Wifi anachukua nafasi yangu,nifanyaje?

hahahaha nashukuru sana baba mkwe Che,
mi nipo single natafuta bado nashukuru kwa mikono miwili hii ofa nono ahsante sana naipokea tena kwa mikono miwili........naomba unikabidi mwali kabisaaaaaa mapema baba mkwe.

halafu we hazikotoshi kweli,yaani bila ya kutoa mahari nikupe mwanangu.kwanza itabidi niangalie progress yako hapa JF,nikiona unafaa nitakubip.Kwetu ni haramu kumpigia mkwe.
 
Unajua uwa unanifurahisha sana,nitakupa mwanangu mmoja uoe,kama haujaoa lakini.Mahari yako ni kunichekesha baba mkwe wako siku nzima.

Ah ina maana mwenzetu huyu atakuwa analipa mahari siku zote za uhai wake?... kaaaaaazi kwerikweri.

Haya Fidel tengua udhu haraka sana. Bado nipo nipo haikufai tena wazeeka sasa ona hizo ndevu zishakuwa na mvi sasa kaka (Joke)
 
Masikini wee, laiti baba mkwe mtarajiwa angekujua ulivyo!..Anyway tusikuharibie bahati yako, hongera na umtunze vizuri mwali kama utapewa lakini!..ha ha ha

Hivi Belinda nitakuwa nina kichaa cha kiasi gani mpaka nikamtupe mwanangu kwa fidel.Hata siwezi kujaribu.
 
Ah ina maana mwenzetu huyu atakuwa analipa mahari siku zote za uhai wake?... kaaaaaazi kwerikweri.

Haya Fidel tengua udhu haraka sana. Bado nipo nipo haikufai tena wazeeka sasa ona hizo ndevu zishakuwa na mvi sasa kaka (Joke)

teh teh teh mi nachekelea tu utafikiri ndo nyie mnao ninyima hata ofa ya maji ya kunywa tu mniache Kitonga....hii tayari yangu,
 
Hivi Belinda nitakuwa nina kichaa cha kiasi gani mpaka nikamtupe mwanangu kwa fidel.Hata siwezi kujaribu.

Watu bana tayari wamesha haribu ridhiki....anyway ridhiki ya Simba ipo miguuni mwake...baba mkwe wasikukatishe tamaa hawa wana wivu tu.
 
Haya Fidel tengua udhu haraka sana. Bado nipo nipo haikufai tena wazeeka sasa ona hizo ndevu zishakuwa na mvi sasa kaka (Joke)

mmesha haribu kitumbua kimeingia mchanga hakiliki tena....itabidi niendelee kuwepo kuwepo tu mi nitaoa nikiwa na 60yrs...
 
Watu bana tayari wamesha haribu ridhiki....anyway ridhiki ya Simba ipo miguuni mwake...baba mkwe wasikukatishe tamaa hawa wana wivu tu.

Wewe usikonde mkwe wangu,si nimekwambia naangalia progress yako itakuwaje.Hapa nilikuwa najaribu kujitutumua nisionekane zoba sana,si unajua mkwe wangu kitabia kidogo hauwaridhishi wengi humu.Mie nakufagilia sana tuu mkwe wangu.
 
teh teh teh mi nachekelea tu utafikiri ndo nyie mnao ninyima hata ofa ya maji ya kunywa tu mniache Kitonga....hii tayari yangu,

Yaani kama nakuona na suruali yako ya kifua, ulimi umekutoka mpaka kidevuni kwa uchu. Mtoto wa watu bado mdogo (tena wa bara huyo) usimharibu.

BCT.
Dada ni kweli mengi umeshauriwa na pia maisha yetu inabidi kumkabidhi Mwenyezi MUNGU ila ikibidi mwenzangu mkalishe baba watoto mweleze na kama ulivyosema umeshamweleza mara nyingi sana hebu jaribu kumtoa out umweleze kwa mapenzi kama haita faa sasa itabidi utumie mjeledi, si wanasema Punda hendi bila mjeredi? mwambie kama haiwezekani basi achague moja kuishi na dada yake au familia yake.

Kwa wifi mkalishe mwambie tena kwa upole kuwa asijisahau pale si kwake ni kwako na wewe kama mwanamke ungependa uwe unajipangia na kuamua mambo ya familia yako kama vile yeye asingependa kuingiliwa na wifi yake au mtu yeyote katika ndoa yake na wewe vivyo hivyo hujisikii vizuri so ajaribu kukupa nafasi.

Akikaidi basi mwambie nahisi wewe si wifi bali mke mwenza so kuanzia leo tunapeana zamu ya kulala na kaka yako na nikiona unammudu zaidi yangu nakuachia wote wote kama zawadi.
 
Inaonekana mumeo yuko karibu sana na dada yake.

Wanawake wengine wa kiafrika nao wako docile sana, mwingine angemwambia mume achague kati ya dada yake au mkewe.
 
Yaani kama nakuona na suruali yako ya kifua, ulimi umekutoka mpaka kidevuni kwa uchu. Mtoto wa watu bado mdogo (tena wa bara huyo) usimharibu.

.....hapana sitamharibu maana ni ubavu wangu wa kushoto nikimwaribu nitakuwa napiga story na nani? Alafu nitakuwa naishi na wifi yake hapo hapo nyumbani ambae ni dada angu awe anamfundisha mila na desturi.
 
Karibu,lakini si umesema umeshaoa japo upo upo,ukimaanisha your ndoa is not working.Labda umuache kwanza huyo ndo umuoe mwanangu,bado mdogo si wakupata frustration mapema kiasi hiki ya uke wenza.

mkwee mbona mnoko hivyo?
ukimbania sana utakuta anaweza kuwa anajirusha na mjamaa ambaye ana ndoa za mitala za kufa mtu kwikwi
 
Mimi ni mdada mtu mzima tu nimeolewa miaka si chini ya mitano, nina watoto wawili. Nimekuwa nikishindana na wifi yangu ambae ni dada wa damu wa mume wangu, ushindani wetu ni kama mtu na mke mwenzie lakini si hivyo.

Kwanini unashindana naye? Inatakiwa umweleze vitu ambavyo usingependa aingilie kwenye ndoa yenu.

Kabla sijaolewa na huyu mwanaume tulikuwa kwenye uhusiano wa mbali kwani mimi nilikuwa nasoma Ireland na yeye alikuwa Tanzania. Kipindi chote hicho hakukuwa na matatizo yeyote kati yangu na dada yake.

Usingeweza kuona mapungufu yake kama mlikuwa hamkai nyumba moja! Hata hivyo kwa vile hukuwa mke bado asingeweza kuwa na nguvu yoyote. Kumbuka kwa mila nyingi (zimepitwa na wakati!) ukoo wa mwanaume hujihisi kama wameoa(i.e. wewe ni mke wa ukoo) na hii inapelekea mawifi kuwa na nguvu kubwa tu juu ya mke wa kaka yao (katika kesi yako ni even worse kwa sababu ni mkubwa kiumri kuliko mumeo).

Baada ya kumaliza masomo nilihamia England kufanya kazi ambako ndiko tunaishi mpaka sasa. Ndoa yetu ilifungiwa Tanzania na Mume wangu akanifuata huku na baada ya muda tukasaidiana na kumleta dada yake ambaye ndio wifi yangu huyu mwenye vituko kila kukicha ambavyo vinahatarisha ndoa yangu.

Mlimleta kwa ajili ya nini? Hiyo sababu iliyowafanya mumlete bado ipo(i.e. ni lazima kuendelea kukaa nae)?

Imefikia hatua wifi yangu kuchagua nini kifanyike ndani ya nyumba yangu, aina gani ya vifaa vinunuliwe ikiwa tunafanya marekebisho hapa ndani, wapi tuende au tusiende, tukamtembele nani nalini na kinachonikasirisha zaidi ni kaka mtu kumsikiliza dadake na sio mimi mkewe.

Ikitokea mimi na mume wangu tumejadili jambo la kufanya kwa ajili ya familia yetu ndogo mume wangu anachukua simu na kumwambie kila kitu mdogo wake na kitakachosemwa na mdogo wake basi ndio kitakachofanywa na sio mimi hata kama sehemu ya jambo hilo pesa zangu zinahusika. Yaani imekuwa kama akili ya mume wangu haifanyi kazi basi anatumia ya dada yake kufanya maamuzi.

Hapa inabidi na wewe uwe mwangalifu kidogo. Si mara zote mawazo ya mawifi ni mabaya! Wanaweza kutoa ushauri mzuri tu! Inawezekana hiyo ndio sababu mumeo anamsikiliza yeye zaidi kuliko wewe. Napata hisia kwamba suala hili umelilea kwa muda mrefu kwa sababu si kawaida sana mawifi kuingilia kwa kiasi unachokieleza. Jaribu kupata historia kati mumeo na dadake - ukaribu wao ni lazima una nguvu kubwa sana nyuma yake!

Kitu kingine kinachoniumiza roho na kunipa donge ni pale ninapotoka kazini jioni au siku za mwisho wa wiki wote tuko nyumbani, badala mume wangu atumie muda huo na mimi yeye atakuwa kwenye simu na dada yake wakiongea maongezi yasiyoisha tena kwa kilugha chao na kucheka.

Hapa kama unanichanganya kidogo! Huyo wifi hamkai nyumba moja? Kuhusu kuongea kilugha na dadake sioni kama ni tatizo. Kuna uwezekano mkubwa hiyo ndio lugha yao ya kwanza na hivyo inaflow vizuri zaidi kuliko lugha nyingine. Dawa ni wewe kujifunza hiyo lugha angalau ujue nini wanazungumza!

Nimevumilia sana na nimefanya vikao na ndugu wa pande zote mbili na hata kuzungumza na mume wangu lakini hakuna mabadiliko yeyote, nimekuwa mkiwa ndani ya ndoa yangu na sijui nini cha kufanya, japokuwa nampenda mume wangu lakini kama suluhisho ni kutoka kwenye hii ndoa basi nitatoka ili kutafuta amani na furaha kwingine lakini sio ndani ya ndoa hii.

Ndoa ni uvumilivu lakini ni lazima ujiwekee limit! Inatakiwa mumeo afike mahali achague ama dadake ama wewe! Kama mnakaa naye nyumba moja, ingekuwa vema kama akaondoka na kukaa kwake.
 
Na huyo wifi mtu mzima aliyejibanza kwa kaka yake mpaka leo hii anatafuta nini jamani? Tena ni dada mkubwa wa kaka, sasa ni sisi ndio tukae kwako au wewe ukae kwetu? Cha kwanza ni hicho, sista atafute kiota chake mwenyewe!
 
"

Wifi yangu huyu ni mkubwa zaidi ya mume wangu, ameolewa na anawatoto kadhaa wote wako Mkoani Kagera Tanzania.
Naombeni ushauri ndugu zangu"

Duuh..ebwanaeeeeeheheeee...sikiza bibie...mbona unaonekana UMEMUOA huyo fa--r--a lakini hutumii nguvu yako ya VETO ya "kumwoa" na kumpa masharti magumu kama hayawezi achape mwendo arudi kijijini akalime mwani...kama nitakuwa nimekosea naomba unisahihishe...ulikuwa unasoma abroad ukaja tzania mkafunga ndoa kisha ukaondoka naye huyo mmeo...then nakonkludi kuwa ULIKUJA KUMWOA NA KUONDOKA NAYE KUMHAMISHIA NYUMBANI KWAKO...ndio..kama angekuwa kakuoa angekaa na wewe kwake i.e tzania....unayo haki ya msingi ya kumwambia achague moja..dadake au wewe "mme wake"...kuhusu ukionacho wewe ni tatizo..WIFI YAKO...huyo naye mie naona mbona mwepesi tuuu...mtafutie ticket achape mwende mpaka kagera akalee wanawe na mmewe pia...aache ungese wa kukaa kwenye nyumba za watu na kuingilia mambo yao...natumai kama vile hapungui 45yrs na bado anakaa kwenu?..thats a shame....hii nayo ni nyingine na ni kwa taarifa yako....hawa ndugu zetu wa kagera wanamambo yao (wengi wao na sio wote..na pia nisamehewe kwa kuweka ukwseli huu)....naamini huyu wifi yako ameshakuwa-swahiba wa kaka yake katika kumtafutia totozi hasa hizi za jamii ya kagera pia...ndoa ya wakagera huwa inaenda vizuri wakiwa wao-kwa - wao ndio wahusika...sasa wewe dada yangu intruder wa mila za watu naona umegeuzwa buzwagi..wanakula shavu ....kama unakifua wamwage wote..naona kama wanakuwa mzigo kwako mara 2...kiuchumi...unahangaika wanakula na kulala...then wanakutesa kwa mambo yao ya kipuuzi.......wanaume wapo kibaooo tu...single parent familiez kibaoooo tuu na HAPPY LIFE GOES ON
 
Ikitokea mimi na mume wangu tumejadili jambo la kufanya kwa ajili ya familia yetu ndogo mume wangu anachukua simu na kumwambie kila kitu mdogo wake na kitakachosemwa na mdogo wake basi ndio kitakachofanywa na sio mimi hata kama sehemu ya jambo hilo pesa zangu zinahusika. Yaani imekuwa kama akili ya mume wangu haifanyi kazi basi anatumia ya dada yake kufanya maamuzi.

Kitu kingine kinachoniumiza roho na kunipa donge ni pale ninapotoka kazini jioni au siku za mwisho wa wiki wote tuko nyumbani, badala mume wangu atumie muda huo na mimi yeye atakuwa kwenye simu na dada yake wakiongea maongezi yasiyoisha tena kwa kilugha chao na kucheka.

Ukiyaangalia haya uliyoyaandika, utabaini kuwa tatizo ni huyo mume wako na wala si wifi
 
Duuh..ebwanaeeeeeheheeee...sikiza bibie...mbona unaonekana UMEMUOA huyo fa--r--a lakini hutumii nguvu yako ya VETO ya "kumwoa" na kumpa masharti magumu kama hayawezi achape mwendo arudi kijijini akalime mwani...kama nitakuwa nimekosea naomba unisahihishe...ulikuwa unasoma abroad ukaja tzania mkafunga ndoa kisha ukaondoka naye huyo mmeo...then nakonkludi kuwa ULIKUJA KUMWOA NA KUONDOKA NAYE KUMHAMISHIA NYUMBANI KWAKO...ndio..kama angekuwa kakuoa angekaa na wewe kwake i.e tzania....unayo haki ya msingi ya kumwambia achague moja..dadake au wewe "mme wake"...kuhusu ukionacho wewe ni tatizo..WIFI YAKO...huyo naye mie naona mbona mwepesi tuuu...mtafutie ticket achape mwende mpaka kagera akalee wanawe na mmewe pia...aache ungese wa kukaa kwenye nyumba za watu na kuingilia mambo yao...natumai kama vile hapungui 45yrs na bado anakaa kwenu?..thats a shame....hii nayo ni nyingine na ni kwa taarifa yako....hawa ndugu zetu wa kagera wanamambo yao (wengi wao na sio wote..na pia nisamehewe kwa kuweka ukwseli huu)....naamini huyu wifi yako ameshakuwa-swahiba wa kaka yake katika kumtafutia totozi hasa hizi za jamii ya kagera pia...ndoa ya wakagera huwa inaenda vizuri wakiwa wao-kwa - wao ndio wahusika...sasa wewe dada yangu intruder wa mila za watu naona umegeuzwa buzwagi..wanakula shavu ....kama unakifua wamwage wote..naona kama wanakuwa mzigo kwako mara 2...kiuchumi...unahangaika wanakula na kulala...then wanakutesa kwa mambo yao ya kipuuzi.......wanaume wapo kibaooo tu...single parent familiez kibaoooo tuu na HAPPY LIFE GOES ON

Mkuu
napenda tu kukutaarifu kwamba mie (kama si wengi humu) nashindwa kusoma posti zako kwa kuwa zipo zigzag mno. unachanganya sana rangi, bold, caps n.k.
pls shekhe kuwa mpole ktk hilo basi
 
Mkuu
napenda tu kukutaarifu kwamba mie (kama si wengi humu) nashindwa kusoma posti zako kwa kuwa zipo zigzag mno. unachanganya sana rangi, bold, caps n.k.
pls shekhe kuwa mpole ktk hilo basi

hehehehe huyu bana anaonyesha msisitizo lakini amepitiliza katika msisitizo wenyewe.
 
Awape ukweli wote wawili unahofia nini kwakati wewe ndio ulowaleta 'mjini'? Si ajabu bila wewe huyo mume na dadake wangeishia kuisikia England maredioni na kwenye Luninga tu. Hebu mume na akupe heshma yako kama mke na wifi awe wifi akumbuke kuwa yeye ni dada na kamwe hawezifikia umuhimu wako wewe kwa kakie angeweza kakie angemuoa yeye tangu mwanzo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom