Why NoT Jakaya Kikwete

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Jamani mkutano wa G20 unaendelea Canada! wakuu wa nchi hizi tajiri duniani zinaweka mikakati ya kukuza uchumi wa dunia na nchi zao. Nadhani Kikwete angekuwa yuko Canada angetumia muda huo kuomba misaada ya kuinyanyua Tanzania, kama kujenga daraja la Kigamboni, umeme vijijini...hii ingepunguza safari za mkuu wa nchi yetu, maana kuwa Canada angeonana na viongozi hao na kuwapa maombi ya misaada, Obama, Cameroun, Sarkozy wako wote huko. huenda misaada hiyo ingesaidia hata kampeni zake na uraisi na CCM lol.
 
kUPOKEA SIMU TU ANAOGOPA NDIYO IWE KWENDA HUKO?
 
Masa, najua mkuu wa Kaya anatamani angeenda kujua Canada, maana nadhani hajawahi kufanya ziara huko!!!
Huenda hakualikwa..... nahisi pia wakubwa watakuwa wamemchoka na wimbo wake wa misaaada, na umasikini Tanzania!!!

Kwenye issue kubwa kama G20 they are serious with issues not songs!!!!!! Not this singing and dancing :dance:
 
Niliposoma heading kwa mara ya kwanza nilifikiri unampigia debe la uchaguzi (nikachukia kidogo)

Anyway, kule wanaitwa watu "serious" na implementation. The people who walk the talk. Labda angekuwa Bush angemualika.
 
Hahahahaah niliamua kuweka hiyo heading makusudi....Mkuu wetu hana tofauti na Matonya....kila siku mguu na njia eti anatafuta wawekezaji LOL!
 
Masa, najua mkuu wa Kaya anatamani angeenda kujua Canada, maana nadhani hajawahi kufanya ziara huko!!!
Huenda hakualikwa..... nahisi pia wakubwa watakuwa wamemchoka na wimbo wake wa misaaada, na umasikini Tanzania!!!

Kwenye issue kubwa kama G20 they are serious with issues not songs!!!!!! Not this singing and dancing :dance:

Mkulu wetu anaweza kujipeleka tu akizunga anawakilisha nchi masikini sana mradi aweze uza sura na wakuu wengine serious wa dunia!
 
atatuwakilisha dk slaa au mbowe

Aaah MS, umeamka!!
Mimi nilidhani walikupiga zile dawa za vichaa maana nasikia dozi zote za malaria zimedunda!!

Karibu mkuu, sasa hawa watatuwakilisha vipi, si unajua anayealikwa ni head of state?
 
Mkulu wetu anaweza kujipeleka tu akizunga anawakilisha nchi masikini sana mradi aweze uza sura na wakuu wengine serious wa dunia!

Mkuu mimi nahisi wamemchoka!!
Haiwezekani wewe uwe kila sik unalia lia tu!! Yaani ina maana tu wa kutupa kiasi hicho!!!

Jamaa mpaka anaboa.... akiwa nje ya nchi. LOL!!!
 
Mkuu mimi nahisi wamemchoka!!
Haiwezekani wewe uwe kila sik unalia lia tu!! Yaani ina maana tu wa kutupa kiasi hicho!!!

Jamaa mpaka anaboa.... akiwa nje ya nchi. LOL!!!

Jamaa aliniacha hoi alipokuwa kwenye World Economic Forum, Davos, Switzerland...wenzake walikuwa waweka mipango na michakato ya kuku chumi zao mzee mzima anasisitiza misaada na mikopo nafuu. Si shangai alishindwa jibu kwanini Tanzania ni Maskini. Ajabu atarudi tena Madarakani LOL!
 
Masa, najua mkuu wa Kaya anatamani angeenda kujua Canada, maana nadhani hajawahi kufanya ziara huko!!!
Huenda hakualikwa..... nahisi pia wakubwa watakuwa wamemchoka na wimbo wake wa misaaada, na umasikini Tanzania!!!

Kwenye issue kubwa kama G20 they are serious with issues not songs!!!!!! Not this singing and dancing :dance:

Kwenye red: And protecting mafisadi!
 
mwacheni jk aponde nchi, hivi hamuoni kaamua kuinvest bagamoyo kwa nguvu zote? bandari, uwanja wa ndege, viwanda vya kumwaga,, kila kitu sasa ni bagamoyo, kweli kazi ipo.
 
Jamani mkutano wa G20 unaendelea Canada! wakuu wa nchi hizi tajiri duniani zinaweka mikakati ya kukuza uchumi wa dunia na nchi zao. Nadhani Kikwete angekuwa yuko Canada angetumia muda huo kuomba misaada ya kuinyanyua Tanzania, kama kujenga daraja la Kigamboni, umeme vijijini...hii ingepunguza safari za mkuu wa nchi yetu, maana kuwa Canada angeonana na viongozi hao na kuwapa maombi ya misaada, Obama, Cameroun, Sarkozy wako wote huko. huenda misaada hiyo ingesaidia hata kampeni zake na uraisi na CCM lol.

Kikwete angekwenda huko na kuanza kuomba omba angeonekana kituko kweli kwani hao washikaji wake wana matatizo yaliyowazidi kimo; Obama anapambana na deni la Taifa [national debt]n ambayo iko kwenye matrililoni, Cameron ndio huyo ana mzigo wa deni la Taifa pia licha ya zigo la kuinusuru BP na tatizo la Oil Spill huko marekani , Mama wa ujerumani anapambana na weak EURO baada ya GREECE kufilisika!! Msanii wetu wakati wenzie wanapambana na kuwanusuru wananchi wao na ugumu wa maisha yeye anatumia mabilioni kuleta timu ya Brazil!! Kweli Rais tunae.!!
 
Mkuu tatizo sio Kikwete isipokuwa nchi nzima..Kuomba JK awepo Canada ni sawa na kufikiria kwa nini Taifa Stars haikushiriki kombe la dunia..

Waliokutana TO ni nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea....Kama Tanzania ni nchi sijui ya tano toka chini, sio tu nchi maskini bali ni katika nchi zinazozidi kudidimia ktk Umaskini ZAIDI! (mbiu ya JK)..Sasa Unaweza kweli kufikiria kuhudhuria kwaJ K ktk mkutano huu...Kagame angeweza kufikiriwa kabla ya JK..JK ni miongozi mwa Marais wasiofahamika duniani hata huyo mchovu Mugabe yuko juu. Na amini maneno yangu Zimbabwe itakuja kuwa juu yetu tena kiuchumi wala haitachukua muda mrefu.
 
Mkandara! unauchungu na nchi yetu, ila ukiangalia kwa makini sana ni kama kila mtu anapoteza tumaini. Wale ambao tuliwategemea wametuangusha zaidi, sihitaji kuweka mifano hapa. Angalia suala nzima la Dowans ama Richmond utakuwa na majibu. Siasa na mapinduzi ya kifikra hayana uelekeo. Wasomi na waelewa wa mambo wamekuwa wajinga mbumbu wa reli, wengine wapo hapa JF wanatangaza kabisa nia zao za kutaka kuendeleza ufisadi bila kuangalia mtanzania wa kawaida atanufaika vipi walau apate milo mitatu. hatuna uongozi wala uelekeo kama taifa. Kuna siku nilimsikiliza Kikwete akisifu safari zake za nje nilichoka nikaweka TV channel kwenye mambo ya kikubwa walau kujipa raha. Sababu ya hii post yangu nikuonyesha kutoridhishwa na ujinga wa kuamini na kunyenyekea mataifa makubwa kuomba misaada!
 
Mkuu upo sawa kabisa.....Kama watu hawajaelewa maneno ya Nyani Ngabu ya kwamba sisi MIAFRKA NDIVYO TULIVYO, itakuwa kazi kubwa kufahamu mengineyo kwani inachukua muda mfupi tu kumwelewa kwa sababu kila siku hapa JF ni JK hivi JK vile hali hakifanyiki kitu chochote tofauti na yeye..Nchi yetu haikuwa maskini kwa sababu ya JK na wala tusitegemee uongozi bora kutoka kwa JK hali sisi wenyewe hatufahamu zaidi ya kumkosoa JK na ahadi zake..Anaudhi sana JK lakini sisi wenyewe hatuna tofauti naye kabisa..

Frankly speaking, hivi kweli watu waliamini zile ahadi za JK zingetuwezesha sisi kuondokana na Umaskini?..Ile Kauli mbiu ya - Maisha bora kwa kila mwananchi ingeweza vipi kupatikana ikiwa serikali imeshindwa hata kupunguza Umaskini acha mbali kuutokomeza! Haya maisha bora yatapatikana vipi? kwa kugawana umaskini!...

Na zaidi ya yote haya tunampinga JK kwa kila hoja lakini nani kasimama msitari wa mbele kuongoza jahazi hili la kimapinduzi - HAKUNA tunawarudia kuwapigia kura watu wale wale kina Mrema, Mtikila, Lipumba na Cheyo ambao pia hawana vision zaidi ya kukosoa makosa yaliyokwisha tendeka ambayo hata mtu asiyekwenda shule anayaona!

JK ni msanii kweli lakini hana tofauti na sisi wote..jambo ambalo lanifanya niwaamini Wakenya wanapotutukana na kutuita Miswahili ya TZ mineno mingi sana... ndio Usanii huu.. Hivyo tegemeo la JK anapokwenda huko nje ni kufanya kile anachokijua vizuri sana kama mtu maskini na msanii..Hao waliokuja To ni voiongozi waliozikuta nchi zao tayari tajiri au tayari zile ktk kuendelea hawana jipya zaidi ya nguvu iliyokwisha wekwa na wale waliowatangulia.

Obama is who he is kwa sababu ni rais wa Marekani lakini kama angekuwa rais wa Kenya no one would give a damn! Cameron, Harper na wengine woote wamezaliwa nchi zao zikiwa ktk hali nzuri na walio ziwezesha kufika hapo ni wananchi wazawa ambao hawakukubali kudhalilishwa, wakauweka Uzalendo wao mbele ya matamanio, wakapigana dhidi ya adui zao wakubwa ambao ni Umaskini, Ujinga na Maradhi..

Haikuwa coinsidence huduma hizi kuwa ni RIGHT ya kila mwananchi walipoanza kupambana na maadui hawa. Woote iwe Marekani, Uingereza, France na hata Japan wote waliweka huduma hizi kama ni RIGHT ya kila mwananchi na ndilo jukumu la kwanza la serikali ktk uongozi na zilitolewa bure hadi walipofikia kutokomeza maadui hawa na kuzaa Utajiri ndipo walipoweza kubadilisha mfumo huu na kuwa biashara ktk kugawana Utajiri..
Pasipo Uhuru na haki kwa wananchi, kuwana malengo ya kuondoa madhara makubwa ya jamii umaskini hauwezi kwisha kwa kuweka mikakati ya IMF.

Sio sisi Miafrika tumeingia Ubepari majuzi tu na maskini wa kutupa tayari huduma hizi leo ni privilege..How can U eradicate Poverty, illiteracy and Diseases if we treat them as privilege! - Hii ndio akili ya mtu mweusi mkuu wangu.

Kwa hiyo pengine JK, asipoomba omba misaada yawezekana tunakufa njaa..kwani wakati JK anapokwenda kuomba misaada nje sisi uzalishaji nchini unazidi kupungua siku hadi siku na watu wanafanyiza vibaya vibaya... Haya, kila nyumba ya Mtanzania wana vijakazi sii chini ya wawili hali wavivu wa kufanya kazi, wengi wetu ni wavivu wa kujituma kazi kusikikiliza majungu ya Hekaheka na Clouds.

Ajira kubwa mjini ni Ulanguzi na Udalali wenyewe wanasema TUNAZUNGUSHA - lakini hakuna tunachozalishwa zaidi ya kuchukua mali toka kona A hii na kuipeleka kona B tax free, as if Tanzania ni freetrade state...Haya ndio maisha ya Wadanganyika..

Fika mijini utakutana na wasanii watakulilia shida within 2 minutes utaingiza mkono mfukoni na kumwacha na kilo 2..Huyu kwa siku nzima anaweza kuomba omba hivi hadi akapata Tsh10,000 tax free, kipato bora kuliko mfanyakazi ofisa wa benki anayelipwa Laki mbili kwa mwezi na kukatwa kodi..Huu ndio mfumo wa maisha ya Mtanzania wa leo ambaye hana tofauti na rais wake kwa sababu sisi kama wasanii hatuna mbinu kabisa ya kuondokana na Umaskini,Ujinga na Maradhi isipokuwa kwa kuomba msaada. That is reality ambayo hatupendi kuisikia....JK is doing us a big favor!

Na sii kwamba hatuna vichwa, kama ulivyosema wapo tena wengi tu wamejichimbia nyuma ya pazia, wengine wamefukia vichwa vyao mchangani kama mbuni..Mkuu inachosha sana hata kuendelea na mijadalakama hii kwa sababu hakuna tofauti baina ya JK na sisi wenyewe..Waafrika ndivyo tulivyo ina maana moja tu sisi WANAFIKI hata kwa maisha yetu wenyewe (Usanii)..na ndio maana tumeipata laana ya kudumu.
I Dare U all who think or swear they are not -Ndivyo Tulivyo, to stand up and join the fight kinyume cha hapo tusiendelee kujenga usanifu wa kuponda JK na serikali yake hapa kijiweni na magazetini hali nafsi yako haikutumi kujiunga na wenzako kupambana mwaka huu..Na lau kama huwezi basi bila shaka kubali kuwa ktkkundi la Ndivyo Tulivyo...
 
kaaaaaaaaaaaaaziiiiiiiiiii kweli kweli.

we umemuona nani anacheka cheka kule?
 
Back
Top Bottom