wiki ya miti na sokoine university!

julius deya

New Member
Apr 7, 2012
2
1
hello!
mwaka uliopita 2011, Africa ilipoteza mwanaharakati wa Mazingira aliepumzishwa ili aweze anza safari yake ya pili kwa namna ambayo ni ya kirafiki dhidi ya mazingira.
Prof. Wangari M. mwanamazingira toka nchin Kenya na mshindi wa tuzo ya Oscar alifariki dunia na mwili wake kuchomwa moto kisha majivu yake kuzikwa jijin Nairobi katika nchi ya Kenya.
Enzi za uhai wake, marehemu alikuwa kifua mbele kutetea na kuhifadhi mazingira kwa ujmla huku akisisitiza zaidi kwenye upandaji miti.
leo chuo kikuu cha Sokoine kimeanza upandaji miti katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji mjini Morogoro na vitongoji vyake, zoezi hilo limefuatia huku kukiwa na usitiswaji wa baadhi ya ratiba chuon hapa ili kuweza fanikisha zoezi zima la upandaji miti. Zoezi hilo linalosimamiwa na kitivo cha Misitu na uhifadhi limepata utekelezaji chanya kupitia wanafunzi wa sokoine university pamoja na staff.
Afrika tuamke, tusimamie mazingira pamoja na uhifadhi wake kwa manufaa yetu ya sasa, baadae na vizazi vitakavyofuata. sote kwa pamoja tumuenzi Prof. Wangari kwa kupanda miti.
R.I.P Prof. WANGARI M.
 
Hongereni wasuaso..ila upandaji wenu wa miti wa kuchimba shimo na kuzamisha mizizi sio mzuri..fuateni kanuni za upandaji miti..
 
hongereni ila siku ya panya au nyuki lini?nataka kuja kuona ujuzi wenu kwenye hayo mambo nimesikia mnasomea na mnafuga
 
Prof. Wangari M. mwanamazingira toka nchin Kenya na mshindi wa tuzo ya Oscar alifariki dunia na mwili wake kuchomwa moto kisha majivu yake kuzikwa jijin Nairobi katika nchi ya Kenya.

Kumbe Profesa Wangari aliwahi shinda tuzo ya Oscar? Alicheza filamu gani? Sina ufahamu na hilo naomba kufahamishwa maana mi nilidhani alishinda tuzo ya Nobel.
 
Hongereni sana wasuaso. Msiwasikilize kina prakatatumba wakiwakebehi, someni hayo makitu ndo yana soko siku hizi! Kila siku wahasibu hapa wanalia wamekaa bila ajira miaka 3. Wahitimu wa SUA hawadodi, japo hata u-clerk bank ikishindikana kabisa.
 
king'asti kwan we hutaki kwenda kuona wataalamu wetu wa degree ya panya, maua, wanyama?we unataka miti tuuu
 
Back
Top Bottom