Tanzania haikuwa na viwanda cha kutengeza Siagi au sindano, kila kitu kilitoka Kenya yaani toka jikoni hadi hadi kalamu ya kuandikia shuleni au ofisini. Tanzania ilikuwa haiwezi kuuza kitu chochote zaidi ya mali ghafi tena hata Pamba, kahawa na Chai vilipelekwa Kenya na kurudi kwetu kama finished Product na tukinunua kwa bei ya juu..Sisi tulikuwa Consumer wakubwa wa mali za Kenya wakati hatuna cha kuuza kwao isipokuwa cash crops.

Na mtihani mkubwa alokuwa nao Nyerere ni kuanzisha viwanda vyetu wenyewe at least tuwe na kitu cha kuuza ndani na nje kuboresha Uchumi ktk mzunguko wa fedha na hakuna njia bora zaidi ya kuweka masharti kama ya kutoagiza mali za nje ili mali zetu zipate kununuliwa. Sasa toka nchi ambayo haikuwa na kiwanda hadi kuweza kujenga vichache ilikuwa kazi ngumu sana na adha kubwa ambayo Watanzania wengi walilaani Ujamaa japokuwa lengo lilikuwa kutuwezesha kujitegemea ktk mahitaji ya ndani. Kwa Wadanganyika waliozoea vya kunyonga tulilaaani sana Ujamaa badala ya kutazama kwamba uhaba na matatizo yetu yametokana na sisi wenyewe kutokuwa na vyanzo vya uzalishaji toka kutawaliwa.. Tanzania haikuwa daraja moja Na Kenya wala Uganda!

Tukaua Ujamaa na kuingia Ubepari lakini hadi leo hii hatuna viwanda, bado ni wahitaji wa mali kutoka nje na kibaya zaidi tunaagiza kutoka China na Ulaya. Hii Jumuiya ya EAC ni kufungua tena soko la Kenya kuja kwetu Tanzania sisi bado hatuna kitu cha kuuza kwao. Tunarudi ktk kukidhi mahitaji yetu japkuwa kiuchumi hatufaidiki..Free trade haiwezi kutusaidia kitu ikiwa sisi hatuna cha kuuza isipokuwa kutuwezesha kuagiza mali za Kenya ili kuficha adha za kutokuwa na viwanda kama ilivyomtokea Nyerere. Na nina hakika kuna mabillioni ya fedha tunapoteza ktk Utalii kwa sababu Mtalii hatakuwa na sababu ya kulipia mashirika ya Tanzania ambayo hayajulikani wala kujitangaza vyema nchi za nje. Kenya ndio watafaidika zaidi yetu wakati sisi tunazidi kuporwa hata kidogo tunachoingiza kiuchumi..

Na swala la Ajira, Haya sii makosa ya Kenya hata kidogo bali ni Ulimbukeni wetu sisi wenyewe kutaka watu wanaoongea kiingereza zaidi. Tuna kiharusi cha kupenda Foreigners hata awe Mzaire au MGhana maadam sii Mtanzania wa kuzaliwa..Ni makosa yetu sisi wenyewe pia kuwa matapeli, tumejaliwa kuishi kiujanja ujanja hata kazini tofauti na Mkenya anajua nidhamu ya kazi na hata siku moja elimu yake hawezi kuitumia kama silaha au msingi wa kubeza na majigambo isipokuwa ni nyenzo itakayomletea maisha bora lakini sisi watanzania kwa mtu yeyote aliyesoma hii ni silaha kwake ni kama amekabidhiwa bunduki na risasi za moto. Kwa mwajiri hii ni hatari kibiashara bora kumwajiri Mkenya anayefahamu maana na matumizi ya elimu.

Tunahitaji sana kujiandaa sisi wenyewe kuijenga Tanzania ambayo inaweza kushindana lakini sio kujiingiza ktk Jumuiya ilio mradi nasi tushiriki hata Hiyo Olimpiki wana kiwango cha kukimbia mita 100 kama huwezi kupata kasi ya dakika sijui 10 min/100m huwezi kushiriki..Sisi tunang'ang'aniza tu tushiriki. Watazame Wazambia leo wamechukua Ubingwa wa Africa, mnafikiri wameiweza kufika hapo walipo pasipo mhanga!..Eeehh! Sisi tumefanya nini baada ya kuingia Ubepari ama tumefanya nini kujifunza kutokana na makosa ya awali? - NOTHING!
 
- Bob point taken, nimekusikia sana na tupo one page sana bro!, I mean binafsi sina tatizo na Jumuiya lakini muhimu ni what is in it for us Taifa? Leo bajeti ya EAC ni USD $ 55, Million kutoka USD $ 28 Million ilipoanza Mwaka 1999, well swali langu ni what are we getting back Taifa to compare na what we contribute, ni lazima wananchi na Taifa zima wajue na ni kazi ya Wabunge wetu huko EAC!

- Na my outmost respect respect kwa mheshimiwa Leticia Nyerere kwa ujasiri wake.

MUCH RESPECT

fmES!
 
Safari that is not an-ishu hapa the ishu ni what is EAC na ni Wabunge wa aina gani tunataka waende huko? Hili la ID umelisema tayari kwamba unaaamini unachoamini meaning kwamba wewe ni Admin, sasa si uchukue hatua bro kuliko kuharibu mjadala muhimu kwa wananchi na Taifa?

Much REspect Bro!

FMeS!
 
- Bob point taken, nimekusikia sana na tupo one page sana bro!, I mean binafsi sina tatizo na Jumuiya lakini muhimu ni what is in it for us Taifa? Leo bajeti ya EAC ni USD $ 55, Million kutoka USD $ 28 Million ilipoanza Mwaka 1999, well swali langi ni what are we getting back Taifa to compare na what we contribute, ni lazima wananchi na Taifa zima wajue na ni kazi ya Wabunge wetu huko EAC!

