Hapa napenda kusumbua kidogo:Conclussion:Mzungu ni mtu mwenye asili ya bara la ulaya mwenye tabia ya kuzungukazunguka.kwa hiyo hata kama yupo US,TZ,RSA bado ataitwa mzungu kwani origin yake ni ulaya.
Kuhusu asili ya neno mimi nimesikia yafuatayo (lakini siwezi kuyathebitisha):
Wazungu wa Kwanza Afrika ya Mashariki walikuwa Wareno lakini hawakuitwa "wazungu".
Neno hili limetokana na hao wapelelezi wa Afrika na tabia yao ya kuzunguka kote bila kukaa mahali pamoja. Yaani watu hao kama Livingstone, Burton, Speke na wengine.
Labda pia wa sababu kutokana na kuzunguka kwao walionekana kama watu wenye hali ya kizunguzungu?