Geor Davie ni nani?

utemi

Senior Member
Mar 27, 2011
167
23
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?

Nasikia ni “Nabii”

Je, huduma yake ipo wapi?

=============

Huyu ndugu jina lake halisi ni George David Kasambale. Ni mwenyeji wa Singida. Mimi nilianza kumfahamu miaka ya tisini, alikuwa tarishi pale world vision, Arusha. Alikuwa pia mwanamziki wa nyimbo za injili ktk mikutano mbalimbali na alikuwa anasali ktk kanisa la Siloam Gospel Assembly lililokuwa linasali ktk shule ya msingi Uhuru Arusha.

Kwa kipindi hicho, mimi nlikuwa mwanafunzi wa primary. Tulikuwa tunamuita Nyakizanya kwa sababu ya wimbo wake maarufu ''Nyakizanya umeokoka'', ila alikuwa kijana wa kipindi kile na alikuwa ana mambo yake ya ujana kama kuvaa mabegi na kunyoa pushback, kitu kilichomfanya asikubalike na wachungaji wengi wa kiroho hapa Arusha.

Sikumsikia tena hadi miaka ya kuanzia 1996 hivi. Alikuwa na studio ya nyimbo za injili iliyoitwa Supreme na baadae ikawa radio station ila ilikuwa inasikika baadhi ya sehemu za Arusha. Ila kutokana na ujanja ujanja wake na ambitions yake aliweza kukutana na wazungu na kufungua kituo cha watoto wa mitaani ingawa alikuwa anao kama watano hivi wa kuzugia.

Kituo hichi kilikuwa majengo karibia na Sacon, Opposite na kanisa la KKKT Burka, baadaye alihamia Kisongo baada ya kuwa na fedha, aliwaondoa wale watoto kwa namna mbaya sana mmojawapo ni rafiki yangu ni fundi TV, ndio ghafla tukasikia Nabii GeoRDavie, kanisa lake liko Kisongo Mnadani na ofisi zake ziko huko ktk mashamba yake maarufu kama ''mji wa Daudi''. Kwa kweli huduma yake imejaa contrevesial sana, maisha yake pia yana utata.

Means jinsi anavyo-behave, pamoja na family life yake kwa ujumla watu wanaomfahamu tangu kitambo hawamuelewi. Ila hatuwezi kusema sana tusije tukakufuru ila kwa upande wangu mmhh.

Simkubali na hii ni kutokana na matendo yake, yaani tabia, huwezi kuwa na upako kiasi hicho afu matendo ni design kama yake. Ila sijui!

Siwezi sema ni mtume wa Mungu au la ila kuna maswali mengi sana kuliko majibu.

============
Mhe. Nabii GeorDavie ni mtumishi wa Mungu. Anaijua kazi yake, anajiamini, ni shujaa, anajitambua na anaielewa kazi yake. Anamwakilisha Mungu ipasavyo. Anamwelewa boss wake vizuri na hana mashaka naye. Hajali maneno wala haogopi vita kwa kuwa anamwelewa Mungu aliyemwita na kumtuma. Kama tujuavyo shetani ni mpinzani wetu hivyo kurusha makombora ni kitu cha kawaida.

Maelfu ya watu yameshuhudia matendo makuu ya Mungu. Mara nyingi shuhuda zimekuwa zikiwekwa kwenye Radio ya Ngurumo FM Hata hao wakina Channel na watumishi wote waliokengeuka kwa sababu zao wanazojizua walishuhudia, tena walikuwa hawamjui Mungu lakini wamefungua makanisa. Ikiwa wanakufuru matukufu ya Mungu na kusema ni Nguvu za giza, je wao wanatumia nini na wamejifunzia pale?

Tena channel alishuhudia na kusema upako huu ni mtaji kwangu! Wivu ni wa nini watu wa Mungu? Mara ooh kuna mwanamke alifunga macho na alipofungua akaona nyoka mara akafa, inaingia akilini??? Tunaomba kumjua huyo mwanamke ayekufa na ushahidi.... Ni uongo wa Ibilisi jamani, nendeni mkajionee matukufu ya Mungu... Shetani anaharibu kazi ya Mungu lakini ameshindwa.... Kazi ya Mungu inasonga mbele!

Mnashangaa misafara na magari ya kifahari, Mungu ni tajiri atumie hata ndege za angani kumtukuza Mungu! Eti anaitwa mheshimiwa, sasa kama mafisadi wanaitwa waheshimiwa vipi watumishi wa Mungu?!!

Mimi ninasema GeorDavie amemwelewa Yesu na ndiye mtumishi anayemwakalisha Mungu ipasavyo. Hivi mimi kama ninatembea peku na ninakuambia Mungu ni tajiri anaweza kukusaidia kiuchumi utanielewa kweli?!! Unajua mtu ajionavyo ndivyo alivyo.

Ukimwona Mungu unayemwamini hawezi kuponya, kwako kitu kama hicho kitabaki kuwa story, ukiona Mungu unayemwamini anatawala mbinguni na kumiliki duniani na mamlaka alishatupatia ndivyo itakavyokuwa kwako. Wengi hapa wamebaki kumuhukumu na kumkatisha tamaa kwa kazi anayoifanya, na kupakaza mambo ambayo hayana maana. Ila kwa muelewa inaonyesha wazi ni maadui, wivu, chuki kwani sielewi kwanini kinawauma sana.

Kama kweli mnampenda Mungu na mnamjua Mungu, kwanini msimwombee? Mnampiga vita yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Wengi walisema anatumia nguvu za giza, wakafunga na kukemea na kuharibu ikaishia GeorDavie kuinuliwa nao wakashushwa! Mwacheni Mungu aitwe Mungu! Mungu akimpenda mtu na kumchagua afanye kazi yake atamtumia mpaka atakapomaliza haijalishi chochote!

Yeye ndiye atakayemhukumu na wala sio mwanadamu! Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote kwani anaangalia utayari wa mtu alionao. Kweli GeorDavie ni shujaa katika mashujaa otherwise angekuwa mtu wa kawaida katika vita zote alizopitia angekimbia na kumwaibisha Mungu. Lakini yeye anasonga mbele akicharaza mapepo. Mungu anawapa watu karama tofauti.

Na maandiko yako wazi, alisema wengine ni Manabii, mitume, wachungaji, waalimu na wainjilist kama yeye amepewa upako wa Kinabii wivu ni wa nini wanadamu??? Hamna jema.

Mtumishi asipotembea na Nguvu za Mungu mnasema hajaitwa, akiwa na nguvu za Mungu mnasema anatumia nguvu za giza, lipi jema kwenu!? Acheni kumnyoshea mtumishi wa Mungu kidole, angekuwa hajatumwa tangu mmeanza kumpiga vita ametikisika??!! Huduma imekufa???

Kitu cha Kimungu hata upambane vipi huwezi kukiharibu! Hamtamweza Nabii huyu mpaka Mungu akamilishe kusudi lake aliloweka ndani yake. Haijalishi punda amechafuka au amelowana lazima safari aimalize na kusudi la Mungu litimie! Lakini ole wake yule ambaye hakumsaidia punda kukamilisha kusudi la Mungu kwa wanadamu! Je, umehusika kufanya nini?? kumchafua, kumwangusha, ulimlisha, ulimtemea mate, ulimpaka marashi?? Ulishiriki vipi kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele??

Mungu kumtumia mwanadamu hamaanishi ni malaika! Shida watu hawasomi maandiko na kuelewa neno la Mungu. Nchi yetu hii inanishangaza, kazi kupinga watumishi wa Mungu na kuwaombea mabaya huku wakiwainua watumia mizizi waliojaa udanganyiifu!


Nabii akiwaambia huko siko wanakimbilia hawamtaki Yesu! sasa wanaanza kulalamika ooh tulidanganywa... Tafuteni uso wa Mungu wanadamu na kumwabudu yeye pekee dunia hiini ubatili mtupu.
 
Bongo inaongoza kwa "manabii" pori, na huyo ni mmoja wao!

=================
ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie' wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako' lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa' iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.

Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.

Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.

Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.

Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK'.

"Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona," alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.

"Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?" alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.

Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.

"Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud," alisema Fred Mushi.

Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.


Bravo Hongera ASKOFU na Nabii George David
 
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Nabii
je huduma yake ipo wapi ?

jamaa msanii kinoma. Nilihudhuria mkutano wake mmoja pale Biafra miaka minne iliyopita, jamaa akaanza kusema eti kila mtu aandike jina la mtu anayehisi amemruga kisha yeye Geordavie atafanya dua itakayomfanya huyo mrozi wako apooze na kuteseka hadi mauti yamchukue.
 
Huyu ndugu jina lake halisi ni George David Kasambale ni mwenyeji wa Singida mi nlianza kumfahamu miaka ya tisini alikuwa tarishi pale world vision, Arusha alikuwa pia mwanamziki wa nyimbo za injili ktk mikutano mbalimbali na alikuwa anasali ktk kanisa la Siloam Gospel Assembly lililokuwa linasali ktk shule ya msingi Uhuru Arusha.

Kwa kipindi hicho mi nlikuwa mwanafunzi wa primary tulikuwa tunamuita Nyakizanya kwa sababu ya wimbo wake maarufu ''Nyakizanya umeokoka'' ila alikuwa kijana wa kipindi kile na alikuwa ana mambo yake ya ujana ka kuvaa mabagi na kunyoa pushback kitu kilichomfanya asikubalike na wachungaji wengi wa kiroho hapa Arusha.

Si kumsikia tena hadi miaka ya kuanzia tisini na sita hivi alikuwa na studio ya nyimbo za injili iliyoitwa supreme na baadae ikawa radio station ila ilikuwa inasikika baadhi ya sehemu za Arusha. Ila kutokana na ujanja ujanja wake na ambitions yake aliweza kukutana na wazungu na kufungua kituo cha watoto wa mitaani ingawa alikuwa anao ka watano hivi wa kuzugia.

Kituo hichi kilikuwa majengo karibia na Sacon Opposite na kanisa la KKKT Burka, baadaye alihamia Kisongo baada ya kuwa na fedha, aliwaondoa wale watoto kwa namna mbaya sana mmojawapo ni rafiki yangu ni fundi TV, ndio ghafla tukasikia Nabii GeoRDavie, kanisa lake liko kisongo mnadani na ofisi zake ziko huko ktk mashamba yake maarufu ka ''mji wa Daudi'' kwa kweli huduma yake imejaa contrervasial saana maisha yake pia yana utata.

Means jinsi anavyiobehave pamoja na family life yake kwa ujumla watu wanaomfahamu tangu kitambo hawamuelewi. Ila hatuwezi kusema sana tusije tukakufuru ila kwa upande wangu mmhh.

Simkubali na hii ni kutokana na matunda yake yaani tabia huwezi kuwa na upako kiasi hicho afu matendo ni design ka yake ila sijui? Siwezi sema ni mtume wa Mungu au la ila kuna maswali mengi sana kuliko majibu.
 
huyu ndugu jina lake halisi ni George David Kasambale ni mwenyeji wa Singida mi nlianza kumfahamu miaka ya tisini alikuwa tarishi pale world vision, Arusha alikuwa pia mwanamziki wa nyimbo za injili ktk mikutano mbalimbali na alikuwa anasali ktk kanisa la siloam gospel assembly lililokuwa linasali ktk shule ya msingi uhuru, Arusha kwa kipindi hicho mi nlikuwa mwanafunzi wa primary tulikuwa tunamuita Nyakizanya kwa sababu ya wimbo wake maarufu ''Nyakizanya umeokoka'' ila alikuwa kijana wa kipindi kile na alikuwa ana mambo yake ya ujana ka kuvaa mabagi na kunyoa pushback kitu kilichomfanya asikubalike na wachungaji wengi wa kiroho hapa Arusha, sikumsikia tena hadi miaka ya kuanzia tisini na sita hivi alikuwa na studio ya nyimbo za injili iliyoitwa supreme na baadae ikawa radio station ila ilikuwa inasikika baadhi ya sehemu za Arusha. Ila kutokana na ujanja ujanja wake na ambitions yake aliweza kukutana na wazungu na kufungua kituo cha watoto wa mitaani ingawa alikuwa anao ka watano hivi wa kuzugia, kituo hichi kilikuwa majengo karibia na sacon opposite na kanisa la kkkt Burka, baadaye alihamia Kisongo baada ya kuwa na fedha ,aliwaondoa wale watoto kwa namna mbaya sana mmojawapo ni rafiki yangu ni fundi TV, ndio ghafla tukasikia Nabii GeoRDavie, kanisa lake liko kisongo mnadani na ofisi zake ziko huko ktk mashamba yake maarufu ka ''mji wa Daudi'' kwa kweli huduma yake imejaa contrervasial saana maisha yake pia yana utata means jinsi anavyiobehave pamoja na family life yake kwa ujumla watu wanaomfahamu tangu kitambo hawamuelewi. Ila hatuwezi kusema sana tusije tukakufuru ila kwa upande wangu mmhh! Simkubali na hii ni kutokana na matunda yake yaani tabia huwezi kuwa na upako kiasi hicho afu matendo ni design ka yake ila sijui? Siwezi sema ni mtume wa Mungu au la ila kuna maswali mengi sana kuliko majibu

Mkuu hebu eleza zaid kuhusu huduma yake ya sasa ni ki2 gan kina kupa walakini, weng wanao jiita manabii mi huwa siwaelew maana hawahubir wokov bal uponyaj na mafanikio. kakobe namkubali asilimia 100 coz anafundisha kwel ya neno la MUNGU
 
Ni nani anayemjua vyema huyu ndugu?
Nasikia ni Nabii
je huduma yake ipo wapi ?


Hivi we hujui kwamba VITABU VYOTE viliandika kuhusu ujio wa MANABII WA UONGO? Huyu naye alishaandikwa. Anafuata mpango! Hana jipya! Usiende kupoteza pesa zako bure. Kwani Mungu ana haja gani na pesa zetu ilhali yeye ANAMILIKI KILA KITU DUNIANI? Hivi nyie HAMUELEWI?
 
Mkuu hebu eleza zaid kuhusu huduma yake ya sasa ni ki2 gan kina kupa walakini, weng wanao jiita manabii mi huwa siwaelew maana hawahubir wokov bal uponyaj na mafanikio. kakobe namkubali asilimia 100 coz anafundisha kwel ya neno la MUNGU
Kwanza kipindi cha kufundisha neno ni kidogo sana ktk ibada ni ka dk 15 tu, muda mwingi ni miujiza na blah blah, halafu ana injili ya vitisho ka vile usipotoa sadaka biashara yako itafilisika na vitu ka hivyo, na ktk mahubiri yake hujisifu sana na kutumia kauli ka Roho mtakatifu ni mbabe n.k kama unalijua neno ukisikiliza mahubiri yake utaguna mpaka ung'ate ulimi. Mbali na hayo ana kashfa nyingi sana za uzinzi na hadi kuna ndoa amezivunja na ushahidi uko, pia jinsi anavyowatreat wasaidizi ni vituko
 
Mkuu uliyosema ni ukweli kabisa, mi nipo Arusha Majengo so jamaa namjua sana, alikataa jina la Kasambale coz wazungu walikuwa wanapata shida kulitamka, sasa hivi hana nguvu sana na kusanyiko lake kwa sasa ni ukiwa mtupu.... hana watu..!!! waliokuwa wana msaidia huduma wametawanyika na kufungu huduma sehemu mbalimba kisa ni jamaa kula wake za watu... kuna jamaa mmoja hapa sakina ni dereva wa tours (jina ninamwifadhi) amechukuliwa mke na huyu Geor Devil... mke wa jamaa alikuwa msaidizi wake.......

Sawa sawa si mke wa yule kijana mtoto wa yule mzee wa kiarusha anayekaa kibanda maziwa sakina. Pia hata watoto wake ambao huwatumia kwenye huduma mh! Hawana ushuhuda kabisa kuna yule mkubwa Niki a.k.a Nisher kulikuwa na post yake ktk jamii photos ka usher wa bongo. Hivi kuhusu wasaidizi wake waliohama na watu na kwenda kufungua huduma zao vp? Kuna mmoja anaitwa Channel yuko kisongo mbele ya Ngurumo kidogo mwezi wa 12 nilikuwa kansani kwake ktk mahubiri yake alidai kuna majambazi na wachawi toka Ngurumo ya Upako walitaka kumuua duh! Dini bana siku hizi ka siasa. Tumwachie Mungu tu, ila tutawatambua kwa matunda yao
 
Nilishawahi kuona bango lake hapo Arusha la Kutangaza mkutano wake wa injili akijiita MTUKUFU MHESHIMIWA NABII GEORDAVIE!!!!!
 
Mkuu hebu eleza zaid kuhusu huduma yake ya sasa ni ki2 gan kina kupa walakini, weng wanao jiita manabii mi huwa siwaelew maana hawahubir wokov bal uponyaj na mafanikio. kakobe namkubali asilimia 100 coz anafundisha kwel ya neno la MUNGU

Mkuu, Bukudu ameeleza vema na amekuwa makini ili uongeze na zako....kifupi jamaa ni msanii kwa sana tu na yuko kifedha zaidi ukienda kanisani kwake usiopo angalia utajikuta umetoa sadaka pesa yote uliyoenda nayo.

Mfano kila msitari ukikugusa unatakiwa ukatoe sadaka kwa kumbia kwenda mbele na kutoa pesa na kushika nguzo, utata mwingine nilio uona masharti yake kama unaenda kanisani kwake hutakiwi kula chochote na mkifika nikuimba mpaka atakapo kuja.

Mfano umefika saa mbili halafu yeye akaja saa saba na tangu saa mbili ulikuwa unaimba tu na kusimama/kukaa akija ndiyo hivyo tena itambidi uongezee na kukimbia kimbia huku vilio kwa kwenda mbele halafu jaama anaanza kukuombea anakushika kichwa na kukusukuma utaacha kuanguka.

Kuna siku mimi nilienda lakini nikapiga chai yangu vizuri nikasubili nianguke tuliimba mpaka saa tisa ndiyo tukatoka kanisani nikajiuliza sana kuwa hata huku kuanguka kwa watu mara nyingine siyo mapepo ni njaa tu na uchovu.

Kingine ulinzi wake sija wahi kuona mtumishi mwingine anae lindwa kama huyu jamaa ana mabaunsa kama zaidi ya 15 wanao valia suti nyeusi au nyeupe na miwani mieusi sijui ni kwasababu alimlamba mke wa Mbunge wa Arusha wa zamani(Mh. Felex Mrema) hivyo ana wasiwasi na maisha yake.
 
Mbali na hayo ana kashfa nyingi sana za uzinzi na hadi kuna ndoa amezivunja na ushahidi uko, pia jinsi anavyowatreat wasaidizi ni vituko[/QUOTE]

Mkuu ebu elezea kidogo kuhusu hili....
 
Huyo ni mmoja wa wale manabii waliotabiriwa kuwa watatokea nyakati za mwisho.....
 
Kwa nyie mliowai kwenda kwenye izo ibada zake aliwai kuwasomea sadaka alizopata?!! Mimi ni Mkatoliki na kila kanisa ninaloenda Jumapili lazima waseme Jumapili iliyopita sadaka ilikuwa shilingi ngapi.

Nimeshughudia mara nyingi mapato na matumizi yakisomwa kila mwisho wa mwaka. Waumini wa kawaida wanaongoza halmashauri ya kanisa husika ndo hufanya kazi hii sio mapadre wala watawa wengine.

Kama hili halitokei kwenye kanisa lako au ilo la geordavie (ngurumo ya upako) ni kwanini mliowai kwenda huko mnakubali kuibiwa? Ni kwamba hamna akili au mna mileha ya KIFISADI?

Hapa ndo naona umuhimu wa haya makanisa yanayochipuka kila uchao yawe yanafanyiwa "Auditing" otherwise ni uizi na utapeli mtupu.

Geodarvie alikuwa maarufu sana, nakumbuka dada mmoja mwaka 2006 nilipomaliza tu Chuo na kufika Arusha alinishawishi sana niende ila nikagoma kwenda.

Baadae niliyoyasikia yanayofanyika huko nilishukuru MUNGU kwa kukataa ule mwaliko. Ukikosa maarifa unaangamia sababu hata kwenye Dini siku hizi majizi na matapeli yamejaaa. Lazima tuwe makini sana jamani
 
252508_213815088649455_100000628976775_663505_1350309_n.jpg 149137_140171606032710_132279533488584_188196_2575409_n.jpg

Mke wa GeorDavie ni yupi katika hawa?
 
Kwa nyie mliowai kwenda kwenye izo ibada zake aliwai kuwasomea sadaka alizopata?!! Mimi ni Mkatoliki na kila kanisa ninaloenda Jumapili lazima waseme Jumapili iliyopita sadaka ilikuwa shilingi ngapi.

Nimeshughudia mara nyingi mapato na matumizi yakisomwa kila mwisho wa mwaka. Waumini wa kawaida wanaongoza halmashauri ya kanisa husika ndo hufanya kazi hii sio mapadre wala watawa wengine.

Kama hili halitokei kwenye kanisa lako au ilo la geordavie (ngurumo ya upako) ni kwanini mliowai kwenda huko mnakubali kuibiwa? Ni kwamba hamna akili au mna mileha ya KIFISADI?

Hapa ndo naona umuhimu wa haya makanisa yanayochipuka kila uchao yawe yanafanyiwa "Auditing" otherwise ni uizi na utapeli mtupu.

Geodarvie alikuwa maarufu sana, nakumbuka dada mmoja mwaka 2006 nilipomaliza tu Chuo na kufika Arusha alinishawishi sana niende ila nikagoma kwenda.

Baadae niliyoyasikia yanayofanyika huko nilishukuru MUNGU kwa kukataa ule mwaliko. Ukikosa maarifa unaangamia sababu hata kwenye Dini siku hizi majizi na matapeli yamejaaa. Lazima tuwe makini sana jamani
Wazee wa kanisa na wasaidizi wake huchagua yeye mwenyewe, kwani hujui kuwa ni nabii anaona wenye mioyo safi wenye nia ya kumtumikia Mungu? Na amekuwa na kawaida ya kufukuza na kubadilisha wasaidizi na wazee wa kanisa wake mara kwa mara, ndo maana hata akagombana na kina Channel ambao wamefungua makanisa na kuhama na watu wake kibao. Kwa sasa watoto wake ndo wasaidizi wake wakubwa na ndo wanahusika sana
 
hivi nimeanza kukudoubt wewe utemi are you not one of them unapima ka watu wanamchukulia vipi mheshimiwa, mstahiki, mtukufu nabii GeorDavie, nahisi ur among his teammembers kwa sababu jina unalotumia lina relation na ngurumo ya upako kumbukua gazeti lake linaitwa UTEMI WA UPAKO linatoka kila jpili na wewe unaitwa utemi duh! What a coincidence bwahaa haaaa haaaaa nahisi nakujua wewe si flani ..........
 
Back
Top Bottom