- Na my outmost respect respect kwa mheshimiwa Leticia Nyerere kwa ujasiri wake.

MUCH RESPECT

fmES!
Mkuu wazungu wanasema Put your money where your mouth is! kama wewe unaamini hii Jumuiya ni kitu kizuri hakuna sababu ya kujiuliza hizo Usd 50m zinatufanyia nini wakati tumezitoa kama sadaka. We have nothing to sale mkuu wangu - NOTHING isipokuwa kurudisha undugu na urafiki baina yetu. Kama leo tunashindwa ku create ajira nyumbani unafikiri huko Kenya ndio itatusaidia vipi?..

Nyerere aliona mapungufu ya Jumuiya Kiuchumi tukauvunja lakini tukashindwa kuvumilia rumba kali, na bila kujirekebisha tumerudi palepale halafu mnataka kujua in return? Bila shaka tutadumisha undugu wetu, ujirani mwema kwa kuletewa vitu vya Kenya maana wao viwanda vyao havikufa, vyetu vilikufa tunawaongezea ajira na soko..It's Clear and simple!
 
- Bob no hizo hela ni za wote nchi Tano swalilangu ni zetu ngapi na tunarudisha ngapi? @ Mambo Jambo hapo kwenye green mimi sijui lolote bro!

REspect!

Es!
 
Kuna kipindi alikwenda jimboni kwa mzee wake kupima upepo kama anaweza kumuondoa LUSINDE naona alikuta mambo ni magumu sasa anaangalia jinsi ya kwenda huko EAC
 
Kuna kipindi alikwenda jimboni kwa mzee wake kupima upepo kama anaweza kumuondoa LUSINDE naona alikuta mambo ni magumu sasa anaangalia jinsi ya kwenda huko EAC

- Alikuta mambo magumu na huu ni Mwaka 2012 kuna Miaka 3 zaidi kufikia 2015 ni mingi sana kwenye siasa, anything can happen, kutembelea jimbo sio kugombea jimbo, ni mpaka mgombea atangaze ndio ina make a sense kumjadili mgombea! Uwe na amani sana bro, 2015 ni bado mbaaali sana a lot can happen! Usijiaminishe kihivyo cause hujui kinachoendelea ingawa unafikiri unajua!

- JF ninasema tujifunze ku-support another JF anapogombea nafasi za uongozi wa Taifa, akiingia ni plus kwa JF nzima najua tuna tofauti zetu za itikadi, lakini ifike pahali tujali Taifa kwanza, badala ya personalities na majina au Chama ndio maana ninasema Mh. Leticia ni jasiri sana na anahitaji heshima sana!

FMeS!
 
- Bob no hizo hela ni za wote nchi Tano swalilangu ni zetu ngapi na tunarudisha ngapi? @ Mambo Jambo hapo kwenye green mimi sijui lolote bro!

REspect!

Es!
Nakuelewa sana mkuu wangu... Ninachoshindwa mimi kukuelewa ni kwamba kama tullikuwa hatuna jibu, hatuhjafanya upembezi yakinifu kabla ya kujiunga inasaidia nini kuambiwa leo faida ya EAC?.. Binafsi yangu kama mchumi mbuzi ninawekeza fedha yangu pale nilipokwisha piga mahesabu na kuona faida gani naipata kiuchumi. Kinyume cha hapo ndio ile ya kuweka fedha pale ulipo mdomo wako - Kazi ya kanisa!.

Sasa nikitazama hii ya EAC, kusema kweli Tanzania tumewekeza fedha yetu ili kurudisha Ujirani mwema na it's more about Pan Africanism lakini kichekesho ni kwamba nchi zote hizi zimejiunga kutokana na kuiga UE ilihali kilichotakiwa kufanyika ni Pan Africanism ambayo ilikuwa na malengo tofauti kabisa ya Kijumuiya na yale ya Ulaya. Ni pamoja na kujenga nguvu ya Umoja hata ktk maswala na hoja za kimataifa..Ikiwa tunafikiria ni Biashara basi tumelewa na kuuvaa mkenge. Kwa hiyo upande mwingine nakupa tu sura nzima ya EAC ili hao kina (pale green) wajue tunakwenda wapi!
 
- Bob Siamini kwamba tumepotea na EAC, ninaamini kwamba tupo sawa ila marekebisho tu yanatakiwa na ni lazima tupelekea Strong MPs huko, wanaoweza kusimamia interest ya Taifa letu, badala ya siasa zaidi. Nina tatizo na Sarafu Moja na Free Movemment ya wananchi wa Members States kwenye hayo mawili ninasema we need to be very carefull ama sivyo tutaumia sana na pia la Ajira kwa maoni yangu halijakaa sawa linahitaji marekebisho, lakini yote yanajadilika!

- Binafsi ningependa kuona kamati maalum ya Taifa ya Bunge on EAC, ambayo ni independent na mchanganyiko wa vyama na Wabunge wetu EAc kurudi ku-report all the ishus back kwa Bunge on a special sessions ili kupata maoni ya Wabunge wetu wa Jamhuri, ambao siku hizi wamekwua makini sana na ishus za interest kwa wananchi na Taifa!

- Well, people naomba kuwaomba radhi kwamba sasa ninatoka, tutaonana tena soon!

FMeS!
 
Mkuu Es na Bob

Mnanikumbusha enzi zile wakati JF ilikuwa hoja kwa hoja tu, kulikuwa hakuna kupoteza muda kwenye mambo ya msingi.

Ni wakati sasa wa kuirudisha JF ilikotoka.

Kudos wakuu.
 
Back
Top Bottom