Whats wrong with this picture part 1

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
03_11_way0pn.jpg

03_11_e0pw2s.jpg

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akipewa maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha huduma za Forodha cha Mamlaka ya Mapato nchini (TRA),Victor Msuya wakati Rais alipofanya ziara kwenye kituo hicho mjini Dar es Salaam.Kulia kwa Rais ni Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na Kamishna wa Forodha na Ushuru,Walid Juma.
14.jpg

Rais Jakaya Kikwete(wa tatu kushoto)akisikiliza Hotuba ya waziri a Fedha Mustapha Mkulo wakati alipokua akitoa ripoti ya utekelezaji wa mambo mbalimbali ya wizara hiyo.Rais Jakaya Kikwete ametembela Wizara hiyo kwa Mara ya Kwanza Tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka Jana
13.jpg

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini Harry Kitiya(kulia)na Gavana wa Benki Kuu Dk Benno Ndulu wakiwa kwenye Mkutano ziara ya fedha na Uchumi leo Jijini Dar es Salaam ambao Rais Jakaya Kikwete aliudhuria
12.jpg

Rais Jakaya Kikwete(kulia)akikaribishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapa Mkulo Muda Mfupi baada ya Kuwasili Wizarani Hapo Jijini Dar es Salaam Leo
10.jpg

Msemaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ingiedi Mduma(mbele) akiwaongoza Kamishna Mku wa Mapato Nchini(TRA) Harry Kitilya(Kulia)na Gavana Mkuu Dk Benno Ndulu Kwenda Kumpokea Rais Jakaya Kikwete leo alipotembelea Wizara ya Fedha na Uchumi Jijini Dar es Salaam
5.jpg

2.jpg

Picha juu ni baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Uchumi wakimsubiri Kumpokea Rais Jakaya Kikwete wakati alipotembelea Wizara hiyo leo Jijini Dar es Salaam​
 
Kwa hesabu ya haraka haraka hapo ni kama wafanyakazi kwa kukisia ni 100.

Tuseme wamekaa kumpokea Rais wizarani na nategemea wengi wao baada ya hapo wamerudi makwao.

Kwa hiyo masaa 10*100 wafanyakazi ni 1000 masaa ya kazi yamepotea na sisi tunalia uchumi ni mgumu.

Hapo sijaeka masaa ya watumia barabara ambazo zilifungwa......Je kweli tunahitaji huu uzembe?
 
SLIDINGROOF ana point fulani hapa lakini kwa ninavyojua members wengi watakuja kuagalia picha tu na kuponda wakati kuna jambo la msingi la kujadili.

Kulikuwa hakuna haja ya wafanyakazi karibu wa ofisi nzima kuwa nje kumsubiri mtu mmoja, nimgekuwa mimi rais ningewaambia nashukuru lakini nyie ni wazembe siku nyingine msirudie kuacha kazi zenu kuja kunipokea, ndiyo maana wazungu hufanya kazi na kulipwa kwa masaa.
 
JK hajapiga suti.. Hapa nampa tano.. Sijui kwa nini huyu jamaa (sharobaro) utawala wake umekuwa mgumu hivi
 
SLIDINGROOF ana point fulani hapa....Kulikuwa hakuna haja ya wafanyakazi karibu wa ofisi nzima kuwa nje kumsubiri mtu mmoja,

Kweli kabisa ndugu

nimgekuwa mimi rais ningewaambia nashukuru lakini nyie ni wazembe siku nyingine msirudie kuacha kazi zenu kuja kunipokea.

Nadhani unapokuwa kiongozi si busara kutumia lugha hiyo
kwasababu wanaweza kuchukulia vibaya, wataona una dharau.

Ni vizuri kutoa ujumbe kidiplomasia kama vile Nyerere alivyomwambia
JK kua, wewe bado mdogo.
 
Ni wafanyakazi wa serikali sio. Haya ndio mafanikio ya Kikwete sio? All they have pics za image ya low vision ya kikwete. Why not taking picture in presidential office when kikwete is dowans's signing deal
 
Kwa hesabu ya haraka haraka hapo ni kama wafanyakazi kwa kukisia ni 100.

Tuseme wamekaa kumpokea Rais wizarani na nategemea wengi wao baada ya hapo wamerudi makwao.

Kwa hiyo masaa 10*100 wafanyakazi ni 1000 masaa ya kazi yamepotea na sisi tunalia uchumi ni mgumu.

Hapo sijaeka masaa ya watumia barabara ambazo zilifungwa......Je kweli tunahitaji huu uzembe?

Jamani tuwe siriaz!!!! kufunga barabara wakati ikulu na hazina zinatazamana? ni kiasi cha kuvuka barabara tu! hivi nalo hilo linakuwa suala gumu? ingekuwa na barrack anatembea tu....
 
For the 1st time, nimemwona kikwete akiwa serious bila ya kucheka cheka ovyo!
Pia hao wafanyakazi wamenona na wanaonekana kama matawi flani.
Kikwete mvi kibao na sura imechoka kimtondo.
 
JK hajapiga suti.. Hapa nampa tano.. Sijui kwa nini huyu jamaa (sharobaro) utawala wake umekuwa mgumu hivi

Heeh kumbe hizi suti nyingine kaka "Kaunda Suit" na "safari suit" siyo suti? Sema hajapiga suti ya kimagharibi.
 
Rais anatembea na kundi kubwa sana la watendaji wengine wabaki maofisi kutekeleza majukumu ya ujenzi wa taifa
 
Ninachokiona hapa ni kufungwa kwa ofisi na huduma kusimama kwa sababu tu rais kaja kutembelea ofisi yetu! Huu ndo uzuri wa kufanya kazi ofisi za serikali
 
JK hajapiga suti.. Hapa nampa tano.. Sijui kwa nini huyu jamaa (sharobaro) utawala wake umekuwa mgumu hivi

upresident si kula na kunywa, kusafiri hovyo na kuponda raha bila mpangilio kama anavyofanya
 
jamaa haelewi anachoelezwa,anasikiliza tu kutimiza wajibu..........coz he iz a politician by profession:tongue:
 
Mkulo na Kitilya wamevaa beji zenye picha ya rais, hii inamaanisha nini?
 
hakukuwa na sababu za mkuu kutumia usafiri wa gari angeweza tembea tu ofisi zote ziko eneo moja . lakini binafsi nimefurahishwa na jinsi alivyokuwa anaonekana alionekana yupo makini sana na hakuwa anacheka cheka. alipopatiwa taarifa alizinakiri kwenye note book yake , pia akasikiliza matatizo ya wananchi japo walinzi wake hawakupenda.

nadhani tupunguze mashambulizi kwa jk sababu sioni kama yanabadilisha chochote . nawasilisha
 
Back
Top Bottom