Why Mkapa alimchukia sana Chachage Chachage (R.I.P)

nakumbuka wakati ule kulikuwa na "silent killer" ni kumbusheni huyu mwalimu wetu alikufa kufa je? Che che nkpa alihusika?
 
Tukiwa tunaelekea miaka miwili toka Mpiganaji Chachage Chachage Afariki dunia,,Naomba tukumbushane mambo machache yaliyowahi kumkuta au aliyowahi kuyaongea Chachage katika harakati zake...

Moja ya vitu vinavyonifanya leo hii nimkumbuke ni kitendo cha yeye kuchukiwa hadharani na rais wa wakati huo bwana Mkapa hadi kufikia kusema
"Watanzania tusiwe kama Chachage Chachage maana yeye kila siku anakosoa tu na kuangalia mabaya kwa serikali"

Yote hayo yalitokana na chachage kua anapiga kelele sana katika vitendo vyote visivyokua vya kheri kwa jamii ya watanzania.

Je, tukiangalia yanayomkuta Mkapa sasa hivi je, Chachage alikua na uwezo wa kuona mbali zaidi?????

KARIBUNI

Kiukweli jamani tuache masihara, hii mambo ya kudharau wasomi na mawazo ya wachache hata kama yana faida ni kosa kubwa na limekuwa likifanyika ktk awamu zote huku matokea yake yakiwa ni kuongeza umaskini na utegemezi ktk nchi na wananchi kuwa fukara na watumwa ndani ya nchi yao, huu ni mfano mzuri sana kwa jinsi baadhi ya wasomi kwenye miaka ya 90 walivyopiga kelele kukataa utaratibu wa ubinafsishaji, leo hii mashamba yote yaliyokuwa Ranchi za Taifa yamekufa, mashamba ya mkonge, mashamba ya kahawa, mashamba ya ngano, viwanda, mashirika ya uma n.k. manyang'anyi wachache waliiopewa jina la wawekezaji wengine viwanda vimefanywa Gowdown, wanakodisha mashamba kwa wananchi na wameua mashirika yote. Nakumbuka sana kati ya watu waliosimama kidete kukataa Ubinafsishaji ni Marehemu Prof Chachange (rip). Jamii yote iliona kama hana lolote hana chochote. Nakumbuka miaka ile hata Maswali ya ubinafsishaji yalikuwa yanaulizwa ktk mitihani ya form 4 na form 6, tukafundishwa na kukaririshwa vitu vya kipuuzi ambayo leo matokea yake sie vijana tunazunguka na bahasha miaka nenda rudi ajira hakuna, kisa mashirika yamekufa na viwanda vimekufa.
I think we young people need to jump in for the betterment of our sons and daughters, IKIWEZEKANA HATA KWA KUINGIA MSITUNI AISEE, DUH, KWELI INAUMA SANA, SIJUI NANI AMETULOGA WATZ
 
Tukiwa tunaelekea miaka miwili toka Mpiganaji Chachage Chachage Afariki dunia,,Naomba tukumbushane mambo machache yaliyowahi kumkuta au aliyowahi kuyaongea Chachage katika harakati zake...

Moja ya vitu vinavyonifanya leo hii nimkumbuke ni kitendo cha yeye kuchukiwa hadharani na rais wa wakati huo bwana Mkapa hadi kufikia kusema
"Watanzania tusiwe kama Chachage Chachage maana yeye kila siku anakosoa tu na kuangalia mabaya kwa serikali"

Yote hayo yalitokana na chachage kua anapiga kelele sana katika vitendo vyote visivyokua vya kheri kwa jamii ya watanzania.

Je, tukiangalia yanayomkuta Mkapa sasa hivi je, Chachage alikua na uwezo wa kuona mbali zaidi?????

KARIBUNI

Mkapa nae...
 
Back
Top Bottom