Who is visiting "Ze Utamu"? Athari za Utandawazi na haki za Utamaduni wa mtanzania

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Who is visiting "Ze Utamu"? Athari za Utandawazi na haki za Utamaduni wa mtanzania

Kuna hii web site inayosumbua akili za watanzania wengi sana nimeamua kuitumia kuelezea suala la usimamizi wa habari tando. Sipendi kwenda kwa undani sana kuhusiana na habari zinazoandikwa humo. Suala langu nataka kujua, je sheria za Tanzania katika kusimamia uhuru wa habari zinaendana na kasi ya teknolojia ya sasa. Ukichukulia kabisa ya kwamba Internet imechukua nafasi ya conventional news media.

Ntakupa mfano mzuri wa sheria za Uingereza na Marekani kuhusu masuala ya libel [kuchafuliana majina]. Sheria za Uingereza zimeenda mbali sana na kuweka mazingira ya kuweza mushitaki mtu Uingereza (Libel Tourism). Mfano wa kesi moja ya Libel ni ya Mwandishi wa habari wa marekani Rachel Ehrenfeld, ambaye alimtuhumu tajiri wa Saudi Arabia: Bin Mahfouz na familia yake kwamba wanafund magaidi. Kitabu cha huyu mwandishi kilichapishwa Marekani lakini kiliuzwakopi 20 kupitia mtandao uliosajiliwa huko Uingereza. Ehrenfeld aliamua kutokutokea mahakamani kukanusha madai ya hiyo kesi.Alipigwa faini ya paundi 10, 000 na gharama nyingine za kuendesha kesi. Mwandishi huyu alijua ya kwamba kama hiyo kesi ikifunguliwa Marekani isngefika popote kwa sababu ya haki kubwa za kikatiba (freedom of speech under 1st Amendement) zingemlinda. Lakini kwa Uingereza ni tofauti.

Swali la msingi ni je, Tanzania ifuate mfumo gani katika kusimamia habari zinazochapishwa kwenye mitandao. Je, tufuate Freedom of speech mode as granted by the First Amendment of the U.S. constitution au tufuate mfumo wa Uingereza ambao umeweka mazingira magumu katika uhuru wa habari.

Kumbuka wanasiasa na watu maarufu Marekani hawana kinga kubwa ya masuala kama sedition au defamation kwa sababu Supreme Court ya marekani imesema ya kwamba ndiyo dhaama za umaarufu na kuwa mwanasiasa kwa hiyo maisha yako yanakuwa sehemu ya jamii.

Naomba kuwakilisha.
 
Tanzania ifuate mfumo gani katika kusimamia habari zinazochapishwa kwenye mitandao.

Mimi naona tusifuate mfumo wowote, kwa sababu matatizo yetu hayafanani na Marekani au Uingereza. Hao waliofikia kuweka mifumo ya kulinda habari leo walishapitia hapa tulipo sisi leo (uhuru wa habari mtandaoni). Hivyo wacha Watanzania wawe huru kuandika habari. Cha msingi habari ziwe na ukweli, leo tumeona jinsi tunavyoweza kupata habari nyeti mtandaoni. Zenye ukweli first class. Watanzania tumefungiwa uhuru wa uandishi wa habari kwa miaka mingi sana. Kila kitu kuhusucho nchi, utawala au kiongozi ilikuwa ni SIRI KUU.
Huo usiri mkuu umetufikisha kwenye hali hii:
1) poor education system and facilities
2) poor health care system
3) poor infrastructure syatem etc.

Kwa sababu hakuna aliyekuwa na haki ya kuhoji chochote. Tumetawaliwa kama mazumbukuku hadi leo hii. Ni aibu sana.

Usiri ulikomaa na kuzaa uoga miongoni mwa watendaji katika nchi.
Usiri ukashika mimba na kuzaa udikteta mamboleo ambao umeota mizizi na kuzaa mjukuu UFISADI.

Mjukuu Fisadi amelelewa na kumbelezwa hata anatu-cost our life. Lakini bado tumembepa.

Fisadi huyu amefanya maisha ya walemavu (Albino) kuwa hatarini.

Hebu niambie ni Mtanzania gani mwenye uwezo wa kununua viungo vya Albino kwa Milioni 30???? Kama siyo Fisadi mwenye pesa za wananchi?

Fisadi wameshindwa kuwalinda Albino.

Fisadi amesababisha mwananch usilale usingizi kwa sababu ya ujambazi. Kisa yeye ana mitambo ya kumlinda.

Mimi nasema: Asante technologia hii ya tovuti ambayo imeweza kuuanika uchafu wa ufisadi hadharani. ...ni Mtanzania gani angeweza kusimama hadharani na kumnyoshea kidole fisadi??? Ni Wangapi waliojaribu kumnyoshea kidole fisadi na wemeishia kuwa nyama ya udongo???
Vyombo vya habari vingapin vimeadhibiwa kwa kuandika ukweli dhidi ya fisadi?

Tanzania tuna-baby-sit mafisadi. Hasa viongozi tuliowapa dhamana, huenda nao wananufaika na ufisadi huu.

Mimi nasema: HAKUNA KUFUATA MFUMO WOWOTE WA HABARI MPAKA TANZANIA IWE HURU, KIUFISADI.

Huko Uingereza na Marekani tunawaona wanavyowajibika na kuwajibishwa pindi ijulikanapo ufisadi umenukia ktk sekta. TANZANIA TUMEFANYA NINI???

Ni aibu kusema tuige mfumo upi? ni bora tusiige, kwa sababu mengi tunayosema tunayafuata toka njee in reality HATUYATEKELEZI IPASAVYO.

mimi nasema: HAKUNA KUFUATA MFUMO WA HABARI WA UINGEREZA AU MAREKANI.

Ningekushukuru sana maada hii ungeileta namna hii: TANZANIA TUWASHUGHULIKIEJE MAFISADI, KU-UINGEREZA AU MAREKANI.

IKIBIDI HATA KI-ARABU TUTUMIE, HAO MAFISADI WAPIGWE MAWE MPAKA WAFE. NDIO CHANZO CHA GIZA KUKITHIRI Nchini (ktk technologia hii ya leo kwa nini nchi ikae Gizani?) hii inaingia akilini kweli?????, hivi nasi tunajihesabu tunaishi ulimwengu huuu????

Viongozi wetu kila siku wanatembelea nchi za wenzao, hakuna nachojifunza kweli???? hata mikakati ya kuiweka nchi safi? tunahitaji msaada mzungu aje atuambia ndani kwako kuchafu na hali wewe unaona?

Jamani! wakati umefika, kama viongozi waliopo hawawezi kututumikia basi watokeeee. Tupate watu wenye hali ya kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wananchi na nchi kiujumla.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Tanzania ifuate mfumo gani katika kusimamia habari zinazochapishwa kwenye mitandao.

Mimi naona tusifuate mfumo wowote, kwa sababu matatizo yetu hayafanani na Marekani au Uingereza. Hao waliofikia kuweka mifumo ya kulinda habari leo walishapitia hapa tulipo sisi leo (uhuru wa habari mtandaoni). Hivyo wacha Watanzania wawe huru kuandika habari. Cha msingi habari ziwe na ukweli, leo tumeona jinsi tunavyoweza kupata habari nyeti mtandaoni. Zenye ukweli first class. Watanzania tumefungiwa uhuru wa uandishi wa habari kwa miaka mingi sana. Kila kitu kuhusucho nchi, utawala au kiongozi ilikuwa ni SIRI KUU.
Huo usiri mkuu umetufikisha kwenye hali hii:
1) poor education system and facilities
2) poor health care system
3) poor infrastructure syatem etc.

Kwa sababu hakuna aliyekuwa na haki ya kuhoji chochote. Tumetawaliwa kama mazumbukuku hadi leo hii. Ni aibu sana.


Chamtu... Heshima yako Mkuu.

Nafikiri mapendekezo yangu ni kufuta ( repeal) baadhi ya vifungu vya sheria ya Utawala wa Taifa( hasa suala la classification of government information...ambayo hiko too general).

Pili sheria ya magazeti ya 1976 ambayo inampa madaraka makubwa sana ya waziri wa habari kufungia gazeti bila hata kufuata natural justice. Mfano : Kesi ya Mwahalisi kufungiwa.

Tatu: Sheria ya FOIA (Freedom of Information) iundwe na kuweka bayana kabisa kwamba serikali inawajibu wa kutoa habari na kukataa kutoa hizo habari hiwe kwa manufaa na usalama wa taifa, Pia hiyo sheria iwape wananchi fursa ya kwenda mahakamani kutafuta haki ya kupata habari za serikali.

Kwa hiyo mimi pendekezo langu ni kuwa na hybrid ya sheria ya uhuru wa habari ya marekani ambayo itakuwa subject to mazingira yetu.

Mwisho je, linapokuja suala la utamaduni wa Mtanzania, ni njia zipi zitumike kuulinda?
 
Shadow hueleweki.....

Mkuu yoyo,

Nimejaribu kuunganisha na kubalance kati ya kulinda uhuru wa habari na kujieleza na kwa upande mwingine kulinda na kusimamia utamaduni wa mtanzania. Au ndo kizazi cha dot com kwamba tuwe kama kokolo tunavua samaki na visivyolika? Je, kuna haja ya kuwa na sheria itakayo ondoa 'kinga' kwa hawa wanasiasa[naongelea suala la sedition kwenye makosa ya jinai na arbitrary rulings za waziri wa habari]. Je, tujaribu kuangalia mfumo wa nchi mbili nilizozitaja hapo juu na kufuta mmoja wapo au tutengeneze mfumo wetu wa 'hybrid' kusimamia haki ya kujieleza na habari( freedom of expression & speech.

Vile vile, Nimetumia mfano wa 'Ze Utamu' kama pro and cons za uhuru wa kujieleza wakati huo huo ukitamani kulinda utamaduni wa Mtanzania(But I have my reservations on the contents of the said blog)

That is the message, I am trying to convey to you and the rest of JF forum.

Wasalaam.
 
ILI SAKATA LA VITAMBULISHO VYA URAI LIKOJE JAMANI !!!!NI KIINI MACHO AU NDO TUMELIWA ???

Ni vyema Waziri mwenye dhamana ya Urai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakatusaidia kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Serikali (CPD) kwenye hili sakata la vitambulisho vya uraia.

Tafiti za sisi wachache "wafia nchi" zimebaini kuwa ipi sheria inaitwa "THE REGISTRATION AND IDENTIFICATION OF PERSONS ACT, ( No. 11 of 1986)Cap. 36 R.E.2002. Madhumuni makuu ya Sheria hii ni kuweka utartibu wa kusajiri watanzania na kutoa vitambulisho vyao na masuala maengine yanayohusiana " to provide for the registration of persons in the United Republic, the issue to them of identity cards and for connected purposes".

Kifungu cha 2 cha Sheria hii kinasomeka hivi kwa lugha ya kigeni:

" This Act shall come into operation on such date as the Minister may, by notice published in the Gazette, appoint"

(yaani kwa kibongo, inamaanisha " Sheria hii itaanza kufanya kazi baada ya Waziri husika kutangaza tarehe ya kuanza kazi kwenye Gazati la Serikali".)

Kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria hii, inatamkwa kuwa Sheria inapaswa kutumika kwa Tanzania Visiwan na Tanzania Bara.

Kifungu cha 5 cha Sheria hii kinampa Waziri mwenye dhamana ya Raia kuteu Msajili wa Urai (Ragistrar) Registration of persons.

Kifungu cha 7 cha Sheria hii kinamataka mtu yeyote anayeishi Tanzania baada ya kuanza kazi kwa sheria hii na amabye ametimiza miaka kumi na nane (1 kuomba kusajiliwa chini ya sheria hii.

Kwa kimombo kinasomeka " 7(1) Subject to subsection (2) and to other provisions of this Act, every person of or above the age of eighteen years who, on or after the commencement of this Act, is or resides in the United Republic and to whom this Act applies may make an application for registration in pursuance of this Act"

Kifungu cha 9 kinaweka utaratibu wa kuwasilisha maombi ya usajili. Sehemu ya Tatu (III) ya Sheria hii inaweka utartibu wa kutoa vitambulisho Kifungu na rejea ya kifungu cha 10 inaonyesha kuwepo kwa aina mbili ya vitambulisho (two types of identity cards) kwa kadiri ambavyo Waziri husika atakaovyoona inafaa ambavyo ni (a) citizens of the United Republic;
(b) aliens resident in the United Republic;

Kifungu cha 10(2) kinabainisha kuwa kitambulisho kitatolewa baada ya mwombaji kulipia gharama na kusajiliwa.

" (2) Upon the registration of a person in accordance with this Act and upon payment by him to the registration officer, of any fee payable in that behalf, the registration officer shall cause to be prepared and issued to that person an appropriate identity card"

KIINI MACHO NA CHA KUSIKITISHA NI KUWA:

  • Wakati utaratibu wa kutafuta wazabuni wa kutengeneza vitambulisho unaendelea, rejea kwenye vitabu vya sheria za Tanzania ambazo zimefanyiwa mapitio mwaka 2002 (Revised Edition) na kuchapishwa na kampuni ya Juta ya Afrika ya Kusini chini ya ufadhili wa Serikali ya Sweden, inaonyesha kuwa Sheria hii itakayosimamia usajili wa Wabongo na pia Vitambulisho vyao hajawahi kutangazwa kutumika hapa nchini tokea kutungwa kwake mwaka 1986 (Not yet in force????).
  • Aidha, hata kama sheria ingekuwa inatumika, bado ingepaswa kwa utartibu uliowekwa na sheria, kwa mtu kupata kitambulisho ni lasima kwanza asajiliwe na ndipo kitambulsho kitolewe.
  • Kama sheria haijatangazwa kufanya kazi ni wazi hakuna ofisi za watendaji akiwemo Msajili, Je ni nani anayeratibu mchakato wa sasa wa vitambulisho vya raia??? Je Waziri mwenye dhamana ya Uraia anapata wapi nguvu hii ya kusimamia sheria isiyofanya kazi???.
EBU MTUSAIDIE JAMANI, ILI ZOEZI LA KUPATA WAZABUNI ILI WATENGENEZE VITAMBULSHO SASA VITASIMAMIWA NA SHERIA GANI???
 
kweli kwa sababu heshima ya mtu ni MALI kama mali nyengine mtu anazoweza kumiliki, sheria zipo zinazolinda uhai na mali ya mtu lakini sheria ya 'kukashifiwa' haijanyooka kulinda heshima ya mtu katika medani za utandawazi, mf.unaweza kusema kuwa fulani ni fisadi lakini ukiitwa pahala useme kafisidi nini hujui , ww unasoma katika mitandao na vyombo vya habari kuwa fulani ni fisadi, na hii ndo maana wana JF wengi hutumia majina yao ya vivuli kwa kuwa baadhi ya post zinakuwa zinazowasema watu fulani na mambo ya ufisadi hazijitoshelezi zinakuwa kama dhana tu na habari za kusikia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom