Why Do We Blame God for Catastrophes? Please Help... What do you Think..

Kwahiyo mimi naamini vitu ambavyo vingeleta matokeo tofauti kama binadamu angefanya kitu tofauti na alichofanya ni makosa yetu wenyewe kwahiyo tuache kulaumu huyu au yule...achilia mbali Mungu!Kwenye psychojia kuna kitu kinaitwa attribution factors..kama binadamu we attribute our failures to situational factor(tunajiaminisha kwamba hatukua na uwezo wa kubadili kilichotokea..it was bound to happen)..Mfano wa mtu aliyefeli mtihani hapa atalaumu mwl...muda..ugumu wa somo badala ya yeye mwenyewe!
 
Jamani ni swali tuu nauliza, hivi harufu ya sigara na pombe inaweza toka kwa kupiga mswaki??? Sivuti sigara na wala sinywi pombe. Just curious

Maybe not lakini mvuta sigara nadhani akila chewing gums, kutokuweka sigara kwenye nguo, usafi wa nguo nadhani unaweza kusaidia.., kwani harufu ya pombe huwa haitoki ?
 
Mimi ninachoamini ni kwamba Mungu amzibii mtu.., ukifanya jambo kama linavyotakiwa lifanywe basi litafanikia.. (ndio maana hata mafisadi na majambazi na watu wabaya pia wanafanikiwa).. sababu wanafata kanuni za kitu wanachofanya zinavyotakiwa zifanywe...., Imani yangu ni kwamba hata wewe leo ungefata steps zote za Bill Gates kama alivyofanya hatua kwa hatua (with the same attitude) na wewe leo ungekuwa kwenye shoes za Bill Gates..., na Bill angefata yote ambayo wewe umefata mpaka leo dakika hii angekuwa anayo yote ambayo umeyapata wewe....,
The Choices we Make Today is What Determines the Opportunities and Blessings we will achieve tommorrow.

Si swala la choices we make???

Kuna blessing za Muumba, kuna watu wanapata wakifuata kanuni zote na kuna watu wanakosa hata wakifuata kanuni zote

Kuna watu wanapata zaidi ya walivyoomba au kufanyia kazi kuna wengi wanaomba na kufanyia kazi hawapati au wanapata kidogo

Assuming kwamba hakuna uzembe wowote unafanya Muumba anaweza kukupa (kiasi) na akampa mwingine zaidi yako japo amefanya kidogo tu na akili zake pia si kama zako...

Binadamu ni ndege anayeruka asubuhi hajui apate wapi riziki yake (juhudi yake ni kutoka tu) anakutana na malisho anayomruzuku Muumba

Usijidai unapopewa ujue upo kwenye mtihani na usisikitike unapokosa ujue uko katika mithani (given hufanyi uzembe, etc) hii itakufanya uwe huru na amani tele
 
Mkulima VoR, wewe huamini Mungu na uwepo wake, so huwezi kumlaumu Mungu. Wanaomlaumu Mungu, ni wale wanaoamini kuwa yupo, na imani zao ndivyo zilivyowafundisha.
 
Hus.., Mfano nimeomba mkopo benki nifanyie biashara lakini, badala ya kufanya biashara nimefuja mali hizo nyumba imepigwa mnada (huyo ni Mungu au Uzembe wangu)?

Badala ya kulala na Chandarua nimeacha mbu wameniuma nimepata malaria
Ukiwembe wangu umepelekea nimepata ukimwi
Kuendesha gari kwangu huku nimelewa kumenifanya nipate ajali na kupooza mwili
Mapepe yangu yamefanya mke na watoto wanikimbie
Kuacha jiko la gesi limewaka kumepelekea nyumba yangu na mtaa mzima kuungua moto
ulevi wangu umepelekea nifukuzwe kazi

Haya Hus.... hapo kweli tunaweza kusema Mungu ndio kaleta hayo majanga au kauzembe kangu ndio kamesababisha?

mungu anatupa nafasi na uhuru wa kufanya tunayoyataka. Hakushiki mkono ukachukue mkopo wala ukazini lakini anatuwezesha kufanya tunayopendezewa nayo na anatusikiliza na ndio maana hata majambazi humuomba mungu wafanikiwe wakienda kuiba na wanafanikiwa.
Kwakila unalolifanya mungu yupo nyuma yako maana yeye ndio anakuwezesha kufanya unayoyafanya.
 
Si swala la choices we make???

Kuna blessing za Muumba, kuna watu wanapata wakifuata kanuni zote na kuna watu wanakosa hata wakifuata kanuni zote
Mkuu ninakubaliana na wewe in so far as Talent kuna mambo ambayo wote hatuwezi kufanya kutokana na maumbile au upeo wetu wa kufikilia.., mfano sio wote wanaweza kuwa Mohammed Ali au Mike Tyson, au Sio wote wanaweza wakawa waimbaji au wanamichezo au waandishi wa vitabu wazuri, hapo ni kwamba unahitaji Talent (kipaji), Exceptional Ability..

Lakini normal day to day things ni wewe mwenyewe juhudi zako ndio zitakufikisha unapotaka kufika.
 
Mkulima VoR, wewe huamini Mungu na uwepo wake, so huwezi kumlaumu Mungu. Wanaomlaumu Mungu, ni wale wanaoamini kuwa yupo, na imani zao ndivyo zilivyowafundisha.

Mkuu hiyo article sio mimi niliyoiandika nimeqoute kutoka kwenye article na mwandishi wa article ameqoute kutoka kwenye Bible Old Testament ambayo am sure haina tofauti sana na Quoran
 
mungu anatupa nafasi na uhuru wa kufanya tunayoyataka. Hakushiki mkono ukachukue mkopo wala ukazini lakini anatuwezesha kufanya tunayopendezewa nayo na anatusikiliza na ndio maana hata majambazi humuomba mungu wafanikiwe wakienda kuiba na wanafanikiwa.
Kwakila unalolifanya mungu yupo nyuma yako maana yeye ndio anakuwezesha kufanya unayoyafanya.
Kwa mtaji huo basi mambo tunayofanya yasipofanikiwa kabla hatujamlaumu Mungu labda kwanza tuangalie tulivyoyafanya labda hatukuyafanya yalivyopaswa
 
Mkuu ninakubaliana na wewe in so far as Talent kuna mambo ambayo wote hatuwezi kufanya kutokana na maumbile au upeo wetu wa kufikilia.., mfano sio wote wanaweza kuwa Mohammed Ali au Mike Tyson, au Sio wote wanaweza wakawa waimbaji au wanamichezo au waandishi wa vitabu wazuri, hapo ni kwamba unahitaji Talent (kipaji), Exceptional Ability..

Lakini normal day to day things ni wewe mwenyewe juhudi zako ndio zitakufikisha unapotaka kufika.

Juhudi si lazima zikufikishe unakotaka kufika?? (unaweza kufika unakotaka ikiwa Muumba ameamua ufike)
 
Mkuu hiyo article sio mimi niliyoiandika nimeqoute kutoka kwenye article na mwandishi wa article ameqoute kutoka kwenye Bible Old Testament ambayo am sure haina tofauti sana na Quoran

Kama sio wewe umeandika, unasimamiaje maudhui ya mwandishi. Ukitaka kusimamia argument hizi kuvaa uhusika hakuepukiki. Kama unamwamini Mungu hutakubaliana na huyu mwanadishi, kama la, basi unakubaliana na mwandishi.

Having said that, yeyote anayeamini uwepo wa Mungu anaamini kuwa kila jambo linasimamiwa na Mungu, ni mapenzi ya Mungu. Asiye amini Mungu, hana sababu ya kuamini katika mapenzi ya Mungu kwenye kila jambo, atasema Mungu anasingiziwa na binadamu kwa makosa yao.
 
Mkuu ninaamini in so far as mambo mengi tunayofanya ni makosa yetu wenyewe lakini tunamlaumu Mungu.., Lakini point yako ya kwamba anayeamini haya basi hana imani na Mungu ndio sikubaliani nayo sababu mwandishi ni muumini mzuri tu na amejaribu ku-qoute mistari ya kwenye Bible.., na sidhani kama kuna mstari wowote kwenye kitabu cha dini kwamba mambo yote ya ajabu yanayofanyika ndio Mungu anasababisha... So from your argument wale waliozika watoto wachanga mwananyamala naye alikuwa Mungu.., Je yule mtu Australia aliyezaa na mtoto wake wa kike kwa kumweka kwenye basement kwa miaka mingi na kumfanya kama mke wake ?... Mmmh What do you say Mr. Uwiano ?
 
Juhudi si lazima zikufikishe unakotaka kufika?? (unaweza kufika unakotaka ikiwa Muumba ameamua ufike)
Ofcourse juhudi sio ingridient pekee.., lakini tofauti na wengine wanavyosema kila mtu anayo fair share ya mambo yote, (mazuri na mabaya), mfano wote tukilima shamba sawa, mvua sawa, sehemu sawa, mbegu sawa na mazingira yanayofanana basi mavuno yetu yatakuwa sawa....
 
Mkuu ninaamini in so far as mambo mengi tunayofanya ni makosa yetu wenyewe lakini tunamlaumu Mungu.., Lakini point yako ya kwamba anayeamini haya basi hana imani na Mungu ndio sikubaliani nayo sababu mwandishi ni muumini mzuri tu na amejaribu ku-qoute mistari ya kwenye Bible.., na sidhani kama kuna mstari wowote kwenye kitabu cha dini kwamba mambo yote ya ajabu yanayofanyika ndio Mungu anasababisha... So from your argument wale waliozika watoto wachanga mwananyamala naye alikuwa Mungu.., Je yule mtu Australia aliyezaa na mtoto wake wa kike kwa kumweka kwenye basement kwa miaka mingi na kumfanya kama mke wake ?... Mmmh What do you say Mr. Uwiano ?

Hapa unadhihirisha kuwa wewe si muumin, waumini hawamquestion Mungu, kila jambo ni mapenzi ya Mungu, mabaya ni majaribu na mazuri yamepangwa. Kwa mantiki hiyo, mchango wako kwenye mjadala kama huu utakuhesabu upande uliosimamia kwa sababu katika mambo ya imani unaweza kuwa moto au baridi, ukiwa vuguvugu huhesabiwi katika makundi hayo mawili.

Okay, kuhusu issue ya baba kumfungia mwanae basement na kumzalisha watoto kadhaa, ilitokea Austria na sio Australia. No kangaroos in Austria.
 
Okay, kuhusu issue ya baba kumfungia mwanae basement na kumzalisha watoto kadhaa, ilitoketa Austria na sio Australia. No kangaroos in Austria.

Kwahiyo kutokea Austria au Australia (thanks for correction by the way) does it make any difference kwamba ni matakwa ya Mungu au sio?, please naomba unijibu with any good argument kwamba Mungu alitaka hayo yatokee kwa mantiki gani ? na wewe hapo nikikuuzi ukaamua unitukane kwenye hii post je ni matakwa ya Mungu..? infact where do we draw the line kwenye matakwa ya mungu na ushetani na ukichaa wetu sisi wenyewe?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom