White Elephants of Africa

Aliyeulizwa kaelewa swali linaelekea wapi, ndio maana kakaa kimya.

Naona amenijibu. Kwa mawazo yangu na kwa kifupi tu uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa kisiasa tofauti na nchi zingine za kiAfrika.

TANU ilikuwa na manifesto ya vitu gani vitafanyika ikishinda uchaguzi. Nadhani moja ya ahadi hiyo ni kujenga njia ya reli kwenda Mbeya (itabidi nipate document ku-support).

Kwenye kupiginia uhuru viongozi wa TANU walikuwa ni activists at best. Wakati uhuru umepatikana ilibidi waanze kutimiza ahadi zao. Na kutimiza ahadi hizo, kilichohitajika ni pesa za matumizi. Hivyo ikabidi katika kipindi cha muda mfupi, viongozi wa TANU ikabidi waache kuwa activists na kuwa executives.

Serikali ya huru haikuwa na pesa ya kutimiza ahadi zake na nchi za magharibi zilikuwa zinaleta ugumu kwenye kutoa misaada. Walitoa ahadi lakini walikuwa wagumu kusaidia.

Katika kipindi katika nchi za kicommunist kulitokea mgawanyiko. Urusi ikawa kiongozi wa nchi za Ulaya mashariki. China wakawa kiongozi wa nchi zinazopata uhuru.

Hivyo China ikajiingiza kusaidia ujenzi wa Tazara hili kuinua profile yake ya kuwa kiongozi wa nchi zinazopata uhuru.

Anyway kuna mambo mengi ya kuongezea lakini hapa sio sehemu yake.
 
Bibie,
Zakumi na mimi tumetoka mbali. Anamaanisha nchi za magharibi zilimkatalia yeye na Kaunda kuwa hiyo project haikuwa feasible.
Wachina wakakubali kuijenga.

Hiyo ni point kubwa. Point zingine. Nyerere hakuwa leftist radical wakati tunapata uhuru. Alikuwa na contact na Labour party ya uingereza. Mpaka Tanzania inapata uhuru Nyerere alikuwa hana uhusiano wowote na China.

Watu waliokuwa na contact na Wachina walikuwa ni Abdulrahman Mohamed Babu na Oscar Kambona. Na walikuwa na contact hizi wakiwa masomoni Uingereza. Na Makachero waliwafuatilia.

Kuna uwezekano kuwa Kambona hakumaliza shule kwa sababu walimuona ni mtu hatari na leftist radical.

Na baada ya muungano Abdulrahman Mohamed Babu na Oscar Kambona walishikilia nafasi muhimu. Babu alikuwa viwanda na Biashara na Kambona waziri wa mambo ya nchi nje. Hawa ndio walioandaa mikataba na ziara zote za mwanzo za Mwalimu kwenda.

Kufikia mwishoni mwa 60 Nyerere akawa ameondoka kwenye siasa za moderate left kwenda kwenye radical left with moderation.
 
Wivu wa kijinga...

Wakati TAZARA inajengwa miaka ya sabini (70) kwa gharama ya dola 500 milioni. jamaa wa west walizua maneno yao ya Ki-kameruni kameruni kama haya, wengine walisema eti wachina watatujengea reli ya mabua na haitatudumu zaidi ya miaka 5, leo hii ni miaka karibia 40 bado inachapa kazi....:A S-coffee:

Tukiwauliza hao wazungu (western countries) katika miaka yote kuanzia ukoloni hadi sasa wamefanya kitu gani cha maana kwa bara la Africa zaidi ya kutuibia rasilimali zetu, kutuuzia silaha pamoja na kutuletea vita na migogoro ya wenyewe ya wenyewe?:lol:
 
Back
Top Bottom