Wifi kazidi dharau

Mpotezee tu huyo wifi yako,
Kwa vile ushamjua wazimu wake ni dharau,
Waambie majirani wasihangaike naye nao wampotezee tu,
Hujui kuna watu wengine bila kudharau wenzao hawajikisii raha,
Cha masingi muuguze kaka yako huyo wifi achana naye.
 
Pole mdogo wangu! Unajua mambo ya ndoa ni magumu wanayajua walioko kwenye ndoa. Wewe umeolewa? Msamehe bure wifi yako maana hapo alishasoma alama za nyakati? Labda nikuulize hao marafiki zako ni wanawake au wanaume? Ungeenda na marafiki wanaume nadhani haingekuwa shida! Kama ni wanawake lazima alishawasoma kwa kuangalia sura tu na kwa kumfahamu mume wake akaamua awakate maini kabisa, wajuute kumfahamu huyo mgonjwa! Alishaona body languages, usikimbilie kusema kuwa ana dharau. Siajabu mavazi yao, walivyojiremba, walikuwa wanajishaua kiaina, wewe unaweza usione lakini watu wazima tunafahamu. Msamehe buree na fikiria hata wewe ungeweza kufanya vituko hivyo maana sababu si juice kama walivyosema wengine ila kuna mengine. Siku nyingine kaka akiumwa usiende kumwona na kundi la warembo ukijua kabisa wanamzidi wifi kwa urembo na manjonjo, nenda peke yako au na ndugu wa karibu.

Hata mimi wifi wa kuniletea marafiki warembo, wenye vinguo vya siku hizi nido nje nje, skin tight za ajabu ajabu kutwa nyumbani kwangu simtaki. Sitaweza kumwambia live peke yake kwani ataona sijiamini, au simuamini mume wangu, wakati mwingine vitendo vinatumika. Akinielewa niko poa sina kinyongo na mtu.....
 
Hili nalo neno, nitamuuguzaje bro. wkt yupo katika himaya ya wifi. Mi namwachia aendelee kumuuguza nitakuwa namjulia khali kwenye simu tu.
 
Hapo na ww utaonekeana huna busara,
Juice ilititupwa ni ya jiran,
Na ww kinachokufanya umsuse kaka yako ni nn?
Acha hasira za kitoto,huyo ni kaka yako wa damu,wifi anaweza ondoka na akaja mwingine,
Kwa vile ushamjua mapungufu yake usimwendekeze muuguze kaka yako hayo mengine achana nayo.
 
Pole mdogo wangu! Unajua mambo ya ndoa ni magumu wanayajua walioko kwenye ndoa. Wewe umeolewa? Msamehe bure wifi yako maana hapo alishasoma alama za nyakati? Labda nikuulize hao marafiki zako ni wanawake au wanaume? Ungeenda na marafiki wanaume nadhani haingekuwa shida! Kama ni wanawake lazima alishawasoma kwa kuangalia sura tu na kwa kumfahamu mume wake akaamua awakate maini kabisa, wajuute kumfahamu huyo mgonjwa! Alishaona body languages, usikimbilie kusema kuwa ana dharau. Siajabu mavazi yao, walivyojiremba, walikuwa wanajishaua kiaina, wewe unaweza usione lakini watu wazima tunafahamu. Msamehe buree na fikiria hata wewe ungeweza kufanya vituko hivyo maana sababu si juice kama walivyosema wengine ila kuna mengine. Siku nyingine kaka akiumwa usiende kumwona na kundi la warembo ukijua kabisa wanamzidi wifi kwa urembo na manjonjo, nenda peke yako au na ndugu wa karibu.

Hata mimi wifi wa kuniletea marafiki warembo, wenye vinguo vya siku hizi nido nje nje, skin tight za ajabu ajabu kutwa nyumbani kwangu simtaki. Sitaweza kumwambia live peke yake kwani ataona sijiamini, au simuamini mume wangu, wakati mwingine vitendo vinatumika. Akinielewa niko poa sina kinyongo na mtu.....

Kama mambo ya mawifi na madada zetu ni magumu hivi, afadhali kubaki Single!
 
inaonekana kuna shida kati yako na wifiyo
inawezekana kuna vitu nyuma ya pazia
jichunguze wewe binafsi, kama unajua huna neno
juu ya wifi yako endela kumwangalia mgonjwa
bila kuonyesha chuki yoyote kwa wifi
baada ya hapo ujitahidi kuwa mbali nae
ili kuepuka kero na dharau toka kwake

Hivi hapo hakuna dalalili za kawivu kweli kati yao hao?
 
Jamani huyu wifi yangu amezidi dharau sana kaka angu anaumwa amelazwa Regency majirani zangu wamenisindikiza na wamemnunulia mgonjwa juice ya Azam box kubwa wifi yangu alivyo fika nakuona ile juice akauliza "nani ameleta uchafu huu yaani mnamletea mme wangu juice chafu hii mnataka ahalishe" heee si tukabaki tumeduwaa akabeba ile juice na kwenda kutupa kwenye dust bin imeniuma sana majirani zangu wameona aibu kwa kweli yaani inasikitisha ukurugenzi wake ndo unafanya adharau mpaka mali zinazo zalishwa hapa nchini? Mi nimempa jibu moja tu wifi si ungemsafirisha kaka akatibiwe ulaya avute hewa nzuri na anywe maji na juice nzuri? akanifyonya

.....Dah! Pole sana! Watu wengine wamesoma lakini hawajaelimika. Angeweza kabisa kwenda kuitupa baada ya nyinyi kuondoka na hakukuwa na haja ya kuleta varangati mbele ya kadamnasi. Umwangalie vizuri huyo binti maana anaweza kabisa kuwa chanzo cha kujenga uhasama mkubwa kati yako na kaka yako.
 
Bi Julieth, hujaleta story nzima hapa. Nadhani kuna tatizo toka enzi. Pia yawezekana aliitupa akijua umeleta wewe. Mbona hujasema kama ulimbebea mgonjwa chakula?
Pili nahisi wewe ni mwenye tatizo. Dunia ya leo nani anasomba marafiki kwenda kumwona mgonjwa? Unless otherwise nyuma ya pazia hao marafiki si marafiki kweli?
Huyo mgonjwa ameumwa kwa muda gani?
Mwache mwenye mume amuuguze mume wake. Akiomba msaada kwenu poa. Yeye si mkurugenzi?

Pia nahisi hamkufurahia alipopanda cheo. Maana sidhani kama dharau inakuja na cheo. Mara nyingi mtu toka siku nyingi ana hulka ya dharau, cheo kinakuza uonekano wa dharau.

Watu wakifanikiwa hata kidogo tu akikarishwa soda na akasema hapana nipe maji, wengine wanasema amewadharau.

Lazima kuna historia hapa kati yako na wifi yako.
 
Hili nalo neno, nitamuuguzaje bro. wkt yupo katika himaya ya wifi. Mi namwachia aendelee kumuuguza nitakuwa namjulia khali kwenye simu tu.
Hata hivyo kumuuguza kaka ni kazi ya wifi ako, wewe kazi yako kubwa ni kwenda kumjulia hali tu, tena hakikisha hubebi hata pipi...usisuse kumtembelea kakako, kikubwa usijiweke mstari wa mbele wakati unajua fika kuwa mkewe yupo na anajiweza....kama wifi hajaomba msaada wako haina haja ya kujitutumua...

Mwisho kabisa huyo wifi ako anasumbuliwa na ushamba kama sio ulimbukeni hivyo msamehe bure... Ukurugenzi ndio nini kama hana UTU?
 
Inaonakana hampendani na hampatani kabisa na wifi yako. Nyote mnashindana na ndio maana aliongea vile mbele ya majirani zako/ shoga zako ambao wanajua bifu lenu naye alitaka kuwaonyesha yeye zaidi; nawe ukamjibu kwa nyodo.

Huyu ni mke wa kaka yako tu, hata ufanyeje. Jitahidi muelewane tu, malumbano na vurugu hazifai.
 
wifi yako kalimbuka na ukurugenzi. Huko ofsn kwake si wanakoma? Ila asikupe presha ukienda kumtembelea kaka yako nendz mikono mitupu ongea na mgonjwa wako tena muda mzuri ni ule ambao wifi yupo ofsn.

Huyo ndo wifi mzuri kihela chako unasave, bajeti saaaafi
 
Bi Julieth, hujaleta story nzima hapa. Nadhani kuna tatizo toka enzi. Pia yawezekana aliitupa akijua umeleta wewe. Mbona hujasema kama ulimbebea mgonjwa chakula?
Pili nahisi wewe ni mwenye tatizo. Dunia ya leo nani anasomba marafiki kwenda kumwona mgonjwa? Unless otherwise nyuma ya pazia hao marafiki si marafiki kweli?
Huyo mgonjwa ameumwa kwa muda gani?
Mwache mwenye mume amuuguze mume wake. Akiomba msaada kwenu poa. Yeye si mkurugenzi?

Pia nahisi hamkufurahia alipopanda cheo. Maana sidhani kama dharau inakuja na cheo. Mara nyingi mtu toka siku nyingi ana hulka ya dharau, cheo kinakuza uonekano wa dharau.

Watu wakifanikiwa hata kidogo tu akikarishwa soda na akasema hapana nipe maji, wengine wanasema amewadharau.

Lazima kuna historia hapa kati yako na wifi yako.

Bi mkubwa nashukuru kwa kuuliza...maana hiyo stori ya dharau ya kutupa Juice ya Azam box imeficha kastori kengine ndani yake....Funguka madam wifi yake!!! Chanzo cha hayo yote ni nini???
 
Jamani huyu wifi yangu amezidi dharau sana kaka angu anaumwa amelazwa Regency majirani zangu wamenisindikiza na wamemnunulia mgonjwa juice ya Azam box kubwa wifi yangu alivyo fika nakuona ile juice akauliza "nani ameleta uchafu huu yaani mnamletea mme wangu juice chafu hii mnataka ahalishe" heee si tukabaki tumeduwaa akabeba ile juice na kwenda kutupa kwenye dust bin imeniuma sana majirani zangu wameona aibu kwa kweli yaani inasikitisha ukurugenzi wake ndo unafanya adharau mpaka mali zinazo zalishwa hapa nchini? Mi nimempa jibu moja tu wifi si ungemsafirisha kaka akatibiwe ulaya avute hewa nzuri na anywe maji na juice nzuri? akanifyonya

Mimi naangalia tatizo hilo kwenye perspective nyingine kabisa, zaidi ya mawifi. Juce ya Azam ni chafu.... a product of Tanzania.........unatoa dharau kama hiyo mbele ya watu? What is wrong with us Tanzanians?
 
mtu kama huyo ni wakumpa maneno ya dharau mara 3 zaidi ya yeye anayoyatoa,hadi akikuona apoteze mood
 
We nae unaonekana una wivu sana
ukurugenzi wa wifi yako unakukatisha mauno ya nini?
Piga kazi na wewe uwe kameneja angalau
kutwa kucha kutuchoshwa na malalamiko ya kitoto ya wifi yako
kaa kwako ulee familia yako wifi yako hakutaki
uko so obsessed na mafanikio yake
she has made it deal with it.

Maisha yamebadilika pindi alipo pata ukurugenzi basi amekuwa juu dharau ndo kabisaaa siku akiukwaa uwaziri au ukatibu mkuu sijui itakuwaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom