Why did you get married?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Ndugu wapendwa
asaalam alheikum,BWANA YESU ASIFIWE...wapendwa naomba leo hii tuanze kutafuta chanzo cha ndoa kuharibika ovyo ..ndoa nyingi za leo hii zimepewa jina la kileo azikai muda wanaachana wengine wanadai love is blind..sasa labda kuwasaidia wale walio njian kwenda kupanda hili basi la NDOA Embu wanandoa tusaidiane kuelimishana kwa nini umeoa??ama umeoolewa??

Yawezekana tunalalamikaa lakini src ni sababu ya ndoa..wengi wanakuwa na mawazo haba labda muda wa umri umeenda naitaji kukabana na hili hili na kufikia kumsingizia mungu huyu ndio kutoka kwa bwana..wengine wanaoa ama kuolewa kutoa GUNDU la familia kwao akuna alieoa ama kuolewa .....,,,,,,,

Nahisi tunaitaji ....kutafuta chanzo /src ya kuvunjwa hizi ndoz...badala ya kusubiri watu waumie tutafute soln mabomu yashalipuka kama GONGO LA MBOTO....

Kwako mwanandoa!!!!@@@@
 
Badala ya kwenda kwenye hoja ya msingi tunaanza kuangalia vitu vidogo vidogo ili mradi kumkwaza tu mtu jambo ambalo si la kiungwana,hakuna ambaye hakosei humu na kama unataka kumrekebisha mtu basi tumia njia ambayo haitamfanya aonekane hajui na ikibidi mpe namna ambayo itamfanya ajifunze zaidi.
 
Kwa ufahamu wangu mimi ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili kuishi pamoja kama mume na mke,makubaliano haya yanalenga katika kuijenga au kuanzisha familia na mambo megine ya kimaisha.Inapokuja pale hakuna makubaliano basi hiyo sio ndoa,au mmoja akaoa/kuolewa "KWA SABABU YA...",hapo hakuna ndoa.asilimia kubwa ya ndoa zetu za sasa hivi hazidumu(huvunjika) ni kwa ajili wengi wetu tunaoa/kuolewa kwa sababu ya... (KULAZIMISHWA,PESA,UZURI,KUFUATA MKUMBO..n.k),Yule aliyekubali kuoa/kuolewa kwa dhati ni yule mwenye kukubali yote yale yanayotakiwa kuwepo katika ndoa ikiwepo UAMINIFU,UKWELI,UPENDO,....na kubwa zaidi ni kumkubali mwanandoa mwenzako jinsi alivyo ikiwemo mapungufu yake au udhaifu wake.Zaidi ya yote uaminifu ndio muhimili mkubwa sana katika ndoa.Wapo wanao owa au kuolewa hali akiwa bado anamahusiano na mpenzi wa zamani,hapo hamna ndoa.Kwa mimi nadhani huo ndio ufahamu wangu katika ndoa,naomba kwa wale wenye upeo zaidi watujuze juu ya hili
 
samaki mkunje angali mbichi....penda mtu anayekusahihisha kwa mambo madogomadogo .
 
ndoa yako imesambarika nini mkuu, nakumbuka kuna thread ulianzisha hapa yale machungu uliyatoa kuhusu ndoa kuvunjika! ukijumlisha na hii ya leo,? life life
 
Umesema vizuri kuhusu ndoa. Ila kuna wengine ambao hubadilika, kabla ya kuoana anakuwa mtu mpole, mwenye upendo wa dhani na kujali mpaka mwenzake anasema huyu ndio mwenza wangu wa kufa na kuzikana. Na akakubali kuoa au kuolewa naye kwa kusema haya mapungufu madogo madogo hayana matatizo nitakwenda taratibu tukirekebishana. Lakini wakishaoana na kuisha pamoja zaidi ya miezi 6 basi makucha ya huyo mwenza yaannza kufunguka na vituko visivyovumilika vinaanza, hapo ndipo doa linaanza na kupelekea baadhi ya ndoa kuvunjika.
Muhimu ni kuwa wakweli tangu mwanzo ili muweze kujuaana kwa undani, jua tabia za mwenzako vizuri. Kikubwa kuliko vyote ni uvumilivu. Mkiishi watu wawili ambao mlilelewa tofauti lazima mtapishana kiswahili kidogo kwahiyo mnahitaji kuvumiliana na kuaminiana, mkufuata hayo mtadumu kwenye ndoa.
 
]samaki mkunje angali mbichi....penda mtu anayekusahihisha kwa mambo madogomadogo[/color] .
hebu tujadili hoja za msingi, makosa haya ni ya kawaida, it doesn't mean kuwa hajui-just a typing error ambayo hata muingereza mwenyewe anafanya. Hacheni kuwa na mawazo "mgando". Kama huna hoja kaa pembeni upige umbeya ma'ke ndo inaonekana fani yako wewe na wengine wa aina yako!:a s 13:
 
Do you get marriage or married?

Huu ni uthibitisho wa kukosekana kwa elimu. La msingi ni kueleweka au kutoeleweka kwa kwa hoja husika kwa maana kwamba ata angetumia kichina bado mtoa mada angeweza kueleweka kwa wachina au waongea lugha hiyo kwa mf.

Tumekuwa watumwa wa kiingereza. Tumesahau kuwa ata Zuzu au Juha wa uingereza kwamf, anaongea kiingereza. Je tumpe tender Ya kutengeneza barabara za Juu na chini kwa mf?
 
ndoa yako imesambarika nini mkuu, nakumbuka kuna thread ulianzisha hapa yale machungu uliyatoa kuhusu ndoa kuvunjika! ukijumlisha na hii ya leo,? life life

hapana mkuu ikosafi niko njian kuanzisha KA NGO CHA KUSULUHISHA NDOA ZA WATU KUZIRUDISHA UJANANI..SASA NIMEKUWA HIVI KARIBUNI NAITWA SANA KUTOA USHAURI KWA NDOA CHINI YA MIEZI MI3 NABAKI KUJIULIZA TUANZE NA SOLN AMA TUTAFUTE SRC
 
umesema vizuri kuhusu ndoa. Ila kuna wengine ambao hubadilika, kabla ya kuoana anakuwa mtu mpole, mwenye upendo wa dhani na kujali mpaka mwenzake anasema huyu ndio mwenza wangu wa kufa na kuzikana. Na akakubali kuoa au kuolewa naye kwa kusema haya mapungufu madogo madogo hayana matatizo nitakwenda taratibu tukirekebishana. Lakini wakishaoana na kuisha pamoja zaidi ya miezi 6 basi makucha ya huyo mwenza yaannza kufunguka na vituko visivyovumilika vinaanza, hapo ndipo doa linaanza na kupelekea baadhi ya ndoa kuvunjika.
Muhimu ni kuwa wakweli tangu mwanzo ili muweze kujuaana kwa undani, jua tabia za mwenzako vizuri. Kikubwa kuliko vyote ni uvumilivu. Mkiishi watu wawili ambao mlilelewa tofauti lazima mtapishana kiswahili kidogo kwahiyo mnahitaji kuvumiliana na kuaminiana, mkufuata hayo mtadumu kwenye ndoa.

shukuuru mungu yanayolipuka ndan ya mwaka wengine wana wajukuu na magari majumba unakosa sababu nini nini??hii n laana ya kuvunjwa wapwa hatari sana..na hizi zimeasisiwa na wazazi wetu,,,wewe mzazi unaenda kukutana na mkeo kwenye harusi ya mwanao baada ya mwaka mmoja ama miwili..uoni unaenda kumuongezea laana..aiwezekani baba mmeachana alafu mtoto aanze mambo yake uende kumsuluhisha kama nani..kwa nini usianze na ndoa yako.....embu ninyi wazee leo nasema ukweli bora muache kwenda arusi za watoto wenu kama mmeachana mnaleta unafiki wa kulishana keki za kina jeniffer,best byt kisa uwepo kwenye mkanda nasema ukome kabisa na harusi ni sehemu takatifu kama ulivyo mwili wa watoto zenu..acheni kwenda kunajisi harusi za watoto wenu aijalishi uko nae vipi...

Rekebisha ndoa na mkeo uende ya wanao..usijiaibishe kwa mambo madogo..kama pilau wambieni wawapelekee m nasema hivi nikimaanisha jamani....nawatakia maisha mema wanandoa walioamua ndoa kutoka mbinguni
 
mi sijaoa lakini nadhani hata nikiwa nje ya game naweza kuona na kusema kitu. Ndoa kwa sasa zimekuwa kama "lazima" hasa kwa wadada ambao wengi wao hushabikia sana harusi. Nadhani tukipenda sana harusi tunaweza kusahau au kupoteza maana halisi ya ndoa.
Wengine pia hukimbilia ndoa kwa sababu tu umri unaenda na anaona kama watoto watamwita babu.
Maisha yalivyobadilika nimeona pia watu wengi hasa wanawake, siwaonei, lakini nadhani ni ukweli kuwa hukimbilia kuolewa na watu wanaowaona kuwa watawapa maisha, nikimaanisha vitu kama nyumba ya haraka, gari la haraka na starehe kibao. Na hii ni kwa sababu ya mazoea labda na asili kuwa mwanaume ndiye atayechangia sehemu kubwa ya mahitaji yenu muhimu ingawa sio lazima. Hii iko sana kwa kizazi hiki cha watu wa mijini. Matokeo yake ni kuoana watu ambao hawajapendana kwa dhati na kutoheshimiana. Kwa hiyo utaona watu wanatoka kwenye nyumba kali, gari usipime, kumbe hata hyo asubuhi hawajasalimiana. Usiku mwanamke katokea upande wake na mwanaume upande wake.
Lakini mitego siku hizi imezidi, kwa wanaume na wanawake, hili lazima tulikumbuke pia. Kwa hiyo hapa sasa ni suala la wanandoa kujiheshimu na kumfikiria yule uliyenaye zaidi na kuachana na mambo na starehe za kupita. Na hili la kuheshimiana huwezekana endapo watu mnapendana toka moyoni.
Yote kwa yote, ndoa lazima itokane na mapenzi ya kweli, kukubali kuheshimiana, kusameheana pale inapowezekana, na kutambua mapungufu ya mwenzako ambayo hayataathiri mapenzi yenu kwa kiasi cha kuyaharibu, mapungufu kama ya elimu, kipato, familia, n.k.
Pesa peke yake isikuingize kwenye ndoa kwani ndoa ni maisha mengine pia ambayo furaha yake hailetwi na pesa pekee.
Harusi isikuingize kwenye ndoa, kwani ndoa ni maisha baada ya harusi ambayo yenyewe ni siku 1 tu. Ni maoni tu
 
Ndoa ni tamu kama asali na tena ni chungu kama shubiri, kwa hiyo furahia maisha wakati una furaha na yakija machungu pia uyakubali, matatizo yameumbwa ili kila mwana adam ayapitie. Nikifikiria heshima nayopata, security, watoto wanavyonipa faraja na raha ya maisha na tendo lenyewe la ndoa lol ni vitu vingi sana vinanifariji na kujipa moyo kupanda milima na kushuka wala havinitingishi niamue otherwise. Ndoa na iheshimiwe na watu wote asema bwana na itabaki kuwa hivyo.
Unajua tunkuwa na maisha ya raha ila linapokuja moja tu gumu kumeza basi mtu utamjaji mwenzako kwa hilo tu na kusahau mema yote aliyoyafanya, ni hii tu roho ya kusahau ndio inayotuandama.Kuna ndoa zingine hazivumiliki hizo zinaeleweka na mpaka watu wa nje mnashuhudia ila utakuta mtu kamwacha mwenzake eti hajui kupika au anakoroma au ana kikwapa au nimechoka nyama ileile huu ni utani sasa

Kwa kweli matatizo yapo ila tuangalie hili swala kwa undani na tukumbuke ule upendo wetu wa kwanza hapo tu utajikuta unaendelea na maisha.tupunguze kusikilizia tamaa zetu za mwili ili tusiwaumize wenzetu kwa kutembea nje ya ndoa, ni doa ambalo hata ukitaka kulifuta na kujisamehe mwenyewe unashindwa. WANANDOA WENZANGU TUJIPE MOYO TUNAWEZA
 
shukuuru mungu yanayolipuka ndan ya mwaka wengine wana wajukuu na magari majumba unakosa sababu nini nini??hii n laana ya kuvunjwa wapwa hatari sana..na hizi zimeasisiwa na wazazi wetu,,,wewe mzazi unaenda kukutana na mkeo kwenye harusi ya mwanao baada ya mwaka mmoja ama miwili..uoni unaenda kumuongezea laana..aiwezekani baba mmeachana alafu mtoto aanze mambo yake uende kumsuluhisha kama nani..kwa nini usianze na ndoa yako.....embu ninyi wazee leo nasema ukweli bora muache kwenda arusi za watoto wenu kama mmeachana mnaleta unafiki wa kulishana keki za kina jeniffer,best byt kisa uwepo kwenye mkanda nasema ukome kabisa na harusi ni sehemu takatifu kama ulivyo mwili wa watoto zenu..acheni kwenda kunajisi harusi za watoto wenu aijalishi uko nae vipi...

Rekebisha ndoa na mkeo uende ya wanao..usijiaibishe kwa mambo madogo..kama pilau wambieni wawapelekee m nasema hivi nikimaanisha jamani....nawatakia maisha mema wanandoa walioamua ndoa kutoka mbinguni

Umeandika kwa uchungu ni wazee wanakuhusu au?? pole sana aisee ni kweli huwa inakera utakuta mama harusi kaja mwenyewe cause baba alimwacha kitambo na kupata dogodogo kwa hiyo sasa baba inabidi akakae high table na bi mdogo basi yule mama mzazi anakuwa kama hausiki vile na hata akihusika basi zee likirudi home litagombezwa na dogodogo wake hakuna rangi ataacha ona aisee
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom