Wiliam Mgimwa unawajibika kwa IMF ama kwa watanzania?

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,320
Nimeona akipigiwa promotion na muwakilishi wa imf kana kwamba uchumi wetu umekua kwa 6.5 hadi 7.5, amejinasibu kupewa ushauri na mu-IMF huyo kuhusu utajiri wetu wa gas, ya kuwa tuweke sera, tutunge sheria n.k kuhusu gas.

Najiuliza, kwa nchi huru Tanzania, mambo haya ya wananchi, kumsikiliza mu-imf na kusahau kuwa ushauri huo ulitolewa bungeni na chadema, leo jitu zima kubwa kama vile linajisifia mbele ya mkewe eti limeshauriwa na muzungu nini cha kufanya, Nisaidieni, huyu waziri anawajibika kwa nani?
 
imf kazi yake kubwa ni kuwanyonya watu maskini kwa ajili ya kuwanufaisha matajiri, bahati mbaya watanzania wengi
hawajui pamoja na baadhi ya viongozi lengo hilo la IMF. Viongozi wanahamini for easy money badala ya kushirikiana na watanzania mijini na vijijini na kukuza uchumi ili kuongeza revenue kwa ajili ya kujenga nchi badala yake wameamua njia
nyepesi ya kupata pesa ni kupitia mikopo bila kuwa na plan yeyote ya baadaye ya kupunguza kutegemea mikopo.
 
Anawajibika kwa imf, ni kawaida kwa viongozi wa serikali ya ccm kuwajibika kwa vyombo vya nje badala ya watanzania.
Hata raisi kikwete anawajibika kwa hao hao wazungu sembuse waziri wake.
 
Ukitaja Mgimwa watu wanakumbuka hazina then mishahara yetu ambayo mpaka leo hajatulipa. Hayo ya Imf subiri kwanza watoto wapate kitumbua nyumbani.
 
Ukitaja Mgimwa watu wanakumbuka hazina then mishahara yetu ambayo mpaka leo hajatulipa. Hayo ya Imf subiri kwanza watoto wapate kitumbua nyumbani.

reflection ya ukuaji wa uchumi hauonekani kwenye maisha ya mtanzania, naona kama serikali imeamua kuyatumia mashirika ya fedha ya kimataifa kutuhadaa kwa kuifagilia baada ya mikakati yao ya kuwahadaa wananchi kupitia tbc kufeli.
 
Ukitaja Mgimwa watu wanakumbuka hazina then mishahara yetu ambayo mpaka leo hajatulipa. Hayo ya Imf subiri kwanza watoto wapate kitumbua nyumbani.

Ile 70% ya bajeti ya taifa, Matumizi ya Kawaida pesa zimeenda wapi? Mbona naskia kilio cha kuchelewa mishahara? Duh! Kweli sikio la kufa halisikii dawa, nani ataipigia kura CCM kama hali itaendelea kuwa hivi?
 
Viongozi wengi wa Africa wamekuwa vibaraka kwa nchi za magharibi, wanalewa sifa zinazotokana na kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Uwezo wa kufikiri kwao umefikia tamati na hawawezi kuona yaliyo nyuma ya pazia ya malengo ya wazungu. Wangekuwa na akili wangejiuliza kama hizi sifa zinamaanisha! Hawajatambua bado kuwa viongozi wenzao wanaosimamia maslahi ya nchi zao ndio wanaoonekana kuwa maadui wa nchi za magharibi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom