Who will bring Kagame to Justice????

............
Nyie wote are equally guilty - mtu akiwasikiliza hawezi kujuwa nani anasema ukweli nani ni Muongo, ...........

Nafikiri Kagame aliliona hili ndio maana akaanzisha kamati za maridhiano yaani "mahakama za GaChaCha".
 
Mkuu hivi yale mabox yaliyo kuwa yamajaa mapanga mapya kutoka uchina yalikuwa yamenunuliwa kwa madhumuni gani? Hivi kweli hile ilikuwa a true story au adithi za kutunga, kusema ukweli mapanga niliyo yaona kwenye video clip ile sikuamini kama kweli Serikali ya Habyarimana ilikuwa imepanga mauaji before hand - kwa nini wafanye hivyo! Kama shida ilikuwa kuuua watu emass kwa nini wasitumie machine gun, hand granade na explosive charges!!!

Kwani upatanishi na RPF ulikuwa una entail vitu gani ambavyo wahutu walikuwa hawa hafikiani navyo, mbona waziri mkuu alikuwa ni mwana mama Mtutsi, kwani ni kitu gani kingebadilika drastically katika utawala wa Habyarimana mpaka kiwafanye Wahutu wa-revolt against Raisi wa kabila lao - it doesn't add UP mkuu.

Ni kweli sehemu nyingi zilikuwa zinadhibitiwa na majeshi ya Habyarimna lakini na majeshi yenu yalikuwa yamekwisha inflitrate mji mzima, mlicho kuwa mna subiri ni tukio la ghafla ambalo lingewafanya jeshi la Habyarimana liamaki liwe in disarry ili nyinyi muweze kutimiza malengo yenu, hamkujali maisha ya Watutsi wenzenu ambao walikuwa Serikalini na vijijini (I am sorry kusema hilo) Si amini kama mlikuwa na nia thabiti ya kuwa na Serikali ya mseto na Habyarimana - ingekuwa vurugu tupu.

Nyinyi watu si rahisi kupatana, tangu nikiwa mtoto mdogo tulikuwa tunapokea wakimbizi kutoka Rwanda, tunaishi nao kama ndugu, wengine wali ishi kwetu zaidi ya miaka 45+ wengi wao walikuwa wanazunguma kilugha chetu wala usingejuwa kama ni Wanyarwanda and besides we gotta lot in common, walipo kuwa wanatusimulia atrocities walizo wahi kukumbana nazo nchini mwao tulikasirika sana, ndio maana wakati mwingine unaniona nakuwa mkali sana linapokuja suala la RWANDA.

Nyie wote are equally guilty - mtu akiwasikiliza hawezi kujuwa nani anasema ukweli nani ni Muongo, mpunguze tabia ya kuwakumbusha wenzenu kwamba "Ujuhi mimi Mtutsi" hii ina set a very bad precedence, kwa nini umfanye mwenzako aji-feel inferior! Bila ku-address mind set zenu hamtaweza kukaa kwa amani kwa muda mrefu, we fikilia nchi yenu ina makabila matatu tu:Watutsi, Wahutu na Batwa mnashindwa kuelewana je mgekuwa makabila 120+ kama Tanzania si ndio ingekuwa balaa! mkiona vipi basi unganeni na Tanzania iwe nchi moja kama ilivyo kuwa wakati wa enzi za Wajerumani, oh yes msabazwe Tanzania nzima na Watanzania wengine wapelekwe Rwanda hiyo ndio ingekuwa final solution.

