wife anapokulalamikia rafiki yako anamtaka....

Mkeo ilikuwaje akampa huyu jamaa namba yake? Mmepanga nyumba moja? au huwa mna share LUKU? sijaelewa hapo

Lakini mkubwa nina wasi wasi sana na huyu mkeo...
 
Sio rahisi katika maisha yenu ya ndoa akawa ametongozwa na mtu huyo mmoja tu!!! Nina maana kwamba kama alishawahi kukwambii wengine!! Asikudanganye mtu, hakuna mwanamke ambaye hatongozwi. Kwa hiyo kutongozwa sio kosa, bali kosa ni kumvulia c***p mtu ambaye sio mume wake. Aidha, walishafanya mchezo mchafu, halafu wakagundua kuwa umeshtukia deal sasa wana-neutralize ili ujue jamaa bado anaimbisha. Je, ujumbe wa mwanaume kuja kwa mkeo uliukuta kwnye inbox?

Wewe shughulika na mkeo tu, achana na third party maana huna ushahidi kuthibitisha kama kweli anamsumbua.
 
Mwanamke mstarabu hawez kukueleza katongozwa, ana malizana na mwanaume yule alie mtongoza kimya kimya na mambo yamekwisha...Mara nyingi sana anamwambia yule mwanaume anaye mtongoza, tukutane basi ktuo cha police station kama wewe mwanaume.
 
Hapa inawezekana huyu demu ameliwa tayari sasa anaweka mambo sawa kama wanavyosema wakubwa hapo juu.

Hizo msg za kumtukana ni geresha toto wamekupanga hapo hehehe
 
Hvi kama angekuwa amemkubalia ombi lake na wakafanya mchezo mchafu angekwambia pia?

Hapa la kufanya ni kumshirikisha mkeo katika mtego wa kumuaibisha huyo jamaan na kama atakuwa anampenda na pengine amewahi kuushiriki mchezo mchafu basi utagundua atakavyokuwa akikwepa.

Hilo litakuwa ndo jibu ya kilichofichika nyuma ya pazia.
 
kuna ka mtihani kananiumiza kichwa kidogo...
kuna jamaa amehamia hapa mtaani kama mwezi mmoja hivi.
baada ya wiki wife akaniambia huyu jamaa anamsumbua kwa kumpigia simu za kumtaka...
nikamwambia aachane nae.
sasa jana nimeshika simu ya wife nimekuta kuna sms za kumtukana jamaa. sasa nipo sielewi nimuadhibu wife kwa kuendelea kuwasiliana na jamaa au nimuadhibu jamaa kwa kutaka kuharibu nyumba yangu.
NIPO NJIA PANDA

Mzee kwa stori yako inavyoonyesha uwezekano mkubwa ni kuwa umeshaumizwa siku nyingi na sasa kinachofanyikai ni kuchezewa dili la kukufanya uamini kuwa hakuna kinachoendelea (bluffing) kati ya wawili hao ili waendelee kujivinjari pasipo kuwa na wasiwasi wowote. Kwa nini usifikirie kwamba hizo mesg ndani ya simu ya mkeo ni danganya toto? Kwa nini uziamini? Zimeachwa kwenye simu makusudi ili uzione, kwa nini, wakati wewe ulishasema mawasiliano na huyo jamaa stop! Fikiri kama mtu mzima!
 
hilo game ni tight. mimi kuna best frnd wangu mmoja ana mke, yule mwanamke alikuwa anacheat na jamaa mwingine (pia ni rafiki yetu) na yeye akafahamu kuwa nimeshajua mchezo wake, ghafla akaninunia hata salamu tulikuwa hatupeani... sasa yule mwanamke akatengeneza mazingira kwa frnd wangu na kumwambia eti mimi huwa namtaka na jamaa akaamini,

mwanamke alimwambia frnd akitaka waachane basi aendelee kuwa na urafiki na mimi. Sasa hapa alinifunga mdomo maana nisingeweza tena kumwambia jamaa na jamaa nae akanichukia na hata salamu yangu alikuwa hapokei kwa miaka mitatu.

Mumewe wakati yupo safari yule mwanamke alikuwa anamwingiza mwizi bila woga tena chumbani kwake mimi joka la kibisa nikiangalia.

Mungu ni mkubwa ilipita miaka 3 rafiki yangu akaja kufahamu ukweli na aliponiuliza nilimpa ukweli wote
 
Back
Top Bottom