WHO yatoa magari 25 akabidhiwa N.Waziri, Mhindi katoa Ambulance 2 kamkabidhi Rais

Wasaidizi wa rais wanachaguliwa na nani?Ili nitumbukize jina langu hapo mapemaa

Wanateuliwa na Rais, hata kama mapendekezo yanaweza kutoka kwa wasaidizi au kwa wakati Serikali hii, washkaji zake.
Kwa hiyo, tatizo ni mwenyewe anayewateua.

Wewe Rais mzima uambiwe kwamba kuna mtu anataka kukukabidhi nwewe Rais magari ya ambulance mawili, nawe unasema 'sawa',

kwanini usiwambie wasaidizi kuwa wamuelekeze Wizara ya Afya akayakabidhi kwa Mkurugenzi wa Tiba?

Kama huyo muhindi ni supplier wa Land Rovers kwa Jeshi, basi vigogo wana faida naye. Mambo ya Percent yao. Ndio maana kumuona mkulu kwake ni jambo rahisi sana.
 
Toka lini mhindi akatoa msaada wa dhati bila malengo unafikiri kweli wao wanapenda kuishi Tanzania hata kama kazaliwa Tanzania wamekuja hapa kibiashara zaidi ya misaada, mbona India kuna wengi tu wanahitaji misaada muulizeni amewahi kusaidia wangapi India.

Wanajua Tanzania ni kwa wajinga waliwao kuna shamba la bibi tukipewa vigari viwili tu basi kesho njoo upate tenda, kama ni msaada kweli kulikuwa na ulazima wa kupiga picha na kuitoa gazetini, ni kweli misaada inayotolewa na mashrika ya kimataifa kama ya UN ni real lakini hii misaada binafsi iwe ya wahindi wazungu warabu wana malengo yao tofauti hata hawa Aga Khan nawasiwasi nao.

Hivi ni watu wa asili ipi huwa wanapenda kutoa misaada bila maslahi?Umewataja wazungi,wahindi na waarabu huwa wana malengo!
 
Wakuu hii imekaaje?

WHO yatoa msaada wa magari ........................... WHICH IS OKAY

Hivi karibuni tuliona kuna yule jamaa wa kihindi alikwenda kukabidhi Ambulance 2 Ikulu kwa Rais na ni kwa shughule kama hizo hizo tu hii imekaaje????

Ni ishara ya bei ndogo kwa mkuu wa nchi na tabia ya omba-omba bila kujali mtoaji, hivyo hata njia ya kumfikia ni ya bei nafuu. Unaweza ukawa na urafiki na mtu mmoja tu ktk serikali akakusaidia kupiga simu ikulu na ukafika kwa mkuu wetu. Lakini anapoitwa na wanannchi walio na matatizo, utaambiwa ratiba yake hairuhusu.

Mashirika makubwa yaliyosajiliwa hupewa jukumu pia la kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali. Ni kwa kufahamu ukubwa na faida ya biashara zao. Tatizo ni hawa wahindi ambao wana duka moja lakini eti mkuu wa nchi anakubali misaada yao bila kujiuliza faida hiyo imetoka wapi! na kwa nini mpaka yeye ndo anyooshe mkono kupokea!
 
acha ubaguzi wewe!!, WHO ni wajibu wao kutupa hayo magari, na hawatoi kwa Tz tu, ni nchi zote wanachama kwa sababu na sisi tunachangia UN, kwa upande wa huyo mhindi ndio tunaweza kuita msaada wa dhati, na hawa watu wanatusaidia sana sana, tusiwe na wivu wa kijinga, miswahili ndivyo tulivyo

Hawa watu! Watu gani wanaotusaidia? Wahindi? No way, Not possible. Jamii iliyojitenga kiasi hicho haiwezi kuwa na msaada kwetu.

Tatizo ni Busara ya viongozi wetu tu, la sivyo wasingepata nafasi kama hiyo.
Viongozi hawajifahamu na hawafahamu impact ya kushiriki ktk matukio kama hayo. Mara magari, mara kufungua hoteli, mara kuchangia ujenzi wa kanisa, mara mwaliko ktk harusi ya fulani mfanya biashara 'maarufu', mara uchafu!
 
acha ubaguzi wewe!!, WHO ni wajibu wao kutupa hayo magari, na hawatoi kwa Tz tu, ni nchi zote wanachama kwa sababu na sisi tunachangia UN, kwa upande wa huyo mhindi ndio tunaweza kuita msaada wa dhati, na hawa watu wanatusaidia sana sana, tusiwe na wivu wa kijinga, miswahili ndivyo tulivyo

Kwani msaada ni mpaka apewe rais ndugu yangu? Tena ashukuru sana? Kesho kutwa huyohuyo mfanya biashara akishtakiwa kwa kuhujumu uchumi, rais utamweka kwenye kundi gani?
 
Back
Top Bottom