Wiki moja kabla ya Machozi... Zitto???

mwanakijiji,if you had been in the STALIN era,definately,definately you would have been exiled to SIBERIA

Haswaaa,.... na siku atakapoanza kuwaliquid tu nitajua kuwa tayari ameshaingizwa kwenye system.... au kapata fitisho

Hahaha keep it up mwanakj. endeleza vita vya kuilinda nchi yetu dhidi ya magaidi
 
Widcard, nimeipata point yako, kelele zote za buzwagi mkataba uko palepale!

Kuna kampuni moja ya ulinzi wanambwa wakubwa na wakali kweli, wakati wanaenda lindoni wanabweka njia nzima tena wanakera kweli, hebu watizame wote wamevalishwa mask! hawawezi kung'ata kamwe!

Hebu tumuulize zitto tangu awe M/kiti wa POAC kafanya nini? sanasana akiongea watu wanaangua kicheko. Tulinganishe utendaji kazi wa Uhuru Kenyatta alivyokuwa M/kiti wa PAC na huu wa zitto.
 
Maoni yangu ni kwamba Mh. Zitto anakubalika vizuri tu ndani ya CCM na Serikalini pengine kuliko hata huko CHADEMA kwenyewe! Aliupigia kelele mkataba wa Buzwagi, bado upo na unatekelezwa kama ulivyosainiwa kule London. Saana ulimpa nafasi kufaidi posho kwenye tume ya Bomani.

Mkuu heshima mbele, siku moja watoto wetu watatuuliza vipi mbunge mmoja nasikia aliweka ukweli wazi kuhusu ubovu wa mikataba ya madini hasa wa Buzwagi, je nyinyi wananchi mlifanya nini baada ya kujua hayo?

I hope tutakuwa na majibu, si umewaona watoto wa siku hizi walivyo aggressive?
 
Mkuu FMES,
Nguvu yetu tulidhani tumeihamishia BUNGENI kwa tuliowachagua. Bahati mbaya Wabunge karibu wote wako pale kusubiri TEUZI za Rais kabla au baada ya kumaliza kipindi chao cha UWAKILISHI.
 
I wish Tanzania na Watanzania tungechukua mfano wa Ufaransa na kuwa kama raia wa huko. Kwa kila kitu ambacho wananchi hawajaridhika nacho ni Demonstration kwa migomo na maandamano...

Watanzania tunaishi katika Riwaya... Inanifanya nikumbuke KUSADIKIKA. Tunaumizwa na kushuhudia Nchi ikiwa ina wadau wachache na tunabaki tukifurahia tu kama Washabiki wa Mpira wa Miguu wakiangalia mechi...tena sio za ndani hapa Tanzania bali zile za nje kama Premier League (UK), Bundes (German). Tumekuwa Washabiki wa Maangamizo yetu wenyewe.

"BE THE CHANGE YOU WANT TO SEE"
 
Bahati mbaya Wabunge karibu wote wako pale kusubiri TEUZI za Rais kabla au baada ya kumaliza kipindi chao cha UWAKILISHI.

Mkuu WildCard,

Heshima tena, unajua mimi na umasikini nimekuwa na tabia ya kuwapeleka watoto wangu kwenye sehemu muhimu za kihistoria ya nchi yetu, na hasa mbuga za wanyama every other summer, na sasa hivi ninapoandika wapo huko sasa nikiongea nao kwenye simu huwa wananiuliza one big question kwamba Dad how come huku kwenye mbuga za wanyama kuna wazungu tu wabongo ni wafanya kazi tu? Huwa ninawajibu kuwa at least you guys sio wazungu ni wabongo, mbona na nyinyi mko huko?

Sasa my point ni kwamba, at least kuna baadhi ya viongozi wetu kama Zitto, huwezi kuwaweka kwenye hilo kundi la kungojea kuteuliwa na rais, n hata wakiteuliwa kazi zao hujisema zenyewe ni kwa ajili ya manufaa ya taifa na wananchi, kwa mfano kazi zilizofanywa na wabunge kama Mwakyembe na Zitto, through hizo kamati si zinajulikana as opposed na kazi za Said Mema na Hosea kwenye kamati kama hizo? Halafu kuteuliwa kwenye kamati ukiwndani ya bunge, ni moja ya responsibility za ubunge anyways, the question hapa kwa hoja yako inapaswa kuwa nini the results ya kuteuliwa kwao kwenye hizo kamati,

Hoja ngu ya msingi hapa ni kwamba si viongozi wote waliooza, na sio kweli kuwa taifa letu zima limeoza, hata kwenye vitabu vya dini Mungu alipoamua kuiangamiza Sodoma, bado kulikuwepo na watu credible kama Mkulu Lot na Noah, ambao aliwa-save kwanza kabla ya soo kuanguka,

Viongozi kama Zitto, tunatakiwa kuwaheshimu sana kwa sababu bila wao, can you imagine kina Rostam wangekuwa wanatufanya nini wananchi wa bongo? I understand your point lakini sio applicable kwa baadhi ya viongozi kama Zitto.

Ahsante Mkuu
 
Na ndio maana mimi nadhani tutafute namna ya kulibadili BUNGE letu. Akina ZITTO, MWAKYEMBE,... wako wengi tu NCHI hii. Taarifa walizozitumia kina Zitto walipewa na Watanzania wenye mapenzi mema kwa NCHI yao.
 

Mag3

ungekuwa Na Busara Japo Kidogo Ungeniuliza Kwa Nini Nimeona Chadema Walikuwa Na Jukumu Na Bado Wana Jukumu La Kulinda Japo Wabunge Wao. Lakini Nitakusamehe Maana Inaonyesha Uwezo Wako Wa Kufuatilia Mjadala Ni Mdogo.

Nitakuelimisha; Chadema Walishaomba Ulinzi Kwa Igp Sio Mara Moja Na Wala Sio Mara Mbili, Sijawahi Sijawahi Kusikia Chadema Wakishukuru Kwa Kupatiwa Ulinzi; Hii Inaonyesha Kwamba Labda Hawakupewa Au Walikubaliana Na Utaratibu Mwingine Kufuatia Ombi Lao. Vyovyote Kati Ya Hayo Ni Jukumu La Chadema Kuhakikisha Wabunge Wao Wako Salama Iwapo Watalindwa Na Dola Kwa Mujibu Wa Katiba Au Sungusungu Kwa Mujibu Wa Jadi.!! Siasa Ni Mchezo Mchafu; Chadema Inajua Hilo Lakini Wamefeli Mtihani.

Wewe Unailaumu Serikali Kwa Lipi Hapa Je Kwa Marehemu Ambaye Ni Mbunge Kupanga Safari Na Kijana Asiyemjua, Asiye Na Leseni, Aliyeendesha Kasi Au Unalaumu Serikali Kwa Sababu Mapenzi Yako Kwa Chadema Yanakufanya Uwe Mvivu Wa Kufikiri. Majukumu Ya Chadema Ni Yapi Kwenye Usalama Wa Chama Na Viongozi Wake...???

NIMESEMA SIASA NI MCHEZO MCHAFU...CHADEMA HAWATAKI KUJIFUNZA LILE JIMBO KWA SASA NDIO KUSEMA LIMESHARUDI KWA CCM. SASA NANI NI ZUZU HAPO CCM AU CHADEMA?? RUDI DARASANI UKAELIMIKE.

Yebo,
Heshima kwa mbele. Pia soma PM yako..
Sasa ukija kwenye issue ni kwamba, usalama wa mtu hata nchi za watu ni kitu ambacho siku zote kiko chini ya SERIKALI YA NCHI HIYO. Hivyo vyombo vua usalama HULIPWA NA KODI YA WANANCHI. Wananchi hao kwa Tanzania si CCM tu ila hata wasio na chama / wote walipa kodi. Kwa hali hiyo nafikiri Tanzania SI RUHUSA kuwa na kijeshi chako. Haya yalishaanza na Al-qaid wakaanzisha jeshi lao la usalama. Nafikiri lilikuja kuvunjwa. CUF pia walionywa juu ya kuanzisha jeshi lao. Ina maana hata CHADEMA hawawezi.
Pia ni kwamba ukiona USALAMA wako uko HATARINI, basi hata wewe UNAHAKI ya kwenda POLISI/UWT na kuwaomba wakupatie USALAMA. Wakikupatia si wajibu wako kwenda na KUWASHUKURU kwa kukupa usalama. Hivi wao wanapochukua MISHAHARA inayotokana na KODI zetu na hata KUTESA kwa pesa hizo, huwa wanakuja na kusema ASANTENI?? Kama wangelikuwa POLISI wa nchi nyingine, hapo sawa. Au uko nchi za watu na ukapotea MSITUNI na wakaja kukutafuta wazee kwenye VOLVO, hapo inabidi wakikupata useme ASANTE, kwani si wewe unawalipa.
Kwa mwenendo wa Wangwe, niaanza kupata wasiwasi kuwa alikuwa anakula kotekote. Na wewe unajuwa kabisa SIASA na MAFIA ni DUGU moja. Ukiwa POLISI na ukashirikiana na MAFIA basi dawa yako ni moja - 6 feet B.G.L. Mwendendo wa Wangwe hakuna aliyetegemea kuwa atakuwa HATARINI kupoteza maisha. Labda yeye mwenyewe ilitakiwa kujua kuwa KACHEZA RAFU na hivyo MAFIA watamtembelea na ANGELIOMBA mwenyewe ULINZI. Kwa katia yetu ilivyo, RAIS ndiyo BOSS wa kila kitu. Yeye aanateuwa WASAIDIZI tu kuanzia PM hadi mahakimu, serikali na taasisi zake zote, mwenyekiti wa Chama Cha MAFISADI, Amiri jeshi na Mkuu wa nchi, mume na baba, boss wa ...... Sasa kwa madaraka haya, kila kitu kikitokea, LAWAMA NI KWA SERIKALI na BOSS wake ambaye ni RAIS. Kama CCM hawataki lawama basi WAPIGANIE katiba ibadislishwe na RAIS apunguzwe madaraka kwa kiasi kikubwa. Hapo lawama na Majukumu yatagawanyika.
 
Huu unaweza kuwa uzushi, lakini kama ndivyo hivyo, naamini Zitto, ambaye naye yumo humu jamvini, na naamini ameshasoma thread hii, angekuwa ameshakanusha hadi hivi sasa.
wandugu, tupime mambo yanayotokea nchini na kwa hakika tutabaini kuwa mengi hayatokei kwa bahati mbaya au coicidence.
Wakati RA anazungumza na wahariri kujibu shutuma dhidi yake kuhusiana na sakata la KKKT Kinondoni alitaja kuwepo kwa kundi la watu maarufu katika jamii, linalotumia uwezo wao kuwachafua wengine.
Nilidhani kuwa Criminal Investigation Department wangeichukua kauli hii na kuanza kuifanyia kazi. Nimefuatilia Polisi mapema wiki hii, nawahakikishia kuwa Polisi wameichukulia hiyo kama "Kauli ya Kisiasa"-ndivyo walivyonijibu.
Leo, zinapotolewa habari kama hizi na kuhusishwa na 'organized crime gangs' may be we can connect the dots kwa kujiuliza;
1. Iwapo genge linalozungumziwa leo linauhusiano wowote na kundi alilolitaja RA?
2. Kwa nini Polisi wameiona kauli ya RA kuwa ni "kauli ya kisiasa"
3. Hivi ni kweli kuwa Zitto ana kiu ya umaarufu kiasi cha kuplot haya yote?
4. kwa nini kuna maswali mengi nyuma ya kifo cha Wangwe?
Tukiacha kuchukulia kila kitu kirahisi rahisi, tutabaini mengi yaliyojificha chini ya uzio mwepesi ambao unaweza kuondolewa kwa kuparuza tu bila kuhitaji nyundo au buldoza kubomoa ukuta wa zege
 
Kumbuka hata ile ajali ya Salome Mbatia ilikuwa imemlenga Zitto, maana siku hiyo Zitto alisimama sehemu kukata kiu kidogo na kwa bahati mbaya/nzuri salome akawa anapita kuelekea uelekeo huohuo na kwa vile magari yao yalifanana basi jamaa wakammaliza Salome wakidhani ni Zitto. Ndo maana Zitto akawa miongoni mwa watu wa kwanza kuona ile ajali.
 
Kwa hali tuliyofikia katika nchi yetu nafikiri kuna haja ya kupeana mafunzo ya self-defence. That is how much the incompetence of a government can be costly! Wananchi, na hasa wana CCM, sasa waanze kuona umuhimu wa kuchagua viongozi makini na wenye uwezo, badala ya kukimbilia watu waliojifika sifa wasizo nazo na kupachikwa uwezo ambao hawakuwa nao.

Ok, michango ya baadhi ya watu hapa inatisha, na inaonyesha mambo matatu: Ama

i) pamoja na kupata vielimu vya darasani, inaonekana baadhi yetu bado tu wa jinga kwa kiwango cha kutisha kuhusu elimu ya siasa, kiasi kwamba hata kazi za msingi za serikali hatuzijui!

au​

ii) Baadhi ya watu humu wana wivu na chuki ya kutisha kwa mafanikio ya baadhi ya wanasiasa wetu. Inaonekana watu wakipata mafanikio huwa wanahuzunika sana, na wakikosea kidogo wanafurahi mno. Na sijui nani aliwaambia kwamba ukifanya vizuri na ukawa shujaa basi huwezi hata siku moja kukosea. Na nani aliwaambia kwamba ukikosea mara moja basi inafuta mazuri yote uliyoyafanya nyuma na unayoweza kuyafanya huko mbele? Watu wengine kaputi kabisa katika fikra!

au​

iii) yote hapo juu.
 
Baadhi yetu TUNAHUKUMU kupita kiasi hasa anapoguswa mpendwa/mtakatifu wetu katika SIASA.
 
Wakati wa zoezi la kutafuta mgombea ndani ya CCM 2005 linaendelea na kuchafuana kukiwa katika kiwango cha juu Sumaye alisema " Ukiona mtu anatumia kalamu (magazeti) kuchafua wenzie kwa gharama kubwa ujue akiwa madarakani anaweza kutumia risasi badala ya kalamu".
Naanza kuamini kauli ile.
 
Tujue kwanza maadui wa ZITTO ni akina nani???????ndo hapo tuanze kuchambua hoja moja baada ya nyingine..je Adui wa ZITTO ni Karamagi?au RA?au EL?lazima tuwafahamu ndo itakuwa rahisi kuwamulika lakini tukiendelea na bla bla za labda tutakuja kushtuka tumempoteza hivi hivi kiutani utani.
 
Wiki moja kabla ya kifo cha Wangwe habari ziliingia kwa njia ya sms zikiwa na ujumbe uliokuwa unamaudhui yafuatayo "tumempoteza mpambanaji mwenzetu Zitto"! Ujumbe huo ulikuwa ni kutaarifu juu ya kifo cha Zitto aliyekuwa safarini Kenya wakati huo.

"Ka Nzi" ka KLHN ambako hakatii kanuni ya muda kameweza kurudi nyuma hadi masaa machache baada ya Zitto kupanda ndege kwenda Kenya; Watu watatu walikuwa wanamfuata. Aligundua anafuatwa walipofika Kenya kwani watu hao walionekana Airport na baadaye Hotelini. Na hata siku ya sms alipokuwa Mombasa watu hao walionekana tena. Zitto aliamini kuwa ni watu wa usalama wa taifa letu (siyo kitu kigeni kufuatwa kama ulinzi). Hakuna na shaka.

Hadi pale sms ilipotumwa ikiwa na taarif hiyo na kwa hakika habari zilikuwa ziendane na ajali. Bahati nzuri (mbaya kwao) ujumbe ulitumwa kabla ya tukio na hivyo alipopigiwa simu kuulizwa kama ni mzima alishangaa kuulizwa kwani alikuwa ni mzima kabisa. Ndipo ika "click". Imetonywa toka vyanzo ndani ya wana usalama kuwa Zitto alipiga simu kuulizia kama kuna "tail" ya UwT na akaambiwa la hasha hakukuwa na mtu/watu waliotumwa na taasisi hiyo kumpatia ulinzi au kumfuatilia.

Mara moja mipango ya kurudi Tanzania haraka ikafanywa na kubadilisha itenerary yake kwa kutumia kile ambacho kinaitwa kama "diversion measures" na kuweza kumrudisha Zitto Tanzania salama na kuevade potential threat. Mtu mmoja aliyeshiriki katika kuhahakisha Zitto anarudi salama na kupewa Ulinzi alitamka kwa uhakika sana "Hawa jamaa wanataka kuua mtu, hatujui ni nani".

Taarifa hizi zilipelekwa kwa IGP na Rashid Othman (refer barua ya Mnyika). Kiongozi ambaye inaonekana alikuwa the most vulnerable. Ni sawa na ndege aliyepweke ndiye mwenye kupigwa na manati! na kama Mbugani ni mnyama dhaifu na anayeenda peke ni rahisi kutafunwa na simba.

Vyanzo hivyo vinanong'oneza kuwa ya Zitto ingekuwa ni ajali iliyotokea nje ya nchi na hivyo almost impossible to associate na foul play. Na kwa maoni ya vyanzo hivyo isije kushangazwa kuwa jambo kama hilo linatokea nje ya nchi (hasa nchi za majirani) na hivyo kufanya uharamia huo kwenda nje ya mipaka yetu.

Nilikuwa na maswali mengine mengi, na ka nzi kamepeperuka! and I'm out!

MMKJ,
Ipi kati ya hizi mbili ni hatari zaidi

(1). Brain Wash au

(2). Brain Drain
 
The saga continues it never end much much easily is like game of chess. I don't know what really bother them whether Castle, Knight ,Bishop or Queen at this time but let wait at the crucial moment its hard to tell really. And Zitto is not an ordinary pawn you must know that so this is just a game.Advanced politrick game.
 
Conspiracy Theories!

Lende, nimeisoma jana kwenye gazeti mojawapo linaloheshimika sana la hapa nchini (Raia Mwema) labda nao wamekuwa spin doctors; itakuwa balaa kubwa na tutaamini gazeti gani sasa maana hat TBC nao hawaaminiki
 
Tunachopaswa kujua ni kujiuliza, je ni nani ambao ni target ya mafisadi? Je ni Mrema, Je Ni Zitto, ni Slaa au mtikila au.... Tuweke wazi hapa na tuwataje kwa majina ili wakipita huko mitaani na kama mambo tunaona yanaenda msambweni tuwashtue. Kwani mlinzi kamili wa kweli ni mwananchi.
 
Back
Top Bottom