Wilaya za Tarime na Rorya hatarini kupelekewa utawala wa kijeshi

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Na Christopher Maregesi, Musoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameupa uongozi wa Mkoa wa Mara muda wa miezi sita kuanzia leo ili kuwasilisha mpango mkakati wa kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika Wilaya za Tarime na Rorya, vinginevyo serikali italazimika kuunda mkoa maalumu wa kijeshi katika wilaya hizo.

Akihutubia wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya serikali za mitaa kilichofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mukendo mjini hapa, Waziri Mkuu alisema mapigano yanayoendelea katika wilaya hizo, yanatia aibu huku serikali ya Mkoa ikiwa imenyamaza bila kuonyesha namna yoyote ya kutatua tatizo hilo.

Pinda alisema endapo uongozi wa mkoa utashindwa kuliondoa tatizo hilo katika kipindi hicho, serikali italazimika kuunda mkoa maalumu wa kijeshi na kwamba utaongozwa na Jenerali wa jeshi.

Alisema lengo kuunda utawala wa aina hiyo ni kurejesha amani miongoni mwa Watanzania.

Pinda alizitaka Halmashauri za wilaya hizo mbili kutokwepa jukumu la kudumisha amani na aliwataka watendaji wengine wilaya hizo, kushiriki kikamilifu katika kumaliza tatizo hilo.

“Ni jukumu la serikali za mitaa kukuimarisha amani na utulivu katika maeneo yao, zikiwemo Halmashauri za Tarime na Rorya, hivyo hakikisheni mnarejesha amani hiyo katika maeneo yenu vinginevyo tutazifuta,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu hadi kufikia jana maiti 32 zilikuwa zimeokotwa porini, nyumba 400 zimechomwa moto huku watu 3000 wakikosa mahala pa kuishi kufuatia mapigano yaliyozuka Juni 25, mwaka huu kati Wajaluo walioko wilayani Rorya na Wakurya wilayani Tarime baada ya kuibiana mifugo.

Mapigano hayo yalianza Juni 25, mwaka huu na kuhusisha wakazi wa kata za Kitenga na Kwisarara, ikidaiwa kusababishwa na wizi mkubwa wa mifugo, unaofanywa na makabila ya Wakurya na Wajaluo.

Kutokana na hali hiyo, timu ya viongozi wa ngazi ya taifa, akiwamo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki, Kamishna wa Polisi Kitengo cha Operesheni Taifa, Paul Chagonja, IGP Said Mwema na maofisa kadhaa wa polisi mkoani Mara, walilazimika kwenda eneo la mapigano hayo kwa helikopta.

Mkoa wa Mara umekuwa na matukio mengi ya mapigano ya koo na kikabila mara kwa mara na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya watu pamoja na uharibifu wa mali.

Miongoni mwa mapigano ambayo hayataweza kusahaulika ni kati ya koo za Warenchoka na Waanchari ambayo pia yaliwalazimisha baadhi ya viongozi wa kitaifa kuingilia kati ili kusuluhisha.

source: Mwananchi Read News
 
kwa hiyo sasa watu wanapewa miezi sita wamalizane kwa kuchinjana au?
 
Mimi nimewahi kushuudia LIVE hayo mapambano.

Kabla ya kwenda kupigana kuna imani za kishrikina zinaingizwa. Watu wanajiandaa kwenda vitani kama kwenye movie za Mel Gibson za kivita za zamani. Tofauti kubwa ni kuwa wanapigana bila mpango wala mbinu maalum.

Hivi vita vimekuwa haviripotiwi tu lakini vipo tokea zamani na zinajulikana wazi kabisa.

Utawala huu umevipa uhuru zaidi vyombo vya habari ndio maana mnavisikia.

Zamani ilikuwa inasemwa ya waanchali na walinchoka (nimekosea spelling) tu lakini VITA VYA WAKURYA NA WAJALUO NI VYA KIJADI. Vilikuwepo na vinaendela.

Sababu kubwa ni Kuibiwa ng'ombe. Sitaki kuwa biased lakini si vita vya kuIBIANA bali kuibiwa. Nikiwa na maana ya kabila mmoja kuiba ng'ombe mara kwa mara za kabila nyingine.

Na hii ilianza zaidi baada ya Vita vya Kagera ambapo watu walirudi na silaha.

Jamani pamoja na yote, ALYATONGA MREMA sijui alikuwa na mbinu gani, lakini alisuluhisha migogoro na kumaliza hivi vita. Huyu jamaa ni simply waziri wa mambo ya ndani kwa kuzaliwa.
Sio huyu brother man wa sasa.

Yangu machache hayo

FP
 
Na Christopher Maregesi, Musoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameupa uongozi wa Mkoa wa Mara muda wa miezi sita kuanzia leo ili kuwasilisha mpango mkakati wa kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika Wilaya za Tarime na Rorya, vinginevyo serikali italazimika kuunda mkoa maalumu wa kijeshi katika wilaya hizo.

Akihutubia wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya serikali za mitaa kilichofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Mukendo mjini hapa, Waziri Mkuu alisema mapigano yanayoendelea katika wilaya hizo, yanatia aibu huku serikali ya Mkoa ikiwa imenyamaza bila kuonyesha namna yoyote ya kutatua tatizo hilo.

Pinda alisema endapo uongozi wa mkoa utashindwa kuliondoa tatizo hilo katika kipindi hicho, serikali italazimika kuunda mkoa maalumu wa kijeshi na kwamba utaongozwa na Jenerali wa jeshi.

Alisema lengo kuunda utawala wa aina hiyo ni kurejesha amani miongoni mwa Watanzania.

Pinda alizitaka Halmashauri za wilaya hizo mbili kutokwepa jukumu la kudumisha amani na aliwataka watendaji wengine wilaya hizo, kushiriki kikamilifu katika kumaliza tatizo hilo.

“Ni jukumu la serikali za mitaa kukuimarisha amani na utulivu katika maeneo yao, zikiwemo Halmashauri za Tarime na Rorya, hivyo hakikisheni mnarejesha amani hiyo katika maeneo yenu vinginevyo tutazifuta,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu hadi kufikia jana maiti 32 zilikuwa zimeokotwa porini, nyumba 400 zimechomwa moto huku watu 3000 wakikosa mahala pa kuishi kufuatia mapigano yaliyozuka Juni 25, mwaka huu kati Wajaluo walioko wilayani Rorya na Wakurya wilayani Tarime baada ya kuibiana mifugo.

Mapigano hayo yalianza Juni 25, mwaka huu na kuhusisha wakazi wa kata za Kitenga na Kwisarara, ikidaiwa kusababishwa na wizi mkubwa wa mifugo, unaofanywa na makabila ya Wakurya na Wajaluo.

Kutokana na hali hiyo, timu ya viongozi wa ngazi ya taifa, akiwamo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki, Kamishna wa Polisi Kitengo cha Operesheni Taifa, Paul Chagonja, IGP Said Mwema na maofisa kadhaa wa polisi mkoani Mara, walilazimika kwenda eneo la mapigano hayo kwa helikopta.

Mkoa wa Mara umekuwa na matukio mengi ya mapigano ya koo na kikabila mara kwa mara na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya watu pamoja na uharibifu wa mali.

Miongoni mwa mapigano ambayo hayataweza kusahaulika ni kati ya koo za Warenchoka na Waanchari ambayo pia yaliwalazimisha baadhi ya viongozi wa kitaifa kuingilia kati ili kusuluhisha.

source: Mwananchi Read News

Poor governance practices, that's all. Never on earth has militarism resolved similar governance problems to reinforce and promote democracy. Shame upon Pinda's face. Shame upon CCM top leadership. Shame, shame, shame... shame!!
 
While I do not advocate militarism per se as put, one might be tempted to think that a cosy talk with Hitler might have avoided world war II.People often forget that the peace maintained in many parts of the world was attained through blood, sweat and tears.The American civil war was brutally put down just as the Igbo rebellion in Nigeria.
We have much to learn from history.
 
Last edited:
Pinda naona naye kachemka. Hivi anadhani mabavu yanasaidia kuondoa tofauti? awaulize waisrael na wapelstina, awalize wamarakani na virtnam, afghanstan, iraq, somalia etc.
sijui huyu uwaziri mkuu kaupata vipi. Hata kama wakitumia mbinu zao za ushushu na kikwete I dont think ni muafaka. Je Hilo jeshi litakaa madarakani for how long? Kama ndiyo viongozi wetu wa karne ya 21 wanasuluhisha matatizo kwa bunduki Tumekwisha!!!!! Pinda wake up! hakuzomewa tu!!! MABAVU, VITISHO, KUTOKUJIAMINI, UELEWA KIDOGO hayo ndiyo matokeo yake!!!! That is the proof alichotapika musoma.
 
Sasa kama wakishaanza kufikria jeshi safi sana na wao wakishindwa pale juu na jk wake wwapishe jeshi...kwanza wanangoja nini???wameshashindwa wanaiba na kulisingizia jeshi ni aibu sana sana....jeshi linafanya nn jamani?
 
Poor governance practices, that's all. Never on earth has militarism resolved similar governance problems to reinforce and promote democracy. Shame upon Pinda's face. Shame upon CCM top leadership. Shame, shame, shame... shame!!

Mkuu mimi naona kama serikali inakwepa jukumu lake kwa wananchi kwa kutaka kulitupia hili swala jeshi. Siamini kama wameshindwa njia zote mpaka atoe tamko hili. Tatizo huyu mtoto wa mkulima nae sijui kawaje kawaje. Yani anatoa kauli za ajabu mpaka mtu utashangaa. Ndiyo tatizo la mtu kupewa cheo ambacho hakutegemea kukigusa maishani mwake.
 
tunachosahau ni kwamba vita kama hivi havitaisha kwa kuhubiri majukwaani wala kuwapa baadhi ya watu deadlines. pia tabia ya tulio wengi kuangalia jambo kwa upeo wa juujuu na outcomes kama hizi za vita. kila litokealo lina chanzo chake na kwa mtazamo wetu inaweza tuchukua hata miaka mia bila utatuzi hata tukipeleka jeshi kwani ndo kwanza watakuwa wamesogezewa silaha karibu. let's look on the background and try to resolve from the source and not the end. ukiwauliza hawa ndugu zetu utaambiwa vifo hadi sasa ni UNDEFINED!!
 
Kwani ni mifugo tu au kuna la ziada kati ya hizo koo?? Mbona kila kukicha tunaona vita vita mishale au vipi
 
..hakuna haja ya kusubiri miezi sita.

..tumepeleka wanajeshi wetu Comoro, kwanini tushindwe kuwapeleka Tarime na Rorya?
 
yes twaweza peleka majeshi yetu as part of management by crisis BUT will it be a permanent solution?
 
Back
Top Bottom