Wife amanichosha nataka kumtema lakini gharama !!-sina raha ya ndoa

Kwanza pole sana kwa matatizo, mtazamo wangu ni kuwa huyo sio responsible wife/ mother, hatua ya kuwabagua watoto inabomoa familia na kujenga chuki miongoni mwa watoto, hata kama watoto ni wadogo wakilelewa ktk mazingira hayo itawaadhiri ktk makuzi yao inaweza kuwafanya watoto wakaathirika kisaikolojia, je ukiongea nae labda anatoa maelezo gani juu ya ukatili wa hawa watoto tuanzie hapa...

Ndugu story ni ndefu sana,kwa ufupi hakubali chochote ni mbishi/mgomvi balaa,kama ningekuwa ninatabia ya kupiga nadhani ningekuwa nimeua,nimekuwa najaribu kutumia technics mbalimbali maana ni muhimu kujihami asije akaleta madhara llakini sioni mwelekeo,ndo maana natafuta mtaalamu/mshauri,anishauri jinsi ya kumtoka bila kuleta madhara.
 
Kaka yaani kati ya mambo ambayo huwa yanaiuma ni hili la kunyanyasa watoto wa mwanamke mwenzangu. Huyu mama hata sijui nikwambieje, yaani sijui umfanyeje but labda nikuulize ulishawahi kumkanya juu ya tabia yake hiyo?? Kama bado kaa naye na uongee naye taratibu juu ya madhara anayoyasababisha kwa watoto na familia yenu kwa ujumla. Na pia umweleze hawezijua na wala yeye siyo MUNGU iko siku atajikuta watoto anaowanyanyasa ndio wanaokuja kuwa msaada mkubwa sana kwake huko mbeleni. Na pia Marehemu huko aliko anaona kila kitu hapendi.

Kama ulishamkanya hasikii, hebu mrudishe kwao kidogo akafunzwe adabu au namna gani vipi wapeleke hao watoto wanaonyanyaswa (na wa kwake kama umri unaruhusu) boarding.

Unajua hadi nimefikia hatua ya kuwaza kumuacha nimejaribu mambo mengi sana,nimemkanya lakini tatizo lake ni kuwa hakubali kosa,na kuhusu kumrudisha kwao sio shida lakini inaonekana amejipanga na kunadalili ya kunisumbua that,s why natafuta technical advice kabla sijachukua uamuzi wowote.asante
 
Pole sana, nafikiri kuwa mke wa pili si jambo rahisi hata kwa huyo mwanamke. Si rahisi sana kulea watoto wa mwanamke mwenzio kama wako....ni rahisi sana kunyoosha kidole lakini ukiyaishi maisha ya mke wa pili na mama wa watoto wasio wako utaelewa. Sisemi anachofanya huyo mama ni sahihi,ila ningetamani sana kusikia mawazo yake kuhusu maisha yake na wanao....wanao wanamchukuliaje na yeye anajisikiaje na anawachukuliaje......na ikumbukwe tu,tafiti zinatuonyesha mwanamke wa pili hawezi kuwa na nafasi katika moyo wa mwanaume kama ya yule wa kwanza....men tend to compare aliyepita na wa sasa na kwa hili unakuta wana wa judge unfairly.

Sikushauri umuache,mweke chini wewe na wazee wa pande zote mbili,mwambie kuhusu mwenendo wake na unavyojisikia,mpe muda na kuwa nae karibu katika kila hatua kuhakikisha anabadilika....lakini pia washauri watoto wako na angalia mwenendo wa watoto wako kwa mama yao.....mama si malaika,kama wanamtenda visivyo ata react tu in a negative way,ila kisa ni mama wa kambo ataonekana mnyanyasaji. Karibu kwa ushauri anytime,its part of my job!
 
Sijui kwa nini mama wa kambo huwa inakuwa tatizo kukaa na watoto waliowakuta. Huu ni mtihani wa pili kwako, baada ya kufiwa na mkeo, sasa hilo ni jingine.
Mkuu hakuna njia nyingine unayofikiria jinsi ya kutatua tatizo lako zaidi ya kuachana? Maana hapo unatengeneza matrix ya watoto wa kambo wengi mno mkuu.
Huyo mama anaweza badilika, nina experience ya mtu wa jirani sana. Mama yao wa kambo aliwatesa sana lakini baada ya muda alibadilika. Na ujue maisha yanaenda.
Ushauri wangu mkuu, badala ya kufikiria kuachana jaribu kuwahamisha wanao hapo nyumbani kwa muda. Familia zetu za Kiafrika unaweza wapeleka kwa bibi, shangazi, rafiki wa karibu na ukawatunza huko vizuri kabisa.
Wakati huohuo hatuna guarantee mtu atakufa lini, andika wosia kwa vile vitu vya muhimu ili wanao wasijetolewa kapa Mungu akikuita ghafla. Na wosia huo uandike kwa mujibu wa sheria (nenda RITA watakusaidia).

Mkuu nakushukuru sana ,hapa nimeshapata point tatu za muhimu sana,lakini suala la kuwapeleka watoto kwa relatives bado naona linaugumu fulani,sio kwamba sina ndugu hapana,lakini watoto wananihitaji sana na sipendi kukaa mbali nao,lakini nitafikiri na kulitathmini hilo wazo bado nina muda kwani sitaki kukurupuka,asante sana.
 
Kama watoto Wakubwa na wanasoma wapeleke Boarding skul, huyo mama huwezi mlazimisha awe na upendo unaotaka wewe hata ajitahidi vipi hawezi kuwa kama Biological mother.

ikifikia point ya kuchagua between watoto wake au ambao si wake lazima atachagua wake hata

wewe ungekuwa yeye ungefanya hivyo. mfano kazi,vitu vizuri etc lazima afanye choice kwa wanawe ni NATURAL.(Binadamu sote tupo hivyo tukifika kwenyepoint ya ku choose lazima tujifanyie feva) japo tutaficha kuonekana tupo equall

CHAKUFANYA NI:

Jaribu kuwaweka watoto mbali na nyumbani kishule au wakaishi na Bibi zao ndugu etc huko watapendwa sababu ni damu moja na pili unapeleka matumizi na kupunguza makali ya maisha,

thats the only solution.

pole sana.

Asante kwa ushauri wako mzuri,taufanyia kazi, asante
 
kaka hazina yako pekee ni watoto,lea watoto wako wakue kwanza at least wafikie college ndipo umtafute mwenza!la sivyo watoto watachanganyikiwa.
 
Wadau suala hili ni very serious na kama kuna mtaalamu wa masuala ya kijamii niko tayari kumuona ofisini anisaidie kuwa free.

Wadau nilifiwa na mke miaka kadhaa iliyopita,akaniachia watoto wawili mmoja wakike na wa kiume.baada ya 2 yrs nikakutana na huyu wife niliyenae sasa hivi akiwa na mtoto mmoja wa kike,na baada ya mda tukapata mtoto wa kiume.
kwa ufahamu wangu FINYU niliamini tukioana na huyu mama tunaweza kucreate new happy,lovely and prosperous family,kwa kuzingatia mazingira yetu,

tulipeana na mwenzangu majukumu yafuatayo.
1.ahakikishe watoto alionikuta nao anakaa nao vizuri kiasi kwamba hawataweza kutofautisha kati yake na mama yao.
2.Mimi nihakikishe mtoto niliyemkuta nae ananifurahia kama baba na kamwe hajuti kukutana na mimi.

Mungu alinisaidia sana kumteka mtoto wa wife kiasi kwamba hata mtu akimuambia mimi si babake mzazi anaanza kulia,KWA UPANDE WA MWENZANGU ALIKUJA KUNISALITI 100% kiasi kwamba hadi vifaa vya ndani anavigawanya,hiki cha watoto wake,hiki cha watoto wangu,KILA KITU KIZURI NINACHONUNUA KWA WATOTO ANACHAGUA VILE BEST ANAWAPA WATOTO WAKE,imefika mahali anampigiza kazi mtoto mkubwa hata zinazozidi umri wake.

wadau nimemchoka na ninataka kumuacha LAKINI NIKIPIGA HESABU NAONA NAWEZA KUIATHIRI FAMILIA YANGU ZAIDI kwani watoto wote wananipenda ila wale wakwangu wanaishi kwa hofu mbele ya mama yao mgeni,

IMEFIKIA MAHALI MKIKWARUZANA NA WIFE HASIRA ZINAMALIZIWA KWA WATOTO,NO PEACE AT ALL.

ADVICE PLEASE!!!!!!!!!

aisee una moyo! Mi ningeshaua, unaishi na shetani? Bora uishi ka padre ka huwez unaweza kuoa kimila, kwani ili iitwe ndoa lazima mkale bata club jimkanaz?
 
Mkuu, Kuna kitu kinaitwa MAOMBI, watakwambia mengi ila usipo mshirikisha BWANA yote ni bure. Lazima ukaze goti. Kuna jambo lolote linalo mshinda BWANA? BWANA kwetu ni kimbilio. U must claim for HIS promises, they are meant for you. Call upon HIM and HE will show you great things!
I will always remember you in my prayers.
Otherwise I really feel extremely sorry for you and May the Good LORD Bless and keep you.
 
nashindwa nikushauri nini,kwa ujumla mimi kwangu damu nzito kuliko huyo mke mpita njia,yaani kwa hizo tabia tayari ujue kuna mambo mengine pia anakusaliti.kashaota pembe huyo.piga chini weka pengo tafuta mwanamke wa kusaidia kulea watoto na sio mke tena
 
pole kaka yangu,
mim tu sio wewe baba ya hao watoto lkn roho imeniuma sana hadi nasikia kulia kwa jinsi ulivyoelezea,
niko weak sana juu ya watoto,
lkn kaka yangu hakikisha wanao hawamdharau huyo mama,
pia watoto wakikosa muache mama awaadhibu kama mama yao,
ila pamoja na yote hatakiwi kuwatesa watoto.
Je huyu mama hajawahi kukulalamikia chochote juu ya tabia za watoto.
hali kama hizi zinakosesha sana raha.
 
.nakuonea huruma na nawaonea huruma hao watoto{napenda sana watoto}na nimepitia mambo ya mama wa kambo,kwa kweli unakuwa mnyonge na unakuwa na donge ambalo ngumu kufutika,mtetezi mkubwa kwa hao watoto ni wewe.kama una uwezo ungetafuta ndugu yako yoyote ukakaa nae,maybe itakuwa dawa kwa huyo mama,na usichoke kuwatetea watoto wako,maana hata wakiwa wakubwa,watajua wewe huna makosa yoyote yale.
 
pole kaka yangu,
mim tu sio wewe baba ya hao watoto lkn roho imeniuma sana hadi nasikia kulia kwa jinsi ulivyoelezea,
niko weak sana juu ya watoto,
lkn kaka yangu hakikisha wanao hawamdharau huyo mama,
pia watoto wakikosa muache mama awaadhibu kama mama yao,
ila pamoja na yote hatakiwi kuwatesa watoto.
Je huyu mama hajawahi kukulalamikia chochote juu ya tabia za watoto.
hali kama hizi zinakosesha sana raha.

Fanyia kazi hapo kaka!
 
Wadau suala hili ni very serious na kama kuna mtaalamu wa masuala ya kijamii niko tayari kumuona ofisini anisaidie kuwa free.

Wadau nilifiwa na mke miaka kadhaa iliyopita,akaniachia watoto wawili mmoja wakike na wa kiume.baada ya 2 yrs nikakutana na huyu wife niliyenae sasa hivi akiwa na mtoto mmoja wa kike,na baada ya mda tukapata mtoto wa kiume.
kwa ufahamu wangu FINYU niliamini tukioana na huyu mama tunaweza kucreate new happy,lovely and prosperous family,kwa kuzingatia mazingira yetu,

tulipeana na mwenzangu majukumu yafuatayo.
1.ahakikishe watoto alionikuta nao anakaa nao vizuri kiasi kwamba hawataweza kutofautisha kati yake na mama yao.
2.Mimi nihakikishe mtoto niliyemkuta nae ananifurahia kama baba na kamwe hajuti kukutana na mimi.

Mungu alinisaidia sana kumteka mtoto wa wife kiasi kwamba hata mtu akimuambia mimi si babake mzazi anaanza kulia,KWA UPANDE WA MWENZANGU ALIKUJA KUNISALITI 100% kiasi kwamba hadi vifaa vya ndani anavigawanya,hiki cha watoto wake,hiki cha watoto wangu,KILA KITU KIZURI NINACHONUNUA KWA WATOTO ANACHAGUA VILE BEST ANAWAPA WATOTO WAKE,imefika mahali anampigiza kazi mtoto mkubwa hata zinazozidi umri wake.

wadau nimemchoka na ninataka kumuacha LAKINI NIKIPIGA HESABU NAONA NAWEZA KUIATHIRI FAMILIA YANGU ZAIDI kwani watoto wote wananipenda ila wale wakwangu wanaishi kwa hofu mbele ya mama yao mgeni,

IMEFIKIA MAHALI MKIKWARUZANA NA WIFE HASIRA ZINAMALIZIWA KWA WATOTO,NO PEACE AT ALL.

ADVICE PLEASE!!!!!!!!!

Hiyo ndiyo hulka ya wanawake! Ni asili yao kupenda vyao tu. Achana nae mpumbavu huyo. Ingekuwa mimi, ningepata uchungu sana manake kwa tabia hiyo ananifanya nimkumbuke mke wangu aliyefariki. Samahani wanawake kama nimewakwaza!
 
Back
Top Bottom