While Zitto is being attacked pls read here

Unajua cha kuchekesha ni kwamba pamoja na chuki ya wazi ambayo u/mnayo kwa Zitto, hamna sababu ya msingi ya kutetea chuki yako/yenu.
Utasikia mara, huyo si mwenzetu tena!, Zitto huyu si yule wa kipindi kile, Msaliti, Anajisikia, na sababu nyingine ambazo ukizichunguza kwa makini utagundua msingi wake ni chuki, majungu, ubaguzi.
Mkumbo heshima sana, ila baada ya muda utawasikia 'mazuzu' flani wakikuita msaliti kwa sababu umemsapoti ZZK 2015.[/QUOTE]

So its all about 2015?
 
Unajua cha kuchekesha ni kwamba pamoja na chuki ya wazi ambayo u/mnayo kwa Zitto, hamna sababu ya msingi ya kutetea chuki yako/yenu.
Utasikia mara, huyo si mwenzetu tena!, Zitto huyu si yule wa kipindi kile, Msaliti, Anajisikia, na sababu nyingine ambazo ukizichunguza kwa makini utagundua msingi wake ni chuki, majungu, ubaguzi.
Mkumbo heshima sana, ila baada ya muda utawasikia 'mazuzu' flani wakikuita msaliti kwa sababu umemsapoti ZZK 2015.[/QUOTE]

So its all about 2015?
kusoma sana siyo kukomboka kiakili.taifa letu limefika hapa sababu ya ma profesional perperte kama kitila na zitto.hawa majamaa wawili kila mwanacdm makini anajua ni mandumila kuwili.ni vigumu sana mimi kufikiri sawa na hawa jamaa.wasilazimishe tukubaliane na ujinga.hivi nani asiyejua kuwa zk aliunga mkono ununuzi wa mitambo ya kifisadi ya dowans?nani asiyejua zk alipinga chadema kutoka bungeni kuonyesha kwao kutoridhika na mfumo wa uchaguzi tanzania?nani asiyejua kuwa zk amejitenga na viongozi wenzake wa chama?nani asiyejua kuwa zk huwa hashiriki matukio ya kitaifa ya cdm kama zinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 jangwani,m4c,je ukaribu wa zk na r.aziz na jack zoka je?siasa si uadui lakini kuunga mkono unafiki wa zitto yakupasa uwe na akili ya maiti.hawa wote wametumwa kazi maalum chadema.tulishawastukia.

mimi nimezipenda baadhi ya hizi hoja. Lakini simuelewi Mkumbo anaposema fikra tofauti sio tatizo. Fikra tofauti ndizo hujenga itikadi tofauti. nimuulize swali moja, ni kwa nn yeye yupo CDM? maana kama fikra tofauti sio hoja basi angekuwa hana chama. angeheshimu zote tu za CCM kulinda na kukumbatia mafisadi na za CDM kuwachukia mafisadi. Watanzania wengi wanaielewa CDM na inachopigania. Ukitoka nje ya msitari tu unaonekana vividly! ndicho kinachomkumba Zitto. Zitto alibahatika sana kuwin confidence za waTZ lakini akatemper nazo, watu wenye akili zao wakabaki midomo wazi. Leo hii hata alete hoja nzuri kiasi gani watu walishamdoubt. Kitila anajua sana kuwa unapomuamini sana mtu na baadaye ukagundua he was not worth it, it becomes almost impossible kurudisha trust kwa kiwango kilekile. WATU HAWAMHATE ZITO ILA WANAMDOUBT HATA ANAPOKUJA NA JAMBO LINALOONEKANA KUWA NI JEMA. reason ya kumdoubt ni history yake na tabia yake ambayo yeye na Mkumbo wanaiita misimamo. Tunasupport fikra na misimamo tofauti lakini ni fikra zile tu na misimamo ile tu sahihi machoni pa wengi waliokubaliana kufuata itikadi fulani.
 
Uwazi gani unaousema wewe wakati waandishi waliambiwa kua hawana uwezo wa kufikiri. Uwazi anaousema Zito sio huo.

Mkuu Morinyo haujaelewa hoja hapo. ZeMarcopolo anazungumzia Sera ya Ukweli na Uwazi katika utendaji wa Serikali iliyokuwa inanadiwa na Serikali ya awamu ya tatu chini ya BWM.Katika sera hii wengi walitegemea hili analolipigania Zitto la Uwazi katika mikatana ya sekta ya Nishati na Madini lingejitokeza lakini wapi
 
Chintu, usichanganye mambo. Msimamo na fikira ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama chama tunapaswa kuwa na msimamo mmoja katika mambo ya msingi, lakini hatupaswi kufanana kifikra. Narudia tena, ni ujinga wa kutisha kutaka Watu wafanane kifikra kwa sababu ni kujaribu kywafanya wasiwe binadamu!
 
Politics has great impact in our daily lives whether negative or positive. Therefore we need to be careful in what Politicians are telling us. This will reduce the negative impacts.
 
WIMBO WA KUTENGANISHA 'WAZO' NA 'MTOA WAZO' NI MTAMU SANA LAKINI SI KWA MASIKIO YOTE WAKATI WOTE NA KWA MAZINGIRA YOTE KWA USAWA ULE ULE

Siku zote MAWAZO MAPYA(new ideas) huumbwa na mtu na ukweli huu hata rafiki yangu Dr Mkumbo analifahamu vema.

Sasa kwa kuzingatia mantiki kwamba hata siku moja mawazo mapya kamwe hayana uwezo wala miguu ya kujisimamia yenyewe isipokua ni mpaka awepo mtu mahala mwenye moyo, muda na msukumo wa kulisimamia hilo wazo jipya ndipo lenyewe liweze kufanyiwa kazi na matunda kuweza kuoneka, basi hadi hapo misingi hoyo yote kati ya UJUMU kwa upande mmoja na MUUMBA UJUMBE kwa upande mwingine ni sharti kutazamwa kwa pamoja pindi mtu unapokua serious kufanyia tathmini wazo husika.

Hivyo basi, Great Thinkers kidogo napata shida wengine mnapojaribu hapa kutusukuma tumini ya kwamba njia pekee na sahihi kwa nyuzi joto za vipimo vyenu ni kule kufanyia tathmini wazo tu (Idea Appraisal) bila kutekeleza nayo tathmini ya muumba ujumbe (Idea Orijinator Appraisal).

Sote tunakubaliana kwamba, kwa mfano tu, kunapozungumziwa mtu kuibuka na wazo la tuseme kitu 'MPANGO MZURI WA MATUMIZI YA RASILMALI ARDHI' - hadi hapo ujumbe tunao juu ya mambo gani yatakiwa kupewa kipaumbele katika watu husika kuweza kutumia rasilmali hiyo kwa faida zaidi kwao. Nasema hadi hapo huo ndio ujumbe unaotakiwa kujdiliwa.

Pamoja na yote, itakua ni ajabu ya kihistoria kwa watu wanaojiita Great Thinkers kuhiari tu kuacha kumjadili pia mtoa wazo ili tupate kujua MAZINGIRA ALIMO NA JINSI GANI MAZINGIRA HUSIKA itakua imechangia kushawishi na kuumba mtazamo wake mzima hadi kuzaliwa kwa wazo hapo juu ya matumizi bora ya rasilmali ardhi. Ili kupata kuendana na hoja yangu hapa ni muhmu kutambua ya kwamba wazo la 'MATUMIZI BORA YA RASILMALI ARDHI' itakua ni ile ile ila ufanisi wa utekelezaji wake unatuamuru kwamba kwanza lazima tujiridhishe na mtoa wazo pamoja na mazingira anamotoka ili sasa tunapotengeneza mkakati kuwepo na uumano kati ya na mazingira ambako wazo husika lahitajika kutekelezwa kwa mafanikio.

Naam, ninachomaanisha hapa ni kwamba wazo hapo juu japo ni maridhawa kweli kweli ila utekelezaji wake katika mazingira halisi ni mpaka upate kwanza jibu kwamba mtoa wazo hilo la 'MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI' ni nani hasa yeye na anatokea wapi ambapo kuna historia gani vile: Ukweli ni kwamba wazo la 'mpango wa matumizi bora ya ardhi' itakua na mantiki tofauti kabisa kwa sisi wa Mbagala ukitulinganisha na wale wenzetu wa ADA Estate Dar es Salaam, nasema japo wazo au ujumbe ni ule ule hapo juu ila utekelezaji wake ni mpaka ujue kwanda undani wa mtoa ujumbe kama anatokea penye ardhi yenye rutuba Sumbawanga au Tukuyu au mtu huyo anatokea Same au Tundra kabisa.

Sasa kurudi kwenu wenzangu Wakuu TIQO, Pasco, Geza Ulole na a high calibre Educationist, Dr Kitila Mkumbo, ni kwa misingi ya arguements zangu hapo juu ndio maana wengu humu kamwe hatuwezi hata siku moja kuhiari kusamehe kutazama picha ya ndugu yetu 'Zitto and The Transitions from a dependable social justice fighter hadi kuwa mtu asiyeaminika kwa jamii, ndipo kutazama kwetu wazo lake na pengine jinsi gani historia hiyo nyuma yake ilivyochangia kushawishi mtazamo wako katika kuumba ujumbe husika.

Hadi hapo wakuu naomba sana huu wimbo mtamu wa kumtenganisha wazo na mtoa wazo ueleweke kuwa si jambo ambalo ni sahihi na yenye kipimo sawa kwa mazingira yote hivyo hatuna budi kufikiria kabla hatujajikuta tu kwere chorus bila hata kujiuliza kwamba hicho tunachokiimbi ndicho hasa kina mantiki gani hiyo.

Nakaribisha wenye mawazo tofauti na ya kwangu waweke hoja zao mezani kwa nini Zitto asihukumiwe na tabia yake ya kutokua a consistent, champion-for-public-good, team-player and a transparent leader himself.

Inasikitisha sana kuona jinsi watu wanavyoacha kujadili hoja na kumjadili mtu! Hizi chuki zitatufikisha wapi Watanzania.

Mchangiaji aliyesema tuna ugonjwa wa kumchukia mtu anayefikiria tofauti has said it all. Watu wako tayari kumpa mtu anayefikiria tofauti na walivyozoea majina mabaya,bila kujali maslahi anayotetea kwa wakati husika.

Zitto alieleza waziwazi kutokubaliana na approach ya Prof. Muhongo kuhusu review anayofanya. Anachosisitiza ni uwazi katika mikataba hii ili Watanzania wengi waweze kuiona na kutoa michango yao,na hatimaye tuweze kuwa mikataba yenye kuwanufaisha Watanzania.

Anaenda mbali zaidi kuwa review kufanyika na bodi yenye watu walewale,waliofanya review zilezile ambazo zilifanywa huko nyuma na kutupa mikataba ileile mibovu inayotuumiza,hii approach haina tija kwa sasa!

Kwa
nini hamtaki kuamini kuwa kuna watanzania wengine wenye uwezo na elimu kupitia mikataba hii,mnatulazimisha kuwaamini watu wachache ambao walishatuingiza kwenye mikataba mibovu.!

Lakini viwavi wa chama badala ya kujadili hili,waangaika kumtazama mleta hoja,sijui hajashiriki M4C,mara hayupo ofisini..do you think hayo ndio muhimu kuliko Tanzania yetu?

Mnahoji nuwepo wake kwenye tume ile ya Bomani iliyofanya review,mlitaka Zitto abadilishe dunia ili msimamo wa serikali ubadilike! Na hili ameshalitolea ufafanuzi kuwa recomendations zote zilizotolewa na tume ya Bomani hakuna nhata moja iliyofanyiwa kazi,bado mnang'ang'ana review..review..give the guy a break!

Huu unafiki na siasa majitaka ndio unaoturudisha nyuma kila siku watanzania. Mawazo haya haya anayotoa Zitto yangetolewa na "rafiki yenu" mngesoma vizuri kila nukta na kukubali anachosema,lakini limeletwa na "adui",hata hoja na maoni yake sio muhimu,aibu gani hii.

Huyu ni mtu potential sana kwenye sekta ya madini,mafuta na gesi,badala ya kumpa moyo na kupongeza kazi anayofanya,mnakuja na itikadi zenu chafu zisizotufaa kwa wakati huu. By the time mnamaliza siasa majitaka,mikataba imeshasainiwa,na rasilimali zinaondoka.

Tuko tayari kukosa kuliko kuwa upande wa mtu anayetetea maslahi ya watanzaniua kwa kuwa hatumpendi. Unfortunately wale mnaowapenda hawana weledi,utaalam wala elimu katika sekta hii zaidi ya siasa pendwa za kujitafutia umaarufu majukwaani.

Zitto ni msomi aliyebobea katika "Uchumi wa madini mafuta na gesi". Na ndio facts anazotoa zinapimika,hakuna siasa hapa kwa sisi tunaoelewa.

Mwenye hoja au maoni mbadala juu ya haya anayopigania Zitto na atoe badala ya kuja na itikadi za kichama,hoja za kumjadili mleta hoja badala ya kujadili hoja.!
 
Zito ni sellout nashangaa watu bado wanamuweka katika maono ya kumwona anapigania maslahi ya Watanzania.
 
Chintu, usichanganye mambo. Msimamo na fikira ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama chama tunapaswa kuwa na msimamo mmoja katika mambo ya msingi, lakini hatupaswi kufanana kifikra. Narudia tena, ni ujinga wa kutisha kutaka Watu wafanane kifikra kwa sababu ni kujaribu kywafanya wasiwe binadamu!

Mkuu Msimamo huja baada ya fikra na msingi wa msimamo ni fikra, Huwezi kuwa na msimamo usiotokana na kushiba kwa fikra unazoziamini, Hivyo sikubaliani na usemi kuwa msimamo na fikra ni vitu viwili tofauti tena unasema KABISA. Naamini Msimamo wa kichama unatokana na kukubaliana katika fikra fulani za msingi. unapochepuka nje ya msimamo wa pamoja maana yake umeamua kuasi fikra fulani zilizowaweka katka msimamo wa kichama. Naomba nieleweke kuwa hilo sio shida, ila shida ni pale ambapo hutoi hoja zenye mashiko na kueleweka. Hivi kulikuwa na hoja gani katika kushauri tununue mitambo ya kitapeli ya DOWANS? najua mtu anaweza kusema mbona tumeshimdwa kesi na tunatakiwa kulipa? Hiyo haiwezi kuwa hoja kwa kuwa yeyote mwenye akili anajua uhuni uliochezwa katika hiyo kesi.
 
Chintu, hakika humo kichwani mwako kuna kitu cha thamani, hakika swala la ndg yetu zitto linawatatiza wanachama walio wengi, sintofahamu zimegubika akili zao hao wanachama, labda nikuulize kaswali kadogo, kwa kuwa ndg yetu zitto haijadhibitika kuwa yy ni divient, afanye nini ili arudishe imani kwa watz wapenda mabadiliko? na nini salama yake ndani ya chama?
 
Judi acha" ukabila" na "ukaskazini"......huwa nasoma thread zako nyingi ila kwa hili unazidi kutuchefua roho sisi tusio wa huko.
 
Wooow woooow wooow Wanaomchafua Zitto mwisho wasiku watakimbia tuu'waendelee kumkomaza kisiasa'#TeamZitto
 
Chintu, hakika humo kichwani mwako kuna kitu cha thamani, hakika swala la ndg yetu zitto linawatatiza wanachama walio wengi, sintofahamu zimegubika akili zao hao wanachama, labda nikuulize kaswali kadogo, kwa kuwa ndg yetu zitto haijadhibitika kuwa yy ni divient, afanye nini ili arudishe imani kwa watz wapenda mabadiliko? na nini salama yake ndani ya chama?

Sisi tuna imani na zitto!labda wewe ndio huna imani nae sababu either ni mkaskazini , umefanywa msukule bila ya wewe kujijua,au na wewe ni miongoni mwa wasioijua kweli ya nini kinaendelea cdm!
Kama upo kwenye hilo kundi la tatu basi nakushauri utafute kuijua kweli maana kweli ina tabia yakumuweka mtu huru.
Lakini kama upo kwenye kundi la kwanza na la pili basi pole yako.
Kiama chako chaja.
 
Chintu, usichanganye mambo. Msimamo na fikira ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama chama tunapaswa kuwa na msimamo mmoja katika mambo ya msingi, lakini hatupaswi kufanana kifikra. Narudia tena, ni ujinga wa kutisha kutaka Watu wafanane kifikra kwa sababu ni kujaribu kywafanya wasiwe binadamu!

Dr mkumbo nimekuwa nikifatilia mijadala yako mbalimbali,una maono ya mbali sielewi kwanini hujawa katibu mkuu wa cdm.
your very objective and you have a good mission and vision for the party and national as well.
Kubishana na hao wavaa vinyago ni kupoteza mda wako.
Jimbo la kinondoni linakufaa sana japo nasikia unaenda singida ilamba!
Jimbo linahitaji mtu makini kama wewe .
Karibu kinondoni.
 
Chintu, usichanganye mambo. Msimamo na fikira ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama chama tunapaswa kuwa na msimamo mmoja katika mambo ya msingi, lakini hatupaswi kufanana kifikra. Narudia tena, ni ujinga wa kutisha kutaka Watu wafanane kifikra kwa sababu ni kujaribu kywafanya wasiwe binadamu!

True 100%
 
Unajua cha kuchekesha ni kwamba pamoja na chuki ya wazi ambayo u/mnayo kwa Zitto, hamna sababu ya msingi ya kutetea chuki yako/yenu.
Utasikia mara, huyo si mwenzetu tena!, Zitto huyu si yule wa kipindi kile, Msaliti, Anajisikia, na sababu nyingine ambazo ukizichunguza kwa makini utagundua msingi wake ni chuki, majungu, ubaguzi.
Mkumbo heshima sana, ila baada ya muda utawasikia 'mazuzu' flani wakikuita msaliti kwa sababu umemsapoti ZZK 2015.[/QUOTE]

So its all about

Nashauri waziri wa elimu wa zitto 2015 awe dr kitila mkumbo,anafaa sana .
Nimekuja kujua ndio sababu kila siku anapanda vyeo pale udsm mala mwenyekiti wa udasa,mala head of education department,saizi tena nasikia kawa dean wa duce college! Jamaa ana akili nyingi sana huyu.

Nimeamini kweli huwezi kuwa na marafiki werevu ilihali wewe ni mjinga. Mjinga anamfata mjinga mwenzake.

My take! Acha wafu wawazike wafu wenzao!
Kitila karibu kinondoni jimbo lipo.wazi,limekosa mtu makini.japo wana ilamba wanakuhitaji pia!
 
Chintu, hakika humo kichwani mwako kuna kitu cha thamani, hakika swala la ndg yetu zitto linawatatiza wanachama walio wengi, sintofahamu zimegubika akili zao hao wanachama, labda nikuulize kaswali kadogo, kwa kuwa ndg yetu zitto haijadhibitika kuwa yy ni divient, afanye nini ili arudishe imani kwa watz wapenda mabadiliko? na nini salama yake ndani ya chama?
Ni rahisi sana.
1) Atolee maelezo controversies zote zilizotuchanganya juu yake. Tuzijadili kiuwazi ili tuone kama tunamdoubt bila sababu au tuna sababu za msingi kumdoubt.

2) Kulikuwa na taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa na Mwanahalisi juu ya mahusiano tata na watu ambao hutuhumiwa sana na CDM. Ile makala haijawahipata majibu yanayoeleweka kutoka kwa Zitto zaidi ya kulalamika kuingiliwa privacy zake ambayo haitusaidii kutupa ufafanuzi wowote. Aseme basi kama uhusiano ule ulikuwa ni wa kirafiki tu au wa kikazi. Halafu tujadili mantiki ya uhusiano wao. KITAELEWEKA TU.

3) Mwisho akishindwa kujibu hoja atoke openly na kuomba radhi kwa jinsi alivyotuumiza na kuua matarajio yetu makubwa kwake.

4) Zitto ajue kuwa hoja nzuri anazozileta sasa hazitamsafisha kamwe, watu wataendelea kudoubt tu because of the SHADOW OF THE PAST. He has to clear that shadow first then aendelee na hoja zake nzuri. TUTAMUAMINI.
 
Mkuu Morinyo haujaelewa hoja hapo. ZeMarcopolo anazungumzia Sera ya Ukweli na Uwazi katika utendaji wa Serikali iliyokuwa inanadiwa na Serikali ya awamu ya tatu chini ya BWM.Katika sera hii wengi walitegemea hili analolipigania Zitto la Uwazi katika mikatana ya sekta ya Nishati na Madini lingejitokeza lakini wapi

Mkuu nadhani utakubaliana na mimi kua hiyo sera ya ukweli na uwazi ilikua katika maneno tu na si katika matendo. Sisi tunataka sera ya ukweli na uwazi katika matendo na si katika maneno.
 
vipi hii habari?Kwa mwenendo wake ni kwamba sasa ndio anafanya haya rasmi.


[h=1]Siri za Zitto nje[/h]
picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 09 December 2009

Mawasiliano yake yanaswaAponzwa na mwandishi wa habari


zitto_2.jpg



SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.
Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge "hata kabla ya akina John Mnyika…"
Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.
Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.
Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.
Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya "ushujaa" wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku "akichukiwa" na viongozi wake wakuu.
Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, "Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni."
Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, "CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu."
"Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana," imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.
Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:
"Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…"
Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.
"Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma," anaeleza.
Anasema, "Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha."
Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, "Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…"
Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, "Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana." Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: "Muhimu na haraka."
Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.
Naye anaandika kwa Msacky, "tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo."
Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika "zitto" na kwingine anaandika "Zi."
Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, "take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha."
Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya "CHADEMA kwa mawasiliano ya siri" na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. "…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali," alieleza.
Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema "Sina la kusema."
Alipong'ang'anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, "Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA."
Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, "Sina la kusema."
Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, "Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.
"Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote," alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.
MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe "Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe."
Msacky aliulizwa, "Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?" Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.
Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni "Mtanzania mwema."
Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.
"Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu," alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, "labda umuulize Zitto."
Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, "Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, "tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA."
Alisema, "Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake."
Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.
Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. "Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa," ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, "Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa."
Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.
 
hakuna kipya kwa zitto,zaidi ya yaliyoandikwa na mwanahalisi.Kijana yupo naive,katongozwa katongozeka,akili imewehuka kabisa.

Kafikia mahali pabaya sana.Sasa mnyika ni Mbunge na kipindi kifupi kamfunika mbaya, mbowe ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, dr. Slaa kasimama katika simplicity na ukweli auaminio.Wana CDM wamempa go ahead aitoe CCM kwanza ndipo watu wafikirie gombea urais na si kuharibu kasi ya kuwang`oa CCM just because dogo kaona kuwa kuna uwezekano wa kuchukua nchi ndio anataka kuanza gombania anachokiona kuwa maslahi.
 
Moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti. Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu. Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima. Zitto ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.

Dr KITILA nakuheshimu sana lakini sikubaliana na hoja yako sababu tunaomlalamikia ZITO tumekuwa tukitoa hoja nyingi mimi nadhani kufikira kitofauti si kitu kibaya na utagundua watu hawana tatizo nalo tatizo ni yeye kuishi kunafiki na kushindwa kushiriki operation za kichama ambazo huhitaji kuwa na Phd kama ili kujua kuwa zinakisaidia chama na zina tija kubwa nadhani pia unashindwa kutambua kuwa sisi wananchi tunahitaji mabadiliko kwa kasi ya ajabu na sio siri CCM wameshindwa kuongoza hii nchi hivyo mtu akiwa anatutumia sisi vijana kama sehemu ya malengo yake ya kupata madaraka hakika HUKUMU yake ipo njia halafu unafikiri kitofauti inatakiwa ufikiri kulingana na mahitaji ya watu waliokuzunguka sasa kama ZITO anafikiri kitofauti halafu anaishia kupata lawama nadhani inatakiwa ajiangalie mara mbili tatizo litakuwa kwako na nyie mnaompa kichwa ndo mnampoteza kabisa...AUNGANE NA WENZIE KUJENGA CHAMA PERIOD.
 
Back
Top Bottom