Who is IGP Mwema? CV Please!

Ni kikwazo kikubwa kwa vijana na wasomi askari kujiendeleza ndani ya Jeshi . Ameleta sera ya kuajiri vijana waliomaliza std 7 pamoja na form 4 waliofeli,kwani kwa mtazamo wake wasomi wanakimbia Jeshi,anatakiwa Mwema afanye utafiti wa Kina sababu ni zipi? zinafanya vijana wasomi..waache kazi .je ni maslahi madogo? hawathaminiwi ?.
 
kwa mtazamo wangu he is doing fine, ingawa ana maadui wengi (ACPs na CPs) ndani ya jeshi ambao hawakubaliani kabisa na polisi jamii
 
The little i know about Mwema ni kwamba ana shahada ya kwanza ya sheria (LLB) kutoa UDSM.,alipata kuwa RPC-Mbeya, then akaenda INTERPOL-Nairobi, mpaka anachukua U-IGP.,but if we compare him with the other guy from Morogoro at least he has some added value in his tenure of service
Hivi na huyo unamuweka kati ya watu? mimi kwangu alikuwa kama d*g wa polisi tu. Huwezi kufikiri mtu mzima na cheo chake kama angelikuwa anafanya mambo ya kijinga vile. Kazi kubwa ilikuwa kushirikiana na majambazi tu.
Mnakumbuka alivyotuonyesha visu kuwa vilikuwa imported by CUF alafu angekosa wapi kukubambikia kesi mtu wa vile?
 
- Ni mwanaume
- ni Mtanzania
- Ni Inspekta Generali wa Jeshi la Polisi -Tanzania chini ya wizara ya mambo ya ndani
- Amesoma LLB Chuo kikuu cha Dar es Salaam
- Ameoa na ana watoto
- Katika utendaji wake wa kazi yupo commited
 
Huyu jamaa siyo siri kajitahidi kinoma wakati wa kampeni, lakini aliboronga alipokuli kuwapa demotion wakuu wa mikoa ambako CDM imeshinda kwa kishindo na wale walioshinikiza wasimamizi kutangaza matokeo halali kama ARusha, mwanza etc.

Kwa hiyo hana jipya ni wale wale tu
 
Anatokea mkoa wa Kilimanjaro Moshi maeneo ya PASUA kuna vibaka wengi sana mtaani kwake!
 
Huyu naye sijui kakurupuka kutoka pango gani. Hakuna sehemu hiyo post uliyonukuu imetaja mahusiano ya kazi na kupendelewa. Acha hijabu nyumbani wakati mwingine ili uone vema

Monsignor hebu soma vizur between the lines halafu uelewe ndiyo utowe comments zako. Kuna post za nyuma hapo wameainisha kwamba ana uhusiano na huyo mkuu wa kaya na labda ndiyo akapewa post hii. Ndiyo mimi nikauliza hivo. Ila wewe umekurupuka na hizo hijabu zako unazozionea wivu.

Kamnunulie mdogo wako basi avae mbona masista wa kikatoliki wanavaa na wanapendeza?
 
......... Ameleta sera ya kuajiri vijana waliomaliza std 7 pamoja na form 4 waliofeli, kwani kwa mtazamo wake wasomi wanakimbia Jeshi, anatakiwa Mwema afanye utafiti wa Kina sababu ni zipi? zinafanya vijana wasomi..waache kazi .je ni maslahi madogo? hawathaminiwi ?.

Mbona sera ya serikali inasema kuajiriwa kiwango cha chini ni Form IV yeye hao darasa la saba amewatolea wapi? Jituoriginal huwachi yakhe!

Jee Afisa Utumishi huwa anafanya nini hapo Wizarani mpaka yeye atoe maelekezo yanayopingana na maamuzi ya Serikali?

Na Form IV gani aliyepasi atakwenda polisi, si atakwenda Form V ili akajiendeleze zaidi?
 
INTERPOL media release
02 March 2006 INTERPOL regional bureau head assumes top post at Tanzanian police
LYON, France – The head of the INTERPOL Sub-Regional Bureau in Nairobi, Saidi A. Mwema, has been appointed to lead the Tanzania Police Force. ..............
............. As head of the INTERPOL Sub-Regional Bureau (SRB) in Nairobi, Mr Mwema provided support and direction for all INTERPOL activities in the region and oversaw the implementation of initiatives to address specific crimes in eastern Africa, including During his tenure, Mr Mwema oversaw the relocation of SRB Nairobi to an improved site, facilitated the signing of various regional agreements and enhanced co-operation with international bodies.


Mbona comments hamna alipopata mafanikio??????
 
- Ana shahada ya kwanza ya sheria LLB-UDSM
-Amewahikufanya kazi BOT enzi za Exchange Control akiwa kitengo cha upelelezi
-Amewahi kuwa CID wa Mkoa
-Amewahi kuwa RPC wa mkoa
-Amewahi kufanya kazi Interpol-Nairobi
-Ameo wake wzaidi ya moja
-Ana watoto
-ni mpole
-Ni msikivu
Ni mwema kama lilivyo jina lake
 
huyu jamaa ni mchapakazi sana maana sasa ana mchakato wa kukiboresha kitengo cha Forensic science katika jeshi la polisi.
Tanzania nasi tutajidai kwa kupitia uongozi wake.

Sawa, lakini tungepata full CV ingeuwa imekaa vema sana.
 
huyu jamaa ni mchapakazi sana maana sasa ana mchakato wa kukiboresha kitengo cha Forensic science katika jeshi la polisi.
Tanzania nasi tutajidai kwa kupitia uongozi wake.




Mbona umeweka picha ya bibi Nyoni na kumfagilia sana kaka yangu
 
Kama sio msukumo wa kisiasa, ni mchapakazi mzuri, mwelewe, intelligent n.k... otherwise, yeye kama binadamu pia anaweza fanya makosa. naamini pia kuwa, yaliyotokea Arusha hakuyapenda na nahisi atakua anaumia kimya kimya
 
Back
Top Bottom