Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wikienda: Penzi ni kama nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 12, 2010.

  1. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #1
    Mar 12, 2010
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 30,346
    Likes Received: 2,295
    Trophy Points: 280
    Nashika tena kalamu
    Niseme lilo muhimu
    Ya lile lenye utamu

    Penzi ni kama ua
    likichanua
    Nyakua!

    Niseme vipi na nene
    Kwa dufu tena ninene,
    Mwenye macho na aone

    Penzi ni kama barua
    Huitaji kurarua
    Fungua!

    Ya nyonda'angu niseme
    Nikishindwa niheme
    Vinginevyo nihame

    Penzi ni kama tunda
    Ukilipenda
    Panda!

    Ya'rabi wangu jalia
    Mja wako saidia
    Na moyo uje tulia

    Penzi ni kama gilasi,
    Ukipewa kiasi
    Usiasi!

    Mtima wangu tetema
    Umepewa sasa tama
    Kama maji tuwama

    Penzi ni kama upepo
    Likiwepo
    Ni pepo!

    Ya konde tena nang'onda
    Penzi nimelipenda
    Sasa nayeya na nyonda!

    Penzi kama maji,
    Yupo mpaji,
    Usihoji!

    Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
     
  2. Preta

    Preta JF-Expert Member

    #2
    Mar 12, 2010
    Joined: Nov 28, 2009
    Messages: 23,719
    Likes Received: 2,070
    Trophy Points: 280
    wonderful
     
  3. PakaJimmy

    PakaJimmy JF-Expert Member

    #3
    Mar 12, 2010
    Joined: Apr 29, 2009
    Messages: 16,234
    Likes Received: 96
    Trophy Points: 145
    I wish!
     
  4. FirstLady1

    FirstLady1 JF-Expert Member

    #4
    Mar 12, 2010
    Joined: Jul 29, 2009
    Messages: 16,199
    Likes Received: 100
    Trophy Points: 160
    Binamu una wish nini??
     
  5. FirstLady1

    FirstLady1 JF-Expert Member

    #5
    Mar 12, 2010
    Joined: Jul 29, 2009
    Messages: 16,199
    Likes Received: 100
    Trophy Points: 160
    Hongera Mwanakijiji watu mna fani mbali mbali...
     
  6. Lily Flower

    Lily Flower JF-Expert Member

    #6
    Mar 12, 2010
    Joined: Oct 16, 2009
    Messages: 2,561
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 0
    Very good poem.
     
  7. Fisherscom

    Fisherscom JF-Expert Member

    #7
    Mar 12, 2010
    Joined: Mar 13, 2008
    Messages: 1,072
    Likes Received: 26
    Trophy Points: 145
    Thanx mkuu,ujumbe mzito huo.
     
  8. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #8
    Mar 12, 2010
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 30,346
    Likes Received: 2,295
    Trophy Points: 280
    hope your Friday is merrier
     
  9. Regia Mtema

    Regia Mtema R I P

    #9
    Mar 12, 2010
    Joined: Nov 21, 2009
    Messages: 2,975
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 0
    Daa,kweli my friday will be murua.Mwanakijiji sikuwezi duu,shairi zuri lakini pia umeniacha hoi jinsi ulivyolipanga,hapo katikati..Aisee uishi mpaka miaka 140....
     
  10. C

    Canady Member

    #10
    Mar 12, 2010
    Joined: Jan 1, 2009
    Messages: 10
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    napenzi ya wikiend ni mapenzi ya kudanganyana tuu kwani mapenzi yahajui time or period, ni kitu hakina mwisho na kila siku nimapya .
     
  11. Baba_Enock

    Baba_Enock JF-Expert Member

    #11
    Mar 12, 2010
    Joined: Aug 21, 2008
    Messages: 6,724
    Likes Received: 58
    Trophy Points: 145
    MKJJ

    Nimefurahishwa sana na "shape" ya mashairi

    Kama hii vile[​IMG]!!!
     
  12. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #12
    Mar 12, 2010
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 30,346
    Likes Received: 2,295
    Trophy Points: 280
    peke yangu!?
     
  13. Regia Mtema

    Regia Mtema R I P

    #13
    Mar 12, 2010
    Joined: Nov 21, 2009
    Messages: 2,975
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 0
    Na watakao kuwa duniani kwa wakati huo.watakuwepo wengi tu,watoto wangu na wengine kibao.
     
  14. Ben Saanane

    Ben Saanane Verified User

    #14
    Mar 12, 2010
    Joined: Jan 18, 2007
    Messages: 14,571
    Likes Received: 3,279
    Trophy Points: 280
    -Shairi tamu sana.Big up bro!
     
  15. H

    Haruna JM Sauko Member

    #15
    Mar 20, 2010
    Joined: May 17, 2008
    Messages: 24
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Hongera mwanakijiji kwa kutongoa vyema, tenzi zimetulia haswa
     
Loading...