Wildebeeste wasusa migration, Tanzania watashindwa hii biashara?

chash

JF-Expert Member
Jun 5, 2012
548
230
Hivi majuzi Wildebeests (Nyumbu) walikatisha ziara yao ya miezi mitatu kule Mara na wakarudi kwao Serengeti baada ya wiki tatu tu. Haijulikani ni kwanini waliamua kukatisha hiyo ziara, ila inaelekea mabadiliko ya mazingira kule Mara inaweza kuwa Imechangia. Pamoja na nchi jirani kuendelea kulazimisha utunzaji bora wa mazingira kati ka Serengeti wameshindwa kufanya hivyo kwao. Inaelekea hata hapo mwanzo wanyama hao walikuwa hawajaaamua vizuri kuanza hiyo ziara kwa sababu walichelewa kutoka hadi ikasemekana moto uliowashwa na wasonjo wa Serengeti ndio uliowazuia kuondoka.

Sasa, kama hawa wanyama wataacha kabisa migration,( huo wasi wasi upo)
Masai mara starring into the face of disaster
Standard Digital News : Business : Masai Mara staring into the face of disaster

Watanzania wataweza kuwa wabunifu kuivuta biashara ya utalii kwa ajili ya wildebeest ije Serengeti au ndio basi watalii waliokuwa wanaenda kutizima hawa wanyama watafute sehemu nyingine ya kwenda? 'Mara' uingizia nchi jirani zaidi ya $20m kila mwaka kwaajili ya Wildebeeste wa Tanzania. Kazi ni kwenu Serekali na kampuni za kitalii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom