Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

Ukweli ni kuwa TTCL inamilikiwa na mmiliki hostile kwake. Yaani, serikali isiyokuwa na clue inafanya nini (inachotaka ni utajiri kwa viongozi tu), na mbia wa nje anayefanya kila hila kuhakikisha kampuni inakufa.
 
I had time to talk with Some TTCL members/staff in previous time and were not happy that TTCL is not leading. TTCL is the first company to have the biggest network web ever in Tanzania (I believe it still leads). TTCL have independent Internet gateway, TTCL mobile, the news goes on saying, was planned to release its cheapest mobile service in form of TTCL mobile but its release was late and hence missed the business timing....TTCL was tricked into producing enemy of its own by its own costs, that is Celtel then Zain then Airtel Tz.

Let us discuss, why is TTCL not leading, who are marring it to the current status and what should be done. I hope there are TTCL members here to make it hot for the good of TZ
TTCL inaelekea kimbari kama ilivyo kwa Tanesco
 
Matatizo ya kiuongozi TTCL yapo ndio, lakini yanaletwa na serikali. Angalia hii;
  • Mwaka 2009, baada ya menejimenti ya wazungu wa Canada kuondoka, TTCL ilibaki bila uongozi. Serikali ikateua menejimenti ya muda.
  • Mwezi October mwaka huo huo, serikali ikatangaza nafasi za kazi za watendaji wakuu wanne; yaani CEO na wasaidizi wake watatu (Finance, Comercial, Technical).
  • Baada ya Mchakato wa muda mrefu, Mwaka 2010 mwezi May Nafasi mbili tu zikajazwa; ya CFO na CTO. Hawa wanaokaimu nafasi za Biashara na Mtendaji mkuu wa kampuni (CEO) wakaambiwa hawajafanikiwa.
  • Hadi leo Januari 30 2011, nafasi hizo hazijajazwa, waliopo hawana authority kwani kazi zilitangazwa wakafanya interview wakaambiwa hawafai. Ila wameachwa waendelee kuwepo wepo tu.
  • Kumbuka hao ambao wapo wapo tu, ndo moyo wa TTCL, yaani CEO na Chief wa Biashara. Kwa hiyo kampuni inaendeshwa bila CEO wala Kiongozi wa biashara kwa sababu waliopo waliambiwa wameshindwa interview, ila hadi leo haijasemwa nani alishinda hizo interview.
  • Uongozi huo ulitakiwa uanze kazi Januari 2010, leo tunaingia Februari 2011 bado uteuzi wa uongozi haujafanyika.
  • Ni kampuni gani inaweza kuendeshwa wakati CEO wake na Mkuu wake wa Biashara wameshaambiwa hawafai kwa mwaka mzima?
  • Tafakari na uchukue hatua!!
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!

Mkuu thanks for this shocking and sad information..., watu wengi hatujui the extent ya ubadhilifu lakini deep down tunajua kwamba things are not right..., I hope mkuu mnaojua mgefanya jitihada za kufanya hizi habari kuwa zinaleak kwenye vyombo vya habari ili wananchi waelewe ni kiasi gani taifa lao linaendeshwa kimafia
 
[*]Ni kampuni gani inaweza kuendeshwa wakati CEO wake na Mkuu wake wa Biashara wameshaambiwa hawafai kwa mwaka mzima?
[*]Tafakari na uchukue hatua!!
[/LIST]

Mkuu mimi nimetafakari lakini hatua nyie mliomo ndani ndio rahisi kuchukua, asante kwa hii first step ya kutujuza...., tafurahi sana hizi habari siku moja nikiziona kwenye front page ya magazeti yetu...
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,

  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
  • Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
  • Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
  • Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
  • Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
  • Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
  • Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
  • Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
  • Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
  • Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
  • Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
  • TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!

Asante sana ndugu Shingo kwa kutujuza tulio gizani.

Binafsi ni mteja wa TTCL. Ila nasikitika sana kuiona TTCL ikisuasua. Kumbe kuna mafia wanataka kui-dedisha? Very sad! Mlioko huko ndani TTCL fanyeni kila linalowezekana kampuni/shirika hii isife. Iwe fahari ya nchi.
 
Look...TTCL ni kampuni ya simu iliyo na network kubwa nchi nzima.

Tatizo ni maslahi binafsi ya viongozi.

Ukiachana na celtel, ambao walipata free ride kwa miaka ya mwanzo kwa gharama za infrastructure wakihemea kwa ttcl wakati wakijenga ya kwao,ffodaacom ndio sababu ya ttcl kutokunyanyuka.

Bila shaka wajua vigogo ambao wako katika kampuni hii.Wakati wao wanazindua mitambo yao Mbeya na Arusha, ilibidi ya ttcl izimwe kwanza kwa sababu yao ilikuwa na nguvu kidogo(mwingiliano wa frequency)

Sasa niambie nani ana mamlaka hayo ya kutoa order kama hizo kama si vigogo hao?
 
yup! Niliambiwa na moja ya staff kuwa hata TTCL mobile ilicheleweshwa kwa makusudi ili kampuni nyingine zisiende mrama maana ingekuwa cheap sana. Je inawezekana uongozi wa juu kuna mapandikizi yaliyopo kwa interest ya kampuni nyingine?
Hata wafanyakazi wa chini hawapo motivated sana! So what should we do ili tuiokoe kampuni yetu?

Mkuu TTCL ilianza kuhujumiwa tangu kuingia kwa Celtel then Zain now Airtel. Watu hawa walitumia (na wanaendelea kutumia) miundo mbinu ya TTCL huenda kwa malipo kidogo sana au bure kabisa. Na inasemekana mojawapo wa viongozi waliotumika kuihujumu TTCL ni Mwandosya (akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi enzi hizo) na kundi lake (may be Mramba included akiwa waziri wa fedha). Na huenda mpaka sasa wako vigogo wakubwa wenye hisa katika kampuni hiyo wakiendelea kuiwekea mizengwe TTCL isisonge mbele.
 
Shingo,

If all you said is true, basi haitachukua mda kwa TTCL kufa.

Inaonekana hamna wa kuisaidia ukitoa hao wazalendo wachache waliobaki humo ndani.

What are the smartest moves to play on the defense of TTCL?

It's sad kuona bado mtu yuko upande wa CCM na serikali yao na vitu hivi vikitokea.
 
I had time to talk with Some TTCL members/staff in previous time and were not happy that TTCL is not leading. TTCL is the first company to have the biggest network web ever in Tanzania (I believe it still leads). TTCL have independent Internet gateway, TTCL mobile, the news goes on saying, was planned to release its cheapest mobile service in form of TTCL mobile but its release was late and hence missed the business timing....TTCL was tricked into producing enemy of its own by its own costs, that is Celtel then Zain then Airtel Tz.......

Haya maswali niliwai kujiuliza nyuma sana. TTCL ambayo kwa infastracture ilizonazo basi hat akama wameshapigwa bao kwenye VOICE ila kwenye Data yaani interernet wanataiwa kuwa ndio viongozi kwa kutoa Reliable na Cheapest service.

TTCL wanawemza kutoa TRue broadbad DSL service sbabau infastrure zao za lanndline mitaani ziko misused kwa sasa

Mimi nadhani hata ndani ya TTCL kuna watu wanaosabotage tena inawezekan wanapkea mishaahara mara mbili TTCna kwenye kampuni nyingine

Pia wanasiasa wentu ndio hivyo Sabotager( teh teh kingereza hiki) wa kwanza wa makampuni yetu

Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,
  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • ................
Aiseeeee Mkuu inauma sana na inatia hasira
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,
  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
  • Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
  • Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
  • Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
  • Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
  • Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
  • Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
  • Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
  • Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
  • Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
  • Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
  • TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!
Huu si ukweli mdogo. Ikiwa kuna kiongozi yeyote wa serikali (TTCL) ayakane haya. Haki ya Mungu kila yanapozungumzwa madudu ya serikali ninaporomokwa na mabega:sick:. Masikini nchi yetu! Masikini Watanzania!:twitch:
 
Nilikua nashangaa kila siku ni acting CEO. jamani hivi wapi tunakwenda. Raisi anajua amekaa kimya, waziri mpya kaja naye ameka kimya. jaamani muda wa kuanza kazi kama waliyo fanya wenzetu egypt na tuniasia umefika.
 
Mimi kitu ambacho huwa kinaniuma sana kuhusu baadhi ya Watanzania wenzetu ni hili la kukosa uzalendo; si hilo tu vile vile tuna tabia nyingine ya kufanya mbinu za kuwakwamisha wataalamu wa kutoka nje wanapokuja kujaribu kuweka mambo sawa kwenye mashirika yetu ya umma ambayo tumeyafirisi sisi wenyewe.

Chukulia hili shirika la TTCL ambalo lilikuwa na miundo mbinu hiliyo jengwa siku nyingi Tanzania nzima and beyond na lingeweza kabisa kuwapiku cellular operators wote, lakini kwa kukosa uzalendo wakashirikiana na Wachina wajanja kuingiza mfumo wa CDMA ambao walijuwa fika kwamba ni nchi chache duniani zinazo tumia mfumo regardless ya uzuri wake kiusamabazaji mawimbi.

Viongozi walio husika na scam hii hawakuwa na muda hata wa kutumia akili kidogo kwa kujiuliza hivi ni kwa nini CELTEL/ZAIN, VODACOM, TIGO/MOBITEL na Ulaya nzima inatumia GSM na siyo CDMA, kwani wanataka kusema kampuni zote hizo ni wajinga hawajuhi cost benefit za CDMA? Hivi leo hii wanaweza kueleza ni wateja wangapi wanatumia simu zao za mikononi ni mteja gani atakubali kutumia simu ambayo inamfunga kwenye kampuni moja tu. \

Mimi nilitegemea Serikali yetu tukufu ingewachukulia hatua kali watu walio tia Taifa hasara ya kijinga kwa ukosefu wao kuwa Wazalendo wakati walisomeshwa na Taifa hili bure lakini wala hawajali hasara waliyo litumbukiza Taifa hili kimaksudi. Mimi nimesoma hoja zote zilizo andikwa humu kuhusu matatizo ya TTCL, lakini jamani tuwe wakweli tuache kulaumu Serikali; wenye matatizo ni Wakuu wa Mashirika kukosa ubunifu na uzalendo, mimi siamini kwamba wakuu wa mashirika wakienda na maoni mazuri tu ya kuendeleza mashirika yao bila ya kuweka mbele masirahi yao Serikali inaweza kuwakatalia - hiyo si kweli.

Kuna wakati fulani TTCL ilikuwa na wahandisi mahili kuhusu mawasiliano, hawa wangeweza kabisa kununua transmitters/repeaters/antennas, SERVERS na software zake kwa ajili ya kuongozea mfumo mzima wa GSM Network nchi nzima. Shirika lenyewe lilikuwa na minara ya microwave nchi nzima walicho kuwa wanatakiwa ni kuongezea urefu wa minara yao inapobidi ni hiyo ingekuwa ni gharama ndogo tu.

Samahani nita andika maoni marefu kidogo, hii nafanya kwa nia nzuri tu baada ya kuchoshwa na visingizio ambavyo havitajenga nchi hii hata kidogo tunapashwa kubadirika, sina shaka watu watauliza hivi kweli ingewezekana TCCL kununua hivyo vifaa wakavifunga wakawa na network ya GSM? Jibu ni kwamba wangeweza kabisa na wataalamu wa mawasiliano sina shaka wapo wakufanya kazi hiyo. Kumbuka si VODACOM, TIGO, AIRTEL wala ZANTEL wanaunda vifaa hivyo vya RADIO wote wananunua kutoka makampuni ya Motorola, Siemens, Erricsson, Phillips na kampuni za Kichina Huewei na ZTE cha muhimu hapa ni kujuwa utataka mfumo gani wa mawasiliano ya simu na data: CDMA au GSM basi.

Vifaa hivyo vya mawasiliano vinapatikana kirahisi tu na Watanzania wenye huwezo kufanya kazi hii wapo lakini kasumba ya baadhi ya viongozi wa mashirika hawapendi kabisa kuwatumia. Wanao nisikitisha ni wafanyakazi wa kawaida wa TTCL, mimi natoa rahi kwa viongozo wa Shirika hili wawe wabunifu na kuwa na bussiness acumen wahachane na mambo ya kulalamika tu, kama hamko tayari kubadilika sioni mantiki ya kuomba sijuhi mabillioni mangapi kutoka Serikalini eti kufufua Shirika.

Humu nimeandika kwa lugha ya kawaida tu not in technical jargon hili watu wa kawaida tu waelewe ninacho zungumza na kiswahili changu siyo kizuri sana, lakini nafikiri ujumbe umefika, mwisho nisije kueleweka kwamba labda namshambulia mtu binafsi, hapana mimi ninacho fanya hapo ni kusema ukweli kwa ajili ya ustawi wa nchi hii.
 
Tatizo sio ttcl, tatizo mkataba ambao serikali ili ingia na celtel (msi) ambao unaifanya celtel kuwa na share ya 40% ndani ya ttcl, wakati wote wanafanya biashara zinazofanana yaani internet na simu. prof msola alikuwa anataka kuvunja mkataba huo wenye share waliopo serikalini wamehakikisha haludi pale wizarani.( msi) ni warioba, salim, maua daftari,Ttcl kila ikifanya mipango yake msi wanapinga au wanachelewesha inapitwa na wakati, dawa ni kvunja mkataba kati ya TTCL na MSI ili ttcl ijiendeshe yenyewe
Mtaalam, hebu elezea kidogo kuhusu hii kitu MSI. wengi hatuifahamu na mambo yake mbofumbofu!
 
Labda sikusoma vizuri title ya thread! .
SMU,
TTCL ina resources zote na uwezo wa kuongoza ktk soko, si kwa sababu tunataka wawe monopoly bali kwa kuwa resources wanazo. kama wana kila kitu, kwa nini hawaongozi? Ni kama swali la kama sisi tuna madini yoote haya kwa nini ni maskini?
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,
  • Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo
  • Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.
  • Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
  • Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)
  • Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
  • Baadaye TTCL ikanyang'anywa shea zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina shea na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha
  • Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.
  • Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.
  • Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.
  • Mwaka 2007, serikali ikaleta menejinti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.
  • Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.
  • Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)
  • Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzani, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndo wenye mali serikali ni msimamizi tu.
  • Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.
  • TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.
  • Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!
CCM and it all ministers must go!....I feel thirsty, anyone with water?
 
Tatizo sio ttcl, tatizo mkataba ambao serikali ili ingia na celtel (msi) ambao unaifanya celtel kuwa na share ya 40% ndani ya ttcl, wakati wote wanafanya biashara zinazofanana yaani internet na simu. prof msola alikuwa anataka kuvunja mkataba huo wenye share waliopo serikalini wamehakikisha haludi pale wizarani.( msi) ni warioba, salim, maua daftari,Ttcl kila ikifanya mipango yake msi wanapinga au wanachelewesha inapitwa na wakati, dawa ni kvunja mkataba kati ya TTCL na MSI ili ttcl ijiendeshe yenyewe
I will definitely go for this comment ni kweli kabisa tatizo sio TTCL tatizo ni mkataba walioingia serikali na (Celtel to Zain to Airtel) ambao nashindwa kuelewa ni kwanini wao wana shares ndani ya TTCL,hiki ni kitu ambacho kinajulikana na viongozi serikali ambao kwa asilimia kubwa wamechangia kuifikisha TTCL ilipo kwa ajili ya maslahi yao binafsi ni kitu kilicho wazi na hii ndiyo ilimfanya Prof Msola apigwe chini this time maana waliona anataka kuingilia maslahi binafsi ya watu
 
Matatizo ya kiuongozi TTCL yapo ndio, lakini yanaletwa na serikali. Angalia hii;

  • Mwaka 2009, baada ya menejimenti ya wazungu wa Canada kuondoka, TTCL ilibaki bila uongozi. Serikali ikateua menejimenti ya muda.
  • Mwezi October mwaka huo huo, serikali ikatangaza nafasi za kazi za watendaji wakuu wanne; yaani CEO na wasaidizi wake watatu (Finance, Comercial, Technical).
  • Baada ya Mchakato wa muda mrefu, Mwaka 2010 mwezi May Nafasi mbili tu zikajazwa; ya CFO na CTO. Hawa wanaokaimu nafasi za Biashara na Mtendaji mkuu wa kampuni (CEO) wakaambiwa hawajafanikiwa.
  • Hadi leo Januari 30 2011, nafasi hizo hazijajazwa, waliopo hawana authority kwani kazi zilitangazwa wakafanya interview wakaambiwa hawafai. Ila wameachwa waendelee kuwepo wepo tu.
  • Kumbuka hao ambao wapo wapo tu, ndo moyo wa TTCL, yaani CEO na Chief wa Biashara. Kwa hiyo kampuni inaendeshwa bila CEO wala Kiongozi wa biashara kwa sababu waliopo waliambiwa wameshindwa interview, ila hadi leo haijasemwa nani alishinda hizo interview.
  • Uongozi huo ulitakiwa uanze kazi Januari 2010, leo tunaingia Februari 2011 bado uteuzi wa uongozi haujafanyika.
  • Ni kampuni gani inaweza kuendeshwa wakati CEO wake na Mkuu wake wa Biashara wameshaambiwa hawafai kwa mwaka mzima?
  • Tafakari na uchukue hatua!!

:twitch::twitch::twitch: Nashangaa sana ila kuna kitu kuna siku nilienda ofisi za TTCL wafanyakazi wanaonekana demoralized kabisa
 
Mimi kitu ambacho huwa kinaniuma sana kuhusu baadhi ya Watanzania wenzetu ni hili la kukosa uzalendo; si hilo tu vile vile tuna tabia nyingine ya kufanya mbinu za kuwakwamisha wataalamu wa kutoka nje wanapokuja kujaribu kuweka mambo sawa kwenye mashirika yetu ya umma ambayo tumeyafirisi sisi wenyewe. Chukulia hili shirika la TTCL ambalo lilikuwa na miundo mbinu hiliyo jengwa siku nyingi Tanzania nzima and beyond na lingeweza kabisa kuwapiku cellular operators wote, lakini kwa kukosa uzalendo wakashirikiana na Wachina wajanja kuingiza mfumo wa CDMA ambao walijuwa fika kwamba ni nchi chache duniani zinazo tumia mfumo regardless ya uzuri wake kiusamabazaji mawimbi. Viongozi walio husika na scam hii hawakuwa na muda hata wa kutumia akili kidogo kwa kujiuliza hivi ni kwa nini CELTEL/ZAIN, VODACOM, TIGO/MOBITEL na Ulaya nzima inatumia GSM na siyo CDMA, kwani wanataka kusema kampuni zote hizo ni wajinga hawajuhi cost benefit za CDMA? Hivi leo hii wanaweza kueleza ni wateja wangapi wanatumia simu zao za mikononi ni mteja gani atakubali kutumia simu ambayo inamfunga kwenye kampuni moja tu. Mimi nilitegemea Serikali yetu tukufu ingewachukulia hatua kali watu walio tia Taifa hasara ya kijinga kwa ukosefu wao kuwa Wazalendo wakati walisomeshwa na Taifa hili bure lakini wala hawajali hasara waliyo litumbukiza Taifa hili kimaksudi. Mimi nimesoma hoja zote zilizo andikwa humu kuhusu matatizo ya TTCL, lakini jamani tuwe wakweli tuache kulaumu Serikali, wenye matatizo ni Wakuu wa Mashirika kukosa ubunifu na uzalendo mimi siamini kwamba wakuu wa mashirika wakienda na maoni mazuri tu ya kuendeleza mashirika yao bila ya kuweka mbele masirahi yao Serikali inaweza kuwakatalia - hiyo si kweli. Kuna wakati fulani TTCL ilikuwa na wahandisi mahili kuhusu mawasiliano, hawa wangeweza kabisa kununua transmitters/repeaters/antennas, SERVERS na software zake kwa ajili ya kuongozea mfumo mzima wa GSM Network nchi nzima. Shirika lenyewe lilikuwa na minara ya microwave nchi nzima walicho kuwa wanatakiwa ni kuongezea urefu wa minara yao inapobidi ni hiyo ingekuwa ni gharama ndogo tu. Samahani nita andika maoni marefu kidogo, hii nafanya kwa nia nzuri tu baada ya kuchoshwa na visingizio ambavyo havitajenga nchi hii hata kidogo tunapashwa kubadirika, sina shaka watu watauliza hivi kweli ingewezekana TCCL kununua hivyo vifaa wakavifunga wakawa na network ya GSM? Jibu ni kwamba wangeweza kabisa na wataalamu wa mawasiliano sina shaka wapo wakufanya kazi hiyo kumbuka si VODACOM, TIGO, AIRTEL wala ZANTEL wanaunda vifaa hivyo vya RADIO wote wananunua kutoka makampuni ya Motorola, Siemens, Erricsson, Phillips na kampuni za Kichina Huewei na ZTE cha muhimu hapa ni kujuwa utataka mfumo gani wa mawasiliano ya simu na data: CDMA au GSM basi. Vifaa vinapatikana kirahisi tu na Watanzania wenye huwezo kufanya kazi hii wapo lakini kasumba ya baadhi ya viongozi wa mashirika hawapendi kabisa kuwatumia. Wanao nisikitisha ni wafanyakazi wa kawaida wa TTCL, mimi natoa rahi kwa viongozo wa Shirika hili wawe wabunifu na kuwa na bussiness acumen wahachane na mambo ya kulalamika tu, kama hamko tayari kubadilika sioni mantiki ya kuomba sijuhi mabillioni mangapi kutoka Serikalini eti kufufua Shirika.Humu nimeandika kwa lugha ya kawaida tu not in technical jargon hili watu wa kawaida tu waelewe ninacho zungumza na kiswaili changu siyo kizuri sana, lakini nafikiri ujumbe umefika, mwisho nisije kueleweka kwamba labda namshambulia mtu binafsi, hapana mimi ninacho fanya hapo ni kusema ukweli kwa ajili ya ustawi wa nchi hii.

inaelekea una maneno mazuri, ila please hebu weka kidogo paragraphs tusome kwa raha
 
Huwa nikiangalia TTCL, Airtle na historia nikiikumbuka huwa nashindwa kumuelewa Mwandoswa hata kidogo, mnakumbuka ule umbea kuwa mwanae alipelewa na kulipiwa Chuo kikuu nchi fulani hivi, sikumbuki ila ilikuwa skendo kwa wakati ule. (sikumbuki kama alikanusha au la)
Inaniuma sana TTCL, masikini.
Kumbe wahujujumu wake hawajaiachia?
mie ningeomba huu utata uwekwe hadharani na magazeti na media nyingine ili ionekane na wengi, itasaidia kupunguza maamuzi machafu.
asanteni kwa kutujuza uozo wa nchi yetu,
Hivi nasikia kuna mtu competent kutoka Vodacom ameajiriwa kama CEO TTCL, ni kweli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom