why do u cheat??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,052
--una roho ya uzinzi??
--mkeo/mumeo kakuudhi??
--una laana ya kutoka nje ya ndoa kwenu??
--ukuwa umejiandaa kuoa/kuolewa sasa cha moto unakiona??
Goodmorning
najua na mengine mengi tu yawezekana wewe ni muathirika wa kutoka nje ya ndoa....ndugu zangu leo hii tuanze kuangalia jinsi gan ya kutatua matatizo ya watu ili tuwe na baraka majumban mwetu..akuna anaependa kuona wanandoa wakiwa kwenye magari wakiangalia opp sied like if jaman nafika saa ngapi...ni kweli atukatai ndoa ni nzito na ngumu na inaitaji swala la commitment kweli na si kuoa ama kuolewa sababu babu bibi amezeeka asife bila kumuona mjukuu wapo wanaooa kwa sababu ndugu wote wameoa ama kuolewa bado yeye,wapo wanaofunga ndoa sababu ya kutoa GUNDU kwenye familia yaani kwao akuna aliewahi kusikia ndoa wote wanazalishwa/wanazalisha majumban mwao na kuendelea kuishi bila ndoa wachilia kubariki hata baada ya kujifungua....lakini je haya yote yanatulazimu kucheat na hili ndio soln ya ndoa yenye matatizo..la hasha kwenu wapendwa binafsi naomba nianze kwa kusema kucheat sio soln ya shida zilizopo kwenye ndoa..zitabaki hiyo hivyo na haziishi zaidi ya kuongeza matatizo anyway sihukumu kwa kucheat la hasha Lengo ni kupata sabbu za kucheat ba ukiwa kama mwanandoa angalia sababu hizi na uangalie tutasaidianaje kuachana na kucheat....
 
Pdidy nadhani ndoa yako ni paradise ndogo
hebu saidia hiyo namba mbili tunaitatuaje ?
 
Pdidy nadhani ndoa yako ni paradise ndogo
hebu saidia hiyo namba mbili tunaitatuaje ?

my dear FL1

hii ni kwa maombi huku akitumia juice ya alovera yenye kopo la rangi ya njano usiogope bei inasaidia kuweka brain stable kwa ajili ya mitikisiko ya ndoa, naona hata tukimjazia neema za ndoa atabaki na nature na anapoelekea atakwambia MR II Baada ya nature,ngoja tusubiri ma dear wengine tutajazia
 
Pdidy nadhani ndoa yako ni paradise ndogo
hebu saidia hiyo namba mbili tunaitatuaje ?
km njia za kidplomasia hazifai au hazilet muafaka kwa pbm hii basi shost anza kuhudhuria mazoez na matumla then akikuudh mpango kamili...nkitaka kuolewa natafuta mwanaume mwembaaaaaaaaaaaaa yan kanyorodeka then akiniboa ahh namkata mangumi ..nazani njia nzuri katika kukinga presha na stress za apa na pale
yan ntakuwa nakiduuuuuuuuuuuunda vya kutoshaaaa....ha wanachosha awa watu kazi itakuwa iyo tu!!!!!
 
Ni kuendekeza tamaa zetu na hapo hapo hatutaki kusikia wake zetu wanafanya tunayofanya shows how selfish we are kila mtu ana uwezo wa kuweka mambo sawa bila kucheat ila tatizo linakuja kama mmojawapo ana kiburi na mara nyingi ukianza kuonja nyama za watu huachi( si unajua yale mambo ambayo watu hawafanyi ndani hukoo sasa) hata ukipewa cha kwako utaona bado kuna kitu unakosa kutulia tena ina kuwa ngumu
 
uzinzi tu ndo unawasumbua hamna lolote,
ulimbukeni wa kushindwa kucontrol tamaa za kimwili,
kutoka nje ya ndoa yako takatifu ni ushamba,period!
 
km njia za kidplomasia hazifai au hazilet muafaka kwa pbm hii basi shost anza kuhudhuria mazoez na matumla then akikuudh mpango kamili...nkitaka kuolewa natafuta mwanaume mwembaaaaaaaaaaaaa yan kanyorodeka then akiniboa ahh namkata mangumi ..nazani njia nzuri katika kukinga presha na stress za apa na pale
yan ntakuwa nakiduuuuuuuuuuuunda vya kutoshaaaa....ha wanachosha awa watu kazi itakuwa iyo tu!!!!!

Kumbe haujaolewa okay subiri uolewe basi, uanze pia kumdunda kabla hajakuoa sawa mama
 
People cheats because INFIDELITY created opportunities for it...! And the only solution is completely eliminating INFIDELITY within our families...!
 
mithali 6:26

kwa malaya mtu hutiwa ktk hali ya huitaji kipande cha (mkate),na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani

6:29

ndivyo hivyo amuingiliaye mke wa jirraani yake kila amgusaye huyo atakuwa na hatia

6:32
AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA AFANYA JAMBO LITAKALOMWANGAMIZA MWENYEWE

BADO UNA NAFASI YAMSAMAHA UKIAMUA KUTUBU LEO NA KUACHANA NA UZINZI
 
1-Maisha ndiyo yanayosababisha!
2-New generation
3-Hakuna ugumu kutongoza
4-Muingiliano wa maisha unasababisha
5-Nenda mwenge jioni uone watoto!au kaa posta.....lakini hata zamani kwenye vitabu vitakatifu kuna vifungu watu wanaelezea jinsi watu walivyo opoleana why now??
Hizo ndo sababu za msingi!kikubwa ni No2
 
Sometimes wanandoa wanafanya kukomoana,kwwa kumnyima mwenzake,what do you expect???akitoka akitokea mtu hata hatumii nguvu nyingi kumshawishi,na akionja nje tu anapewa vyote anachanganyikiwa.Hivyo suala la kunyimana wakati mmeoana ni sababu mojawapo ya kufanya wanandoa watoke nje.Ongeeni mambo yenu wawili,kama hujaridhika,au kutosheka usiogope kumweleza mwenzi wako.
Sababu ni mtu kusafiri na kuwa nje na mwanandoa mwenzake kwa muda mrefu,kuna wakati nilisafiri nikawa nairobi kwa wiki mbili,fikiri baridi ya nairobi,unakula vizuri na kulala maana ilikuwa ni workshop iliyokuwa inaisha saa tisa kila siku.
Sababu nyingine ni vishawishi tu.Mfano oficn kulikuwa na mama mmoja aliyeolewa,kukawa na kijana mmoja akawa kila siku anamweleza yule mama kuwa najua una mme ila nakupenda,yule mama alikuwa mkali ila yule kijana aliendelea kumweleza kila alipomwona,Haikuchukua mwaka yule mama alimkubalia yule kijana,kuanzia hapo ndio mwanzo wa kutoka nje ya ndoa yake na hakuacha.
Sababu nyingine ni kuwa mtu anaweza kutoka nje ya ndoa il kulinda kosa lake,kuna dada alipewa gari na mume wake,mumewe akasafiri,huyu dada akitokea kazini akagonga gari nyingine,sasa katika ugomvi akampigia simu kijana wanayefanya naye kazi ili aje kumsaidia katika ule ugomvi,jamaa alikwenda kumsaidia kutoa gari na kupeleka gereji,jamaa baada ya msaada huo naye akaomba msaada mwingine,ndio mwanzo wa kutoka nje ya ndoa.
Ziko sababu nyingi,ila dawa ni KUMTANGULIZA MUNGU KATIKA MAMBO YOTE.Maana hatuwezi kuwazuia kutoka nje ya ndoa,wewe mwanaume unaweza ukawa mwaminifu mkeoje??mwanamke aweza kuwa mwaminifu mumeoje? Na sio kwamba wanaume ndio wanaotoka nje ya ndoa tu,wanawake wanaotoka ni wengi mno sema tofauti yao na wanaume ni kuwa wao wanaweza kuficha siri na huwa wanajificha sana.
 
Sababu ni mtu kusafiri na kuwa nje na mwanandoa mwenzake kwa muda mrefu,kuna wakati nilisafiri nikawa nairobi kwa wiki mbili,fikiri baridi ya nairobi,unakula vizuri na kulala maana ilikuwa ni workshop iliyokuwa inaisha saa tisa kila siku.


HII MKUU NI UZINZI PURE..WAPO TUNAKAA NJE KWA TRAINNING MIEZI KADHAA NA KWENYE BARIDI LKE SAFRICA NA BADO MUNGU ANAMTULIZA JOGOO WANGU SO UKIAMUA SIZINI UNAWEZA HATA UKAE NJE MUDA GANI

UKIANGALIA HAPO JUU SABABU KUBWA NI TAMAA YA MWILI AKUNA LINGINE...TUZIID KUMTAZAMA MUNGU
 
Mm nashindwa mumkatalia X wangu maaana sikuwahi kumchukia. Akitaka nampa .Kwake yeye hacheat .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom