Who is Salim Ahmed Salim?

Thanks Guys kwa kukata issues za uongozi hapa. Lakini Ukweli unabakia pale pale siasa ni mchezo ambao rafu zake hukera. Siasa huweza kuibua watu usiowategemea na kuwadumaza watu usiotegemea.
Kwa siasa za Tanzania sasa hivi Salim ku qualify kuwa rais ni ndoto unless Tanzania mazingira ya ya kampeni na mitandao na rushwa vikome. fanya utafiti utagundua kuwa kuanzia serikali za mitaa, wabunge na hata Rais kuchaguliwa kwao si sera zao madhubuti bali ilitegemea walikata kiasi gani. Ufisadi umezidi pale ambapo kuchaguliwa kwako inategemea How much mfisadi you are. Viongozi madhubuti hawachaguliwi. kumbukeni kauli ya Kingunge wakati wa uchaguzi wa CCM. ALISEMA HAKUWA TAYARI KUTOA RUSHWA LILI ACHAGULIWE. Je Salim how keen is he in corruption? Pili viongozi walio wengi siasa ni proffession ya mkato kupata mali kwa chee and easy.

Salim ana CV nzuri, lakini wakati wake umeisha jamani. he is too old now. mwacheni apumzike sasa. Tangu akiwa na miaka 19 tu sijui 22 tayari balozi. Je ina maana alikuwa na udiplomasia kiasi gani kupata ubalozi? wakati wengine miaka 22 tuko form 2 wkati huo!!! sometimes BAHATI NAYO. Of course kwa salim alikuww anamwakilisha FAVOURS ZA BABA YAKE! vIONGOZI MADHUBUTI TUTAWAPATA SIKU WATANZANIA WAKING'AMUA KWA THITHIEM BOMU!na miungu wadogo eti kwa sababu ilitoka na TANU na ASAP vyama vilivyoleta uhuru wa TZ.(Hata Jongwe alileta uhuru zimbabwe lakin sasa hivi ahafi!!!) WAPINZANI WACHUKUE NCHI THEN KUANZANIA HAPO MAMABO YATAKUWA mswano SIO KULAMBANALAMBANA!!

ukweli ni kuwa huyo salim hana lolote, na alipata huo ubalozi wake kipindi kile nyerere kawafunga watu wasione mbali, hebu piga picha kama angekuwa kipindi hiki angepata hata ukatibu tarafa na miaka yake 22?

na kama kasoma na CV zake ni za kufa mtu je anaitumiaje elimu yake kwa kusaidia japo kukemea uharo unaofanywa na wenzie wa CCM? au elimu yake kanyamaza nayo tu huku anaangalia watanzania wanavyoteseka kila kukicha? sasa hii ni akili au ni matope?
 
Mh. Zitto,

Hiyo tiketi ni ya kufikirika zaidi.Salim na Slaa compatibility ndogo. Kimtazamo hata kihistoria.


Halafu hatuna private candidates Tanzania, kwa hiyo watakwenda na tiketi ya CCM au CHADEMA?

Salim should have engaged himself with a greater hunger for leadership than he did.But then again the whole country except myself and a very few keen observers were swept by Kikwetemania.

Some have questioned his complacency as undesirable and unpresidential.Kama alijua Kikwete ni mtu gani hiyo ingekuwa sababu kubwa zaidi kwake yeye kupigana tooth and nail ili nchi isiende to the dogs kama inavyoenda sasa hivi.But did he do that? No.

Katika watu wote waliokuwa wanataka nafasi ya urais nilifikiri Salim was the most qualified.
 
Hivi ni nini kweli achievement yake OAU... Rwanda, Liberia, Ivory Coast, Sierra Leone...na uchafu mwingine wote africa ulitokea under his watch, labda mtu atueleze zaidi ya kuwa diplomat wa muda mrefu na kuishi nje...ni nini kweli achievement yake...all i see is ceremonial medals and honorary degrees.

I think Prof was more qualified...( to enter politics un-opposed for 2 terms consecutively and then running for presidency (a rookie) defeating old veterans of ccm... i think he suprised many. ndo maana anapigwa vita, ni threat huyu jamaa....

But then again...Im sure he wouldnt have taken us down this path like muungwana
 
This Journal gives a good background...Salim was implicated by the Znz regime in the treason trial..i think it was because he was with the Umma Party whom its members where despised by ASP. Nyerere pretty much saved their lives by offering these Umma party people high positions in the new Union Govt.


"...Not surprisingly, one of the first issues to be addressed by Karume and his associates was that of the ASP/Umma Party relations. Karume demanded, and got, a merger of the two organisations, all other political parties being banned.

Although this merger gave Karume a greater degree of administrative control over the ex-Umma Party cadres it could not, of course, resolve the fundamental political differences, which were rooted in the clash over the class character of the new regime; although they also, more mundanely, reflected rival personal ambitions, tendencies towards ethnic solidarity, etc.

Indeed, in so far as this merger tended to organisationally unite the ex-Umma Party cadres and the more militant left wing of the ASP, and helped transcend the superficial Arab-Comorian character of the Umma leadership, its long-term implications were not entirely favourable to the Karume bloc of the ASP. This was a fact clearly discerned by the astute Karume who, shortly after this merger, actively 'encouraged' major Umma leaders to depart Zanzibar.

Among those who left the islands, following the union of Tanganyika and Zanzibar in April 1964, were Babu, Salim Ahmed Salim and Ali Mafoudh. (Salim had been the editor of the Umma Party newspaper; he went on to serve as Tanzania's ambassador to the U.A.R., India and the People's Republic of China, and is at present their ambassador to the U.N. Mafoudh subsequently held the second most important post, that of Chief of Operations, in the Tanzanian People's Defence Force. All three of these men were directly implicated by the Zanzibari autho- rities in the alleged treason plot, although Salim was never charged.)

Karume was aided in this endeavour by the Tanganyikan President, Julius Nyerere, who was already uneasy about the general leftward drift of the islands, about the openly expressed Marxist views of the Umma cadres and their impact on Zanzibari policy, and about the possibility of a disruptive clash on the islands, which were of some strategic sensitivity to Tanganyika.

Nyerere opened high positions in the Tanganyikan administration to the former Umma leaders, whose political impact was more easily diffused within the larger Tanganyikan administrative apparatus, especially in view of their lack of a mass base in the larger entity."

...The Zanzibar Treason Trial
Author(s): Hank Chase
Source: Review of African Political Economy, No. 6, (May - Aug., 1976)
 
Mwanahabari,
Labda leo ndio siku ya kusema ukweli ambao siku zote umekuwa tukifichwa na serikali yetu. Habari nilizozipata ni kwamba Umma party ndio waliopindua serikali ya Sultan wakisaidiwa na wahuni akina Okello sio kabisa Afro Shiraz na kina Karume, hawa ni opportunist waliozuka kunyakua tonge mdomoni.

Ni baada tu ya Mapinduzi hayo, hawa jamaa (Umma party) waliwekwa kitako na Nyerere wakafungiwa kanyaboya kwani mapinduzi hayo muhimu yasingeweza kudumu.

Sasa leo hii hawa CCM wanapomwita Salim ati mwarabu na mwanachama wa Hizbu ni kumtukana matusi ya nguoni na kutokuwa na shukran kwani Salim alikwisha toka chama hicho na kuwa mwanachama wa Umma (Wa komunisti) ambacho kilipingana sana na Hizbu (Usultan) na pia mrengo wa wa ASP. Hii ni njama makusudi kabisa za kumshusha Salim kwa sababu kila kiongozi wetu leo hii macho yao ni Ikulu.
Kwa hiyo hizi hadithi za kumsakama Salim hazina base hata kidogo isipokuwa huyu jamaa ana kipaji fulani ambacho ni hatari kwa watawala wetu weusi ambao waliyachukua Mapinduzi ya Zanzibar na kuyafanya yao (kina Karume)

Na kama nakumbuka vizuri Abrahman Babu alikuja kuwa wanted kwa sababu alikisiwa kuwa alihusika na mauaji ya Karume (wakisema Umma party ndio walipanga baada ya karume kuwazidi Ujanja) which we came to learn haikuwa kweli lakini too late kisha safer kishenzi. Kifupi wanachama wote wa Umma party walikuwa na wakati mgumu zaidi kuliko tunavyofikiria kwani hadi leo hii hawapo ktk picha ya historia na Mapinduzi ya Zanzibar.

Hizi ndizo siasa za Africa, kupika majungu na kumtafutia mtu Fitna kiasi kwamba Salim anafahamu hapendeki ndani ya CCM wala Zanzibar kwenyewe kwa sababu he was on the wrong side...
Hivyo mkitegemea mtu kama Salim kujitoa mhanga wakati anafahamu kwamba hana wafuasi zaidi ya watu wana question race yake, imani yake na pengine hata Watanzania wenyewe hawamfahamu bado baada ya ku serve Taifa letu kwa zaidi ya miaka 40, leo mnataka kweli ajitokeze mahala ambapo Watanzania wenyewe hawakuweza kusimama kumtetea alipoitwa Mwarabu na Hizbu.

Ni jukwaa gani ambalo ataweza kusikilizwa ikiwa maswali yenyewe ndio haya ambayo yamejaa dhihaka, upuuzaji na uvivu wa kumbukumbu.
Jamani jamani kwa nini sisi kila siku tunahitaji Mtume?.. yaani Yesu wa kubeba msalaba kwa ajili ya madhambi yetu sisi wenyewe!.

When sisi Watanzania tutaweza kusimama nyuma ya viongozi wetu waadilifu na kuwatetea kila wanapokutana na vikwazo kama alivyowahi kutana navyo Salim.

Kusema sana haiwezi kusaidia kitu kwani hata kina Warioba, Butiku na wengine wengi tu wameweza zungumzia kuhusu mafisadi lakini kimefanyika kitu gani?..Je, ni kweli watu wote waliozungumzia Ufisadi ndio viongozi wanaotakiwa kutuongoza maanake hata Mkapa alikuja na sera zake za UWAZI lakini kulikuwa na UWAZI gani zaidi ya kuibiwa zaidi.

Nitasema kweli daima kwamba hakuna kiongozi bora kwa Mtanzania leo hii isipokuwa yule atakayeweza kusimama dhidi ya Ufisadi kwa vitendo na hadi sasa hivi namwona Dr. Slaa na Zitto kama watu walioshika usukani, yet hadi sasa hivi siwezi kuweka madai kwamba ndio wanafaa nafasi ya Urais kwa sababu kiti hicho kina mengi zaidi ya kauli ya mdomo.
 
Mkandara,
Kweli nimekuwa nikisoma journals za siasa za uhuru na kufuatilia kilichotokea Zanzibar, ni maajabu kweli hawa ASP walivyokuwa wanaua watu huko kwa visa vya kisiasa, naona Nyerere aliwalinda sana hawa Salim na hata Babu, ilikuwa bora wawe nje ya nchi na Babu aliruhusiwa kutorokea UK kuliko kurudishwa Zenj maana makundi ya Karime yangewaua hawa jamaa kwa mambo yasiyo na msingi.

Hawa watu wa CCM kweli walimchafua sana Salim, CCM mimi nilisema kwamba lazima kijisafishe amasivyo nchi hawana 2010 . Ni uozo mtupu huu tunaoona sasa, na wamejipanga kwenye sehemu nyeti za sheria (Mwanyika, Hosea, etc) so inasikitisha kweli kwamba sheria haitafuatwa kabisa kuwahujumu mafisadi kwasababu wanalindana.

Salim anaheshimika sana, ila in substance i just believe we really need to disect his achievement as to what he has done that has directly helped a Zanzibari or a Tanzanian. He is honourable and respected, but this is due to the position he was in for many years. I am interested in knowing his achievements as Prime Minister and a Minister (I hope to hear from someone who has studied Dr. Salim thoroughly). Tumeshaona JK alikuwa Waziri for many years, look at whats happening now.

With these positions, I agree with you that it is what they do in those positions are all that counts...we must ask all the questions we can no matter how high the position is.

I hope tutapata kiongozi wa maana baada ya huyu wa sasa
 
Nashindwa kukuelewa Ben, Makamba anahusishwa vipi na na uchimi, yeye si katibu tu wa Chama?, nafikili kushindewa kwetu kwa uchimi na nchi jirani ni swala la rais na wizara husika

usiwe na chuki binafsi na chama, hayo ni maoni tu


Makamba ni Katibu mkuu wa chama kinachotawala(Si kinachoongoza).Yeye ndiye msimamizi mkuu wa sera za hicho chama tawala.Makamba kwa nafasi yake ya ukatibu angekua na uwezo wa kufuatilia kwa karibu kama utendajia wa Rais na cabinet unaenda vyema ili kuwaletea wananchi maisha bora amabyo waliahidi.

Angalia tangu tuhuma za ufisadi ziibuke,ulishawahi kusikia tamko la CCM au hatua za CCM kuwaita watuhumiwa na kuwashughulikia kimaadili wao kama CHama? Ufisadi ni jambo amablo linadumaza uchumi.Kushamiri kwa ufisadi ndani ya chama na hatimaye serikali ni kudidimia kwa uchumi.Hapo ndipo Kenya wanapotuburuza.Hapo sawa?


Chama tawala kingekua na viongozi waadilifu na wachapa kazi leo hii tungwekua na serikali adilifu!

Pia,hilo suala la kuichukia CCM umesema wewe! Hata hivyo nina sababu za kuichukia,siwezi kuuchukia ufisadi halafu niikumbatie au niipende ccm kwani hawa ni chanda na pete.Kwani hilo jina la pili la CCM,UFISADI.

Nachukia tabia ya CCM ya usaliti kwa wananchi

Tabia ya usaliti kwa mashujaa wetu wa uhuru


Tabia yao ya kuamua kuwa wakoloni na kuukandamiza uma au makundi flani ktk jamii ya Mtanzania

Tabia ya kulundika wabinafsi na wahujumu uchumi huku mtanzania anepigika na maisha kila siku akilipa kodi ambayo wachache wamelimbikiza nje ya nchi.

Sitaki kuendelea zaidi maanake nina uchungu na matendo yao
 
CV ni mzuri sana hila ukweli ni kwamba rais wa nchi masikini kama Tanzania anatakiwa kuwa zaidi ya CV na diplomasia.

Urais wa nchi kama Tanzania unahitaji sana vitendo, na mtu anayeweza kuchukua risk ktk kutoa maamuzi mazito, ambayo nikimuona mweshimiwa huyu pamoja na diplomasia anakosa.
 
CV ya Salim ni nzito sana, lakini pia CV zetu wananchi wa Tanzania ni suspect,

However, kama anataka urais, Salim anahitaji kushinda kwa kura , kuanzia za mizengwe ndani ya CCM, na hatimaye taifa, ambako so far kote kumemshinda, na kwa bahati mbaya Tanzania hatuna system ya kumpa kiongozi urais kwa kutmia CV yake nzito,

The man is arrogant na sio a true politician, kwa sababu angekuwa, basi katika vipindi vyake vyote vya uongozi angejaribu ku-deal na his two big political problems, ambazo zote zilishawahi kuwa raised mara nyingi sana huko ndani ya CCM, alikuwa na muda wote duniani kuzijibu on his political time, lakini yeye akanyamaza kimya na kuendelea na huko nje, akisubiri time aje kugombea bongo!

Uarabu wake na kifo cha Karume, ni ishu mbili ambazo zimekuwa zikimla toka mwaka 1985 wakati Mwalimu anatoka, sasa toka then mpaka 2005, kama kweli Salim ni mwanasiasa wa kweli angeweza kuyajibu haya maswali in a very smart political fashion na kuyazima, lakini wapi?

Sasa labda abaki tu huko Abuja na CV yake, haya maneno ya tiketi ya Salim na Slaa, ni matusi makubwa sana kwa sisi wananchi tuliochoshwa na uozo na ufisadi, he had his time sasa ni saa ya wengine kujaribu, believe me wako wengi sana hapa bongo, wenye uwezo na CV nzito!

Ahsante Wakuu!
 
CV yake ni ya kufa mtu kweli , mengine sitasema maana wamesha yasema vyema ila the bottom line ni kwamba Salim hauwezi Urais wa Tanzania .Hatakuwa natofauti na hawa wa leo .Hana historia ya uongozi bora ila ana historia ya Diplomasi bora .
 
Field Marshall Es,

Hapana mkuu hiyo arrogant ni rangi alopakwa Salim na CCM ili watu wote wapate kuamini hivyo...na kama ulivyokwisha sema wewe mwenyewe kuwa viongozi wetu ni reflection yetu! wanafahamu Mdanganyika ni mwepesi kukubali uongo unaokubalika.

Ebu Mtazame John Malecela, huyu amepitia nafasi kama za Salim as a fact alikuwa na sifa zote za Urais ktk viti alivyowahi kushika.. Yuko wapi leo tunaambiwa hafai wala hauziki wakati Ngombale Mwilu aliyeyasema haya kamzidi Malecela kwa Umri..Je, ni sifa gani za uongozi tunazotafuta wakati hatuna data za wizara walizowahi kushika kama mawaziri. Who qualify kiti cha urais Tanzania kwa kufuata mifano alokwisha ifanya? as a fact Nyerere alikuwa na sifa gani kabla hajachukua kiti cha Urais, Mandela au Nkurumah nambieni ni sifa zipi zilizotangulia?

Je, ni umri ndio tatizo letu ama ni kiongozi ambaye anaweza kuleta mapinduzi ya kiuchumi na amani kati ya bara na visiwani. JK kijana kaweza kufanya yapi yanayoashiria Ujana!..
Pili tatizo letu hatuna malengo ya kugombea Urais ktk kila awamu (Priority zetu).

Kikwete alipopita Urais maswala mawili makubwa yalikuwa mbele yetu..
1. Muungano
2.Umaskini na Maradhi - Maendeleo ya kiuchumi kuwafikia wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu yetu tupate kuwa Taifa lisilo tegemea misaada.

Sasa ukija tazama muungano wetu Salim was the right person kwa wananchi achana na mtazamo wa chama kwani ASP wamekwisha vamia utawala toka Mapinduzi, hawa hawana tofauti na Saadam Hussein hivyo kubomoa CV ya Salim wameshindwa isipokuwa kumpaka tope.

Tujiuliza sisi wenyewe raia, Je wananchi wa Zanzibar na Bara hawamkubali Salim?.. Je kweli kuna mtu anayeweza kusimama na Salim ktk uchaguzi wa rais (popular vote) pande zote mbili!... jibu hakuna na sio kwamba Salim hapenda kusimama kugombea isipokuwa hana nafasi hiyo kafungwa kamba za miguu na hawa CCM mpya, so is Malecela, kina Warioba na Sarakikya...

Kama mbuzi hana pa kwenda na ajabu ni kwamba sisi wananchi tunamwita Arrogant kwa sababu bado yupo kwenye kamba..

Halafu mkuu kama umesoma vizuri maelezo yangu hapo kuna fumbo moja zito sana ambalo sidhani kama wengine mmeweza kulitazama kwa mapana..

Nimezungumzia Salim na jinsi alivyonaswa ktk mtego wa CCM ambapo the only person aliyekuwa akimlinda alikuwa Nyerere. Alipoondoka Nyerere basi Salim became Political lamb...na huduma zake zote za miaka 40 zimefukiwa kaburini kiasi kwamba hakuna Mtanzania anayemfahamu Salim kama kiongozi. Tumeshasahau kabisa kuwa media Tanzania ilikuwa controlled na serikali na kiliandikwa tu kile kilichotakiwa kuandikwa.. besides hakuna mtu aliyepewa sifa za ufanisi wa kazi zaidi ya mwalimu mwenyewe hata kama kilifanywa na Salim Warioba ama Malecela..The only Prime Minister ambaye anaweza kusimama kwa sifa fulani alikuwa Sokoine wakati wa kupambana na mafisadi wa ndani.

Ni hadithi hiyo hiyo naiona kwa watu kama kina Zitto na Dr. Slaa ambao wameyafanya mengi kwa wakati huu lakini ipo hatari kubwa ya watu hawa kumezwa na kufungwa kamba na CCM. 20 years from now mtakuja sahau na pengine kujiuliza hawa kina Zitto wamefanya nini na pengine kumkumbuka zaidi Pinda kwa sababu kuna problem ya ndani.

Think about it, sio kwamba najaribu kumuuza kwenu Salim isipokuwa nausema ukweli ambao serikali yetu haipendi wananchi tufahamu.

Ebu jiulize kitu kimoja mkuu, ilikuwaje CIA waingie ktk Mapinduzi ya Zanzibar wakisema nchi hiyo inakwenda kuwa ya Kikomunist wakati sio Hizbu wala ASP walikuwa na mrengo wa kikomunist?.
Mapinduzi halisi hayakuchukua masaa lakini aftermarth kilichotokea baada ya mapinduzi na Karume kushika nchi hadi leo ni kumbukumbu mbaya sana ya Saadam kwa Kurdish... ajabu kama Saadam, watoto wake ndio wamepangana kutawala visiwani wakigawana mali za nchi hizo utadhani Mungu kawaandikia mirathi hiyo!

Come on now FMES, p[roblem kubwa ya nchi yetu sio Salim na watu kama yeye isipokuwa ni swala letu sisi kuwa wavivu na wapuuzaji wa mabo muhimu yanayojitokeza. Arrogant ni Mkapa na aliweza kutuonyesha wananchi wote yet aliweza kaa miaka 10 na sifa kubwa kapewa za Unyapala wake.
 
Kuna mtu amezungumzia kumhusisha Dk Salim kwenye mwafaka!
Labda niulize swali... WHY Mwafaka??
KWanini waafrika hatujifunzi demokrasia?
Mbona US baada ya uchaguzi wa 2000 hakuna aliyezungumzia kuundwa kwa serikali ya mseto kati ya Bush na Gore.. tofauti ya kura ilikuwa 0.2%!!

Mbona hii miafaka iko Afrika tu?

Kama mtu akishindwa uchaguzi then analilia serikali ya mseto kuna haja gani basi ya kupiga kura.. kwa nini tusikubaliane tu . leo Rais anatoka CUF... VP CCM... baada ya miaka mitano zamu ya CCM.. VP atoke CUF.???????

Serikali inazidi kunenepa tu lakini tasa! Badala ya kufanya Reforms za maana tumekalia longolongo.. kuanzia bungeni hadi wenyeviti wa mitaa!

Inabidi tujifunze demokrasia. Chama kimeshindwa uchaguzi.. basi subirini next 5 years. In between, kaeni chini fanyeni uchambuzi yakinifu mlikosea wapi ili next time msishindwe uchaguzi... na kama chama kimeshinda uchaguzi kihakikishe kinatekeleza ilani yake ya uchaguzi ili next 5 years kiwe na evidence kwamba turudisheni madarakani.. we promised A, B , C... et cetera.. and we did it!
Si ndio maana watu wanasoma Political Science.. au kudesa kumezidi ikifikia ku-apply mambo tunaota matege kichwani??

Ingekuwa busara kama hela za walipa kodi zingetumika kwenye "vikao" vya kurekebisha katiba na kuboresha sheria za uchaguzi ili kuondoa mapungufu yanayojitokeza kila siku kama si kuyafuta kabisa!

Haya mambo ya Washington kutuamuru cha kufanya, sijui serikali ya mseto... ni Ukoloni tu!
Mbona wao hawajaribu huu upuuzi?
Washatuona Waafrika mazuzu.. akili kumkichwa Zero!
inabidi tuache kuwa dictated na wakoloni!

Kila mtu anajua kuwa Pemba strategically ni ngome ya CUF kama Republicans walivyo na ngome kubwa Southern States. Ila si sababu ya kupiga propaganda kwamba bila CUF kuwa ndani ya serikali basi Pemba haitaendelea au sijui kama CCM itatoka madarakani basi kutatokea machafuko ...crap!!
Tuko kwenye karne ya 21, hakuna kitu kinachoshindikana.

It is always possible to possibily the impossibilities... watu wamesulubiwa, wakafa, wakafufuka na kwa mkwala wakapaa mbinguni.. then wakaahidi watarudi kama walivyopaa... sembuse waafrika kujitawala bila kutegemea wakoloni????



Acha kunananisha limau na machungwa kwa kuwa yote ni tu ni matunda. Tofauti ya Zanzibar na USA ni kuwa Zanzibar CCM waliiba kura ama kwa lugha nyepesi uchaguzi ulivurugwa- Ndio maana MUAFAKA unahitajika wakati ambapo huko USA walikubaliana. Zanzibar kunahitaji usuluhishi manake siasa imekuwa uadui.

Aidha dhana ya mseto mbona imetumika nchi nyingi tu za ulaya pale matokeo yanapokaribiana sana?

We si umeona wajerumani mpaka wamefanya grand coalition?

Asha
 
Biography of Dr. Salim Ahmed Salim
Dr. Salim Ahmed Salim, who concluded his term of office as Secretary General of the Organization of African Unity on 17 September 2001 after serving an unprecedented three terms covering a period of twelve years, is now involved in several activities. He has functions and responsibilities at national, continental and international levels.

At the national (Tanzania) level he is serving as the Chairman of the Board of Trustees of The Mwalimu Nyerere Foundation. He is also the Chancellor of the Hubert Kairuki Memorial University.

At the continental level, following the invitation of the President of the African Development Bank, he has since March, 2002 been acting as African Water Ambassador whose responsibilities include advocacy, sensitization, and mobilization of support on African water issues. He also serves as:

Chairperson, Advisory Board, Institute of Security Studies (ISS) based in Pretoria, South Africa.
Chairperson of the International Board of Trustees, Africa Humanitarian Action (AHI) based in Addis Ababa, Ethiopia.
Member and Chairperson of the Advisory Board of Trustees of the Institute of Peace, Leadership and Governance, Africa University, Mutare, Zimbabwe.
At international level, Dr. Salim serves in the following Boards, Panels/Commission

Co-chair, Eminent Persons Group (EPG) on Small Arms and Light Weapons (Secretariat, based in Washington DC);
Member of the Board of the South Centre (Secretariat based in Geneva);
Member, Policy Advisory Commission, World Intellectual Property Organization (WIPO);
Member of the Foundation Council, Centre of Humanitarian Dialogue based in Geneva.
Previous Experience and Positions Held:
Dr. Salim Ahmed Salim was elected Secretary-General of the OAU on 27 July 1989. He formally took over on 19 September 1989. Prior to his election, Dr. Salim held public office in his country, the United Republic of Tanzania, where he served in various capacities for 27 years. He was Prime Minister from 1984 to 1985 and then served as Deputy Prime Minister and Minister of Defense and National Service from 1985 until his election to the helm of the OAU General Secretariat.

Dr. Salim also held other key positions in the Government of the United Republic of Tanzania. He served for many years in the Tanzanian diplomatic service which he also steered as Minister for Foreign Affairs for four years from 1980 to 1984. His rise to the top of Tanzania’s Foreign Service was preceded by many years of grounding in international diplomacy as Ambassador. He served as Ambassador to the Arab Republic of Egypt (1964-1965), High Commissioner (i.e. Ambassador) to India (1965-1968). He was, for one year, the Director of Africa and Middle East Division in the Ministry of Foreign Affairs in Dar-es-Salaam before his posting as Ambassador to the People’s Republic of China in 1969. In 1970, he was appointed Tanzania’s Permanent Representative to the United Nations in New York, where he remained for more than ten years. During his period at the United Nations, Dr. Salim was concurrently accredited as Ambassador to Cuba, High Commissioner to Guyana, Barbados, Jamaica and Trinidad and Tobago.

During his service at the United Nations, Dr. Salim was elected as President of the United Nations Security Council in January 1976 and went on to serve as President of the Thirty-Fourth Session of the United Nations General Assembly in September 1979. During his one year tenure of office, he also presided over the Sixth and Seventh Emergency Special Sessions of the United Nations General Assembly in January and July 1980 respectively. In September 1980, he equally presided over the Eleventh Special Session of the United Nations General Assembly.

Dr. Salim was Chairman of the United Nations Security Council Committee on Sanctions Against Rhodesia from January to December 1975, President of the International Conference on Sanctions against South Africa in 1981 as well as the Paris International Conference Against Apartheid in 1984. Between 1972 and 1980, he chaired the United Nations Special Committee on Decolonization (Committee of 24). During this period under his chairmainship, the Committee played a key role in steering many colonies and non-self governing territories to full sovereignty and independence. Dr. Salim also served on the Palme Independent Commission on International Security Issues and the Independent Commission on International Humanitarian Issues.

Dr. Salim has attended and/or chaired numerous Summits, International Conferences, Seminars, Workshops and Colloquia under the auspices of the United Nations, the Organization of African Unity, the Non-Aligned Movement and others throughout the world.

Educational Qualifications and Honorary Degrees:
Dr. Salim undertook studies at the University of Delhi, India (1965-1968) and proceeded to obtain a Masters Degree in International Affairs in January 1975 at Columbia University in New York. He holds six Doctorates (Honoris Causa) including: Doctor of Laws, the University of Philippines at Los Baños (1980), Doctor of Humanities, University of Maiduguri, Nigeria (1983), Doctor of Civil Law, University of Mauritius (1991), Doctor of Arts in International Affairs, University of Khartoum, Sudan (1995), Doctor of Philosophy in International Relations, University of Bologna, Italy (1996), and Doctor of Laws, University of Cape Town, South Africa (1998).

Honours and Decorations:
Dr. Salim holds a number of decorations/honours (including some of the highest national honours). Among them are the Star of Africa (Liberia, 1980), the Order of the United Republic of Tanzania – Nishani Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, 1985), Order of Mille Collines (Rwanda, 1993), Grande Croix de l’Ordre Congolais du Dévouement (Republic of Congo, 1994), Grand Officier de l’Ordre du Mérite (Central African Republic, 1994), Medal of Africa (Libya, 9.9.99), Grand Officier de l’Ordre National du Lion (Sénégal, 2000), Order of the Two Niles (Sudan, 2001), Ordre El-Athir (Algeria, 2001), Ordre du Mono (Togo, 2001), Commandant de l’Ordre National (Mali, 2001).

Born in Zanzibar on 23 January 1942, Dr. Salim Ahmed Salim is married to Amne. They have three children: Maryam, Ali and Ahmed.

Dar-es-Salaam
April 2002

This is a very nice CV in writings but very poor in actions.

For the positions he has held, he would have left legacy in the lives of may Africans and Tanzanias.

Now then we have water ambassodor who has never given any statement regarding the shortage of water that is affecting women in his country.

This guy would have been better than Kikwete, the irony of Mwenyechongo katikati ya vipofu but sure he was note strong enough. He is not he best.

He has served in higher positions for almost 40 years with no apparent legacy.

Mwanakijiji's writings of few years have legacy than Salim or Zitto's and Dr Slaa's for that matter.

This guy is a YES man like Dr Shein, we would serve better to be a Vice President under DR Nyerere than being the president himself.


Ana unafiki wa kidimplomasia, ndio maana baada ya wakina Kikwete kumweka vidole vya macho alichoona cha maana ni kukimbilia Darfur na kuacha siasa za nyumbani kwake.

hebu niambieni hizo PHD zake nyingi za heshima zimasaidia vipi watanzania na waafrika?

Huyu naye ni mnafiki mwingine tu wa Chama Cha Mafisadi, anashindwa kabisa kuwakemea wenzake.

Ni ukweli huyu jamaa sio fisadi ila kitendo cha yeye kuwavumilia mafisadi kwa miaka mingi kinafanya niamini hata akiwa Rais hatawachukulia hatua.

Aendekeza yale yale kwa kisingizio cha Diplomasia.

Asha
 
Field Marshall Es,

Hapana mkuu hiyo arrogant ni rangi alopakwa Salim na CCM ili watu wote wapate kuamini hivyo...

Come on now FMES, p[roblem kubwa ya nchi yetu sio Salim na watu kama yeye isipokuwa ni swala letu sisi kuwa wavivu na wapuuzaji wa mabo muhimu yanayojitokeza. Arrogant ni Mkapa na aliweza kutuonyesha wananchi wote yet aliweza kaa miaka 10 na sifa kubwa kapewa za Unyapala wake.

Ninachokupendea ni historia. Watu wengi hawapendi historia hata kidogo na ndio maana hata hoja nyingine zinakuwa ngumu kidogo. Wakati Salim anakuwa Waziri Mkuu mimi nilikuwa darasa la kwanza mwaka 1984. Ninakumbuka shida ya njaa ya wakati ule, kunywa uji na ugali wa yanga (msaada wa mahindi kutoka marekani) na kuvaa mashati ya shule ambayo kimsingi yalikuwa ni vitambaa vya sanda. Viatu vyangu vya kwanza kuvaa vilitengenezwa Bora Shoes na viliitwa asante Salim.

Alifungua milango ya biashara. Misururu ya maduka ya ushirika ikaisha. Tukaanza kuvaa vizuri. Magendo yakapungua.

Wanajeshi ambao walikuwa wameanza kuchoka na coup was eminent, wakaangaliwa upya kwa kubadilishiwa uniforms na mabadiliko makubwa jeshini mara baada ya yeye kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mnakumbuka kwa nini alikuwa Naibu Waziri Mkuu? Kumsaidia Warioba ambae alikuwa PM lakini pia kupoza Watanzania ambao walikuwa wanamtaka sana.

Nashangaa sana kuna watu wanaweza kuja hapa na kusema hakufanya kitu. Alikuwa Waziri Mkuu mwaka mmoja na nusu tu. Lakini mabadiliko yaliyofanyika ni makubwa sana. Hata kwenda kwake OAU haikuwa kwa yeye kupenda bali alitolewa nyumbani na kuachwa huko mpaka siasa za nyumbani zimsahau. Nilikuwa kijana mdogo sana, lakini nakumbuka hali ilivyokuwa nchini.
Inawezekana Salim hawezi kuwa Rais sasa.

Hawezi akiwa peke yake kwani nchi inhitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo. Lakini ni moja ya Watanzania wachache waliopo ambao wanaweza kutuvusha katika kipindi cha mpito cha kukabidhi nchi katika generation ya AZIMIO - yaani Watanzania waliozaliwa kati ya mwaka 1967 na 1992. Mabadiliko yeyote ya kiuongozi Tanzania yanahitaji mtu mwenye kuona mbali, aliyetayari kuongoza muhula mmoja lakini akiacha 'legacy' kubwa. Mtu ambae atakubalika na pande zote za kisiasa na asaidiwe na no non-sense people kama Dr. Slaa hivi.

Pundit, maoni yako ni kweli kwamba hawa watu sio compatible. Lakini hali ya sasa inahitaji mpito na mpito unataka watu wasiwe compatible. Au unasemaje?

Mjadala huu ni muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu. Nimeupenda sana.
 
Biography of Dr. Salim Ahmed Salim
Dr. Salim Ahmed Salim, who concluded his term of office as Secretary General of the Organization of African Unity on 17 September 2001 after serving an unprecedented three terms covering a period of twelve years, is now involved in several activities. He has functions and responsibilities at national, continental and international levels.

At the national (Tanzania) level he is serving as the Chairman of the Board of Trustees of The Mwalimu Nyerere Foundation. He is also the Chancellor of the Hubert Kairuki Memorial University.

At the continental level, following the invitation of the President of the African Development Bank, he has since March, 2002 been acting as African Water Ambassador whose responsibilities include advocacy, sensitization, and mobilization of support on African water issues. He also serves as:

Chairperson, Advisory Board, Institute of Security Studies (ISS) based in Pretoria, South Africa.
Chairperson of the International Board of Trustees, Africa Humanitarian Action (AHI) based in Addis Ababa, Ethiopia.
Member and Chairperson of the Advisory Board of Trustees of the Institute of Peace, Leadership and Governance, Africa University, Mutare, Zimbabwe.
At international level, Dr. Salim serves in the following Boards, Panels/Commission

Co-chair, Eminent Persons Group (EPG) on Small Arms and Light Weapons (Secretariat, based in Washington DC);
Member of the Board of the South Centre (Secretariat based in Geneva);
Member, Policy Advisory Commission, World Intellectual Property Organization (WIPO);
Member of the Foundation Council, Centre of Humanitarian Dialogue based in Geneva.
Previous Experience and Positions Held:
Dr. Salim Ahmed Salim was elected Secretary-General of the OAU on 27 July 1989. He formally took over on 19 September 1989. Prior to his election, Dr. Salim held public office in his country, the United Republic of Tanzania, where he served in various capacities for 27 years. He was Prime Minister from 1984 to 1985 and then served as Deputy Prime Minister and Minister of Defense and National Service from 1985 until his election to the helm of the OAU General Secretariat.

Dr. Salim also held other key positions in the Government of the United Republic of Tanzania. He served for many years in the Tanzanian diplomatic service which he also steered as Minister for Foreign Affairs for four years from 1980 to 1984. His rise to the top of Tanzania’s Foreign Service was preceded by many years of grounding in international diplomacy as Ambassador. He served as Ambassador to the Arab Republic of Egypt (1964-1965), High Commissioner (i.e. Ambassador) to India (1965-1968). He was, for one year, the Director of Africa and Middle East Division in the Ministry of Foreign Affairs in Dar-es-Salaam before his posting as Ambassador to the People’s Republic of China in 1969. In 1970, he was appointed Tanzania’s Permanent Representative to the United Nations in New York, where he remained for more than ten years. During his period at the United Nations, Dr. Salim was concurrently accredited as Ambassador to Cuba, High Commissioner to Guyana, Barbados, Jamaica and Trinidad and Tobago.

During his service at the United Nations, Dr. Salim was elected as President of the United Nations Security Council in January 1976 and went on to serve as President of the Thirty-Fourth Session of the United Nations General Assembly in September 1979. During his one year tenure of office, he also presided over the Sixth and Seventh Emergency Special Sessions of the United Nations General Assembly in January and July 1980 respectively. In September 1980, he equally presided over the Eleventh Special Session of the United Nations General Assembly.

Dr. Salim was Chairman of the United Nations Security Council Committee on Sanctions Against Rhodesia from January to December 1975, President of the International Conference on Sanctions against South Africa in 1981 as well as the Paris International Conference Against Apartheid in 1984. Between 1972 and 1980, he chaired the United Nations Special Committee on Decolonization (Committee of 24). During this period under his chairmainship, the Committee played a key role in steering many colonies and non-self governing territories to full sovereignty and independence. Dr. Salim also served on the Palme Independent Commission on International Security Issues and the Independent Commission on International Humanitarian Issues.

Dr. Salim has attended and/or chaired numerous Summits, International Conferences, Seminars, Workshops and Colloquia under the auspices of the United Nations, the Organization of African Unity, the Non-Aligned Movement and others throughout the world.

Educational Qualifications and Honorary Degrees:
Dr. Salim undertook studies at the University of Delhi, India (1965-1968) and proceeded to obtain a Masters Degree in International Affairs in January 1975 at Columbia University in New York. He holds six Doctorates (Honoris Causa) including: Doctor of Laws, the University of Philippines at Los Baños (1980), Doctor of Humanities, University of Maiduguri, Nigeria (1983), Doctor of Civil Law, University of Mauritius (1991), Doctor of Arts in International Affairs, University of Khartoum, Sudan (1995), Doctor of Philosophy in International Relations, University of Bologna, Italy (1996), and Doctor of Laws, University of Cape Town, South Africa (1998).

Honours and Decorations:
Dr. Salim holds a number of decorations/honours (including some of the highest national honours). Among them are the Star of Africa (Liberia, 1980), the Order of the United Republic of Tanzania – Nishani Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, 1985), Order of Mille Collines (Rwanda, 1993), Grande Croix de l’Ordre Congolais du Dévouement (Republic of Congo, 1994), Grand Officier de l’Ordre du Mérite (Central African Republic, 1994), Medal of Africa (Libya, 9.9.99), Grand Officier de l’Ordre National du Lion (Sénégal, 2000), Order of the Two Niles (Sudan, 2001), Ordre El-Athir (Algeria, 2001), Ordre du Mono (Togo, 2001), Commandant de l’Ordre National (Mali, 2001).

Born in Zanzibar on 23 January 1942, Dr. Salim Ahmed Salim is married to Amne. They have three children: Maryam, Ali and Ahmed.

Dar-es-Salaam
April 2002

Can someone give me a book written by Dr Salim? Can someone tell me his vision on Tanzania, Africa or even the world? Can someone give me his most quoted speech or his most quoted quote? Or is he another routine CEO?

Asha
 
Katika moja ya vitabu ambavyo Salim A. Salim aliandikia CCM ambacho nilikipenda kile ambacho kilikuwa kinazungumzia namna ya kuondoa umaskini katika wananchi na hasa wakulima na wale wa kipato cha chini(KCC). Yeye katika kitabu hicho aliwataja kwa jina la "Wavuja jasho"
 
Muda wa Salim kuwa rais umepita wengine tutatawala lini?
 
Dua,
Nadhani kichwa cha mada hii kilisema MASHUJAA WETU!..
sasa nashangaa watu wanapoanza kuunda hoja ya Salim kuwa rais kesho sijui imetoka wapi.

Pili huyu Dada Asha kama anavyozungumza sielewi anachotaka kufahamu ikiwa Salim alipokuwa madarakani pengine yeye alikuwa badoi hajazaliwa ama ndoa akivaa nepi...

Asha Abdala,
Record ya Salim kama inavyojieleza ktk miaka hiyo sidhani kama dada Asha unaweza kutuambia data za hata Nyerere mwenyewe between late 60 hadi 80's maanake maswala ya uhuru wa nchi za kiafrica huko South bado hamzikubali kuwa ni mchango wake mkubwa kwa Africa. Sasa nambie Kikwete ana mchango gani ktk bara Afrika hadi kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya yetu..

Hivi kweli mtu kama J.J Mnyika ambaye kaanza siasa akiwa na umri mdogo mnaweza kutuambia mchango wake leo hii ktk Tanzania?... sidhani hata kidogo kwa sababu wadanganyika wengi hatufuatilii vitu zaidi ya kutazama nani kaleta mboga mezani.

Nina hakika huwezi kunambia mchango wa Mnyika ama kiongozi yeyote yule ktk taifa letu na Africa kiasi kwamba Wadanganyika wanaweza kubaliana na wewe mia kwa mia.

Samahani, lakini hiki ndicho nilichojifunza kuhusu Wadanganyika! hakuna mbora isipokuwa yule anayeubeba msalaba kwa ajili yetu..

Bahati mbaya ni kwamba hatuna Uhuru kamili hadi leo kwa hiyo bado tunamtafuta David ambaye ataweza kupambana na jitu hili la kutisha - CCM.
 
Hapana mkuu hiyo arrogant ni rangi alopakwa Salim na CCM ili watu wote wapate kuamini hivyo...na kama ulivyokwisha sema wewe mwenyewe kuwa viongozi wetu ni reflection yetu! wanafahamu Mdanganyika ni mwepesi kukubali uongo unaokubalika.

Mkuu Bob,

1. Heshima mbele, siasa ninaamini kuwa ni mchezo mchafu sana sasa kuiweza ni pamoja na kuhimili mapigo yake, ikiwa ni pamoja na kuweza kujibu mapigo, kwa sababu hata utakapokuwa rais, kutakuwa na mshambulizi sasa kwenye hili Salim, Malecela, na Warioba wana-fail big time, na ni very important skill kuwa nayo ili kuwa rais wa bongo! Hawa watatu hawakuwa nayo hiyo skill!

2. How did Salim get into our natinal politics? Only Mwalimu who was responsible, sio sisi wananchi wala jimbo lolote la ubunge, kwa hiyo from day one hakuwa mwenzetu alikuwa mtu wa Mwalimu, period, sasa baada ya Mwalimu kuondoka what did you expect na wakati dalili za nyakati za siasa zilikuwa very clear kuwa hakuna aliyependa mambo mengi ya Mwalimu na hasa viongozi wengi aliokuwa akiwaamini? Maana yake ulikuwa pia ni mwisho wa watu wake wa karibu, it was only a matter of time, na besides hata Mwalimu mwenyewe akiwa hai hakuweza kuwashawishi viongozi wenziwe wa CCM kuwa Salim na Mkapa, walikuwa wanafaa, in fact viongozi wengi wa CCM waliokuwa wakiwapinga Salim na Mkapa, walikuwa right on both, ingawa so far locally as a nation, politically tumeweza ku-prove on Mkapa, ndio maana hatukutaka tena kurudia experiment na Salim!

3. Salim amebebwa mno na Mwalimu, mpaka one has to wonder why? Aliyempeleka OAU ni Mwalimu, kwa kumtumia Mandela, baada ya kuona kuwa viongozi wengi wa CCM hawamtaki na walikuwa na sababu za msingi, ninasema Salim ni arrogant asingekuwa basi ange-humble himself na kujaribu ku-deal na his political past, lakini arrogantly, akaamua kumuamini Mwalimu tu kuwa siku zote atamsaidia, kwani sio siri kuwa Salim alihusika na siasa za Babu, na ni Babu personally na agenda zake ndiye aliyempeleka Salim na kina Mahafudhi kusomea u-Komandoo Cuba, ili warudi bongo one day na kuiondoa serikali ya mapinduzi visiwani and it happened, ingawa serikali kule haikuondolewa, sasa je Salim alihusika? sijui lakini ninajua kuwa kati ya aliokwenda nao Cuba kuna waliohusika including Babu mwenyewe, sasa haya sio majungu na CIA walikuwa wanayajua haya yote!

4. Katika miaka yake yote ya uongozi bongo sikumbuki anything serious kwa taifa kilichofanywa na Salim, na pia inashangaza kwamba Mwalimu, the man behind political career ya Salim, alishindwa kumuweka Salim kuwa waziri mkuu kwa a long period of time, ili kumtayarisha na urais kama alivyojaribu mwishoni, WHY?
Ninakumbuka one thing Salima kiwa waziri mkuu ni pale alipoenda mikoa ya kusini na kukuta wananchi wamevaa magunia akaamuru iletwe mitumba, othersiwe sijawahi kuona au kusikia anything serious kama alivyokuwa Sokoine, ambaye alifikia mahali katika kipindi kifupi cha uwaziri mkuu wake akaanza kushindana na sera Mwalimu openly, mpaka kuruhusu dala dala baada ya kujionea kwa macho yake jinsi wananchi walivyokuwa wakihangaika na usafiri wa Mwalimu wa UDA, Salim hakufanya anything kwa taifa kinachoweza kukumbukwa kwa taifa, lakini Sokoine did!

5. Salim hawezi kutuvusha taifa anywhere, kwa sababu kisasa anahitaji kujivusha yeye mwenyewe kwanza kwa kusimama ahesabiwe na taifa letu, ili tumchague. Kwenye uchaguzi wa Dodoma Salim hakuwa na kura za urais kabisa na wala sio siri! Hata hizo kura 500 alizopata mwishoni zilikuwa ni kura za Malecela, aliyeamua kumsaidia dakika za mwisho lakini ikawa too late, lakini sio zake yeye Salim, na hii ni hata kabla Mkapa hajaamua kumtwanga, still hakuwa nazo kura, na the fact kwamba alikuwa akipigiwa debe na Warioba na Butiku never helped his case, maana wajumbe wa NEC wanted nothing to do na hao another Mwalimu's big names lakini politically do nothing people, sasa what all this says about Salim? Ni kwamba he did not have it na ukweli ni simple kwamba hana huo uwezo wa kutuongoza wabongo, he might have a big CV, lakini skill za kuweza kutuongoza ambazo ni pamoja na ungangari wa kusimama ahesabiwe ndani ya CCM, hana.

Binafsi, sikubaliani na dhana yoyote ile inayosema kuwa aliyeshindwa huenda ni bora kuliko aliyeshinda, hapana a loser ni jut another loser, kama ana ubavu agombee next time tuuone, otherwise ake pemebeni na kuwasaidia walioshinda fo the benefit of our nation. Urais hupatikana kwa kushinda kura za uchaguzi, kuanzia za mizengwe huko ndani ya CCM, mpaka za taifa, hatuna njia yoyote nyingine ya kuku-redeeem as a nation. Kama Salim angekuwa na nia na uwezo wa mkuwa rais wetu, huu ulikuwa ni wakati wake muafaka ku-make his case, lakini kama kawaida yake atajificha huko nje and one day form nowhere atarudi na kudai antaka kuwa rais wetu, no way wa-Tanzania tunazo akili za kutosha on this kind of candidate.

Kikwete love or hate him, lakini bado ninamheshimu kuwa alishinda, njia alizotumia zinaweza kuwa debated lakini Salim hawezi kumlaumu kiongozi yoyote on that kwa sababu njia alizotumia Mkapa kumpitisha Kiwete, alifundishwa na Mwalimu, the man responsible kwa political career yake mwenyewe Salim, ninasema hivi Salim bado hajatupa wananchi sababu ya kumchagua, na Dr. Slaa hahitaji kushirikiana na Salim kuisaidia taifa letu, besides Salim amepitwa na wakati, hawezi tena mikiki ya hizi siasa za kusafisha mafisadi, ambazo Dr. Slaa anaziweza tena big time.

Kama ni ushujaa Salim sio shujaa wetu wa taifa, ila ni shujaa wa Mwalimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom