Who is John Tendwa?

Wakati anaandika thesis yake teknolojia ya kutunza kumbukumbu ki-elektroniki haikuwepo, na zaidi ya yote hata alipo apply kazi yake ya mwisho hiyo teknolojia ilikuwa haipo. Kwahiyo hamtampata kwa ki electronicali
 
Tatizo Tanzania wateule wa rais hawapitishwi na Bunge ndiyo maana wengine hata u-research hautagundua chochote kuhusu CV zao

Huhitaji uchambuzi wa Bunge kujua wasifu wa mteule. Unahitaji uchambuzi wa Bunge kubashiri uwezo wa mteule. Haya ni tofauti.

Tunachosema ni, kwa mujibu wa tundiko la kwanza, ni hatujui Tendwa ni nani. Sio anaweza nini. Hilo la anaweza nini ndio linaendana na uchambuzi na mapitisho ya Bunge.

Hili la Tendwa ni nani ni swala la Ofisi ya Habari ya Rais kutupa wasifu wa mteule siku anapoteuliwa. Mwandishi yeyote wa habari anaethamini jina lake hawezi kutuandikia Bwana Tendwa kateuliwa kuwa Msajili bila kuiuliza Ikulu na kutuambia huyu Bwana Tendwa amewahi kutenda nini? Tatizo ni uandishi, sio kutokuwepo na mapitisho ya Bunge.
 
inamaana hata alipochaguliwa nafasi magazeti hawakutuandikia huyu jamaa ni nani?

Labda tutafute baba yake au shangazi yake vinginevyo hakuna habari yake yoyote inayojulikana. Inaonekana hata Elimu yake haijulikani. hata magazeti yameanza kumuandika baada ya 2005.

Yes, hata mimi nataka nimfahamu huyu bwana. Kuna mtu aliniambia wakati alipodai kuwa hana muda wa kuhakiki wanachama wa CCJ kuwa J. Tendwa ni kigeugeu sana atageuza kauli yake! Muda si muda tukamsikia anahakiki wanachama hao. CCJ baada ya kubaini rafu dhidi ya wanachama wake walimwambia Tendwa asitishe zoezi akagoma! Leteni data za J. Tendwa jamani!

Hivi kwanini habari za huyu John Billy Tendwa hazipatikaniki? Inakuwaje mtu mkubwa, muhimu kama yeye tunakosa historia na wasifu wake?

Yaani hata shule na vyuo alivyosoma hakuna?

Ni Jaji John Billy Tendwa... ni wakili vile vile.. mwanzoni alijaribu kuwa impartial lakini baada ya kufokewa kama mtoto mdogo na Mapuri kufuatia angalizo lake kwa CCM alinywea na kujikuta amerudishwa kwenye mstari. Kuanzia wakati huo kile CCM inataka CCM inapata..naam na ziada.

Labda aje na yeye aanzishe yenye kumhusu Mkurugenzi mkuu wa tume ya uchaguzi,bni muhimu tuanze sasa kabla hayajatukuta huko mbeleni.
Sasa nadhani wengi mmeona kuwa Tendwa ni kitendawili kigumu... Well, kuna mdau anaandaa wasifu wake na atatuletea punde.

Naambiwa alikuwa Wizara ya Katiba na Sheria kabla ya nafasi aliyo nayo...
 
probably he too, is just a "joke" ---- he likes utani-utani!!!
 
Well,

Tumeongea naye na yaliyo kwenye blue ink kwenye post ya kwanza ndiyo aliyoongea kwa kifupi
 
Pia alishafanya kazi mahakama ya kazi and gues what? ameacha kimada pale.

NI vizuri tumjue huyu mtu, Pamoja na kuwa mtu ambaye sikupenda hii sisijei (sikutaka tuendelee kugawanyika kipindi hiki) yeye hakupaswa kutofanya wajibu wake na amekuwa mkandamizaji sana. Yes inatakiwa tumjue mienendo yake na tabia zake ili tuweze kujua akili yake huwa inawaza vipi.

Kumjua Tendwa anawaza/anawazishwa vipi inabidi tuunganishe dots kwa aliyekuwa msajili Kabla yake George Liundi https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-taja-mamluki-tuliowapandikiza-upinzani.html.

Huyu mtu alikuwa msajili lakini alipomaliza tu muda wake akaomba ubunge kupitia CCM, japo alipigwa chini na baadae kutaka kuvujisha siri ya kile alichotakiwa kukifanya pale ofisi ya msajili. Ni mawazo kama haya pekee ndiyo yanaweza kukufanya CCM wakuchague uwe representative wao pale kwenye ile ofisi.

Ni mpaka hapo tutakapokuwa na sheria iliyo wazi jinsi ya kuwafanya hawa ma-refree type (Msajili, Tume ya uchaguzi) kuwa na kinga toka kwa aliyewachagua kuwaondoa ndipo tutakuwa na vyombo huru vya kukuza demokrasia
 
Kipindi fulani alikuwa State Attorney kule Tabora.

Ila nasikia katika tukio moja kubwa wakati akiwa katika nafasi hiyo ni pale ambapo alichukua mke wa mtuhumiwa ambaye kesi yake alikuwa anaisimamia upande wa Jamhuri na hatimaye kufikia kumweka kinyumba na baya zaidi siku mojawapo ya usikilizaji wa shauri ilo eti Tendwa aliingia mahakamani akiwa na suti ya mtuhumiwa na kupelekea mtuhumiwa kuanzisha fujo mahakamani kwa kumwambia; mke wangu umenichukulia na suti yangu pia umeivaa tena kuja kwenye shauri la kuja kunifunga?

Mwenye stori kamili juu ya hii skendo amwage hapa jamvini... mi nimeipata mtaani

Mkuu, hii ni kali kuliko! ..... ya kweli laki haya??!!
 
Jamani eeeeh! Hivi kwa nini hatujiulizi pengine mtu huyu ni foreigner? Mi nadhani ni Mkenya maana jina hilo Tendwa pia lipo miongoni mwa Wakikuyu. Ni expatriate huyu kaletwa kuisaidia sisiemu!
 
John tendwa aliwahi kuishi lindi na kisha mtwara kidogo na personally namkumbuka alivyokuwa mnywaji sana wa pombe hadi kupoteza fahamu na kuipa familia yake machungu makubwa, ila baadae kidogo mzee Mkapa akamuhamishia Dar na kumteua kuwa msajili wa vyama.

Basically yeye na mzee Mkapa wamefahamiana akiwa Mtwara.
 
Nilimfahamu Tedwa zamani kidogo by that time alikuwa mwanasheria pale Mwanza.

Kikubwa alikuwa na nyodo saana yeye pamoja na mke wake ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Mbugani.

Miaka ile ya Mwinyi suti zake zilikuwa zinafuliwa Nairobi. Kiufupi ni mfanyakazi wa UWT kwa fani ndo mwanasheria
 
Ana Mtoto wake Southampton anapigabox, ngoja nitamuuliza kama anajua CV ya babake
 
Just a suggestion waheshimiwa...mnaonaje JF ingekuwa na forum special ya CV za viongozi wetu?
 
Just a suggestion waheshimiwa...mnaonaje JF ingekuwa na forum special ya CV za viongozi wetu?

Mtoto wazo lako zuri sana. Hapa wewe si mtoto tena. Nadhani muhimu kulifanyia kazi na katika muda si mrefu katika kile kinachotarajiwa kuonekana suala la CV litazingatiwa kwa mapana yake
 
Back
Top Bottom