La mwisho ni kweli saction kutoka nchi za magharibi linatokana na matatizo ya Congo specifically M-23, lakini usije ukajidanganya kwamba suala ya kutunguliwa ndege ya Habyarimana will go away any time soon. Tunaitakia mema RWANDA, nimalizie kwa kusema msipende pende kupigana vita, vita havilipi.
Kwanza naomba nikusahihishe. Mimi si Mtusi au Mnyarwanda. Mimi ni Mtanzania kamili. Pili, waziri mkuu alikuwa ni Mhutu, lakini yeye aliunga mkono juhudi za mapatano. Habyarimana alilazimishwa na hali halisi kupatana na RPF lakini ndani ya serikali yake, na ndani ya jeshi, kulikuwa na kundi la Wahutu waliopinga kuwashirikishas RPF kwenye utawala na jeshini. Hilo halipingiki. Kuhusu mapanga na siyo machine gun, isingewezekana kununua machine gun na kutoa mafunzo kwa watu wa kawaida bila kujulikana. Na pia angalia role ya radio Milles Collines. Nani aliyewalipa wale watangazaji na kuwaagiza wasambaze chuki kuhusu "inyenzi?" na kwamba kila wanapoonekana inyenzi kazi ni kuwaua tu. Nani aliyeanzisha hiyo redio? These are questions that point to the fact that there were hardliners in the Hutu military who did not want to see RPF incorporated in the national army, and these had a role in the mass killings of the Tutsis in Rwanda.
 
Hapo ndipo napowapendea watutsi, mnajua sana fitina na mnajua sana namna ya kuzicheza kwa hilo nawapeni heko. Na kwa jinsi mnavyojua kucheza fitina hata hiyo issue ya DRC hamtafanywa lolote Kagame atasave mpaka ulimwengu utashangaa. Hivi kwenye mauaji ya kimbari waliouawa ni watusi tu ama na wahutu waliuawa.Lakini kwa jinsi mnavyojua kucheza fitina wanaopelekwa International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) pale Arusha ni wahutu tu maana watusi hawakuua watu waliua wanyama. Hongereni sana kwa hilo maana mnapendwa sana na dunia ndo maana hata hapa kwetu utaskia aaaaaa yule Mnyarwanda mwenye asili ya Tanzania sasa mimi sijui kama huko Rwanda kuna waTanzania wenye asili ya Rwanda na wapo kwenye serikali yenu
 
Ni kweli Fred Rwigema aliuwawa kwa bahati mbaya na Watutsi wenzake wakati walipo anzisha vita dhidi ya Serikali ya Rwanda ya wakati huo, mauaji yenyewe yalitokea karibu na mpaka wa Uganda na Rwanda kama sikosei wakati huo Kagame alikuwa masomoni Merikani, alikatiza masomo yake akaja kuchukua nafazi ya hayati Fred ya kuongoza mapigano. Lakini ukweli unabaki pale pale: Nani alitoa amri ya kutungua ndege ya Habyarimana ambacho kilikuwa ni chanzo cha mauuaji ya kutisha. Mkuu redio haiwezi kuua WATU.
Bahati mbaya Sana hats Fred rwigema aliuliwa name mfuasi wa kagame kwa maagizo ya kagame.rwigema aliletewa jasusi Huyo na kagame kwamba atafaa kuwa bodyguard wake na baada ya Fred kumkubali alimkabidhi bunduki yake ya sniper name ndio iliyomuua kwani huyo bodyguard alimtungua kisogoni baada ya kuwekwa mahali na kina Sam kaka,ili akipewa sign afanye mambo maana walikua na ubishi Fred akitaka waingie Rwanda kidiplomasia zaidi huku kaka na wenzie kina kagame walipanga kuingia by force. kibaya zaidi hata mJane wa fred
Hana maisha ya raha Rwanda na inawezekana kashakimbia pia kurudi Uganda na ndugu zake wote
 
Naona mpotoshaji ni wewe. Kwanza kabisa Fred Rwigema never made it to Kigali. Aliuawa msituni. Ni nani aliyeanzisha Redio Inyenzi? Radio Mille Collines, na walikuwa wanahubiri kitu gani? Umelipwa na Wahutu?

Jasusi kweli wewe ni Jasusi but I am really afraid wewe ni jasusi wa upande mmoja, hivi kweli na ujasusi wako unashindwa kusema ukweli wakati ukweli unaujua. Najua unaijua vizuri historia ya Rwanda maybe kuliko hata mimi maana mimi sio Mnyarwanda lakini wewe kwa jinsi unavoichambua nina shaka na uTanzania wako.
Back to the topic, narudia kusema tena na tena time is a good teacher ipo siku Kagame nae atajibu mashataka ya mauaji ya kimbari kama walivojibu akina Bagosora Thioneste. Watusi mnajua kabisa nyie ndo mlianzisha chokochoko Rwanda msingeanzisha chokochoko wala leo tusingekuwa tunaongelea mauaji ya kimbari lakini kwa kuwa mnajua kutwist mambo basi wanaohukumiwa na Wahutu ambao walikuwa wanalinda nchi yao dhidi ya uvamizi simply because watusi wapo kwenye power, kwa hiyo kwa kuwa mnajua mlichokifanya na kuogopa implication yake mnataka kufuta kabisa kabila la Wahutu wote wale waliokuwa na elimu na upeo kwa kuwasingizia kuwa walihusika na mauaji ya kimbari ili wanyongwe na wafie mbali, mbona kwenye mahakama ya Arusha sijaskia mkulima wala raia wa kawaida akihukumiwa kule,wanaohukumiwa na wahutu mashuhuri waliokuwa wameenda shule na waliokuwa kwenye post. Mfano yule mama ambae alikuwa Uholanzi amekuja tu kumpinga Kagame kwenye uchaguzi basi eti nae alishiriki mauaji du kweli kali
Mkaona haitoshi mkawafuata wakimbizi wa Kihutu waliokuwa wamekimbilia Zaire mkawafyeka wote pale mashariki ya DRC ili muwe na amani lakini yale mauaji waliyoyafanya wanajeshi wa Rwanda mwaka 1997 pale mashariki mwa DRC ambayo wahutu waliokufa ni zaidi ya watusi wa Rwanda wa mwaka 1994 nayo siyo ya Kimbari maana waliokufa ni Wahutu. TIME IS A GOOD TEACHER AND TIME HEAL ALL THE WOUNDS
 
na ndo maana anasita sana kuachia madaraka kipoa,anajua yatakayomfika baada ya hapo,ni mkono wa chuma tu,hutaki unafutwa duniani,ila jamaa chapakazi kama adili vile

Amesita kuachia madaraka kivipi?Kwani kipindi chake kimeisha?Acha uzushi.
 
Naona wazungu wameshamshtukia, wamesitisha financial aid,wanaelekea kumwekea vikwazo!!!Jamaa kamwaga damu sana,na hyo damu lazima tu imcost,time will tell

Tatizo mnasoma headlines tu,hebu jaribu kusoma habari yote ya misaada kwa Rwanda...utagundua hakuna kitu hapo.Kiasi kilichozuiwa na kidogo sana kulinganisha na kile ambacho bado wanapata.
 
Kwanza naomba nikusahihishe. Mimi si Mtusi au Mnyarwanda. Mimi ni Mtanzania kamili. Pili, waziri mkuu alikuwa ni Mhutu, lakini yeye aliunga mkono juhudi za mapatano. Habyarimana alilazimishwa na hali halisi kupatana na RPF lakini ndani ya serikali yake, na ndani ya jeshi, kulikuwa na kundi la Wahutu waliopinga kuwashirikishas RPF kwenye utawala na jeshini. Hilo halipingiki. Kuhusu mapanga na siyo machine gun, isingewezekana kununua machine gun na kutoa mafunzo kwa watu wa kawaida bila kujulikana. Na pia angalia role ya radio Milles Collines. Nani aliyewalipa wale watangazaji na kuwaagiza wasambaze chuki kuhusu "inyenzi?" na kwamba kila wanapoonekana inyenzi kazi ni kuwaua tu. Nani aliyeanzisha hiyo redio? These are questions that point to the fact that there were hardliners in the Hutu military who did not want to see RPF incorporated in the national army, and these had a role in the mass killings of the Tutsis in Rwanda.

Mkuu nimekuelewa some points ziko justified, ila umenichekesha karibu nizimie - sasa tangu lini binadamu wakaitwa "INYENZI"? Je dawa ya inyenzi ni hipi? ni X-Pel mkuu. Kucheka kwangu akunimanishi kwamba nimefurahi, hakuna cha kufurahia hapa - tunacho shuhudia ni chuki zilizo kuwa zimepitiliza kimo, watu wanakuwa brain washed emass - reasoning capacities zao zote zina sublime into thin Air kwa sababu za kusikiliza hate RADIOS!!! Kwa nini walikuwa wana amini walicho kuwa wanasikia kwenye RADIO?

One more thing - kununua bunduki hata kama ni za aina ya ASR au mapanga, kama kuna mpango wa kutumia silaha hizo kwa ajili ya kuangamiza kundi fulani wangejulikana tu, hivyo ununuzi wa mapanga usingeweza kuzuia siri kufichuka i.e either way you look at it ingejulikana tu, kwa hiyo mantiki ya kusema ununuzi wa mapanga ulisadia kuficha an impending catastrophe - I don't buy IT. I trust janga hili alitajirudia TENA.

The question is: How're you gonna MELLOW civilian/ex-military HUTU hardliners?
 
Bahati mbaya Sana hats Fred rwigema aliuliwa name mfuasi wa kagame kwa maagizo ya kagame.rwigema aliletewa jasusi Huyo na kagame kwamba atafaa kuwa bodyguard wake na baada ya Fred kumkubali alimkabidhi bunduki yake ya sniper name ndio iliyomuua kwani huyo bodyguard alimtungua kisogoni baada ya kuwekwa mahali na kina Sam kaka,ili akipewa sign afanye mambo maana walikua na ubishi Fred akitaka waingie Rwanda kidiplomasia zaidi huku kaka na wenzie kina kagame walipanga kuingia by force. kibaya zaidi hata mJane wa fred
Hana maisha ya raha Rwanda na inawezekana kashakimbia pia kurudi Uganda na ndugu zake wote

Well said mkubwa na naunga mkono hoja yako, katika watu waliokuwa wamekwenda shule na wanajua mambo alikuwa Fred Rwigema hakuwa anataka mambo ya vita maana alikuwa anajua madhara ya vita, alipigana Msumbiji enzi za FRERIMO, alipigana kumsaidia Mseven mtusi mwenzake kuikamata Uganda so alitaka watu watumie diplomasia maana alikuwa anajua madhara ya vita lakini kwa kuwa Kagame mikono yake ilikuwa tayari inanukia damu na kwa kuwa alikuwa anajua kuwa kama wakimaliza salama basi Fred Rwigema lazima angechukua nchi na Kagame angebaki na post ya kawaida akaona bora ampigilie mbali maana angemletea kauzibe, so mtu alieua mwanaharakati mwenzake hakuona sababu ngumu kuwateketeza watusi wenzake waliokuwa ndani ya Rwanda ili yeye atimize azma yake.

Nachosema Rwanda hata kama Kagame aipaishe kinamna gani bado si salama kwa sababu ya Kagame ameshatengeneza maadui ambao walikuwa rafiki zake, mfano mzuri ni General Kayumba Nyamwasa amabe kila siku anakoswakoswa kupigwa risasi akiwa uhamishoni Johannesburg maana Kagame anajua kuwa jamaa ni threat kwenye utawala wake. Ukimgoogle unaona anavosimulia mambo mengi ya uozo na mauaji ya kila mara ya Kagame ndani ya serikali yake kwa kila mtu anaedhani kuwa anampiga anampotezea mbali
 
Amesita kuachia madaraka kivipi?Kwani kipindi chake kimeisha?Acha uzushi.

Hivi unafikiri Kagame ataachia madaraka kirahisi rahisi, uchaguzi wa vyama vingi umefanyika 2010 na Kagame kabadilisha katiba kutoka miaka 5 mpaka 7 this means atamaliza ngwe yake ya kwanza 2017 so akipiga tena miaka mingine 7 ataachia urais mwaka 2024 sasa huyo ni wa kutoka kweli leo, labda Mungu tu amchukue mapema
 
The good thing ni kwam a western donors wa rwanda wameanza kuangalia bad side ya kagame. game imeanza kugeuka ni Jana tu donor mwingine mkubwa anayewasapoti Belgium amekata msaada wa kijeshi.
 
Hapo ndipo napowapendea watutsi, mnajua sana fitina na mnajua sana namna ya kuzicheza kwa hilo nawapeni heko. Na kwa jinsi mnavyojua kucheza fitina hata hiyo issue ya DRC hamtafanywa lolote Kagame atasave mpaka ulimwengu utashangaa. Hivi kwenye mauaji ya kimbari waliouawa ni watusi tu ama na wahutu waliuawa.Lakini kwa jinsi mnavyojua kucheza fitina wanaopelekwa International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) pale Arusha ni wahutu tu maana watusi hawakuua watu waliua wanyama. Hongereni sana kwa hilo maana mnapendwa sana na dunia ndo maana hata hapa kwetu utaskia aaaaaa yule Mnyarwanda mwenye asili ya Tanzania sasa mimi sijui kama huko Rwanda kuna waTanzania wenye asili ya Rwanda na wapo kwenye serikali yenu
Kwanza nakuomba uniombe msamaha. Kama nilivyomweleza mwanzishi wa mada mimi ni Mtanzania halisi. Usinipachike Ututsi. Pili, ni kweli kuna Wahutu waliouawa kwenye mauaji haya ya kimbari. Mhutu aliyemwoa Mtutsi aliombwa na Interahamwe amuue mkewe. Alipokataa alikatwa panga. Pia kuna Wahutu ambao hawakuunga mkono mauaji hayo ya kikabila. Hawa pia waliuawa na Interahamwe. Kumbuka Interahamwe ilikuwa ni movement ya kuhakikisha kuwa mamlaka ya dola yanabaki mikononi mwa Wahutu. Ukweli ni kwamba majority ya wauaji walikuwa ni Wahutu. Usininyang'anye Utanzania wangu.
 
Jasusi kweli wewe ni Jasusi but I am really afraid wewe ni jasusi wa upande mmoja, hivi kweli na ujasusi wako unashindwa kusema ukweli wakati ukweli unaujua. Najua unaijua vizuri historia ya Rwanda maybe kuliko hata mimi maana mimi sio Mnyarwanda lakini wewe kwa jinsi unavoichambua nina shaka na uTanzania wako.
Back to the topic, narudia kusema tena na tena time is a good teacher ipo siku Kagame nae atajibu mashataka ya mauaji ya kimbari kama walivojibu akina Bagosora Thioneste. Watusi mnajua kabisa nyie ndo mlianzisha chokochoko Rwanda msingeanzisha chokochoko wala leo tusingekuwa tunaongelea mauaji ya kimbari lakini kwa kuwa mnajua kutwist mambo basi wanaohukumiwa na Wahutu ambao walikuwa wanalinda nchi yao dhidi ya uvamizi simply because watusi wapo kwenye power, kwa hiyo kwa kuwa mnajua mlichokifanya na kuogopa implication yake mnataka kufuta kabisa kabila la Wahutu wote wale waliokuwa na elimu na upeo kwa kuwasingizia kuwa walihusika na mauaji ya kimbari ili wanyongwe na wafie mbali, mbona kwenye mahakama ya Arusha sijaskia mkulima wala raia wa kawaida akihukumiwa kule,wanaohukumiwa na wahutu mashuhuri waliokuwa wameenda shule na waliokuwa kwenye post. Mfano yule mama ambae alikuwa Uholanzi amekuja tu kumpinga Kagame kwenye uchaguzi basi eti nae alishiriki mauaji du kweli kali
Mkaona haitoshi mkawafuata wakimbizi wa Kihutu waliokuwa wamekimbilia Zaire mkawafyeka wote pale mashariki ya DRC ili muwe na amani lakini yale mauaji waliyoyafanya wanajeshi wa Rwanda mwaka 1997 pale mashariki mwa DRC ambayo wahutu waliokufa ni zaidi ya watusi wa Rwanda wa mwaka 1994 nayo siyo ya Kimbari maana waliokufa ni Wahutu. TIME IS A GOOD TEACHER AND TIME HEAL ALL THE WOUNDS

Ndugu yangu, nimeshamjibu Bornagain na nakujibu wewe kwa mara nyingine pia kwamba mimi ni Mtanzania halisi.
Mimi si Mtutsi ingawa sina ugomvi na wote Wahutu na Watutsi, nafurahi kuwa nimekulia kwenye Tanzania ya amani iliyolelewa na Julius Kambarage Nyerere na daima nitamuenzi mzee wetu. Kuhusu Wahutu, unasema kuwa Watutsi ndio walioanzisha chokochoko. Kuanzia mwaka 1959 hawa walifanywa wakimbizi, wakikimbilia Uganda na Tanzania. Sasa wewe ulitaka waendelee kuwa wakimbizi huku wakijua kwao ni Rwanda? Kama wakulima wa kawaida walihusika katika mauaji ya kimbari, walioshtakiwa ni wale waliochochea na viongozi wa mauaji hayo. Interahamwe ilikuwa na structure yake, ni kama vile Ujerumani ya Hitler hata kuna raia waliolazimishwa kuwapeleka Wayahudi kwenye kambi za mauaji lakini waliotakiwa zaidi katika kesi za Nuremberg walikuwa ni viongozi wa zoezi hilo. Kwa mara nyingine tena ndugu yangu usinipokonye Utanzania wangu.
 
Bahati mbaya Sana hats Fred rwigema aliuliwa name mfuasi wa kagame kwa maagizo ya kagame.rwigema aliletewa jasusi Huyo na kagame kwamba atafaa kuwa bodyguard wake na baada ya Fred kumkubali alimkabidhi bunduki yake ya sniper name ndio iliyomuua kwani huyo bodyguard alimtungua kisogoni baada ya kuwekwa mahali na kina Sam kaka,ili akipewa sign afanye mambo maana walikua na ubishi Fred akitaka waingie Rwanda kidiplomasia zaidi huku kaka na wenzie kina kagame walipanga kuingia by force. kibaya zaidi hata mJane wa fred
Hana maisha ya raha Rwanda na inawezekana kashakimbia pia kurudi Uganda na ndugu zake wote

Mkuu Fred alikuwa na akili sana na alikuwa na hand on experience kwenye nyaja za vita, Kagame alijuwa uwezo mkubwa wa Fred lakini sina uhakika kama wangeweza wote kukaa zizi moja baada ya Kufanikiwa kumuodoa Habyarimana madarakani. Kama wenzangu wanavyo sema humu, Kifo cha Fred haikikuwa cha bahati MBAYA.
 
Ndugu yangu, nimeshamjibu Bornagain na nakujibu wewe kwa mara nyingine pia kwamba mimi ni Mtanzania halisi.
Mimi si Mtutsi ingawa sina ugomvi na wote Wahutu na Watutsi, nafurahi kuwa nimekulia kwenye Tanzania ya amani iliyolelewa na Julius Kambarage Nyerere na daima nitamuenzi mzee wetu. Kuhusu Wahutu, unasema kuwa Watutsi ndio walioanzisha chokochoko. Kuanzia mwaka 1959 hawa walifanywa wakimbizi, wakikimbilia Uganda na Tanzania. Sasa wewe ulitaka waendelee kuwa wakimbizi huku wakijua kwao ni Rwanda? Kama wakulima wa kawaida walihusika katika mauaji ya kimbari, walioshtakiwa ni wale waliochochea na viongozi wa mauaji hayo. Interahamwe ilikuwa na structure yake, ni kama vile Ujerumani ya Hitler hata kuna raia waliolazimishwa kuwapeleka Wayahudi kwenye kambi za mauaji lakini waliotakiwa zaidi katika kesi za Nuremberg walikuwa ni viongozi wa zoezi hilo. Kwa mara nyingine tena ndugu yangu usinipokonye Utanzania wangu.

Hapo tunaweza tukakesha tusipate mwafaka hata kidogo, the stpry of Hutu and Tutsi is really complicated for sure. Wewe unasema kuwa watusi walikimbilia uhamishoni mwaka 1959 enzi zile za Mfalme Kaibanda kama sijakosea so wasingeweza kufia uhamishoni nakubakliana na wewe kabisa kwamba wasingeweza kufia uhamishoni but so long as Rwanda is for Hutu and Tutsi walitakiwa kuondoa matabaka kuwepo na power shairing btn two tribes so as to end this endless drama lakini kwa kusema kuwa eti watutsi walikaa uhamishoni tokea 1959 so wasingekubali kufia uhamishoni itazidi kuwa na sura nyingine kabisa maana hata wahutu waliofukuzwa mwaka 1994 na RPF nao watarudi Rwanda kupigana kwa sababu hawatakubali kukaa uhamishoni for such a long time and at the end of the day Rwanda itakuwa kila baada ya muda flani ni vita kwenda mbele.

Hakuna wakimbizi duniani waliokuwa wamebalikiwa kama waNyarwanda wa Kitutsi na kama huamini just do your research, waliokimbilia Tanzania mwaka 1959 walifikia sehemu moja huko wilaya ya Mpanda mkoa wa Rukwa inaitwa Mwese na wote walipewa uaraia na hayati Mwalimu Nyerere na pia kabla ya kupelekwa huko UN alifanya research kuhakikisha kuwa wanapewa eneo ambalo linafanana hali ya hewa na nchi yao ya Rwanda ama karibu sawa na Rwanda walikotoka kwa hiyo akili kumkichwa ushapewa uraia sasa unasubiri nini kama sio kujichanganya kwenye system na kuendelea kula maisha.

Watusi waliokimbilia Uganda rais Mseven aliwaweka kwenye serikali yake direct baaada ya vita vya msituni kwa sababu walishiriki kikamilifu ndo maana hata Fred Rwigema mwenyewe alikuwa mkuu wa usalama wa Uganda kabla ya kwenda vitani Rwanda umauti ulipomkutia, Kagame, James Kaberuka wote hao walikuwa wanajeshi kwenye jeshi la Uganda so in short ni vile tu nyumbani ni nyumbani watutsi hawakutakiwa kabisa kuanzisha chokochoko za mauaji maana hakuna hata kimoja walichokuwa wamekosa walikuwa wakimbizi kwa jina tu.

Back to the HUTU's yaani utafikiri wana laana hili kabila, ukiwa MHUTU wewe ni mkimbizi hata kama uwe London, New York, Dar Es Salaam so long as wewe ni MHUTU basi ni mkimbizi na haki zako zingine kwisha habari yake. Mfano mzuri ni wakimbizi wa Burundi waliokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1972 walihifadhiwa kwenye makambi ya wakimbizi ya Katumba, Mishamo yaliyopo Mpanda - Rukwa na Ulyankuru lililopo Tabora. Hawa wanaendelea kuwa wakimbizi mpaka leo na watoto wao waliozaliwa Tanzania ambao hata hawaijui Burundi hawaruhusiwi na wala hakuna sehemu iliyoandikwa kuwa wanaweza wakaukana uraia wa wazazi wao. Hii yote inafanyika kwa msaada wa watusi walioko Burundi na Rwanda kuhakikisha kila alipo MHUTU hawezi kuinua kichwa na kujua dunia inakwendaje. Hata makambi ya wakimbizi wa Burundi yaliyoko Kigoma sasa serikali imeamua iyafunge eti warudi kwao eti kwa sbb Burundi kuna amani, mbona Rwanda kuna amani tena tele lakini sijawaisikia serikali inafunga kambi ya Watusi waliopo Mwese - Mpanda

HITIMISHO
WATUSI Mungu anawapenda sana na msiache kumwomba maana siku ikiwa kwa upande mwingine itakuwa balaa kubwa sana maana ulimwengu utawajua kupitia picha nyingine ambayo imejificha sana mpaka uwe na maono ndo unaweza kuiona
 
Mkuu Fred alikuwa na akili sana na alikuwa na hand on experience kwenye nyaja za vita, Kagame alijuwa uwezo mkubwa wa Fred lakini sina uhakika kama wangeweza wote kukaa zizi moja baada ya Kufanikiwa kumuodoa Habyarimana madarakani. Kama wenzangu wanavyo sema humu, Kifo cha Fred haikikuwa cha bahati MBAYA.
Another big lie.Fred alikuwa ni mwanamapinduzi na mara nyingi alikuwa ana maamuzi ya haraka haraka yaliyosababisha maafa kwake.Kagame alikuwa mtu wa mahesabu,na ndio maana yeye alikuwa kwenye intelligence ya Uganda kama kiongozi wakati Fred alikuwa mtu wa mapambano,combat man ambaye mara nyingi alitenda kwa haraka bila kufikiria au kupanga mipango madhubuti.Uhusiano wa Fred na Kagame ni kama ule wa Ernesto Guevarra na Fidel Castro.Castro alikuwa mtu wa ujasusi dhaidi ilhali Guevarra alikuwa na 'moto' wa pupa ulioleta kifo chake.Tujaribu kuisoma historia vizuri.kama ilivyo kwa Fidel kuhusishwa na kifo cha Che Guevarra ndivyo Kagame anavyohususishwa na kifo cha Fred...uzushi mtupu kwa wale waliosoma historia vizuri.
 
Ukiifuatilia kwa undani historia ya Fred Rwigema na Paul Kagame utagundua tofauti kubwa kati yao.Wote walikuwa vijana wa umri mdogo tu,chini ya miaka 25 wakati wanaanzisha kikundi cha RPF huko Uganda.Wote walikuwa wanalengo moja lakini walitofautiana kwenye mbinu na utendaji.Fred alitaka waivamie Rwanda kwa haraka ilhali Kagame akimsihi wasubiri wajenge kikosi bora chenye nidhamu.Kwenye harakati za mipango yao,Marekani ikawapa scholarship kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi,Fred alikataa kwenda akitaka kuanzisha mapambano haraka.Kagame alienda kusoma Marekani huku nyuma Fred akaongoza kikosi dhaifu kwenda kuipindua serikali ya Rwanda.Matokeo yake ni kushindwa vibaya mno kwa kina Fred kwa kuwa kikosi licha ya kuwa na ari na nia hakikuwa na nidhamu ya kijeshi,nidhamu ya kutambua wakati wa kushambulia na wakati wa kurudi nyuma...Ni historia ndefu lakini ina mafundisho mengi,please take your time to read it from reliable sources ili tuachane na uzushi uzushi wa kusikia na kuungaunga maneno ya vijiweni.
 
Hivi unafikiri Kagame ataachia madaraka kirahisi rahisi, uchaguzi wa vyama vingi umefanyika 2010 na Kagame kabadilisha katiba kutoka miaka 5 mpaka 7 this means atamaliza ngwe yake ya kwanza 2017 so akipiga tena miaka mingine 7 ataachia urais mwaka 2024 sasa huyo ni wa kutoka kweli leo, labda Mungu tu amchukue mapema
Kagame anamalizia muhula wake wa mwisho.Na amesema hagombei tena kama katiba isivyoruhusu.Mbona tunapenda stori za kuungaunga?
 
Kagame anamalizia muhula wake wa mwisho.Na amesema hagombei tena kama katiba isivyoruhusu.Mbona tunapenda stori za kuungaunga?
Kwani na Mseven alikuwa hajamaliza muda wake mbona aligombea tena, mambo ya siasa ni magumu na wala usiusemee moyo wa mwenzio
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom