ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Hivi kwanini jamii inachukulia kama kubadili msimamo ni weakness? Mtu anaweza kubadili msimamo baada ya kupata taarifa zaidi juu ya swala husika, na hilo ni jambo jema na lenye manufaa.
Cha msingi ni mtu aliyebadili msimamo kutoa sababu ya kubadili msimamo na hivyo basi mijadala ielekezwe kwenye uzito au wepesi wa hiyo sababu.
Kuhusu Zitto - anachohubiri Zitto sasa hivi kuwa kinachohitajika zaidi ni transparency sio kitu kipya Tanzania. Labda tukumbushane tu kuwa katika awamu ya tatu serikali ilikuwa na kauli mbiu ya UWAZI NA UKWELI. Zitto alichobadilisha ni lugha tu lakini anazungumzia uwazi na ukweli uleule aliouhubiri Rais Mkapa. Sasa kila mtu apime mwenyewe kama uwazi na ukweli wa awamu ya tatu ulifanikiwa kudhibiti ubadhilifu wa mali ya umma. Kama jibu ni ndio basi Zitto anapigania kitu sahihi, kama jibu ni hapana basi Zitto anaelekea siko (kwa makusudi au kwa kutojua: I dont know!).