Who owns BP Tanzania Ltd?

Niliwaambia wana jf hapa jamvini watu waachane na kelele za ewura hao wapo kisiasa zaidi kuliko uhalisia wao.ukweli wa hii saga ni hivi:kama wengi walivyochangia BP ina mshirika ambae ni serikali 50-50 na kweli imeuzwa kwa Puma energy, BP kama makampuni mengine ukiacha Gapco hajaachia mafuta yake kwa suala moja kuu itapata hasara ya mabilioni.

Suala hili haliko kwa ngereja tu, mkurugenzi wa kampuni hiyo siku 4 zilizopita aliitwa wizarani maneno yakaishia Ikulu kwa Mr Luhanjo BP imeweke hesabu wazi na maamuzi ya kuuza au kutouza yako mikononi mwa bodi ya kampuni hiyo.

Katika hili EWURA hawaelewi ngoma wanayoicheza kwa sababu wanaonekana kupotosha umma wa watanzania kwa kigezo cha kunyang'anya leseni.Nikweli hapo kati bei imekuwa ikipanda kidogo kidogo lakini kushuka kwa bei zaidi ya sh.200 na zaidi unategemea nini?

TRA walishachukua kodi zao,hapa janvini hayupo mtu TRA aweke ushahidi???wako kimyaaa kama hawahusiki kuwajuza watz kuhusu hili.
 
chama legelege huzaa serilkali legelege,chama corrapt kilichowekwa na wayu mafisadi hiyo ndio jibu,tunakokwenda kubaya sana.mkulu yupo kimya kama hakuna kitu
 
Serikali hakika ni legelege kabisa huwezi kuwa na watu wasiojua jinsi kuendesha wizara alafu utarajie mambo mafanikio .......................... Ila yote hii nikutokana na kuwa na serikali ya Ushoga, ujomba nk
 
Complience order ya EWURA inaanzia saa ngapi na kuishia saa ipi?
 
Sishanagai kwani board zetu huwa ni za kusingizia na kukusanya posho siyo za kutetea maslahi ya umma ndiyo maana wanapewa vikongwe ambao hawawezi tena kufanya lolote
 
Mmiliki mwingine kwa sasa ni BP yenyewe kupitia Africa arm. Ingawa kwa wale waliobahatika kusoma press release ya FCC (fair competition commission), BP wameuza kwa Puma Energy (subsidiary of Trifigura).

Kuhusu kugoma,hilo swali kwa kweli ni gumu kwani maamuzi ya kuuza au kutouza yanafanywa na board members ambayo 50/50 kati ya BP na Serikali. Hilo ni moja lakini la pili ambalo ndilo ninalohisi ni sababu ya tatizo lenyewe ni kwamba,haya macampuni ya kigeni (i.e Oryx,BP,Total etc), mfumo wao wa biashara ni kwamba, kituo kinakuwa chini ya umiliki wa kampuni lakini uendeshaji anapewa dealer ambaye kazi yake ni kununua mafuta kutoka kwa kampuni yake lakini anakuwa na 100% mamlaka ya uendeshaji wa kituo, kwa lugha ya kigeni wanaita "Company owned but dealer operated" sasa kutofungua inawezekana supplier ambaye ni BP ameamua kutouza mafuta au huyu dealer ameona hatapata faida kama akinunua mafuta kwa bei ambayo atauziwa na supplier wake.

This is my view

.

Ulichoeleza kila kitu ni kweli except hapo kwenye red.
Mauzo ya mafuta yakiwa chini, Ukifunga kituo ama kugoma kuuza mafuta bila ridhaa ya Corporate office whether ni ya Total, Gap Oil etc ama kampuni yoyote inayomiliki hiyo filling station basi unaweza kupokonywa kituo. Unless kituo ni chako, pumps ni zako na underground tanks ni zako na unatumia jina tu hapo utakuwa na jeuri. Kwa hiyo wanaohusika na hili tatizo ni hizi supplying companies na sio wenye vituo
 
Kama serikali ya Tz inamiliki 50% ya hisa za BP tanzania iweje kampuni hii "igome" kuuza mafuta?ina maana serikali imeamua kuhujumu watu wake?
Huyu mmiliki mwingine ni nani?ana uwezo upi wa kuzuia uuzaji wa mafuta?

Jamani hii nchi hatupaswi kuuliza maswali kama hayo...haya ni mambo ya kawaida kwa serikali ya kisanii na isiyojali watu wake...nadhani tutaendelea kuenya sana kwasasa..........
 
50 % Serikali ya CCM; Inaonyesha hii ni ya ajabu kweli; watu wafanyao kazi Serikalini chini ya wakurugenzi ni wafanyakazi wa NCHI bila kujali Chama Cha Siasa...

Lakini inaonekana PB wote ni wafanyakazi wa CCM ndani ya Serikali
 
Kuna mashirika mengi hapa nchini ambayo Serikali inamiliki sehemu ya hisa lakini usimamiaji/ufuatiliaji wa umiliki huo aidha haupo na kama upo ni kwa faida ya kikundi fulani na sio Taifa kwa ujumla. Msajili wa Hazina kama msimamizi wa mashirika ya umma akiulizwa idadi ya mashirika ambayo Serikali ina hisa humo hana jibu la moja kwa moja aidha kwa kushindwa kujua wajibu wake ama anatumia udhaifu huo kujinufaisha binafsi. Inasikitisha sana kuona jinsi Serikali inavyoacha kwa makusudi rasilimali za Taifa ziishie mikononi mwa wajanja wachache. Kwa upande wa BP ni kweli kabisa kuwa Serikali ina hisa humo lakini inasikitisha na kutia shaka jinsi ambavyo imeshindwa kutoa tamko katika sakata zima la mafuta kwa BP na makampuni mengine. Na sio BP pekee kwani hata Kampuni ya Oryx ambayo ilinunua TIPER Serikali ina hisa humo lakini ukiuliza hakuna kiongozi anayeweza kutoa jibu lenye maana.
 
Kampuni ya mafuta ya BP bado inaendeleza mgomo wa kuuza mafuta licha ya kupewa "24 hrs Complience Order" na Ewura tangu juzi.
Licha ya kwamba serikali inamiliki 50% ya hisa katika kampuni hiyo lakini ndiyo imekuwa kinara katika kugoma kuuza mafuta kwa wananchi.
BP wanatoa wapi kiburi hiki?????
 
Kampuni ya mafuta ya BP bado inaendeleza mgomo wa kuuza mafuta licha ya kupewa "24 hrs Complience Order" na Ewura tangu juzi.
Licha ya kwamba serikali inamiliki 50% ya hisa katika kampuni hiyo lakini ndiyo imekuwa kinara katika kugoma kuuza mafuta kwa wananchi.
BP wanatoa wapi kiburi hiki?????

Pamoja na TOTAL, vituo vyao vingi haviuzi mafuta ukiondoa makao makuu na mlimani city.

BP na TOTAL kitakuwa kipimo kizuri kwa meno ya ewura kama ni ya chuma ama plastiki.
 
Tulishasema Jk anang'ata na kupuliza watu wakasema tunamtukana rais.. Sasa tunasema serikali ya Kikwete na CCM ndio wamegoma kuuza mafuta kwa wananchi waliowapigia kura...shame up on those who are behind this scene...
 
Kampuni ya mafuta ya BP bado inaendeleza mgomo wa kuuza mafuta licha ya kupewa &quot;24 hrs Complience Order&quot; na Ewura tangu juzi.<br />
Licha ya kwamba serikali inamiliki 50% ya hisa katika kampuni hiyo lakini ndiyo imekuwa kinara katika kugoma kuuza mafuta kwa wananchi.<br />
BP wanatoa wapi kiburi hiki?????
hili ndio swali la msingi!
 
Serikali ya Tanzania inakosea sana Huwezi kulazimisha kampuni binafsi wauze mafuta kwa bei unayotaka!!!. Serikali inabidi iruhusu ushindani na mambo ya bei na kuchanganya siasa na biashara inabidi iache. Kama wanataka wanaweza kununua mafuta ya ziada kwa wakati wa matatizo lakini serikali inabidi ijitoe kwenye biashara ya kupanga bei na tatizo si BP bali ni Serikali!!. Kama wanataka bei ipungue waongeze ushindani na kupunguza kodi kwa muda lakini sio kulazimisha bei!!!
 
Haya mambo mengine ni magumu kuchangia,tupeni data kamili kuwa serikali inahisa kiasi gani.
 
Wana JF hivi karibuni Puma Energy ya Ulaya ilinunua nusu (50%) ya hisa za BP Tanzania Tanzania na huku serikali ikibaki na asilimia 50%. Kisheria BP international waliipa fursa ya kwanza(priority) serikali ya Tanzania inunue hisa hizo na nasikia serikali kupitia hazina ilikataa na ndipo wakaingia Puma Energy ambao ni mwezi jana walipata baraka za Fair Competition Commission ya kwetu.

Ninaomba tujadili kwa nini serikali ilikataa kununua kampuni yote ya BP Tanzania ambayom tayari inamtandao mzuri tu wa uagizaji na usambazaji wa mafuta na badala yake ikangangania kuanzisha COPEC!

Pili nasikia tetesi kwamba uongozi wa BP Tanzania kupitia BODI yao walipeleka taarifa kwamba kama wangeuza mafuta kwa bei elekezi ya EURA wangepata hasara ya bilioni 3 na wakaomba kwamba serikali ikiridhia hasara hiyo kwa maana wao BP?Puma wabebe nusu yake (1.5 bilioni) na serikali ibebe 1.5 bilioni basi bpT watauza mafuta. JIBU las serikali likawa NO/HAPANA.

Sasa kama rai mtumiaji wa mafuta nain hana uchungu na wananchi na nchii hii - uongozi wa BPTanzania au serilkali yetu?

Ninawakilisha.
 
Back
Top Bottom