Why Foreign Aid is hurting Tanzania and other African countries!

Sijui lini we will learn au lesson. Sikio la kufa....

This methali should be in Tanzanian katiba, ili kujikumbusha majukumu, responsibilities, uwajibikaji(yea, different meaning ili kujikumbusha vizuri)

Perfect say for us...
 
Ndio maana mimi sipendi misaada! Misaada inatufanya tuwe watumwa wa wanaotupatia hiyo misaada. Hakuna uhuru wa kweli kama wewe ni tegemezi!
 
kama si hiyo misada si tutakufa njaa ?

Hatuwezi kufa njaa bali itatufanya tupate akili ya kukusanya mapato kutokana na rasilimali zetu tulizonazo. Fikiria ni matrilioni mangapi tumepoteza through dubious contracts (IPTL, Richmond, Makampuni ya Madini, Makampuni ya uwindaji, TICTS, Kiwira, Agreko, Songas, Netgroup Solution, EPA, Meremeta, Deep Green, Radar, Ndege mbovu ya rais, Ununuzi wa silaha etc). Hizi loopholes zinakuwepo kwasababu tunajua kesho tutapata misaada vinginevyo tungeweka mazingira ya kubana mianya ya rushwa na mikataba mibovu na kuwawajibisha ipasavyo wahusika.
 
Mkuu akili ya kukusanya mapato tunayo sana. Mkapa aliweka base nzuri tu ambayo tuatakiwa kuiendeleza. Tatizo ni kuwa nchi yetu haina uwezo wa kutumia pesa. Tunatumia kwa mambo yasiyostahili. Ukiangalia magari wanayotumia viongozi wetu na yale wanayotumia viongozi wa Uingereza unaweza kusema sisi ni matajiri kweli! Ukiangalia miradi ya wenzetu na ya kwetu utaona kuwa sisi ni wajinga kweli. Mwenye akili timamu hawezi kutupatia fedha ambazo tunachezea au ambazo zinatufanya tuchezee fedha zetu, unless awe na ajedna yake ya siri.
Hii ni blessing in desguise, we have to thank the dutch!
 
Huu uoga wetu unatuponza kweli! In fact unatufanya tunasahau hii misaada mara nyingi wala haiwafikii walengwana zipo taarifa zinazodhibitisha haya. Wacha watunyime! Kama wanakula wachache ya nini? Inatuletea matatizo tuuuuuu! Its hight time wote wajitoe...kisa cha baba kupanga budget huku anachungulia wallet ya baba wa nyumba ya jirani ni nini Hasa! Wengine walipe kodi huko magharibi sisi tusubiri kuomba!
 
Habari yenyewe mboni haieleweki..ipo nusu nusu tu..inaeleaelea..

Mkuu nami nipo njia panda.

Ninajiuliza kwamba je Waziri huyo wa maendeleo wa Uholanzi ana mamlaka ya kufuta misaada ambayo inapitishwa na Bunge?

Na pili je kama yeye anayo hayo mamlaka, basi uendeshaji wa serikali ya Uholanzi ni wa aina ya pekee kiasi cha waziri kufanya maamuzi makubwa kama hayo ambayo yanahusu ushirikiano wa kidiplomasia na nchi maskini ya Tanzania halafu ndio aandike barua kulitaarifu bunge?
 
Kuna vacuum kubwa sana kwenye story nzima..yaani ni balaa..Yanai waziri anajiamulia tu kukata funds? lahaula lakwata..halafu eti sababu ni kuwa Tz sio reliable partner kwa sababu kuna mjasiriamali wa huko amelizwa?

Mi naona nyotanyota tu...
 
Labda sababu zilizopelekea huyo mwekezaji "to loose his investment" zingeelezwa labda tutaweza kung'amua ukweli.
 
Labda sababu zilizopelekea huyo mwekezaji "to loose his investment" zingeelezwa labda tutaweza kung'amua ukweli.

Mkuu kama wewe ni mtanzania na unajua mambo yanaendaje hapa nyumbani basi sidhani kama una haja ya kuuliza hili swali. Kama uko majuu naweza kukubaliana na wewe. Unaweza kujiuliza pia, ni kwanini toka tuanze kupewa misaada umaskini haupungui? na wenyewe wanaona ujinga.
 
Katika link ifuatayo Ubalozi wa Uholanzi unaelezea ushirikiano wa maendeleo na Tanzania au development coorperation.

Kinachotia mstuko ni paragraph ya kwanza kwamba umaskini haupungui!

Average per capita income in Tanzania is US$280 a year. 20% of the population live on less than US$1 a day; 60% on less than US$2 a day. Poverty is not decreasing, despite relatively stable economic growth. Tanzania is IDA-eligible and has LDC status.

Taarifa nzima ni kama ifuatavyo:

Ambassade Dar es Salaam (EN) - Development Coorperation
 
waache waende. wakitupatia msaada kwani ni lazima kuwafaidisha wawekezaji wao? hapo si itakuwa wanauchukua tena ule msaada wao. mwekezaji akija hapa anatakiwa kushindana na wenzake toka nchi zingine na hawa wa humu ndani. akishindwa kushindana, atadondoka na alalem mbele. kwani wao Netherlands hawapati faida yoyote kwetu wabongo? wamekuja tuuu kutusaidia sisi? waache walale mbele, baadaye wao wenyewe watarudi. hapa sina sababu kuilaumu selikali. ni sawa na yule mwekezaji wa uingereza aliyeshitaki Tz kwenye bunge lao kuhusu Benjamin Mengi.
 
kama si hiyo misada si tutakufa njaa ?
Wewe nawe Msaada unakusaidia nini? mimi naona unawapa kiburi tu viongozi kutofanya kazi zao vizuri maana wana cheap sources of fund! (bakuli). Ndio maana kiongozi anaweza kufanya sherehe kwa kufutia madeni? (shame)
Go Go Netherland wakatae na wengine wote watie akili, waje na mbinu za maana au waachie ngazi wachukue wengine?
 
Ndio maana mimi sipendi misaada! Misaada inatufanya tuwe watumwa wa wanaotupatia hiyo misaada. Hakuna uhuru wa kweli kama wewe ni tegemezi!
misaada inawezakumfanya mtu hawe mtumwa kama anaitumia vibaya misaada hio.kama mtu unatumia misaada vizuri basi ni rahisi kujiendeleza na kupunguza mahitaji ya misaada hio.sema kwa vile viongozi wetu wanafuja misaada ndio maana wamekuwa kama watumwa.
 
Kuna vacuum kubwa sana kwenye story nzima..yaani ni balaa..Yanai waziri anajiamulia tu kukata funds? lahaula lakwata..halafu eti sababu ni kuwa Tz sio reliable partner kwa sababu kuna mjasiriamali wa huko amelizwa?

Mi naona nyotanyota tu...
Nadhani maamuzi yalishafikiwa na baraza la mawaziri na yeye waziri alikuwa na wajibu wa kuliandikia bunge kuelezea uamuzi huo (ingawa umepitishwa na baraza lakini unaonekana kuwa ni wa waziri).

Huku nyuma nimezungumza na Mkulo anasema kweli wanazo taarifa za kufutwa kwa msaada kutoka Dutch. Kisa chenywe ni mfanya viashara mmoja wa Kidachi aliyekuwa anataka upendeleo kwenye biashara ya magogo akawekewa ngumu. alifika mpaka kwa Pinda akamrudisha kwa Mwangunga ambaye alisisitiza kuwa ni lazima afuate taratibu na ndio akaamua kuwasiliana na ubalozi wao
 
Ndio maana mimi sipendi misaada! Misaada inatufanya tuwe watumwa wa wanaotupatia hiyo misaada. Hakuna uhuru wa kweli kama wewe ni tegemezi!
Nadhani sasa viongozi wetu wata rudi kutafakari namna ya ku-contain aibu hii.
Nyerere alianzisha siasa ya kujitegemea na tunaipuuza kwa kubariki mifumo ya siasa ya kutegemea misaada.
BAahati mbaya wako viongozi wengi wanao amini kuwa bila misaada tutakufa!
Duniani hakuna kitu cha bure! hatimaye mtu utalipa tu hiyo misaada, kama si wewe basi wanao.
Serikali haiupi kipaumbele mikakati ya biashara na nchi za nje,mikakati ambayo ndio msingi mkubwa wa kuondokana na misaada.Pengine ni kutokana na dhana kuwa kuomba na kukubaliwa misaada viongozi wengi wanaona ni rahisi zaidi kuliko kuweka mikakati ya kibiashara ya kuwawezesha waTanzania wengi, tena wazawa.
 
Nyerere aliwahi kutuambia kwamba haoni tatizo la ujamaa na kujitegemea. Tusipoacha kutumia akili na uwezo wetu kujiendeleza tutegemee aibu kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom