Why Do We Blame God for Catastrophes? Please Help... What do you Think..

Kwahiyo kutokea Austria au Australia (thanks for correction by the way) does it make any difference kwamba ni matakwa ya Mungu au sio?,

Nope, hiyo ya Austria na Australia ilikuwa weka facts sawa. Haihusu katika subject.

Narudia kuandika anayeamini Mungu, yaani muumini; anaamini kila jambo limepangwa na Mungu, mabaya yote yanayotokea ni majaribu. Muumini hawezi kuquestion 'qadar' - uwezo wa Mungu. Utapojikuta unaquestion hili, na kusema kwamba binadamu yu responsible kwa mambo yake, unakuwa unarefute 'qadar' - yaani uwezo wa Mungu, hivyo wewe sio Muumin. Na kama wewe sio muumin, basi mbele ya wenzio- wasio waumini- mtakubaliana kuwa binadamu yuko responsible kwa lolote linalomtokea, zuri au baya.

Kama mchangiaji wa mada hii atakuwa muumini, hawezi kukubali n argument kuwa binadamu yuko reponsible na yanayomtokea, mazuri au mabaya, na kwamba kumlaumu Mungu ni kutafuta kisingizio. Mchangiaji aipokuwa muumini, atasema kuwa mwandishi yuko right, kuwa matukio yanayomtokea binadamu, anayasababisha mwenywe. Hivyo basi, conclusion ya mada hii inakuwa controlled na factors 2, kuwa au kutokuwa muumini.

Kwa mfano, refer kwa post yako inayofuata, tuseme umeanza safari ya kwenda Dodoma, na ikatokea hujafika, sababu kubwa itakuwa Mungu hajajaalia ufike Dodoma, huwezi kuconclude eti ni makosa yako kutokufika Dodoma wakati nia yako ilikuwa hiyo.

Sana tu Mungu akinijalia siku nikija Dom naona zitanikoma..., hivi bado zipo kwa wingi?

please naomba unijibu with any good argument kwamba Mungu alitaka hayo yatokee kwa mantiki gani ?

Una maana gani unaposema nikujibu with good argument? Kama unaona argument zangu sio 'good' ina maana good argument unazijua na unataka kuzisikia kutoka kwangu. Mungu hajapanga bado nikujibu kwa good argument.
 
Kwa mfano, refer kwa post yako inayofuata, tuseme umeanza safari ya kwenda Dodoma, na ikatokea hujafika, sababu kubwa itakuwa Mungu hajajaalia ufike Dodoma, huwezi kuconclude eti ni makosa yako kutokufika Dodoma wakati nia yako ilikuwa hiyo.
Inategemea ni kwanini sijafika Dodoma ?Je sikutaka kukata tiketi ili nisafiri bure lakini konda akanishika akanishusha?
Je nilichelewa kwenda kituoni sababu ya kuchelewa kuamka sababu ya kutokuseti alarm?
Je badala ya kukata tiketi mapema nimengoja mpaka last minute nikakuta tiketi zimekwisha?
Je badala ya kupanda basi ili kusave pesa nimeamua kwenda na baiskeli nikashindwa kufika sababu nimechoka
Badala ya kupanda basi la kwenda Dom kwa makosa yangu nimepanda basi la kwenda Arusha...

Mkuu on all the above issue naona kuna jambo moja tu ambalo limesababisha mimi kutokwenda Dom na kushindwa kula zabibu? nao ni uzembe wangu mwenyewe..
 
Una maana gani unaposema nikujibu with good argument? Kama unaona argument zangu sio 'good' ina maana good argument unazijua na unataka kuzisikia kutoka kwangu. Mungu hajapanga bado nikujibu kwa good argument.
Kwahiyo watu wanavyotukanana humu JF huwa ni mpango wa Mungu?
 
Inategemea ni kwanini sijafika Dodoma ?Je sikutaka kukata tiketi ili nisafiri bure lakini konda akanishika akanishusha?
Je nilichelewa kwenda kituoni sababu ya kuchelewa kuamka sababu ya kutokuseti alarm?
Je badala ya kukata tiketi mapema nimengoja mpaka last minute nikakuta tiketi zimekwisha?
Je badala ya kupanda basi ili kusave pesa nimeamua kwenda na baiskeli nikashindwa kufika sababu nimechoka
Badala ya kupanda basi la kwenda Dom kwa makosa yangu nimepanda basi la kwenda Arusha...

Mkuu on all the above issue naona kuna jambo moja tu ambalo limesababisha mimi kutokwenda Dom na kushindwa kula zabibu? nao ni uzembe wangu mwenyewe..

Basi usimshirikishe Mungu kwa kusema Mungu akijaalia. Sema nisipofanya uzembe nitakuja Dodoma kula zabibu.

Kwahiyo watu wanavyotukanana humu JF huwa ni mpango wa Mungu?

Hapana, ni mpango wa shetani, anayewaletea watu majaribu ili waende kinyume na anavyotaka Mungu.
 
Basi usimshirikishe Mungu kwa kusema Mungu akijaalia. Sema nisipofanya uzembe nitakuja Dodoma kula zabibu.
Sijasema Mungu hausiki katika maamuzi..., namoumba Mungu niamke siku hiyo na Nguvu na bila matatizo.., ila kuzembea kwangu kuseti alarm ili niamke na kupanda basi la Arusha badala ya Dom siwezi nikalaumu kwamba Mungu hakutaka niende Dom
 
Kwahiyo kipimo cha mke/mume kutoka kwa Mungu au kutokutoka kwa Mungu ni furaha au huzuni katika ndoa ?, Kumbuka kuna mambo ambayo hayavumiliki mfano abuse (mental and physical) sidhani kama Mungu atapenda yeyote akumbane na haya majanga, na hawa wanaopiga wake zao nadhani ni ushetani/ukichaa uliowakumba ukubwani

Je hawa tuseme Mungu amewatenga ili wasipate wenza wao, au atawachagulia watakaovumilia kuwa abused ? Na ninajua kuna Dini haziruhusu Divorce.., je unapogundua kwamba huyu sio chaguo la Mungu utafanyaje ili uombe Mungu akupe chaguo lako?

Kama nilivyosema tangu mwanzo,
Mungu anatupenda na anatuwazia mawazo ya Amani. Ikiwa tuitii sauti yake na matakwa yake.
Na hata kama tunakosea tukirudi na kutubu anatusamehe.

Ni kweli kuna wakati Mungu anatujaribu, au anaruhusu jaribu, lengo ni kutuimarisha katika Imani, na kutupa nguvu ya kumtafuta kwa juhudi zaidi. Na Mungu yeye hawezi kutujaribu kupita tuwezavyo, anatupa jaribu sawasawa na kiwango cha Imani tulicho nacho.
Na lengo la Mungu sio tusishindwe bali tushinde. Biblia inasema hivi. HATA PAMOJA NA HILO JARIBU NITAFANYA MLANGO WA KUTOKEA.
Refer hata ile safari ya wana Israel, walipokuwa wanatoka Misri. Walipitia majaribu mbalimbali tena mazito, lakini yale yaliwafanya wamheshimu Mungu, nakumuona wa pekee, na msaada katika shida. Angalia maisha ya Mfalme Daudi, alipita katika mapito lakini yeye anamtukuza Mungu kwa nyimbo na Zaburi kwa sababu alimuokoa katika mapito yote aliyopitia. Kwa hiyo majaribu au Mitihani inayotoka Kwa Mungu mwisho wake ni faida na wala sio hasara.

Kuna majaribu yanayotoka kwa shetani, na yanayotokana na Tamaa zetu wenyewe. Biblia inasema Mtu hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe na kudanganywa. Tamaa mbaya inakuongoza kufanya dhambi na dhambi ikikomaa inazaa mauti.
Na mwisho wa tamaa mbaya matusi, dharau, vinyongo, visasi, mauaji, na mambo kama hayo ndiyo Mauti yenyewe iliyozaliwa na dhambi.

Kama wakati unakwenda katika uovu wako, ukagundua ukarudi kwa Mungu na kutubu na kunyenyekea Mungu ni wa Rehema, anakusamehe,
na maisha yanakuwa ya furaha tena katika Mungu wako.

Kipimo cha furaha na Amani katika nyumba ni UWEPO WA MUNGU KATIKATI YENU. Ni namna gani mnamshirikisha Mungu katika furaha na shida zenu.
NI vipi mnamuona Mungu wa maana katika kusimamia maisha yenu.
Hata kama unafika mahali unashindwa kuishi na mwenzako, lakini ukiwa uko karibu na Mungu atakuongoza ufanye nini, uondoke,
au amrekebishe amuumbe upya ili mfanane?

Kwa hiyo mimi bado naamini Mke/Mume Mwema kwako/kwangu lazima atoke mikononi mwa Mungu, ili awe sababu ya furaha na Amani yangu.
 
Hapo kwenye Bold unasema Mambo yakienda Vibaya kwenye Ndoa tunaweza kuomba Mungu ambadilishe mwenza, au uondoke (divorce)...., Je huoni hiyo ni kama short cut ya sisi kutokuvumilia shida zetu na kuachana kwa kusema kuwa Huyu hakuwa chaguo la Mungu... Ofcourse majaribu yapo na ndio maana wana Israel waliendelea na safari yao wangesema haa tumechoka ngoja turudi..., Je nao wangeweza kusema kwamba Mungu Hakutaka tufike ?

Point yangu ni kwamba binadamu wengi wameshajiwekea excuse kwamba mambo yakiharibika wanasema ni upendo wa Mungu wakati kumbe hawakufanya bidii mpaka mwisho wa kipimo chao.., je unakumbuka ile hadithi ya talanta (vipaji) ambavyo walipewa watu ili wazalishe.., mwingine akaziweka, mwingine akazalisha na mwingine akazitumia na kupata hasara ?
 
Ni kweli VOICE, sasa napata jawabu la swali lako, halafu nalielewa swali lako vizuri nafikiri.
Kuna mpango wa Mungu, wa Mwanadamu na wa Shetani!!

Biblia inasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe!!

So ukishindwa kufanya mambo kwa busara, hekima na maarifa ukifeli, Usimlaumu Mungu!!
Mshinde shetani kwa kuzitii sheria za Mungu, ili akuwezeshe kushinda hila za huyo mwovu shetani.

Ukisoma biblia kitabu cha YONA, utaona jinsi Yona alivyokataa maagizo ya Mungu akaenda Tarshishi badala ya Ninawi,
lakini Mungu alimrudisha kwa gharama ya gharika na kulala kwenye tumbo la samaki siku tatu mpaka alipotapikwa pwani ya NInawi.

Sasa basi, kama utakuwa umeingia kwenye ndoa na mtu ambaye sio sahihi, Mungu anaweza kukutoa huko kwa gharama yoyote!!
Kwa maumivu na kumezwa na samaki ili mradi kusudi la MUngu litimie. Kama Mungu anaona kabisa Voice kuishi na mimi sio furaha yako na mwisho wako utakuwa mbaya lazima atanitenganisha na wewe!! Na hii ni kwa sababu wakati mwingine tunafuata mapenzi yetu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu.

Na haya mambo yamekaa kiimani zaidi, inatakiwa kumwamini Mungu na utendaji kazi wake, kuelewa ukuu na uweza wa Mungu pamoja na kuamini kuwa yeye yupo na anafanya mambo. Binafsi naamini hivo.
 
Na haya mambo yamekaa kiimani zaidi, inatakiwa kumwamini Mungu na utendaji kazi wake, kuelewa ukuu na uweza wa Mungu pamoja na kuamini kuwa yeye yupo na anafanya mambo. Binafsi naamini hivo.

Ni kweli haya mambo ni ya imani zaidi, na Mungu anaweza yote.., umesema labda ukipata Mme ambaye sio chaguo la Mungu anaweza akakutoa kwa Gharama yoyote (lakini huoni kwamba mambo yote yanayotokea kwenye ndoa ni majaribu ambayo yapo kwenye ndoa zote na inabidi tuyategemee na tushukuru tu kile tunachopata) Mfano ukifiwa na Mwenza... (Binadamu wote tutakufa.., hilo ni jambo la kawaida na sio kwamba litakukuta peke yako ila ni kuomba litokee later na sio sooner). Ugomvi mwingi ndani ya nyumba (mkiwa wastaarabu basi mtasolve mambo yenu na mtaishi kwa raha).., mmoja wenu kuwa tasa na kukosa watoto (uzuri mnaweza mka-adopt mtoto na mkampenda kama wenu na mkaendelea na maisha yenu vizuri) Kwahiyo am sure mkifata Imani yenu na mkaishi vizuri kama wanandoa nadhani mtafanikiwa na ndoa yenu itakuwa na Baraka.... Tatizo watu wengi wanadhani wenyewe ndio wanamatatizo kwenye ndoa zao na hawajui popote watakapokwenda matatizo yatakuwepo tu... Kuna huu Msemo.....

"If we are threw our Problems in a Pile, and Saw Everyone Elses...., Most of Us Will Grab Ours Back and Depart....."
 
Ni kweli haya mambo ni ya imani zaidi, na Mungu anaweza yote.., umesema labda ukipata Mme ambaye sio chaguo la Mungu anaweza akakutoa kwa Gharama yoyote (lakini huoni kwamba mambo yote yanayotokea kwenye ndoa ni majaribu ambayo yapo kwenye ndoa zote na inabidi tuyategemee na tushukuru tu kile tunachopata) Mfano ukifiwa na Mwenza... (Binadamu wote tutakufa.., hilo ni jambo la kawaida na sio kwamba litakukuta peke yako ila ni kuomba litokee later na sio sooner)."[/SIZE]

Yes kuna majaribu na mapito mbalimbali na yote ambayo Mungu ameyaruhusu anayatoa kwa wakati na yanakwisha kwa wakati, na mengine anatupa neema ya kuchukuliana nayo. Na ndio maana mi narudi palepale kwamba Mungu anajua kabisa wewe Voice kwa kiwango cha Imani ulichonacho unaweza kuchukuliana na utasa wangu (mfano lol), lakini mtu mwingine kwa sababu ya imani yake changa na uwezo wa moyo alionao kuwa mdogo anashindwa kuchukuliana na utasa wangu, nyumba inakuwa na vurugu na hatimaye lazima tuachane au tuishi mradi liende, lakini na yeye akatafute mtoto wa damu yake.

Tukija kwene swala la kifo, bado naamini Mungu anajua mwanzo wetu na mwisho wetu, na Mungu anajua kabisa baada ya mwaka mmoja wa ndoa Voice ataondoka, ataniandaa kiimani kukabiliana na ile hali ya ujane, atanipa moyo wa kumuamini yeye na kuona kuwa yeye ni mume wa wajane!! Atanipa neema yakuchukuliana na hiyo hali.

Na ndio maana kuna mtu anaweza akafiwa na mume wake na akakaa kwa uaminifu kabisa bila kuolewa tena mpaka kifo chake.
Na kuna mwingine hawezi kutokana na jinsi alivyoumbwa na kiwango cha Imani yake, basi Mungu anamfungulia mlango anaolewa tena.

Daaa matendo ya Mungu yanatisha kama nini. Na Mungu hafanyi mambo kwa kubahatisha, hasa ikiwa umekabidhi maisha yako kwake na unamwamini asilimia mia moja. Nampenda Mungu.
 
Nampenda Mungu Pia LD;
Hivi huwa tunaumbwa na Imani au tunapata Imani ulimwenguni kutokana na Mafunzo ? (mfano ningezaliwa China huenda ningekuwa Budha, India ningekuwa Hindu na Imani zangu zingekuwa tofauti)

Na kwa mtaji huo kama tuna excuse ya kutokea kwamba makosa haya ya ndoa kuharibika ni sababu ya kuwa na mtu ambae Mungu hakunipangia..., nitatofautisha vipi kwamba sio shetani ameingia kwenye ndoa au ni majaribu ambayo Mungu ananipa au sisi wenyewe kukosa maadili ya ndoa au ujana unatusumbua ?
 
UBARIKIWE KWA SABABU UNAMPENDA MUNGU,
Kama nilivyosema majaribu yanayotoka kwa Mungu yana faida ya kutuimarisha na huwa yanaisha, hayadumu, ni swala la wakati fulani tu.

Lakini haya mengine yanayotokana na nafsi zetu, shetani na tamaa zetu, mara nyingi yanaumiza sana, hayatujengi kiimani, na mwisho wake mara nyingi huwa mbaya. Labda Neema ya Mungu iingilie kati.
 
Back
Top Bottom