Why Did Nyerere Support Biafra?

Swari:

Hivi bila kuwepo kwa mafuta kule, Biafra wangefikiria kujitenga? Hivi bila kuwepo kwa madini kwenye jimbo la Shaba, je vita vingetokea Congo?
Zakumi,
Uamuzi wa Biafra kujitenga haukuhusiana kabisa na uwepo wa mafuta kule. It was a matter of survival. Soma tena thread ya Shwari.
 
Swari:

Aksante sana kwa maelezo yako. Kama inavyoonyesha mwishoni mwa post yako mafuta nayo yalichangia kwa kiasi kikubwa. Watu wa kawaida ambao hawana madaraka au power hawafaidiki na mafuta au resources zozote zile lakini ndio wanaokuwa victims matatizo yanapotokea.

Vilevile kwa kusoma posti yako na kuchukua historia ya kiAfrika. Viongozi wengi wa kiAfrika akiwemo Nyerere iliwachukua muda kuelewa historia ya Afrika kwa sababu wengi wao walifundishwa historia ya Mwingereza.

Nyerere anaposema kuwa serikali Nigeria haikuchukua jukumu la kuwalinda watu wake, je alikuwa anajua kweli fault lines zilizowagawa waNigeria? Vyombo vya serikali ambavyo vingelinda wananchi vilikuwa vimegawanyika. Kambi za kijeshi zilikuwa zimekaa kimajimbo. Je ni ulinzi gani vyombo hivyo vingeweza kutoa?

Matatizo yaliotokea Nigeria 1966 ni sawa na yale yaliotokea Rwanda (1994), Burundi (1994) and Kenya(2008).
 
Labda miye niulize.. tatizo la kanuni aliyosema Nyerere katika kuelezea kwanini Tanzania ilitambua Biafra ina makosa gani? Maana ni kanuni ile ile iliyomfanya awe na mahusiano na PLO na POLISARIO, ANC na FRELIMO. Au watu wamesahau kuwa Nyerere alitambua PLO vile vile kama alivyoitambua ANC?
Mwanakijiji,
Inaongezea point kuwa Nyerere was predictable. Alikuwa na msimamo na msimamo wake ulifahamika.
 
Zakumi,
Uamuzi wa Biafra kujitenga haukuhusiana kabisa na uwepo wa mafuta kule. It was a matter of survival. Soma tena thread ya Shwari.


Jasusi:

Nimeisoma. Na bado Swari hajaiondoa hoja ya mafuta kutoka kwenye equation.
 
Jasusi:

Nimeisoma. Na bado Swari hajaiondoa hoja ya mafuta kutoka kwenye equation.
Suala la mafuta lilikuwa paramount katika uamuzi wa Uingereza kusupport federal government of Nigeria, lakini kama anavyosema Shwari akina Ojuku walikuwa wanatafuta tu mahali ambapo ndugu zao watakuwa salama, mafuta notwithstanding.
 
Nadhani ukisoma maelezo ya Rugemeleza na Shwari utapata majibu mazuri ya yote uliyoyasema hapo juu. Na utaona wazi kuwa Nyerere alifanya yale aliyofanya kwa imani ya ukombozi wa Waafrika na aliamini kuwa unyanyasaji wa Waafrika na Waafrika wenzao ni wa kupigwa vita pia kama ule wa kutawaliwa na kunyanyaswa na Wazungu. Kuhusu suala la Mugabe (ZANU-PF) na Nkomo(ZAPU) aliyekuwa na nguvu ni Mugabe na ndiyo maana Wazungu walifanya jitihada za kumchukua Ndabaningi Sithole, ambaye hakuwa Mshona, kujiunga na serikali yao ya mpito mwaka 1979.

Ukweli mwingine ni kuwa ZANU-PF ilihamia Msumbiji, baada ya Msumbiji kupata uhuru na Nkomo alikuwa Zambia. Mgawanyiko wa ZANU mwaka 1975 kufuatia kuuawa kwa Chitepo kule Lusaka ndiko kulikompatia nafasi Mugabe kuiongoza ZANU-PF. Mgawanyiko huo ulikuwa ni wa kikabila na si wa udini au madhehebu. Lakini wale ambao kwa kweli ninawaona kama ni wale "Wabadlisha Historia" (History Revisionists) wanataka tuamini vinginevyo ili malengo yao ya chuki zinazochagizwa na sababu hewa yafanikiwe.
 
Ogaden walitaka kujitenga kutoka Ethiopia ili waungane na Somalia. Watu wa Ogaden ni Wasomali lakini jimbo lao ni sehemu ya Ethiopia.

Swari:

Kwa hiyo kama Biafrans walikuwa na haki ya kujitenga, watu wa Ogaden nao walikuwa na haki ya kujitenga. Ogaden haikuwa sehemu ya Ethiopia. Wakati Karl Peter na wenzake wanaangahika kuanzisha makoloni, Mfalme Menelik naye alikuwa ana-annex kwangu nchi zilizokuwa sio zake.
 
Suala la mafuta lilikuwa paramount katika uamuzi wa Uingereza kusupport federal government of Nigeria, lakini kama anavyosema Shwari akina Ojuku walikuwa wanatafuta tu mahali ambapo ndugu zao watakuwa salama, mafuta notwithstanding.

Na wakati ule utajiri wa mafuta hakikuwa kitu cha kujivunia kwani bei ya mafuta ilikuwa chini sana na ilikuwa inapangwa na mataifa ya Magharibi. Ugomvi unaondelea sasa katika Bonde la Niger na Ogoni ni ugomvi wa matumizi mabovu ya raslimali na kuwanyima haki watu wa maeneo hayo kunufaika na raslimali hiyo ya mafuta. Madai yao yamekuwa na nguvu na ndio maana serikali ya Nigeria na kampuni za mafuta zinahangaika namna ya kumaliza mgogoro huo kwani watu wa maeneo hayo wanazungumzia lengo lao la kujitenga kutoka katika Shirikisho la Nigeria.
 
But what made Zitto proclaim that unpredictability is a hallmark of good leadership? I am wondering what was going on through his mind at that time. By any stretch, most average minded people wouldn't think for even a second that that is (unpredictability) a desirable quality. So why would he think that it is?

I have previously called into question his judgment as a leader and to me this gaffe is more proof that his is too flawed to be a good leader.
 
Bwana MULANGIRA umeongea kitu cha msingi sana. Inaelekea ni mfatiliaji mzuri sana wa siasa ya nyuma.
 
Naishi Marekani ndiyo, lakini si mnafiki wa kushabikia mambo eti kwa sababu yanafanywa na weusi.
kubali kwamba kuna siasa nyingi za kinafiki na wewe hupo tayari kubadili msimamo.
Hapa Marekani mimi siwezi kuunga mkono watu kama Jersey Jackson au Andrew Young ni wanafiki na mamruki wakubwa.
Watu wengi bado wanawahusudu kwa vile tu walikuwa rafiki na watu wa karibu wa Martin Luther.
Haki za wamarekani zimepiganiwa na Weuzi wengi lakini kuna wazungu kibao wamepoteza maisha yao kupigania haki za weusi.
Sijui ninacho kusikitisha ni nini kuishi Marekani na ulimbukeni wangu ni nini?
Eti wabelgiji wamefahamu muongo mmoja uliopita kwamba wao ndiyo walisababisha kifo cha Lumumba? Sijui ni vipi unaweza kujaribu kuamini usemi huo??
Nyerere anamvumilia Mobuto kwa sababu ana ulinzi mkubwa??
So Nyerere was after guys with small guns?

Mimi sina tatizo na Elimu yako na kwa nini niwe na tatizo?.
Naamini kwa dhati kwamba Wewe ni mtu mwenye uelewa lakini uelewa wako umeganda mahali fulani,kwenye vitabu. Hata ukipewa mazingira ya jambo bado utaendelea kujadili hoja kutokana na vitabu.
News media and books writers can say and write anything they want, be it science or history, to fulfill their purposes.

Che Guevala kwenye kitabu chake amemponda Kabila kwamba ni mtu wa starehe si mpiganaji, pengine naye aliongeza chumvi mimi hilo sijui.

Labda mwishoni nikubali tu kwamba wewe ni msomi huko Havard na mimi ni mkimbizi wa uchumi hapa North West nabeba Mabox na digirii yangu ya Uhandisi na zaidi nimeingilia na kufakamia fani
 
Suala la mafuta lilikuwa paramount katika uamuzi wa Uingereza kusupport federal government of Nigeria, lakini kama anavyosema Shwari akina Ojuku walikuwa wanatafuta tu mahali ambapo ndugu zao watakuwa salama, mafuta notwithstanding.

Unazungumza mambo yaliotokea wakati wa mgogoro. Lakini ukiangalia vitu vilivyosababisha mgogoro huwezi kukataa mafuta kuwepo. Na kuna mtu hapa anakuja kuropoka kuwa mafuta hayakuwa na bei. Bei ya mafuta ilikuwa steady na income flow iliyotokana na mafuta ilibadilisha maisha.
 
Unazungumza mambo yaliotokea wakati wa mgogoro. Lakini ukiangalia vitu vilivyosababisha mgogoro huwezi kukataa mafuta kuwepo. Na kuna mtu hapa anakuja kuropoka kuwa mafuta hayakuwa na bei. Bei ya mafuta ilikuwa steady na income flow iliyotokana na mafuta ilibadilisha maisha.

Je unawez kutuambia bei ya mafuta wakati huo ilkuwa ni kiasi gani na Nigeria ilkuwa inapata kiasi gani cha fedha?
 
Je unawez kutuambia bei ya mafuta wakati huo ilkuwa ni kiasi gani na Nigeria ilkuwa inapata kiasi gani cha fedha?

Rugemeleza:

Kufikia mwishoni mwa 60 na mwanzoni mwa 70 wakati vita vya Biafra, tayari uzalishaji wa mafuta ulikuwa ni zaidi ya mapipa milioni 2 kwa siku. Na bei ya pipa moja ilikuwa kati ya dola 2.5 na 3.0 kwa wakati huo. Hivyo kwa kipindi cha miaka hiyo, sekta hii pekee yake iliweza kuleta Gross ya zaidi $2Bilion kwa mwaka. Hicho ni zaidi ya mapato ya dhahabu yanayopatikana Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
 
Rugemeleza:

Kufikia mwishoni mwa 60 na mwanzoni mwa 70 wakati vita vya Biafra, tayari uzalishaji wa mafuta ulikuwa ni zaidi ya mapipa milioni 2 kwa siku. Na bei ya pipa moja ilikuwa kati ya dola 2.5 na 3.0 kwa wakati huo. Hivyo kwa kipindi cha miaka hiyo, sekta hii pekee yake iliweza kuleta Gross ya zaidi $2Bilion kwa mwaka. Hicho ni zaidi ya mapato ya dhahabu yanayopatikana Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Niliuliza swali hilo makusudi. Huko sahihi kabisa kuhusu bei ya mafuta ya wakati huo kitu ambacho kinaonyesha wazi kabisa kuwa bei ilikuwa ni ya chini sana na kwa wakati ule kampuni zifuatazo ndizo zilikuwa zinatawala uchimbaji wa mafuta huko Nigeria Shell-BP, IVIobil, Tenneco, Texaco, Gulf (sasa Chevron), Safrap (sasa Elf), Agip, Philip na Esso. Nyingine ni Japan Petroleum, Occidental, Deminex, Union Oil, Niger Petroleum and Niger Oil Resources. Kwa Mujibu wa N.K.Obasi katika makala yake "Foreign Participation In The Nigerian Oil and Gas Industry" Nigeria: Foreign Participation In The Nigerian Oil and Gas Industry - OnlineNigeria.com.

Kuhusu suala la kiwango cha mafuta takwimu unazosema si sahihi uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria ulikuwa hivi mapipa 5,000 kwa siku mwaka 1958, 17,000 mwaka 1960 na mapipa 45,000 mwaka 1966. Nigeria ilifikia kiwango cha mapipa 1,000,000 mwaka 1970. Hii ni baada ya vita ya Biafra kwisha. Ukisoma makala ya Obasi utapata maelezo ya kutosha. Ikumbukwe kuwa Nigeria haikupata fedha nyingi kutoka kwenye mafuta kwani kampuni zilikuwa zimepewa vivutio na misamaha mingi. Ilianza kupata fedha nyingi baada ya kujiunga na OPEC mwaka 1971 na kwa kweli mara baada ya Mgogoro wa Mafuta wa mwaka 1973-4 ambapo OPEC ilipitisha azimio kuwa nchi zote wanachama lazima ndizo zinatunga bei ya mafuta na serikali zao lazima zifaidi. Kwa hiyo chanzo cha mgogoro wa Biafra hakikuwa suala la mafuta bali madhira mengi ambayo watu wa huko waliona wanapata katika nchi yao na sana sana baada ya mapinduzi ya mwaka 1966 ambayo yalilepelekea Waibo wengi (30,000) kuuawa katika sehemu za kati na kaskazini ya nchi. Vilevile zaidi ya Waibo 1.8 walikimbia maeneo hayo kwenda kwao. Vita ya Biafra ilianza Julai 1967 na kumalizika Januari 1970. Ni rai yangu iliyotulia kuwa Mwalimu hakukubali kufumbia macho mauaji hayo na hakuliona tatizo lile kama la vita vya Wakristu na Waislamu. Ikumbukwe kuwa Yakubu Gowon ambaye ndiye alikuwa Raisi wa Nigeria, wa wakati huo, alikuwa Mkristu na alikuwa anatoka Kaskazini.

Na hata mwaka 1994 mauaji ya Rwanda yalipotokea Mwalimu alimuomba Mwinyi apeleke Majeshi lakini Mwinyi akakataa kwa sababu ya kuwa Tanzania ilikuwa ndio mpatanishi. Kutokana na hilo Mwalimu alimwomba Mwinyi ruhusa ya kuzungumza na Waandishi wa Habari na kueleza msimamo wake. Mtu asiyeelewa anaweza kumtuhumu Mwinyi kuwa hakujali kwa sababu waliokuwa wanachinjana hawakuwa Waislamu. Lakini kwangu mimi nitamtetea Mwinyi kwani hoja yake ya kuwa Mpatanishi hawezi kuingia vitani dhidi ya wale anaowapatanisha ni ya msingi kabisa. Tunaweza tukasema angepeleka majeshi kwa ajili ya kuwalinda Wakimbizi lakini hiyo ni kutokana na mtu kunufaika na mapito ya historia (hindsight) au (20/20).
 
Labda nianze kwa kusema Imani kwa kweli ni kitu Hatari sana, Mtu mwenye Imani hata Thinking zake zinakuwa Zerro, kabisa, HAta kama mtu ni Prof ama Msomi wa iana gani, lakini likija kwenye Suala la imani ueledi na uwezo wote wa kupambanua mambo unaisha,

Zitto kauliza hilo Swali la Biafra na kutokuwa na Msimamo kwa Nyerere, (why did nyerere support pan africanism and at the same time Biafra? )
sio Kisomi bali kuna kitu kinachomdrive na kana konclusion ambayo anayo,
Zitto plz siasa ambazo umeingia ama ulikuwa nazo na sasa zinaanza kujionesha. sio nzuri kabisa, hakuna nchi iliyofanikiwa kwa siasa za aina hiyo
 
Hii Makala nzuri sana kwa watu tuliozaliwa shamba na kukulia shamba.

Nashukuru wote kwa shule nzito na nitajitahidi nikae chini nisome makala zenu.

Labda pia niseme asante Zitto kwa swali lake maana watu wamejibu hadi inaleta raha kusoma.

Endeleeni kutumwagia shule ya bure na Mbarikiwe.
 
uwezo tunao,Umetumwa sio bure, unaipeleka mada sehemu nyingine kabisa. Si vema kumshmabulia mtu kiasi chote hicho na kusahau kwa nini tupo hapa JF. Jirekebishe mwenyewe otherwise its you who have inner-self conflict
 
..msimamo wa Mwalimu kuhusu Ogaden ulikuwaje?

..maana Ogaden was a totally different ball game.
 
..msimamo wa Mwalimu kuhusu Ogaden ulikuwaje?

..maana Ogaden was a totally different ball game.
jokaKuu,
Nijuavyo Mwalimu hakuunga mkono Somalia's hegemony. Kuunga mkono Ogaden ingekuwa na maana kuwa anaunga mkono pia madai ya Somalia katika eneo la Kenya na madai ya Somalia katika Djibouti. Kuna wakati nimekutana na jamaa kutoka Eritrea wakaniambia wanasikitishwa sana kwamba Mwalimu hajaunga mkono harakati zao za kujitenga na Ethiopia.
 
Back
Top Bottom