While Zitto is being attacked pls read here

Kitila Mkumbo

Mkuu wangu nakubaliana na wewe sana tu isipokuwa Mh.Zitto anatakiwa kuishambulia sana Policies za CCM badala ya mtu kutangulia issue au event husika. Kumbuka kwamba mila na tamaduni za watanzania unapomshambulia mtu, watu huanza kujiuliza pengine kuna chuki baina yenu maana maisha ya Mtanzania yametangiwa na mapenzi/chuki ktk mahusiano ya watu.

Kama simpendi Zitto basi hata afanye nini nitampa pongezi na kama napenda JK basi hata akifanya jambo baya kiasi gani sinta comment. Ni hulka ya Watanzania kupima mawazo ya mtu ktk kipimo cha ajabu kabisa na muhimu sana kwa mwenye kutoa mawazo yake kujiepusha na lawama hizi. Ukimsoma hata Zitto kwa makini utagundua anazungumzia zaidi sera mbovu za CCM, mapungufu makubwa ya utekelezaji yanatokana na mfumo mbovu lakini hata siku moja hawezi kunyoosha kidole mfumo wenyewe kama hili la kutokuwa na gasi na mafuta policy..

Ni jana tu sisi wengine tumekuja gundua hili kutoka kwa Zitto baada ya kuulizwa na Mzee Mwanakijiji. Hapa ndipo ilitakiwa kushindilia maswali mengi sana ambayo hata kauli ya Muhongo ingebakia uchi mtupu. Kumbuka tu sisi tunajaribu sana kupokea mawazo yenu lakini tunaposhindwa kuwaelewa ni vizuri mjitambue ama mjiulize kwa nini wananchi hawakutuelewa badala ya kufikiria sisi ndio wenye matatizo. Binafsi yangu nampenda sana Zitto kwa juhudi zake na mara nyingi hutazama kwa nini Zitto hakueleweka na hivyo kutoa ushauri asimame vipi..
 
Last edited by a moderator:
Kwa hili Zitto Z. Kabwe nakupa big up. Tuko pamoja katika mapambano ya kuhakikisha kuwa nchi yetu na rasilimali zetu ni zetu na ni lazima tufaidike nazo.
 
Kitila Mkumbo,

Umesema kweli mkuu. Zitto anaonekana msaliti ilaanaweza kufikiri. Ila nadhani pia anapaswa kuwashawishi chadema wakubaliane nae
 
Last edited by a moderator:
lazima tukubali ukweli.Dr kitila,

Zitto hanania ya dhati kwa yale yote anayosema na kusimamia.one day you will prove this.

majina anajipachika mwenyewe,wala hakuna anayejipachika.toka lini mtu akitafutiwa jina,majina unajitafutia mwenyewe,anaweza akawa na mawazo mazuri sana,lakini kwangu mimi namfananisha na Bendera inayopepea pale upepo ulipo.

naungana na mchangiaji mmoja kuwa ameona anapotea kwa kasi,sasa anatafuta pakutokea.
He can be what you think Dr kama ataacha utoto na kustick on issues na sikutafuta kwa nguvu matakwa yake.

neno la Mungu linatuambia anayejikweza hushushwa na ashukae mungu humkweza,
 
Kitila Mkumbo, Mkandara,

..kitu kingine nadhani wananchi na haswa wachangiaji wa JF tunapaswa kujifunza kukubali makosa, na kubadili misimamo yetu baada ya kugundua makosa hayo.

..nimeshangaa kwanini wananchi wana msimamo uleule kuhusu Prof.Muhongo hata baada ya kubainika kwamba yeye mwenyewe amebadili msimamo wake pale alipodai kwamba ataheshimu mikataba iliyopo, kwa maana nyingine hakuna kitakachobadilika.

..baada ya taarifa hizo, i expected hata wale waliokuwa wakim-support Prof ktk sakata kubadili misimamo yao, na kuelekeza support yao kwa Zitto Kabwe.

This is a continuous flow of new information into JF. Inashangaza wachangiaji wanapokuwa stagnant ktk misimamo yao.

..binafsi I have very strong reservation on Zitto Kabwe kutokana na msimamo wake kuhusu EAC na ushiriki wa Tanzania, na zaidi ukaribu wake na vigogo wa CCM. Lakini pamoja na hayo, I think huyu kijana amejisumbua ku-research kuhusu sekta ya nishati na madini, nina amini ideas ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa nchi yetu.
 
Mkuu Kitila Mkumbo, thanks for this!.

Humu jf baadhi yetu wametengeneza haki miliki ya they way they think, you have to think like them and have drawn a line of where one has to belong, you are either "with us" or "against us", if you don't sail the same boat then you are an enemy!.

Mimi binafsi nilishajipambanua kumkubali ZZK ila kwa vile mgombea wangu ni EL, then nimeitwa kila majina and in actual fact sijali sana kwa sababu nasimama na kile ninacho amini!.

Ila pia pamoja na tofauti zote za mawazo, ZZK should not keep at distance with the rest, he has not only be together but also seen to be together vinginevyo "maneno huumba", uwongo ukisemwa sana repeatdly kamwe haugeuki kuwa ukweli bali huonekana kama ndio ukweli wenyewe!.

Pamoja sana.

Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Dr. Mkumbo umenena vema, tatizo kwa mtazamo mwingine ni pale watanzania tunapopenda kuweka nguvu nyingi kwa mtoa hoja badala ya kuweka nguvu nyingi kwenye hoja yenyewe.

Mazoea haya yanawaponza watu wanatoa hoja kwani wanaishia kushambuliwa wao badala ya Hoja zao. Nikirudi kwa Mh. Zitto lazima tusema hivi. Zito anaposema hawa watu wa gas wamecheza mchezo ni mchafu ni kweli au si kweli? Anaposema kuna zaidi ya bil 300 Uswizi ni kweli si kweli? Then tushughulike hizo hoja zake.

Zitto awe anasema hayo wakati washutumiwa ni rafiki zake hilo halituhusu na linajipinga automatically? Kama kweli wangekuwa watu wake si wangemnyamazisha? Nani anayependa kugombana na rafiki zake.

Zitto kijana wa MBADALA keep it up.
 
Kitila Mkumbo

Nyie kama chama kwanza mumsaidie na kukanusha hayo anayosingiziwa.Ama unajifanya hujui kuwa watu wamekosa imani naye kutokana na mienendo yake?

Watu wanalalamika kuwa kwanini haonekani kwenye mikutano ya M4C wala ofisini, ninyi kama chama mmeshapinga na kusema Zitto ana majukumu mengine na kwamba huwa yupo ofisini? Haya makundi makundi ndani ya chama yatawamaliza, mark my words.

Kaeni pamoja kama viongozi wenye nia moja kwa chama chenu,wewe unabaki kusema eti ni chuki, acha hizo mkuu. Unajuwa kabisa imani za wananchi wengi dhidi yake zimeyumba,sasa na wewe unakubaliana na wale wenye kusema wanayoyaona hayo ni kwasababu ya dini yake ama kuwa si mchagga?

Unafiki kitu mbaya sana.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kitila Mkumbo, thanks for this!.

Humu jf baadhi yetu wametengeneza haki miliki ya they way they think, you have to think like them and have drawn a line of where one has to belong, you are either "with us" or "against us", if you don't sail the same boat then you are an enemy!.

Mimi binafsi nilishajipambanua kumkubali ZZK ila kwa vile mgombea wangu ni EL, then nimeitwa kila majina and in actual fact sijali sana kwa sababu nasimama na kile ninacho amini!.

Ila pia pamoja na tofauti zote za mawazo, ZZK should not keep at distance with the rest, he has not only be together but also seen to be together vinginevyo "maneno huumba", uwongo ukisemwa sana repeatdly kamwe haugeuki kuwa ukweli bali huonekana kama ndio ukweli wenyewe!.

Pamoja sana.

Pasco.
Kimsingi hamna m2 mwenye chuki na ZZK ndan ya CDM bali hisia mbaya juu yake zinakuja kw sababu kwa hili la mafuta na gesi na mengine mengi hayasimamii nyuma ya CHADEMA bali kama ZZK nahaneshi nia ya dhati katika kuuondoa mfumo mbovu ulio2fikisha hapa ambao ni wa CCM kazi ya mwanachama au kiongozi wa chama chochote cha upinzan ambacho malengo yake ni kukamata dola ni kuzipinga wazi wazi sera mbovu zilizoshindwa za chama kilichopo madarakani hapa ni lazima ujiulize ni ZZK VS MUHONGO AU NI CHADEMA VS CCM BADO KUNA MASWALI MENGI JUU YA ZZK NDAN YA CHADEMA
 
There is nothing wrong for someone to have his own views different from other people but one has to be consistent in his views on similar issues!! Tukumbuke kuwa zitto was in the forefront kutaka mikataba ya madini iwe reviewed and he was rewarded by Kikwete when he was included in the Bomani committee which recommended the changes in those mining contracts; now when Prof. Muhongo advocates the review of the gas and oil exprolation contracts the same Zitto comes out crying that it was not in the best interests of our country to review those gas and oil contracts!!! Zitto's stance on this issue smacks of hypocrisy and incosistency in his arguements!!
Hapa kuna harufu ya "vita vya ubinafsi wa wanasiasa",ni umimi umimi tu,hilo ndo tatizo kubwa,ubinafsi.Lakini bado hawaoni.Kwakuwa mimi nilifanya kile,basi mwingine asikifanye,bila kujali outcomes kama zina manufaa kwa taifa.Kwani ikiwa reviwed utakachokosa ni nini?Si na wewe uliwahi kufanya review?Ama anaogopa kuna ambavyo vitaoneka kuwa alishiriki?Mambo mengine bana,siasa tu.
 
Kitila Mkumbo my friend

Ulichoeleza hapa ni moja tu ya tatizo, na umeangalia uande mmoja tu.

Kuna tofauti kubwa kati ya kufikiri tofauti (ambacho hata mimi namuunga mkono zitto na pia ni mhanga wa mawazo mbadala sehemu nyingi nilipopita maishani) na kutokueleweka

he may have all teh good deed, but in any society, kueleweka ni muhimu na watu huenda shule kujifunza communications skills, networking skills nk. he needs to do that ili asizidi kujiweka mbali na wengi, hasa wanaompenda

I met him once in DC wakati huo nilikua DC na nikahudhuria mkutano wa chadema, he was outstanding, lakini bahati mbaya sana more than 50% ya waliokua pale hawakua na imani na kauli zake, walijua ni opportunists tu... that was really bad. na nilipojaribu kusema hayo ya mawazo mbadala nilionekana naive.... HE NEEDS TO STRAIGHTEN UP A LITTLE WITH HIS CLOSET

NO MATTER HOW GOOD YOU ARE, IF YOU ARE NOT TRUSTED, YOU ARE AS GOOD AS AN ENEMY.... NILIMPA UJUMBE KUHUSU PROFESSIONALS ALIKUPA??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kitila Mkumbo, thanks for this!.

Humu jf baadhi yetu wametengeneza haki miliki ya they way they think, you have to think like them and have drawn a line of where one has to belong, you are either "with us" or "against us", if you don't sail the same boat then you are an enemy!.

Mimi binafsi nilishajipambanua kumkubali ZZK ila kwa vile mgombea wangu ni EL, then nimeitwa kila majina and in actual fact sijali sana kwa sababu nasimama na kile ninacho amini!.

Ila pia pamoja na tofauti zote za mawazo, ZZK should not keep at distance with the rest, he has not only be together but also seen to be together vinginevyo "maneno huumba", uwongo ukisemwa sana repeatdly kamwe haugeuki kuwa ukweli bali huonekana kama ndio ukweli wenyewe!.

Pamoja sana.

Pasco.

nI KWELI KABISA

ILA KUWA INCOGNITO KUNA madhara siku zote

its a community mkuu,
 
"Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea.
ASANTE SANA KWA UJUMBE MURUA, hakika endeleeni kumtia moyo aendelee kufikiri , maana kiongozi asiye fikiri hugeuka poyoyo na msaliti wa taifa lake
 
Zitto transition tangu mwanaharakati wa kutumainika na kutabirika hatua yake ya kesho kwa faida ya Umma wa Tanzania hadi kuwa a fast rate political merchant anayechumia tumbo lake mwenyewe kwa kutumia ujanja ujanja mwingi sana huyu.

Sawa na hadithi za kale mojawapo kwa watoto wadogo, Ndg Zitto hadi sasa amefuzu sana kwa mbinu yake ya kujificha kwenye kichaka katikati ya wanyama KIBOKO kwa upande mmoja na TEMBO kwa upande mwingine huku akiwafunga wote minyororo miguuni na kwa akili kama ya sungura anaendelea kumdanganya kila upande kwamba ni yeye ndiye mwenye nguvu nyingi sana tu (pamoja na udogo wake kimwili alivyo mnyama sungura) anayeendelea kumvuta na kumtoa kmasi kila mmoja wa hawa miamba miwili wa porini - CCM na CHADEMA.

Sisi wengine tulishang'amua tangu siku nyingi aina ya mchezo anaoucheza hapa kutamani kufunga goli la peke yake tangu upande mmoja wa uwanja hadi wa pili. Siku makundi mbalimbali ndani ya CCM yatakapogundua nini anchokifanya huyu ...

Laiti angalisikia na kufuata yale maneno ya hekima ya Mama yake mzazi wakati ule juu ya mienendo yake kisiasa ndani ya CHADEMA ... kila siku kazi kuwaza jinsi gani atakavyoviangusha vyama vyote viwili vya CCM na CHADEMA eti kabla ya kuwaibia mvua kwenda nayo kwenye chama chao ADC.

Bure kabisa na wala hamna kitu pale. Prof Muhongo chonde usianze kufanya madudu hapo kama ni Review, Review kweli na kusawazisha Regulatory framework nzima kwani huyo Masele anao utaalam zaidi juu ya nini sahihi zaidi kifanyike.
 
Hapa kuna harufu ya "vita vya ubinafsi wa wanasiasa",ni umimi umimi tu,hilo ndo tatizo kubwa,ubinafsi.Lakini bado hawaoni.Kwakuwa mimi nilifanya kile,basi mwingine asikifanye,bila kujali outcomes kama zina manufaa kwa taifa.Kwani ikiwa reviwed utakachokosa ni nini?Si na wewe uliwahi kufanya review?Ama anaogopa kuna ambavyo vitaoneka kuwa alishiriki?Mambo mengine bana,siasa tu.

Kuna wengine wanasema kwa vile Prof. Muhongo amebadilisha msimamo kuwa sasa mikataba ya gesi na mafuta haitaangaliwa upya hivyo mawazo ya Zitto yaungwe mkono hiyo nadhani sio sahihi.

Tulivyoirejea mikataba ya madini kamati ya Bomani iligundua mapungufu mengi yalyotokana na watu wetu kutokuwa na uzoefu wa kutosha katika contract negotiations; hivyo hivyo mikataba mingi ya oil and gas exploration iliingiwa na watu wetu ambao hawakuwa na ujuzi wa kutosha ukilinganisha na hayo makampuni ya kizungu, hivyo basi ni sahihi kureview hizi contracts ili kurekebisha mapungufu kabla hatujapata hasara kama tuliyopata kwenye mikataba ya madini!! Katika mikataba ya madini kwa mfano hakukuwa na kipengele cha contract RENEGOTIATION and REVIEW after a certain period, hicho ni kipengele muhimu kuwa kwenye hii mikataba ya gesi na mafuta!!
 
Ndiyo maana nikasema ni ubinafsi,mbona yeye alikuwepo kwenye kamati ya Bomani ya reviewing?Tena walilipwa pesa nyingi sana tu?Ni ubinafasi tu ukiangalia kwa makini.Yote hayo ni kwa gharama ya taifa ili tu yeye kama individual aonekane ndo yuko makini.

Sasa mapendekezo ya kamati yake ni kuwa mikataba ipitiwe,kaja waziri anasema ipitiwe,yeye anakataa,sasa ina maana anapingana na mapendekezo ya kamati aliyuokuwemo?Na hivyo taifa limepoteza pesa zote walizolipwa kufanya kazi hiyo?

Ndo unaona there's something fishy!
 
Kitila Mkumbo

comrade umeniongeza kitu kikubwa sana kataka ufahamu wangu mkuu naidi kuzaliwa upya kupitia ninyi watangulizi asante sana comrade kwa hii comment yako
 
Last edited by a moderator:
Ndinani

Sidhani kama Zitto ana matatizo na ku review mikataba, alichokuwa anaongelea Zitto ni kusababisha unecessary Panic kwa wawekezaji kwakuw abado sisi kama nchi tunawahitaji hawa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom